SURA YA KWANZA
MAZINGIRA
Msamiati
Mazingira ni jurata ya vitu vyote vinavyotuzunguka. Vitu hivyo ni kama vile udongo, mimeo, majengo, wanyama, hewa na maji. Tunachunguza mazingira kwa kutumia viungo mbatimbati vya mwili. Viungo hivyo ni macho, pua, masikio, ngozi na Mimi. Macho hutumika kuona na kutambua vitu. Tunaona vitu vyenye rangi mbatimbati kama vile maua na mavazi..
Pia, tunagundua eneo safi au chafu kwa kuona.
Pua ni kiungo kinachotumika kunusa. Unaweza kutambua mazingira yenye harufu nzuri au mbaya kwa kutumia pua.
Masikio hutumika kutambua na kutofautisha sauti za vitu mbalimbali. Mfano, sauti ya mngurumo wa gari, sauti ya ndege na sauti ya ngoma.
Ngozi hutumika kuhisi vitu mbalimbai katika mazingira. Unapokuwa karibu na kitu chrenye joto, ngozi ya mwiti huhisi hati ya joto. Ukiwa karibu na kitu cha baridi ngozi ya mwi[i kuhisi baridi. ukigusa kitu, n.gozi yahuhisi kuwa kitu hicho ni kigumu, kitaini au kinakwaruza.
Utimi hutumika kuonja vitu mbalimbali kama chakula, matunda na vinywaji. Hairuhusiwi kuonja vitu tusivyovifahamu wakati wa kufanya uchunguzi.Vitu vingine ni sumu.
Viungo mbalimbali
Vitu na viumbe hai
Tazama picha hizi, kisha jibe swab.
Kielelezo Baadhi ya viumbe hai na vituvinavyopatikana katika mazingira
Picha unazoziona zinaonesha ng'ombe, nyasi, mwembe, meza na mkate. Vilevile, zinaonesha chupa ya chai, kalamu, sahani na mpira wa miguu. Katika
picha hizo vitu ni meza, mkate, chupa ya chai na sahani. Vitu vingine ni kalamu na mpira wa miguu.
Vilevile, katika picha hizo viumbe hai ni ng’ombe, nyasi na mwembe
Kuchunguza tofauti kati ya panzi, mende na jiwe kwenye chupa
Mahitaji;
Hatua
Panzi akiwa ndani ya chupa ataonekana anaruka na mende atakuwa anatambaa. Kuruka kwa panzi. Na Kutambaa kwa mende ni kujongea. Kujongea huwasaidia viumbe hai kutafuta mahitaji muhimu kama chakula na sehemu salama. Matundu yaliyopo kwenye chupa yanawasaidia kupata, hewa. Viumbe hai wakikosa. Hewa hufa. Jiwe halioneshi kitendo chochote ndani ya chupa kwa kuwa halina uhai.
Viumbe hai hukua na kuongezeka kimo na uzito. Mfano, binadamu hukua kwa kupitia hatua mbalimbali za ukuaji. Hatua hizo ni kama vile, utoto, ujana, utu
uzima hadi uzee.
Kielelezo Hatua za ukuaji wa binadamu
Pia, mimea hukua kwa kuongezeka kimo.
Kielelezo : Hatua za ukuaji katika mimea.
Vilevile viumbe hai huzaliana. Kwa mfano, mimeo huzaliana kwa kutoa mbegu. Wanyama huzaliana kwa kuzaa watoto au kutaga mayai.
Tazama picha hii, kisha soma maetezo yanayofuata.
Kielelezo: Mbuzi akita majani
Kula ni mojawapo ya sifa za viumbe hai. ili viumbe hai viishi vinahitaji chakula Bila chakula. Bila chakula viumbe hai hufa.
Kwa hiyo, viumbe hai wana sifa za kujongea, kula, Kupumua, kukua na kuzaLiana. ViLeviLe, sifa nyingine za viumbe hai ni kuhisi na kutoa taka mwili.
Kuthamini vitu na viumbe hai
Viumbe hai huthaminiwa kwa kulindwa, kupewa chakula, maji na kuhifadhiwa katika mazingira salama. Hivyo, tunapaswa kutunza mazingira ili kuwezesha viumbe hai kuzaliana, kukua na kuishi.
Kutunza mazingira
Vitu na viumbe hai hatari
Ni muhimu kuchukua tahadhari unapofanya uchunguzi katika mazingira. Hii ni kwa sababu baadhi ya viumbe hai wanauma na wana sumu kali. Vilevile, baadhi ya vitu vinachoma, vinaunguza na hutoa harufu kali.
Kielezo: vitu na viumbe hai hatari
www.learninghubtz.co.tz