Sura ya Kwanza : Tuipende na kuiheshimu jamii yetu
Jamil ni watu wanaoishi pamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali. Wanajamii wema hutengeneza jamii bora. Katika sura hit utajifunza jinsi ya kuishi vizuri na wanajamü wengine. Ili kuishi vizuri na wanajamii wengine unapaswa kujipenda, kujitambua na kuwapenda wengine.
Kujipenda na kuwapenda wengine
Kujipenda
Kujipenda ni kujithamini na kujikubali. Mtoto anayejipenda anatunza afya yake. Vilevile, anaepuka matendo mabaya na anakuwa na tabla njema wakati wote.
Angalia picha hizi, kisha jibu maswali. |
|
Kielelezo namba 1 Matendo ya kujipenda |
Maswali
l . Picha hizi zinaonesha matendo gani?
2. Taja matendo ya kujipenda unayoyafahamu.
3. Je, ni matendo gani ya mtu asiyejipenda unayoyafahamu?
Kazi ya kufanya
Andika kwenye daftari lako matendo matatu ya kujipenda unayoyatenda katika kila eneo.
(a) nyumbani
(b) shuleni
(c) kwa majirani wanaokuzunguka
Zoezi 1. Taja matendo matano ya kujipenda unayoyafahamu. 2. Taja matendo matano yanayofanywa na mtu asiyejipenda. 3. Falda za usafi wa mwili na mavazi ni . . . . . . . , . . . . . . . . na . . . . . . . . . . 4. Soma matendo yafuatayo, kisha eleza matendo haya yanatufundisha nini? (a) Mwanafunzi anapiga mswaki na kuoga kila siku. (b) Mwanafunzi ana marafiki wenye tabla njema. (c) Mwanafunzi amevaa nguo safi na nadhifu. |
Kuwapenda wengine
Matendo kama kusalimiana kwa lugha inayofaa na kuwasikiliza wengine yanaashiria kuishi vizuri. Vilevile, kuwasaidia na kuwaelekeza vizuri wengine inaonesha kuwa una upendo. Mwanafunzi anayewapenda watu wengine huwa tayari kuwasiliana nao na kuwasaidia.Hebu jiulize, utachukua hatua gani ikiwa,
(a) mwanafunzi mwenzako amejikwaa na kuanguka.
(b) mdogo wako analia.
(c) mtu asiyeona yuko kandokando ya barabara akihitaji kuvuka.
(d) mwanafunzi mwenzako hana kalamu wakati wewe una kalamu mbili.
(e) mwalimu anaingia darasani kwenu.
(f) umeamka asubuhi na kukutana na watu wakubwa kwako.
Mwanafunzi anayewapenda wengine huwatakia heri na huwapa pole wanapopata matatizo. Vilevile, huwashukuru wanapomsaidia na huomba msamaha anapowakosea.
Maswali
l . Ni matendo gani ya upendo unayoyafahamu?
2. Je, ni matendo gani ya upendo unayoyafanya kwa wengine ukiwa nyumbani?
3. Je, ni matendo gani ya upendo wanakufanyia wenzako mnapokuwa shuleni?
4. Je, utawasaidiaje wenzako kutenda matendo ya upendo?
Soma habari hã, kisha jibu maswali.
Nuru na Elifuraha ni marafiki. Wote wawili wanasoma darasa Ia tatu katika Shule ya Msingi Tupendane. Marafiki hawa mara nyingi hutembeleana nyumbani. Siku moja Nuru aliamua kumtembelea Elifuraha nyumbani kwao. Alimkuta mama yake Elifuraha amepumzika barazani. Siku hiyo Elifuraha hakuwepo nyumbani. Alimsogelea na kumwamkia mama yake Elifuraha.
