MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA TANO

KUJIREKEBISHA KWA VIUMBE KULINGANA NA MAZINGIRA

Chagua jibu sahihi

1. Wadudu wanapohama toka ua moja kwenda lingine wanafanya hivyo ili:

  1. kuzalisha mimea  
  2. kuepuka maadui
  3. kutafuta nekta 
  4. kutafuta harufu 
  5. kusambaza mbegu
Choose Answer


2. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

  1.  joto na unyevu     
  2.  unyevu na mwanga
  3. upepo na mwanga wa jua               
  4.  mawingu na upepo
  5. unyevu na upepo
Choose Answer


3.  Kinyonga hujibadili rangi yake ili:

  1.  kutafuta chakula         
  2.  kupumua          
  3.  kuzaliana
  4.  kutafuta maadui                          
  5.  kujilinda dhidi ya maadui
Choose Answer



4. Fototropizimu ni kitendo cha mmea kuota kuelekea kwenye:

  1. mwanga 
  2. kani ya mvutano 
  3. maji 
  4. giza
  5. kemikali.
Choose Answer



5. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?

  1. Vyura
  2. Samaki 
  3. Mamba
  4. Mbu
  5. Nyoka
Choose Answer


6.   Uhusiano uliopo kati ya viumbe hai na visivyo hai katika mazingira unaitwa

  1. kutegemeana 
  2. wando chakula 
  3. ikolojia 
  4. mlishano 
  5. mizania asili.
Choose Answer



7. Wanyama wenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu ni wale wa kundi la

  1. Ndege
  2. Amfibia
  3. Reptilia
  4. Samaki
  5. Mamalia
Choose Answer


8.  Panya aliyekuwa amefungiwa kwenye kisanduku kilichokuwa na kipande cha nyama alikufa baada ya siku mbili. Ni kitu gani kilisababisha panya huyo kufa?

  1. Alikula nyama iliyooza
  2. Alikosa hewa ya kabondayoksaidi 
  3. Alikosa hewa ya oksijeni.
  4. Alikosa maji ya kutosha baada ya kula nyama.
  5. Alikosa mwanga ambao ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama.
Choose Answer



9.  Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?

  1. Angani na ardhini
  2. Ardhini na majini. 
  3. Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
  4. Ardhini na mapangoni 
  5. Kwenye misitu.
Choose Answer


10. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya kinyonga?............

  1.  Hubadili mlio wa sauti yake 
  2.  Huchagua aina ya chakula
  3.  Hubadili rangi ya mwili 
  4.  Hatoi taka mwili
  5.  Hubadili mwendo
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256