URAIA DARASA LA III SUBJECT NOTES
SURA YA : 2  Tuipende shule yetu

Sura ya Pili : Tuipende shule yetu

Shule ni sehemu yajamü ambayo huwapatia watoto malezi bora. Ili Shule [we bora inapaswa kuwa na walimu na wanafunzi bora. Shule inapaswa kuwa na madarasa, vyoo, samani, mazingira safi na vifaa vya kujifunzia. Shule yenye vitu vilivyotajwa hapo juu inavutia. Katika sura hit utajifunza matendo ya kuipenda na kujivunia Shule yako. Matendo hayo hujumuisha kutunza mazingira ya shule. Vilevile, kusoma kwa bidii na kuonesha tabla njema shuleni.

Kuifahamu shule

Miongoni mwa mambo ambayo unapaswa kuyafahamu ni vitu vinavyoitambulisha Shule yako. Vitu hivyo ni mipaka ya shule, nembo ya Shule na kaulimbiu. Vitu vingine vinavyotambulisha Shule ni sare na wimbo wa shule.

Tazama picha hii, kisha jibu maswali.

Kielelezo namba 1 Mazingira ya Shule

Maswali

1. Picha hii inaonesha nini?

2. Je, ni vitu gani unavyoviona katika picha hii?

3. Eneo hilt lina umuhimu gani katika jamii?

14. Je, ni mambo gani hufanyika katika eneo hili?

Wimbo

lmba wimbo huu, kisha jibu maswali.

Shule twaipenda, shule twaipenda

Shule twaipenda, shule twaipenda

Twawapenda walimu wetu, wanatufundisha vyema

Twawapenda viongozi wetu, wanatuongoza vgema

Twaipenda nembo ya shule yetu, inatutambulisha vyema

Tunazipenda sare zetu, zinatupa mwonekano bora

Taaluma, nidharnu na mazingira, hii ndio kauli mbiu yetu

Shule twaipenda, shule twaipenda Shule twaipenda, shule twaipenda

Μaswali

Ι. Je, ni mambo gani yanagoitambulisha shule katika wimbo huu?

2. Je, ni mambo gani mengine yanayoitambulisha shule yako?

3. Andika wimbo wa shule gako.

Κazi ya kufanya

Andika vitu vinavgobainisha mipaka ya shule gako.

Kutunza mazingira ya shule

Mazingira ya shule yanajumuisha Vitu vyote vilivyomo katika eneo la shule. Vitu hivyo ni majengo, viwanja vya michezo, bustani, miti na samani. Vitu vingine ni njia za shule, vyoo na vingine vingi. Ili mazingira ya shule yako yapendeze na kuvutia inakupasa kuyatunza vizuri. Kila mwanafunzi anapaswa kutunza mazingira ya shule yake. Unatakiwa kupanda miti na maua, kufanya usafi na kutupa takataka mahali panapostahili. Ni jukumu la kila mmoja kuchukua hatua ya kuzuia uchafuzi wa mazingira.

Tazama picha hü, kisha jibu maswali.


Kielelezo namba 2 Usafi wa mazingira ya shule

Maswali

l . Te, ni matendo gani unayoyaona kwenye picha?

2. Te, ni vitendo gani vya kutunza mazingira unavyovifanya shuleni kwako?

3. Taja falda za kusoma na kucheza kwenye mazingira safi na salama.

Kazi ya kufanya

Shirikiana na wenzako kufanya usafi wa darasa baada ya muda wa masomo.

Kuiletea sifa nzuri shule

Sifa nzuri ya shule inajengwa na mambo mazuri yanayofanywa na wanafunzi shuleni. Mambo kama maendeleo mazuri darasani, mazingira safi na tabla zinazofaa za wanafunzi. Juhudi za walimu huiletea sifa nzuri shule.

Soma majigambo baina ya Amani, Nuru, Upendo na Turnaini. Jibu maswali yanayofuata.

Upendo Mmeiona, zawadi tuliyoipata? Bila mimi kucheza mpira tusingeshinda!
Amani Mimi ni zaidi yako. Nimeshinda kwa kuwa na tabia njema. Jina Ia shule getu litavuma zaidi nje ya shule.
Nuru Mimi ni zaidi yenu. Nimeshika nafasi ya kwanza katika mitihani!

Tumaini

Tamani ninyi nyote ni washindi! Mnastahili kupongezwa kwa kuwa mmeiletea sifa nzuri shule yetu.

Nuru

Hapana! huwezi kulinganisha ushindi wa masomo na wa michezo!

Amani

Ufaulu wa masomo, bila tabla nzuri ni kazi bure.

Upendo

Msüdharau michezo kwani pia hujenga tabla nzuri.

Tumaini

Sifa sio ufaulu wa masomo, michezo na tabla nzuri peke yake bali pia usafi. Tuipambe shule getu na kutunza mazingira.

Amani

Ni kweli, ushindi wa kila mmoja wetu ni ushindiwa shule.

Maswali

1. Je, ni mambo gani yanayoiletea sifa nzuri shule uliyojifunza kwenye majigambo uliyoyasoma?

2. Ni matendo gani zaidi unayoweza kutenda ili kuiletea sifa nzuri shule yako?

3. Te, unashiriki vipi katika shughuli mbalimbali za kuiletea sifa nzuri shule yako?

Kazi ya kufanya

Taja mambo yaliyowahi kuiletea sifa nzuri shule yako.

Msamiati

Kaulimbiu maneno au ujumbe unaohamasisha watu kutekeleza majukumu

Majigambo hali ya kutoa maneno ya kujisifia au kujikweza

Mazingira vitu vinavyotuzunguka katika eneo tunaloishi au kufanya kazi

Mpaka mahali panapotenganisha sehemu moja na nyingine

Nembo alama inayotambulisha kitu au sehemu kama vile shule na chama

Zoezi

1. Taja alama zilizomo katika nembo ya shule yako.

2. Andika matendo unayoyafanya kutunza mazingira ya shule yako.

3. Orodhesha vitu vinavyoitambulisha shule yako.

14. Orodhesha vitu vinavyopakana na shule yako.

5. Orodhesha mambo yanayofanyika shuleni kwako yanayokufanya uipende.



www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256