MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA
MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA
ATHARI ZA NJIA ZILIZOTUMIKA KUDAI UHURU AFRIKA
Chagua jibu sahihi
1. Vita vya Maji Maji vilisababishwa na:
- maji na dawa toka mto Rufiji
- tamaa na ushawishi wa waganga wa kienyeji
- unyonyaji wa Wajerumani
- ukatili wa Wamatumbi wa Songea
- majaribio ya silaha za jadi
Choose Answer
2. Tanganyika ilipata Uhuru wake kwa njia ya:
- matumizi ya bunduki
- vita vya msituni
- mikataba ya kilaghai
- kikatiba
- matumizi ya Veto
Choose Answer
3.Utawala waWaingereza nchini Tanganyika uliisha mnamo .....
- karne ya 15
- karne ya 19
- karne ya 20
- karne ya 18
- karne y 17
Choose Answer
4. Mataifa ya Ulaya yaliyokuwa yakipigania Mto Nile yalikuwa:
- Ufaransa na Ubelgiji
- Uingereza na Ujerumani
- Ufaransa na Ureno
- Uingereza na Ufaransa
- Ubelgiji na Ureno
Choose Answer
5. Mapambano ya kudai Uhuru katika bara la Afrika yalianza baada ya:
- Kuundwa kwa Umoja wa Mataifa
- Kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti
- Vita Kuü ya Pili ya Dunia
- Kupigwa marufuku biashara ya watumwa
- Kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi
Choose Answer
6. Mojawapo ya athari ya utawala wa Waingereza katika visiwa vya Unguja ilikuwa ....
- kukomesha biashara ya utumwa.
- kuanzishwa kwa dini ya kikristu.
- kuondoa umaskini.
- kuanzisha kilimo cha karafuu.
- kuanzisha vyama vya siasa.
Choose Answer
7. Makoloni ya Ujerumani katika Afrika yalikuwa ..
- Naijeria, Namibia na Togo.
- Gambia, Togo na Namibia.
- Kameruni, Togo na Namibia.
- Namibia, Tanganyika na Naijeria.
- Kameruni, Tanganyika na Senegal.
Choose Answer
8. Moja ya mbinu iliyotumika kudhoofisha teknolojia ya Waafrika wakati wa ukolono ni
- kufundisha masomo ya sayansi.
- kuanzisha viwanda vya kisasa katika Afrika.
- kubinafsisha viwanda vya Afrika.
- kuleta bidhaa za viwandani kutoka ulaya.
- kufundisha Waafrika teknolojia ya Ulaya.
Choose Answer
9. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885 uliitishwa na ..
- Carl Peters
- Johann Krapf
- Henry Stanley
- David Livingstone
- Otto Von Bismarck.
Choose Answer
10. Mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma katika Afrika alikuwa ...
- Horace Byatt
- Friedrick Lugard
- Richard Turnbull
- Donald Cameroon
- Edward Twinning
Choose Answer
11.Ni Taifa lipi la kibepari liliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1891 hadi 1918?
- Ujerumani
- Uingereza
- China
- Ureno
- Ufaransa
Choose Answer
12. Kwa nini Berlin ni miongoni mwa miji maarufu katika historia?
- Ni Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa
- Ni Makao Makuu wa Jumuiya ya Madola
- Ni mji uliokuwa kitovu cha biashara ya utumwa
- Ni mji wa Ufaransa ambao uliendesha utawala wa kulisha kasumba
- Ni mji ambao mgawanyo wa Bara la Afrika ulifanyika
Choose Answer
13.Mataifa makubwa ya kibepari yaliyogombania Bara la Afrika yalikuwa
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Ureno
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uchina, Uhispania na Marekani
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Japani, Uhispania na Ubelgiji
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Japani
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Uchina
Choose Answer