SURA YA KWANZA

MAZINGIRA YETU

MAANA YA MAZINGIRA:

Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyotuzunguka. Mazingira huundwa na vitu mbalimbali. Vitu hivyo vinaweza kuwa vya asili kama misitu, milima, maziwa, mabonde, mito, wanyama na bahari. Pia, vipo vitu vilivyotengenezwa na binadamu kama vile majengo, barabara na viwanda. Vyote hivi huunda mazingira ambayo hupatikana maeneo ya kijijini au mjini. Sisi binadamu pia ni sehemu ya mazingira.

Mazingira ya kijijini na mjini.

Bila shaka umewahi kuona au kuishi kwenye nyumba ya bati au nyasi. Pia, umewahi kuketi chini ya mti wenye kivuli. Tena umewahi kuona sehemu zenye mashamba ya mazao na mabomba ya maji. Vilevile utakuwa umewahi kuona mito, misitu, wanyama, milima na mabonde. Hivi vyote ni sehemu ya mazingira

Uharibifu wa mazingira.

Yapo maeneo yenye mazingira mazuri ambayo hayajaharibiwa. Pia yapo maeneo mengine ambayo mazingira yake yameharibiwa.

Binadamu hufanya shughule mbalimbali ambazo baadhi yake husababisha uharibifu wa mazingira. Shughuli hizo ni pamoja na uchomaji wa mkaa. Shughuli nyingine in ujenzi holela na utupaji taka ovyo. Pia, shughuli za viwanda kama vile utiririshaji maji yenye kemikali katika mito, maziwa na bahari. Vilevile, moshi hasa wa viwandani husababisha uchafuzi wa hewa. Mazingira yaliyoharibiwa hayafai kwa shughuli za kilimo wala makazi. Pia husababisha maradhi kwa binadamu, mifugo na viumbe wengine.

Mazingira yaliyoharibiwa huweza kurekebishwa kwa kupanda nyasi na miti. Nyasi na miti hupandwa sehemu zenye mmomonyoko wa udongo na zilizokosa miti. Pia, kulima kilimo cha matuta ya kukinga maji kwenye miteremko. Vilevile, kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti. Hali kadhalika, mazingira machafu husafishwa kwa kufyeka vichaka, kuondoa taka sehemu za makazi na kuzihifadhi kwenye vyombo sahihi na sehemu zinazotakiwa.

Utunzaji wa mazingira:

Utunzaji wa mazingira ni hali ya kutunza, kulinda na kuhifadhi jumla ya vitu vyote vinavyomzunguka binadamu katka maisha yake. Vitu hivyo ni kama vile mito, mabonde, wanyama, milima na bahari.

Shughuli za utunzaji wa mazingira katika nchi hufanyika katika ngazi mbalimbali. Serikali yetu ilianzisha taasisi na ofisi za kusimamia utunzaji wa mazingira. Zipo ofisi za mazingira ngazi ya kijiji, mtaa na kata. Pia, zipo katika ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na taifa. Ofisi hizi husimamiwa na maofisa mazingira katika ngazi mbalimbali. Maofisa hao hushirikiana na viongozi wa serikali katika utunzaji wa mazingira.

Aidha, kwa kila ngazi husika kuna kamati mbalimbali za utunzaji wa mazinga. Kamati hizo ni pamoja na zile za afya na mazingira. Kamati hizi hufanya kazi za kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira. Shughuli hizi ni pamoja na kupanda miti na kuitunza. Ni jukumu la kila serikali ya ngazi husika kuwa na sheria ndogo pamoja na faini kwa kila atakayebainika amechafua mazingira. Mfano, katika baadhi ya maeneo faini ni shilingi elfu hamsini. Tunapaswa kutunza mazingira yetu ili kulinda maisha yetu na viumbe wengine.

Faida za utunzaji wa mazingira.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256