MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A SITA

KUWAJIBIKA NA KUTUNZA RASILIMALI ZA UMMA

MADA YA NANE

  1. Kwa nini tunapaswa kutunza rasilimali za nchi yetu?
  1. Ili ziweze kunufaisha Watanzania wa leo na kwa vizazi vijavyo
  2. Kuwezesha upatikanaji wake kwa matumizi ya sasa tu
  3. Ili wageni wasipore rasilimali zetu
  4. Ili kunufaisha wawekezaji
Choose Answer


  1. Moja kati ya hizi si athari za rushwa katika jamii:
  1. Serikali kushindwa kufikia malengoyake
  2. Kuongezeka kwa gharama za kiutawala
  3. Kukosekana kwa ujasiri na kushindwa kufikia kiwango cha juu cha uadilifu
  4. Kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato
Choose Answer


  1. ipi kati ya zifuatazo ni oja ya mbinu stahiki za kulinda rasilimali za Umma?
  1. Kuzuia kwa wageni ili kupata fedha
  2. Kutoa elimu ya utunzaji wa rasilimali za nchi
  3. Kuzigawa kwa wananchi wazitumie
  4. Kuzuia zisitumike kabisa
Choose Answer


  1. Vipi ni vitendo vya matumizi mabaya ya mali ya umma?
  1. Kuzitumia kwa manufaa ya wananchi
  2. Kuwamilikisha wageni kutoka nchi za nje kiholela
  3. Kuzihifadhi kwa kushirikisha wananch
  4. Kuzuia ujangili na uwindaji holela wa wanyama pori
Choose Answer


  1. Ipi kati ya vifuatavyo si miongoni mwa vitendo vya kulinda nchi yetu?
  1. Kutoa taarifa za uhalifu
  2. Kulinda mipaka ya nchi
  3. Kutoa taarifa kwa wahalifu kuhusu rasilimali zilizopo nchini
  4. Kusimamia sheria na kulinda rasilimali zetu
Choose Answer


6. Usalama wa mali ya shule unaweza kuimarishwa kwa:

  1. kuzuia wageni kuingia katika eneo la shule.
  2. kushirikisha Jeshi la Wananchi la Tanzania.
  3. kuepuka mahusiano ya karibu na jamii inayozunguka shule.
  4. kuwekea bima mali ya shule dhidi ya wizi.
  5. kujenga uzio kuzunguka shule.
Choose Answer


7.  Vyanzo vya mapato ya serikali za mitaani pamoja na:

  1. kodi ya kichwa na kodi ya rasilimali
  2. ruzuku, kodi na michango mingine
  3. kodi ya ardhi, na kodi ya rasilimali
  4. tozo katika mazao ya mali asili 
  5. tozo za leseni za biashara
Choose Answer


8. Ni hatua zipi wanafunzi wanatakiwa kuchukua wanapoona katika eneo la shule wageni wanaowatilia shaka? 

  1.  Kutoa taarifa kwa jeshi la Wananchi la Tanzania. 
  2.  Kutaarifu Kamati ya Shule kuhusu uwepo wa wageni.
  3.  Kuwapiga wageni kabla ya kuwafikisha Mahakamani.
  4.  Kuwakamata wageni na kuwahoji.
  5.  Kutaarifu Walimu kuhusu uwepo wa wageni.
Choose Answer



 9. Jukumu la kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao lipo mikononi mwa

  1. Jeshi la Wananchi la Tanzania
  2. Idara ya Usalama wa Taifa
  3. Jeshi la Magereza
  4. Jeshi Ia Mgambo
  5. Jeshi la Polisi
Choose Answer


10. Wajibu wa serikali katika kujenga maadili ya viongozi ni....................

  1. Kuwakopesha magari viongozi wote
  2. Kuimarisha mfumo wa chama kimoja cha siasa
  3. Kusimamia sheria za utumishi wa umma
  4. Kuhamisha watumishi wasio waadilifu
  5. Kuajiri watumishi wenye elimu ya juu to
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256