MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA
MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA
UJASIRIAMALI
Chagua jibu sahihi
1.Aina kuu mbili za biashara ni:
- biashara ya mkopo na ya malipo
- biashara ya mkopo na kubadilishana
- biashara ya mtaji na fedha
- Biashara ya hisa na ya mitaji
- biashara ya ndani na ya nje
Choose Answer
2.Nini maana ya ujasiriamali?
- Bishara yoyote yenye faida
- Uwekezaji kwenye biashara
- Biashara ndogondogo
- Sekta binafsi
- Ujasiri wa kumiliki mali
Choose Answer
3. Zipo aina tatu za mipango ya uchumi ambayo ni mipango ya ...
- miaka kumi, kumi na tano na ishirini na tano
- Taifa, Mkoa na Wilaya
- kilimo, biashara na viwanda
- muda mrefu, dharura na muda mfupi
- muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu
Choose Answer
4. Ufugaji wa kisasa wa wanyama huzingatia nini? ..
- Utamaduni wa jamii
- Ubora wa wanyama na mazao yao.
- Kuwepo kwa ardhi ya kutosha.
- Mbuga za asili za kulishia mifugo.
- Hali ya hewa.
Choose Answer
5. Ni katika mfumo upi wa kiuchumi ambamo njia kuu za uzalishaji mali wanajamii wote?
- Utumwa
- Ukabaila
- Ubepari
- Ujima
- Ujamaa
Choose Answer
6. Ipi kati ya fursa hizi za kibiashara haipatikani mijini?
- Ufugaji
- Kushona nguo
- Usafirishaji
- Kuuza vyakula
Choose Answer
7. Faida ya ubunifu ni hizi isipokuwa;
- Kuvutia wateja
- Kukabiliana na ushindani
- Kuiga kazi za wengine
- Kuongeza faida
Choose Answer
8. Ipi sio aina ya wajasiriamali?
- Wajasiriamali wabunifu
- Wajasiriamali wafanyabiashara
- Wajasiriamali watumishi
- Wajasiriamali jamii
Choose Answer
9. Tabia hizi zinaweza kukwamisha biashara yako isipokuwa
- Kujituma
- Uvivu
- Kuwa na visingizio
- Kupoteza muda
Choose Answer
10. Ipi sio tabia ya mjasiriamali?
- Uthubutu
- Uaminifu na uadilifu
- Kukata tama
- Ubunifu
Choose Answer
11. Fursa ya ujasiriamali inayopatikana vijijini pamoja na
- Ukulima
- Ufugaji
- Uchimbaji madini
- Zote hizo
Choose Answer
Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.
- Kufanya biashara haramu ni njia halali inayotumiwa na baadhi ya wajasiriamali ili kujiongeza kipato............
View Answer
- Wajasiriamali wanashauriwa kuepuka kujiingiza kwenye biashara haramu kama vile biashara ya kuuza vipodozi vyenye viambato vyenye sumu.............
View Answer
- Ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wajasiriamali hukosesha taifa mapato...........
View Answer
- Ubora wa bidhaa za wajasiriamali huthibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)..........
View Answer
- Namna ya kudhibiti njia zisizohalali katika ujasiriamali ni kutoa elimu kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla..............