MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA TANO

IKOLOJIA

 

Chagua jibu sahihi

 

1. Nini kitatokea iwapo idadi ya wanyama wanaokula nyama katika eneo ni kubwa kuliko idadi ya wanaokula majani?

  1. Majani yatapungua
  2. Majani yatabakia kama yalivyokuwa awali
  3. Majani yatanyauka
  4. Majani yataongezeka
  5. Majani yataliwa
Choose Answer


2 .Kitendo cha bakteria kuozesha kinyesi cha wanyama kwenye shimo pasipokuwa na hewa ya oksijeni husababisha:

  1.  joto kali 
  2.  gesivunde/biogesi
  3.  asidi kali               
  4.  alkali kali        
  5.  haidrojeni
Choose Answer


3.  Kinyonga hujibadili rangi yake ili:

  1.  kutafuta chakula         
  2.  kupumua          
  3.  kuzaliana
  4.  kutafuta maadui                          
  5.  kujilinda dhidi ya maadui
Choose Answer


4. Mlishano sahihi ni:

  1. Mwewe  Nyasi  Chui  mbuzi 
  2.  Nyasi  Mwewe  chui  mbuzi
  3.  Chui    Mwewe  Nyasi  mbuzi
  4. Nyasi  mbuzi  chui    mwewe
  5. Mwewe  chui  mbuzi  nyasi 
Choose Answer


5. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?

  1. Vyura
  2. Samaki 
  3. Mamba
  4. Mbu
  5. Nyoka
Choose Answer


6.   Uhusiano uliopo kati ya viumbe hai na visivyo hai katika mazingira unaitwa

  1. kutegemeana 
  2. wando chakula 
  3. ikolojia 
  4. mlishano 
  5. mizania asili.
Choose Answer


7. Ingawa wanyama huvuta hewa ya oksijeni na kutoa hewa ya kabondayoksaidi, hewa hizi hazipungui wala kuongezeka kwenye mizazi kwa kuwa.

  1. oksijeni ipo kwa wingi kwenye mizazi
  2. kabondayoksaidi hubadilika kuwa oksijeni
  3. mimea hutumia kabondayoksaidi na kutoa oksijeni
  4. kabondayoksaidi huathiri tabaka la ozoni
  5. oksijeni na kabondayoksaidi hurekebishwa na ozoni
Choose Answer


8. Ni lipi kati ya matendo yafuatayo siyo sababu ya uharibifu wa mazingira?

  1. Uchomaji wa karatasi
  2. Maendeleo ya viwanda
  3. Kuoga ziwani
  4. Kutumia mbolea ya samadi
  5. Kuoshea magari mtoni.
Choose Answer


9.  Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?

  1. Angani na ardhini
  2. Ardhini na majini. 
  3. Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
  4. Ardhini na mapangoni 
  5. Kwenye misitu.
Choose Answer



10. Ili mimea iweze kuendelea kuishi katika mazingira yake inahitaji:

  1.  hewa na udongo 
  2.  hewa na maji
  3.  udongo na mbolea 
  4.  udongo na maji
  5.  jotoridi na hewa
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256