Mama yake Elifuraha alimweleza Nuru kuwa anaumwa sana. Nuru alimpa pole na muda huohuo alikwenda kutafuta msaada kwa majirani. Majirani wawili walifika na kumpeleka mgonjwa hospitalini. Alipofika hospitalini alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Elifuraha aliporudi nyumbani alimshukuru Nuru kwa upendo aliouonesha kwa mama yake.
Maswali
l . Je, habari uliyoisoma inatufundisha nini?
2. Je, ni matendo gani ya kuwapenda watu wengine yaliyopo katika habari hit?
3. Je, ni matendo gani mengine ya kuwapenda watu wengine unayoyafahamu?
14. Ingekuwa ni wewe ungemsaidiaje mama Elifuraha tofauti na Nuru alivyofanya?
Kazi ya kufanya
Andika hatua utakazochukua kumsaidia mwanafunzi mwenzako aliyeumia mguu wakati akicheza mpira shuleni.
Kujitambua
Kujitambua ni hali ya kujua uwezo wako wa kutenda mambo. Yapo mambo unayoweza kutenda vizuri na yapo usiyoweza kutenda. Uwezo wa kutenda jambo jema kwa ustadi unaitwa kipaji.
Tazama picha hizi, kisha jibu maswali.
|
|
|
Kielelezo namba 2 Matendo yanayoonesha vipaji |
Maswali 1. Je, ni matendo gani unayoyaona kwenye picha hizi? 2. Wewe unapendelea tendo lipi zaidi? 3. Ni matendo gani kwenye picha marafiki zako watayatenda kwa ustadi zaidi? 4. Wewe una vipaji gani? 5. Ni vipaji gani vingine walivyonavyo marafiki zako? 6. Kati ya matendo yafuatayo ni yapi yanayoonesha vipaji? Pigia mstari majibu yako. (a) Kuimba, kucheza ngoma, kulia, kulala, kuhuzunika (b) Kuchora, kukaa, kufuma, kukimbia na kupiga makofi (c) Kupiga kelele, kupaka rangt, kuigiza na kucheza mpira. |
Soma habari hü, kisha jibu maswali.
Mwalimu Dina anafundisha Uraia na Maadili katika Shule ya Msingi Misufini. Siku moja aliwataka wanafunzi wa darasa la tatu kueleza vipaji walivyonavyo. Kila mwanafunzi alipewa nafasi ya kujieleza. Ashura na Tuma walisema wanaweza kuchora vizuri sana. Mwalimu aligundua Ashura na Juma ni hodari wa kuchora. Sara na Musa walijitokeza na kusema wanaweza kuimba vizuri sana. Grace na Zuberi walisema kwamba wao wanaweza kucheza mpira wa miguu kwa ustadi. Hü ilimfanya mwalimu Dina abaini kuwa wanafunzi wake walikuwa na vipaji tofauti tofauti. Baada ya hapo, Mwalimu Dina aliweka mipango ya kukuza vipaji vya wanafunzi. Aliwasihi kila mmoja aongeze bidü katika kukuza kipaji alichonacho.
Maswali
1. Νί vipaji gani vinavgotajwa katika habari hii?
2. Je, wewe una kipaji gani?
3. Je, utafanya nini kukuza kipaji chako?
Zoezi 1. Orodhesha vitu vitano unavgopenda kufanya. 2. Taja matendo matano unayopenda kutendewa na wenzako. 3. Je, ni vitu gani usivyoweza kufanga vizuri ςαηα? 4. lJtafanya nini ili kukuza uwezo wako wa kufanya vitu hivyo? 5. Je, ni matendo gani unayotenda yanaashiria kuwa unaishi vizuri nawatu wengine? |
Κazi ya kufanya
Andika majina ya watu maarufu unaowafahamu na orodhesha vipaji νγαο.
Msamiati
Kipaji uwezo alio nao mtu ambao humwezesha kufanya jambo vizuri
Nadhifu enye kupendeza, safi
Ustadi kufanya kitu kwa ujuzi
www.learninghubtz.co.tz