SURA YA KWANZA
KUWAPENDA WATU WENGINE KATIKA FAMILIA
Dhana ya familia.
Familia ni kundi la watu wenye uhusiano wa kinasaba yaani wazazi na watoto.
Kwa kawaida familia huwa na mama na baba wanaowalea watoto wao kwa pamoja.
Kuna sababu pia inaweza sababisha familia iwe na mzazi mmoja, baba au mama.
Familia inaweza kuwa tandaa ikijumuisha watu wengine wenye uhusiano wa kindugu wanaotokana na ukoo mmoja.
Nduguhawa wanaweza kuwa bibi na babu kwa pande zote mbili, ndugu wa baba kama vile shangazi na baba wadogo, baba wakubwa, ndugu wa mama mfano, mjomba na mama wadogo, mama wakubwa pamoja na watoto wao.
Mahitaji mbalimbali ya wanafamilia.
- Kila mwanafamilia ana nafasi pekee katika familia, hivyo tukitaka kujenga familia iliyodhabiti na bora, tuna wajibu wa kutambua nafasi ya kila mwanafamilia.
- Wazazi na walezi wana nafasi ya pekee kama viongozi wakuu wa familia.
- Watoto wana wajibu wa kufuata maelekezo ya wazazi na walezi wao.
- Tambua kila mwanafamilia kwa nafasi yake, pia anahitaji kupendwa, kusikilizwa na kuheshimiwa.
- Unapompenda mwanafamilia unamfanya ajiskie kuwa sehemu ya familia, hali ambayo uchangia kukuza ushirikiano katika familia.
- Wanafamilia wenye ulemavu pia wana mahitaji maalum, mfano wenye ulemavu wa viungo, uoni, uziwi, akili na ngozi.
- Pia yapo mahitaji kwa wanafamilia wenye magonjwa, matatizo yatokanayo na uzee, na wanafamilia wenye mahitaji maalum ya kitabia.
- Watoto wadogo katika familia uhitaji uangalizi wa karibu sana.
- Mahitaji maalum ya familia hayawafanyi wakose haki zao kama sehemu ya familia. Tunao wajibu wa kuwapenda na kutoa msaada kwa kila mwenye uhitaji ili kuwawezesha kumudu maisha yao ya kila siku kwa furaha.
Je tunawezaje kuwasaidia wanafamilia wenye mahitaji maalum?
- Kuwapatia vifaa na mazingira ya kumudu maisha yao.
- Kubaini kile wanachohitaji
- Kuwatia moyo na kuwasaidia kufaya kile wanachoshindwa.
Makundi mbalimbali ya familiayenye mahitaji maalumu.
(a) Watoto wadogo.
- Hawa hawawezi kujifanyia baadhi ya mambo.
- Wasaidiwe kujimudu na vile vile wafundishwe taratibu na namna ya kujihudumia wenyewe, kwa mfano, waogeshwe, wavushwe barabara na tuhakikishe mazingira wanayochezea ni salama.
(b) Wazee.
- Hawa hawana nguvu hivyo wanahitaji kusaidiwa.
- Wasaidie kubeba mizigo, kufanya kazi, kufuliwa nguo, kuandaliwa chakula na kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi.
(c) Wenye ulemavu.
- Wanafamilia wenye ulemavu wasaidiwe kuweza kumudu maisha yao kama wanafamilia wengine.
- Wanafamilia wenye ulemavu wa macho wasaidiwe kuyaelewa mazingira wanayoishi.
- Mazingira haya ni kama vile sehemu ya kulia chakula, kulala, kusoma, maliwato na kuchezea.
Kuthamini mchango wa wanafamilia wengine katika ustawi wa familia.
Kwa kuzingatia uhusiano baina ya wanafamilia, familia zinaweza kugawanyika katika makundi mawili makubwa.
- Familia zilizo na maelewano
- Familia zisizo na maelewano.
1. Familia zilizo na maelewano. Familia hizi zina sifa za kuwa na mawasiliano mazuri baina ya wanafamilia. Ili familia ziwe na maelewano ni muhimu wanafamilia kutambua na kuthamini mchango na mahitaji ya kila mwanafamilia.
2. Familia zisizo na maelewano – Familia hizi huundwa na watu wasiosikilizana na kuheshimiana. Hali ya kutokuelewana inaweza kusababishwa na wanafamilia wenyewe, kwa kushindwa kuthamini mchango wa wengine, kutotambua mahitaji ya kila mmoja na tabia ya kutanguliza mahitaji binafsi dhidi ya mahitaji ya wengine.
