SURA YA KWANZA
MAZINIGIRA YETU
Msamiati
Vitu vinavyopatikana katika mazingira
A. Vitu vilivyo hai
Vitu vilivyo hai ni kama watu, ndege, n.g'ombe na nyasi
B. Vitu visivyo na uhai
Vitu visivyo na uhai ni kama vile nyumba, reti, barabara na mawe.
Vitu vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani
Chunguza picha zifuatazo, kisha jibu maswali.
Kielelez- : Vitu vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani
Jibu maswali haya.
VITU VINVYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YA SHULENI
Maswali ya kujadili
Mazingira ya Shule ya Msingi Kisomota
Rabia na Kaluza wanasoma darasa la tatu katika Shule ya
Msingi Kilimani. Siku ya jumatatu walipeleka barua katika shule ya Kisomota. Walipokaribia waliona mazingira mazuri kuzunguka shule.
Soma mazungumzo kati ya Rabia na Katuza, kisha jibu maswati.
Kaluza Naona tumekaribia shule ya Kisomota.
Rabia Kweli tumefika, hata miti na ndege
wanatulaki kwa furaha.
Katuza Aaah! kumbe wana miti mingi ya kivulikutiko sisi. Miti yao inaleta hewa nzuri.
Rabia Jamani, angaLia bustanI zao za maua
zimepangwa kwa ustadi. Zinapendezesha shule.
KaluzaEeeh! Angalia kibao cha shule kimeandikwajina to shule kwa ustadi mkubwa.
Rabia Pia, wana uwanja mkubwa wa michezo,Wee! Unauona?
KaLuza Rabia umeona ile bustani ya mbogainavyopendeza?
Rabia Ni kweli nimeona,watakuwa wan.auza mboga na kupata fedha nyingi.
Katuza Je, umeona majengo ya madarasa yao naofisi za walimu zilivyo nzuri?
Rabia Nimeona, tena zimepakwa rangi na kuchorwa
ramani na vitu mbalimbali vya kuvutia.
Kaluza Tena wenzetu wana kisima cha maji.
Rabia Ni kweli, ndio maana bustani zao za maua
na mboga zimestawi vizuri.
Rabia na Katuza walifurahia mazingira mazuri ya shule ya Kisomota. Baada ya kufikisha barua, watiahidi kurudi tena shuleni hapo kujifunza juu ya mazingira.
Kutunza mazingira ya shule
Tumeona vitu vilivyoko katika mazingira ya shule. Ni muhimu kuyaweka mazingira ya shule katika hali ya usafi. Tunatunza mazingira ya shule kwa kufanya usafi na kurekebisha maeneo yatiyoharibiwa. Aidha, tunapanda na kutunza miti, nyasi na maua. Pia, tunadhibiti takataka na kufanya usafi wa madarasa, vyoo na majengo.
Usafi wa darasa
Ni muhimu kuweka darasa katika hati ya usafi wakati wote. Usafi wa darasa hufanywa na wanafunzi kwa zamu. Usafi huu hufanyika kwa kushirikiana.
Tazama picha, kisha jibu maswali.
Kietelezo namba 3 Wanafunzi wakifanya usafi wa darasa
Jibu maswali haya
Mashindarto ya usafi wa madarasa
Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali.
Ijumaa ni siku ya mashindano ya usafi wa madarasa katika shule yetu. Usafi huo hufanyika baada ya masomo. ljumaa iliyopita tulishirikiana kufanya usafi wa darasa letu. Wakati tukifanya usafi Juma alisema, "Ni muhimu kufanya usafi darasani ili kupendeze". Helena alichukua kitambaa akaanza kufuta vumbi akisema, "Tufute vumbi ili tusichafue nguo". Halima naye alichukua ufagio mrefu na kuondoa tandabui. John alisema, "Halima, umefanya vizuri kuondoa tandabui maana wanaharibu mazingira ya darasa. Takataka pia huwa maficho ya mbu na wadudu wengine". Doto aliongeza kuwa, "Tusipoondoa maficho ya mbu watatuuma na kutuambukiza malaria". Mariamu na Faraja walisafisha meza, kiti cha mwalimu na kabati la vitabu. Kisha, tutishirikiana sote kufagia na kupiga deki darasa Letu. Tulitumia dekio, ndoo, maji na sabuni kudeki darasa.
