MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA TANO

MAJARIBIO YA KISAYANSI

Chagua Jibu Sahihi

1. Nini kati ya vifuatavyo husababisha chupa ya plastiki kusinyaa hewa inapoondoleua ndani?

  1. Hewa ndani ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa zaidi ya hewa nje ya chupa
  2. Hewa nje ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa kuliko hewa ndani ya chupa
  3. Mgandamizo wa nje na ndani ya chupa kulingana
  4. Mgandamizo wa hewa ndani ya chupa kuwa pungufu ya mngandamizo wa kutoa hewa nje ya chupa
  5. Mgandamizo nje ya chupa kuwa sawa na ujazo wa hewa mdomoni.
Choose Answer


2. Nini maana ya dhanio katika utafiti wa kisayansi?

  1. ni wazo tu
  2. ni utabiri wa matokeo ya kubuni
  3. utabiri wa matokeo ya jaribio
  4. wazo la kina
  5. mawazo yaliyojengwa kabla ya utafiti
Choose Answer


3. Mojawapo ya hatua za kufuata unapoandaa jaribio la kisayansi ni:

  1. uchunguzi
  2. udadisi
  3. utambuzi wa tatizo
  4. utatuzi wa tatizo
  5. kuandaa ripoti
Choose Answer



4. Hatua ya kwanza ya utafiti wa kisayansi ni

  1. kuanza jaribio
  2. kukusanya data
  3. kutambua tatizo
  4. kuchanganua data
  5. kutafsiri matokeo
Choose Answer


5. Hatua ya tatu ya utafiti wa kisayansi ni .........

  1. kuchambua data
  2. kutafsiri matokeo
  3. kuandaa na kuanza jaribio
  4. ukusanyaji wa data
  5. kutambua tatizo
Choose Answer


6. Matokeo ya jaribio yanaweza kuwa mojawapo ya yafuatayo:

  1. Kweli au uongo
  2. Yaliyochambuliwa au yasiyochambuliwa
  3. Yenye maswali au yasiyo na maswali
  4. Ya awali au ya kati
  5. Ya awali au ya mwisho
Choose Answer


7. Katika hali ya kawaida, kutu ni matokeo ya mjibizo wa athari za kikemikali kati ya:

  1. shaba, maji na oksijeni
  2. sodiamu, maji na oksijeni
  3. kalsiamu, maji na oksijeni
  4. chuma, oksijeni na maji
  5. maji, oksijeni na potasiamu
Choose Answer


8. Kuna tofauti gani kati ya barafu na maji?

  1. Maji ni mazito kuliko barafu.
  2. Maji yana mshikamano mkubwa kuliko barafu.
  3. Maji yana rangi hafifu kuliko barafu.
  4. Maji yanachukua nafasi ilihali barafu haichukui nafasi.
  5. Barafu ni laini kuliko maji.
Choose Answer


9. Data za uchunguzi zilizochambuliwa huweza kuwasilishwa kwa njia ya:

  1. grafu
  2. ripoti
  3. kukokotoa
  4. kutafsiri
  5. kuchora
Choose Answer



10. Katika uchunguzi wa kisayansi hatua ipi hutumika kukubali au kukataa dhanio?

  1. Kukusanya data
  2. Kufanya jaribio
  3. Kuandika hitimisho
  4. Kutafsiri data
  5. Kudurusu majarida
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256