MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA

MFUMO WA JUA

Chagua jibu sahihi

  1. Moja kati ya mambo yafuatayo huathiri uimara wa tabaka la ozone:
  1. Upepo
  2. Hewa ya oksijeni
  3. Radi na mvua
  4. Gesi ya kloroflorokaboni
Choose Answer


  1. Tabaka la ozoni ni sehemu ya tabaka la chini la?
  1. Angatropo
  2. Angastrato
  3. Angameso
  4. Angajoto
Choose Answer


  1. Mionzo hatari ya jua huchujwa katika tabaka gani?
  1. Tabaka la ozoni
  2. Tabaka la angameso
  3. Tabaka la angajoto
  4. Tabaka la angatropo
Choose Answer


  1. Moshi mzito unaotoka viwandani huwa na vitu gani vinavyoharibu tabaka la ozoni?
  1. Hewa ya oksijeni
  2. Harufu mbaya
  3. Gesi haribifu
  4. Upepo
Choose Answer


  1. Mionzo ya jua ya utravaoleti inaweza kusababisha nini?
  1. Magonjwa ya ngozi kwa binadamu
  2. Wadudu kuzaliana
  3. Vichaka kuungua
  4. Joto kupungua duniani
Choose Answer


6. Ili kupunguza/kuondoa ongezeko la joto la dunia tunapaswa .........

  1. tuongeze utoaji wa hewa ya kabonidayoksaidi
  2. tuongeze hewa ya kabonidayoksaidiinayotolewa na wanyama
  3. tutumie vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira
  4. tuchome vichaka, misitu na nyasi
  5. tukate miti ili kupata eneo la kilimo
Choose Answer


7. Jua la utosi katika mwezi Disemba huwa katika .

  1. Kizio cha Kusini.
  2. Tropiki ya Kansa.
  3. Ikweta.
  4. Kizio cha Kaskazini.
  5. Tropiki ya Kaprikoni.
Choose Answer


8. Jua linaonekana kubwa kuliko nyota zingine kwa sababu ...

  1. lina joto kali kuliko nyota zingine.
  2. lina mwanga mkali kuliko wa nyota zingine.
  3. linatupatia nguvu ya jua.
  4. liko mbali sana na dunia.
  5. liko karibu zaidi na dunia.
Choose Answer


9. Nishati gani kati ya zifuatazo inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira?

  1. Jua
  2. Upepo
  3. Maji
  4. Mkaa.
  5. Kinyesi cha wanyama
Choose Answer


10. Angahewa lina sehemu kuu ngapi?................

  1. Nne
  2. Nane
  3. Mbili
  4. Tatu
  5. Tano
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256