Darasa Letu lilipokauka tulipanga madawati yetu. Tulihakikisha kuwa tunaacha nafasi ya kutosha kati ya dawati na dawati.
Walimu na viranja walipopita kukagua usafi, darasa Letu lilishinda tukawa wa kwanza. Tutipata zawadi ya ngao. Tulishangilia kwa furaha. Kwa pamoja tutikubaliana kuwa usafi wa darasa letu uwe ni suala la siku.
Jadili maswali haya
Tazama picha, kisha jibu maswali.
Jibu maswali haya
Usafi wa mazingira katika Shule ya Msingi Juhudi
Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali.
Amani ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Juhudi. Wanafunzi wa shule yaJ wana nidhamu sana. Amani na wenzake wanawahi shuleni mapema asubuhi. Wanafika shuleni saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Wanapofika shuleni hupangiana maeneo ya kufanya usafi wa shule kwa kushirikiana. Kazi za usafi wanazofanya ni kuokota takataka na kuzitupa katika shimo. Vilevile, hufagia barabara na njia za kupita katika eneo la shule. Aidha, hufyeka nyasi ndefu kwa kutumia mafyekeo. Baadaye hupalilia maua kwa kutumia jembe na kumwagilia maji. Kisha, wanamwagilia maji kwenye miti midogo. Baada ya usafi, wanajipanga kwenye mistari mbele ya shule kusikitiza matangazo. Kisha, wanaingia darasani kuanza masomo.
Jibu maswali haya
Kupanda miti, nyasi na maua
Miti, nyasi na maua ni mimea inayovutia katika mazingira na kuyapendezesha. Pia, huleta hewa na harufu nzuri. Miti, nyasi na maua vikikosekana, mazingira huweza kuwa jangwa. Mandhari yenye harufu nzuri ya maua, huwavutia wadudu kama vipepeo na nyuki.
Soma mazungumzo ya Dotto na Baraka kuhusu hatua za kupanda miti, nyasi na maua.
Dotto:Baraka nimepita shueni kwenu nimekuta viunga
vya nyasi, miti na maua. Vinapendeza sana.
Baraka : Ni kweli, shuleni kwetu kuna bustani za maua, miti na nyasi. inatuletea hewa safi na harufu nzuri.
Dotto:Ooh! Mlianzaje kuwa na mazingira Hayo?Kwanza kabisa tulianza na wazo. Aina gani ya nyasi, maua na miti tunayotaka kupanda katika mazingira yetu.
Dotto Eehee! Nielekeze zaidi.
BarakaHakikisha unachagua sehemu yenye rutuba kupanda nyasi, miti na maua.
Dotto Wazo zuri sana, nimelipenda.
BarakaHatujafika mwisho, pia unatakiwa kusafisha eneo. Eneo liwe tayari kwa ajili ya upandaji wa miti, nyasi na maua.
Dotto Nazidi kufurahia elimu hii. Je, hatua gani zinafuata?
BarakaUnatakiwa kuboresha udongo kwa kuchanganya na mbolea kabla ya kupanda miche.
Dotto Jamani Baraka! Baada ya hapo mnafanyaje?
Tunalima eneo kwa kutifua na kuchagua miche tunayohitaji, kisha tunapanda miche hiyo.
Dotto Kumbe! Ndio maana mazingira ya shule yenu
yanavutia.
Baraka Hata hivyo, tunatunza viunga vyetu kwa kumwagilia na kupalilia kila inapohitajika. Pia tutaweka dawa kwenye viunga vyote vya maua ili wadudu waharibifu wasiharibu.
DottoNashukuru kwa elimu yako. Nakuahidi nitakwenda
kumueleza mwalimu wangu ili tutembelee shuleni kwenu na kujifunza zaidi.
Faida ya mazingira safi
Shule yetu ina mazingira safi. Shule yenye mazingira safi hupendeza na kuvutia. Mazingira machafu huwa maficho ya wadudu na wanyama hatarishi. wadudu na wanyama hao ni kama vile nzi, mbu, panya na nyoka. Viumbe hawa hupenda kujificha katika maeneo machafu. Ni muhimu kuishi kwenye mazingira
mazingira safi huepusha maambukizi ya magonjwa ya kuhara, malaria na tauni. Pia, huepusha uharibifu wa vyakula mashambani na nyumbani. Tufanye usafi kwenye mazingira yanayotuzunguka ili kuepusha madhara yatokanayo na uchafu.
www.learninghubtz.co.tz