URAIA NA MAADILI : SURA YA PILI

KUJIVUNIA SHULE NA KUIPENDA NCHI YETU.

Kujivunia shule yako.

Zipo njia mbalimbali zinaweza kutumiwa kuonesha hali ya kujivunia shule yako.

Kwa nini ujivunie shule yako?

  • Shule yako ndio makazi ya pili baada ya nyumbani, hapo ndipo unapata malezi kutoka kwa walezi.

Hivyo ni jambo la busara kupenda na kuthamini shule yako.

Unaweza kupenda shule yako kwa kufanya yafuatayo.

  • Kuitengeneza kauli mbiu ya shule.
  • Kufahamu na kuimba wimbo wa shule yako
  • Kutunga ngonjera, mashairi na nyimbo za kusifia shule yako.

Kauli mbiu ya shule.

  • Kila shule ina kauli mbiu ambayo hutumika kama kichocheo cha wanafunzi wanapokuwa shuleni na hata wanapomaliza shule.
  • Kauli mbiu ya shule hujengwa na msemo mfupi wenye mantiki kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kujifunza kwa bidii ili kufikia maono ya shule.
  • Kauli mbiu uhamasisha walimu na jumuiya nzima ya shule kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo ya shule.
  • Kauli mbiu ya shule huandikwa kwenye nembo ya shule au kwenye kibao ili kuitambulisha shule.
  • Kauli mbiu katika baadhi ya shule huimbwa kwenye wimbo wa shule.

Mifano ya kauli mbiu ni:-

  • Elimu ni nguvu.
  • Elimu ni ngao
  • Elimu ni ufunguo wa maisha
  • Hekin ni uhuru
  • Juhudi na nidhamu.

Umuhimu wa kauli mbiu.

  • Huleta hamasa kwa wanafunzi katika kufanya kazi
  • Hamasa hiyo husaidia kufikia malengo ya kitaaluma na kinidhamu ya shule husika.

Wimbo wa shule.

  • Ni utambulisho wa shule husika
  • Kila shule ina wimbo wake.
  • Wimbo huimbwa katika siku maalumu iliyopangwa na shule husika.
  • Mara nyingi wimbo huo uambatana na wimbo wa Taifa.

Umuhimu wa wimbo wa shule.

  • Unafanya wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo.
  • Kutunza mazingira ya shule
  • Kushiriki katika michezo
  • Kuwa na tabia njema
  • Kujenga uzalendo kwa shule yao na Taifa.
  • Kukumbuka wajibu wao wa kuipenda na kulinda rasilimali za shule na Taifa.

Je, unawezaje kuiletea jina shule na kuitangaza?

Mambo haya yanaweza kuiletea sifa shule yako. Hii ni pamoja na:-

  • Nidhamu ya wanafunzi:- Wazazi hupenda kupeleka watoto wao katika shule yao. Shule yenye nidhamu husifiwa na kupendwa.
  • Ufaulu wa wanafunzi:- Wazazi hupenda kupeleka wanafunzi katika shule ambazo zinafanya vizuri kitaaluma.
  • Mazingira safi ya kujifunzia:- Mazingira mazuri na safi huiletea shule sifa nzuri. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa shule yako ina mazingira safi na salama ya kujifunzia.
  • Kufanya vizuri katika mashindano ya shughuli zisizokuwa za kitaaluma:- Shule husifika kutokana na kuongoza au kufanya vyema katika michezo mbalimbali, mfano, mpira wa miguu, wa pete, mchezo wa kuogelea, kukimbia n.k.
  • Mwonekano wa wanafunzi:- Mwonekano wan je wa wanafunzi mfano usafi wa mavazi huiletea shule sifa.

Kuipenda nchi yetu.

  • Tunaweza kuonyesha kuipenda nchi yetu kwa kuitangaza kupitia nyanja mbalimbali za kujamii, kisiasa na kiuchumi.

(i) kijamii.

  • Kushiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mifano ni michezo ya jumuiya ya madola, Olimpiki, michezo ya kimataifa ya mpira wa miguu na pete, ngumi za kulipwa n.k.
  • Kumbi kubwa za kisasa za mikutano ya kimataifa kunachangia kuitangaza nchi yetu, mfano, ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, Dar es Salaam na ukumbi wa kimataifa Arusha.

(ii) Kisiasa:

  • Tanzania imejiunga na jumuiya mbalimbali za kanda na za kimataifa kama vile, Jumuiya ya madola, umoja wa mataifa, umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika.
  • Tanzania pia inaendelea kujitangaza nchi za nje kwa kufungua ofisi za ubalozi katika nchi hizo kama vile, Kenya, Uganda, Marekani, Cuba, Uingereza n.k.

(iii) Kiuchumi:

  • Kuna kituo cha taifa cha uwekezaji ambacho kinatangaza Tanzania.
  • Tanzania pia hujitangaza kupitia maonesho ya biashara ya kimataifa, mfano, maonyesho ya biashara ya kimataifa Dar – es – Salaam.
  • Kiutalii – Tanzania ina vivutio vingi vya watalii kama mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, na pia Zanzibar.

MTIHANI WA MWISHO WA MADA.

  1. Toa sababu ya kujivunia shule yako
  2. Taja matendo matatu ambayo unaweza kufanya hili kuipenda shule yako
  3. Kaulimbiu ya shule ina umuhimu gani?
  4. Taja umuhimu wa wimbo wa shule
  5. Taja mambo matatu ambayo yanaweza kuiletea shule sifa
  6. Taja tatu za kutangaza nchi yako
  7. Tutawezaje kulitangaza taifa letu kwa hizi;
  • Kijamii
  • Kisiasa
  • Kiuchumi

MAJIBU YA MASWALI.

1. Shule yako ndio makazi ya pili baada ya nyumbani, hapo ndipo unapata malezi kutoka kwa walezi.

2.

  • Kuitengeneza kauli mbiu ya shule.
  • Kufahamu na kuimba wimbo wa shule yako
  • Kutunga ngonjera, mashairi na nyimbo za kusifia shule yako.

3.

  • Huleta hamasa kwa wanafunzi katika kufanya kazi
  • Hamasa hiyo husaidia kufikia malengo ya kitaaluma na kinidhamu ya shule husika.

4.

  • Unafanya wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo.
  • Kutunza mazingira ya shule
  • Kushiriki katika michezo
  • Kuwa na tabia njema
  • Kujenga uzalendo kwa shule yao na Taifa.
  • Kukumbuka wajibu wao wa kuipenda na kulinda rasilimali za shule na Taifa.

5.

  • Nidhamu ya wanafunzi
  • Mazingira mazuri ya kujifunzia
  • Ufaulu wa wanafunzi

6.

  1. Kijamii
  2. Kiuchumi
  3. Kisiasa

7.

Kijamii-

  • Kushiriki katika michezo
  • Kumbi kubwa za michezo

Kiuchumi-

  • Vituo vya uwekezaji
  • Kiutalii
  • Maonyesho ya biashara

Kisiasa-

  • Tanzania ni mwanachama wa jumuiya mbalimbali na mashirika ya kitaifa.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256