SURA YA PILI
NISHATI
Msamiati
Kwenye mazingira tunayoishi kuna vitu mbalimbali vinavyotoa nishati. Nishati ni nguvu inayowezesha kazi mbatimbali kufanyika. Tunapotumia vitu kama kurunzi, jiko na ngoma tunaweza kutambua aina mbalimbalti za nishati. Kuna aina tatu za nishati. Aina hizi ni nishati ya sauti, joto na mwanga.
Nishati ya sauti
Chunguza picha hizi, kisha soma maetezo yanayofuata.
Kidelezo : Vitendo vya kutoa sauti
Sauti ni aina ya nishati inayotokana na mitetemo ya vitu mbalimbali. Sauti husaidia mawasiliano kufanyika. Nishati hii husambaa kutoka kwenye chanzo kwenda sehemu nyingine. Unapopiga ngoma, filimbi au gitaa kinachotokea ni sauti.
Vilevile, vyanzo vingine vya sauti ni kinanda, tarumbeta, gitaa na kengete. Pia, watu wanapoongea au kuku anapoita vifaranga vyake, kinachotokea ni sauti
Kutambua sauti inavyosafiri katika hewa
Chunguza wakati kengete inapogongwa
Kuakisiwa kwa sauti
Sauti inapokutana na kizuizi au kitu kigumu kama ukuta au mwamba huakisiwa. Sauti iliyoakisiwa huitwa mwangwi.
Kufanya kitendo cha kutoa mwangwi
Ingia kwenye Chumba kisicho na kitu ita kwa sauti kubwa.
Je, unasikia nini?
Kuchunguza kama sauti husafiri katika maji
Mahitaji;
Beseni, maji na jiwe dogo
Hatua;
Jaza maji kwenye beseni. Hakikisha maji yametulia kwenye beseni. Dondosha kipande cha jiwe katikati ya beseni ya maji
Je, unasikia na unaona nini? Andika unachokisikia na kuona
Sauti husafiri katika maji kama ilivyo katika hewa.
Unapodondosha kitu kwenye maji, sauti hutokea pamoja na mawimbi.
Mawimbi yanaonesha jinsi sauti inavyosafiri katika maji. Pia, hata ukiwa ndani
ya maji unaweza kusikia sauti toka sehemu moja hadi nyingine.
Kuchunguza sauti inavyosafiri kupitia kamba
Mahitaji
Hatua
Mwanafunzi mmoja akiongea, mwingine atasikia kupitia spika iiiyounganishwa kwa kamba. Hivyo, inaonesha kuwa sauti husafiri katika kamba.
Chunguza picha, kisha fanya kazi namba 5.
Kieldezo : Kusafiri kwa sauti kwenye chuma
Kuchunguza sauti inayosafiri kupitia chuma
Mahitaji;
Hatua
Tumeona kuwa hewa, maji, kamba ya manila na chuma hupitisha sauti. Hii inaonyesha kuwa vitu vigumu, vimiminika na hewa husafirisha sauti. Sauti inatumika katika mawasiliano
Nishati ya joto
Toto ni mojawapo ya aina za nishati. Nishati ya joto inaweza kusafiri kutoka kwenye chanzo cha joto kwenda kwenye hali ya ubaridi. Nishati ya joto
husafiri katika vitu vigumu, vimiminika na gesi. Kwa mfano, joto husafiri katika chuma (vitu vigumu), maji (vimiminika) na hewa (gesi).
Tazama picha hizi, kisha soma maelezo yanayofuata.
Kielelezo: Vyanzo vya nishati ya joto
Picha a inaonesha jua kama nishati ya joto.Vilevile jua ndio chanzo kikuu cha nishati ya joto: Picha b na c zinaonesha vitendo vya kupika chakula kwa
kutumia kuni na mkaa,. Kuni na mkaa ni chanzo cha nishati ya joto. Picha d nae zinaonesha vitendo vya kupika chakula kwa kutumia umeme na, gesi. Umeme
na gesi pia ni vyanzo vya joto.
Kudhibitisha namna ya kupata Joto
Hatua
Utagundua kuwa msuguano wa aina yeyote ukifanyika joto hutokea
Iota husafiri kwa urahisi katika vitu vigumu (yabisi)kutiko vimiminika au gesi. Baadhi ya vitu vigumu vinavyopitisha joto kwa urahisi ni chuma na bati.
Vipo vitu vigumu visivyopitisha joto kwa urahisi kama vile ptastiki au mbao kutokana na asili ya vitu
Joto husafiri kwa njia kuu tatu ambazo ni;
Matumizi ya nishati ya joto
Vilevile, tunatumia joto kupikia chakuta na kukaushia nguo na vyakula. Matumizi mengine ya joto ni kuchemsha maji ya kunywa, kuangulia vifaranga na
kuchoma nyama.
Nishati ya mwartga
Chunguza picha hizi, kisha soma maelezo yanayofuata.
Vyanzo vya nishati ya mwanga
Mwanga ni aina mojawapo ya nishati. Picha namba a, na c zinaonesha vyanzo mbalimbali vya nishati ya mwanga. Vyanzo hivyo ni vile vya asili na visivyo vya
asili. Jua ndiyo chanzo kikuu cha asili cha mwanga. Vyanzo vya mwanga visivyo vya asiti ni mshumaa, kibatari, karabai, kanditi na kurunzi..
Tabia ya nishati ya mwanga
Kuchunguza mwanga unavyosafiri katika hewa
Chunguza asubuhi na maperna jua linapochomoza.
Je, unaona nini? Weka kumbukumbu ya kile unachokiona.
Ukiamka asubuhi na mapema wakati jua tinaanza kuchomoza utaona miale ya mwanga. Miale hii huonekana inasafiri katika mistari iliyonyooka.
Mwanga ni n.ishati inayotuwezesha kuona. Pia,inawezesha ukuaji wa mimea.
Kuchunguza vitu vinavyopitisha na visivyopitisha mwanga
Mahitaji - glasi, karatasi ngumu isiyo na tobwe, karatasi ngumu yenye tobwe, kitabu, kurunzi na maji
Hatua
Je, unaweza kuona mwanga wa kurunzi katika karatasi ngumu isiyo na tobwe?
Miale ya mwanga imetoka kwenye kurunzi na kupita wenye tobwe. Kisha miale hiyo hupita kwenye maji na glasi na kutoka nje.
Mwanga huweza kupita kwenye baadhi ya vitu kama vile maji na glasi. Mwanga hauwezi kupenya katika baadhi ya vitu kama kitabu na karatasi ngumu.
Tabia za mwanga ni
www.learninghubtz.co.tz