Familia inaweza kuwa na maelewano na mwanafamilia yeyote anaweza kuwa chanzo cha ustawi wa familia, ikiwa atatambua wajibu wake na kuheshimu mchango wa wanafamilia wenzake.
Jukumu la watoto.
- Kuheshimu wazazi, kuwasaidia, kutambua kazi kubwa ya kimalezi inayofanywa na wazazi, au walezi wao.
- Kutambua kuwa hata kama hawapati mahitaji yale bado wazazi wao wana wajibu wa kuhakikisha kuwa familia inapata mahitaji yao ya msingi kama vile malazi, mavazi, chakula, matibabu na elimu.
- Kushiriki kikamilifu kufanya kazi za nyumbani kulingana na umri wao.
- Kusaidia wazazi hasa siku za mapumziko.
Vitendo vya heshima katika familia.
- Heshima ni hali ya kutambua utu wa mtu mwingine kwa kumjali, kumpenda, kuthamini, mavazi yake na kunstahi pale anapokosea.
- Heshima inamwezesha mtu kuishi vizuri na wanafamilia wengine.
Vitendo vya heshima.
- Kuzungumza kwa kutumia kauli zinazofaa.
- Kusalimia wanafamilia kwa nidhamu.
- Kutosengenya watu
- Kuomba msamaha unapokosea.
- Kushukuru unapopatiwa
Sisi wenyewe pia tunapaswa kujiheshimu kwa:-
- Kuvaa kwa staha
- Kuwa na nidhamu
- Kuwa msikivu
- Kusamehe unapokosea.
Angalizo:
- Watu wote bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii wanastahili heshima sana, na si vyema kuwabagua watu kwa hali zao. Unapomheshimu mtu mwingine, unamfanya na yeye akuheshimu.
Kuwalinda wanafunzi dhidi ya vikundi hatarishi.
- Sio watu wote kwenye jamii walio na maadili.
- Hawa wanaweza kuhatarisha jamii bora.
- Watu hawa kwa tabia zao uumiza hisa za watu wengine.
- Watu hawa ni kama:-
- Wanaouza na kutumia madawa ya kulevya.
- Wezi
- Walevi
- Mafisadi
- Wabakaji
- Wanaodhalilisha watoto kingono.
- Wanaowafanyisha watoto kazi kinyume cha sheria.
- Wanaowanyanyasa wazee na wanajamii wenye mahitaji maalum.
- Watu hawa wanaweza kuwa jirani zetu au wapo ndani ya familia zetu.
Kuwalinda watoto:
- Mambo yanayohusu haki na ustawi wa mtoto yameelezwa vyema katika sheria ya mtoto namba 13 ya mwaka 2009, na tafsiri yake ya mwaka 2014. Kwa mujiby wa sheria hii, wajibu wa mtoto ni:-
- Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamano wa familia.
- Kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake na watu wazima muda wote na kuwasaidia pale inapohitajika.
- Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kimwili na kiakili kadri ya umri na uwezo wake.
- Kutunza na kuimarisha mshikamano wa jamii na Taifa.
- Kutunza na kuimarisha mambo mema katika utamaduni wa jamii na taifa kwa ujumla. Katika uhusiano wa wanajamii au Taifa.
Haki za watoto.
- Sheria hii pia inaeleza haki za watoto ikiwemo kulindwa dhidi ya kuteswa na kushalilishwa kijinsia.
- Watoto wasipolindwa na kupewa uangalizi wa karibu wanaweza kujiingiza au kudhurika na makundi hatarishi kwenye jamii.
- Wajibu wa kila mwanajamii ni kulinda watoto dhidi ya watu wasio na maadili.
- Watoto pia wana wajibu wa kujilinda dhidi ya vikundi hatarishi.
Wajibu wa watoto katika jamii ni:-
- Kujilinda: Kuepuka tabia zilizo kunyume na maadili yetu hata kama tabia hizo zinafanywa na watu tunaowaamini.
- Kuchukua tahadhari unapokuwa nje ya familia yenu. Mojawapo ya tahadhari ni kuongozana na watu wenye maadili wanaoweza kukusaidia unapo kutana na hatari.
- Kutoa taarifa:- Toa taarifa unapofanyiwa vitendo vya kikatili, mfano kupigwa, kuchomwa na maji moto, kukatwa na vitu vyenye ncha kali, vile vile toa taarifa unapoguswa sehemu za siri au kudhalilishwa kingono.
Angalizo:
Serikali ina wajibu wa kutengeneza mifumo ya kushughulikia vikundi hatarishi. Pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya vikundi hivyo.