MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA TANO

MAGONJWA YA MLIPUKO

 

         Chagua jibu sahihi kati ya majibu uliyopewa katika kila swali

  1. Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na………………..
  1. Bakteria
  2. Virusi
  3. Viroboto wa nyani
  4. Ukosefu wa maji mwilini
Choose Answer


  1. Dalili za ugonjwa wa ebola huanza kuonekana kwa mgonjwa ndani ya siku ……………baada ya maambukizi
  1. Nne hadi saba
  2. Tano
  3. Mbili hadi ishirini na moja
  4. Mbili hadi tano
Choose Answer


  1. Zifuatazo ni njia ambazo ugonjwa wa ebola unaweza kuenezwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, isipokuwa………………
  1. Kugusana na mgonjwa wa ebola
  2. Kushika damu ya mtu mwenye virusi vya ebola
  3. Kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana na kuhudumia mgonjwa wa ebola
  4. Kukaa mbali na mgonjwa wa ebola
Choose Answer


  1. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa ebola, isipokuwa……………
  1. Kuvuja damu puani na sehemu zingine za mwili
  2. Maumivu ya tumbo na misuli
  3. Kutokwa na malengelenge ambayo hupasuka na kuisababishia Ngozi michubuko
  4. Maumivu ya koo
Choose Answer



5. Kwa nini ni muhimu kuosha matunda kabla ya kula?

  1.  Kuondoa sumu 
  2.  Kuondoa vimelea
  3.  Kuondoa utomvu 
  4.  Kuondoa harufu mbaya
  5.  Kuondoa chumvichumvi
Choose Answer


6. Magonjwa yapi kati ya yafuatayo huzuiliwa kwa chanjo?................

  1.  Surua na kifaduro 
  2.  Kichocho na malaria
  3.  Kuhara na mkamba 
  4.  Ukimwi na kisukari
  5.  Kifua kikuu na tetekuwanga
Choose Answer


7. Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa

  1. UKIMWI 
  2. Trikomona
  3. Kaswende 
  4. Klamedia
  5. Trakoma
Choose Answer


8. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?

  1. Wote walioko hewani 
  2. Basili
  3. Plasimodiamu 
  4. Fungi 
  5. Amiha
Choose Answer


9. Magonjwa ya zinaa huambukizwa kwa njia ya:

  1. kugusana 
  2. kupeana damu
  3. kucheza pamoja 
  4. kuchangia vikombe
  5. kujamiiana
Choose Answer


10. Ugonjwa wa surua huenezwa kwa njia ya:

  1. inzi 
  2. sindano 
  3. kugusana
  4. mbu
  5. hewa
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256