SURA YA PILI

HALI YA HEWA

Msamiati

  • Chachamaa- shikilia simamo wa jambo
  • Jokofu- Chombo kinachohifadhi vitu katika hali ya ubaridi ili visiharibike
  • Jotoridi- kiwango cha joto au baridi katika hewa
  • Kipimajoto- chombo kinachotumika kupima jotoridi
  • Kujikunyata- kujikunja
  • Majigambo- hali ya kutoa maneno ya kujisifia
  • Mgolole- shuka nzito inayopitishwa juu ya mabega
  • Pangaboi- Kifaa kinachozalisha msukumo wa hewa
  • Thubutu- haiwezekani hata kidogo
  • Tutumua- vimbisha, tunisha

Katika sura hii utajifunza kuhusu hali ya hewa ya mazingira yako. Hali ya hewa inahusisha jotoridi, mvua, mawingu na upepo wa sehemu husika. Katika sura hii utajifunza kipengele kimoja to cha hali ya hewa. Kipengete hiki kitahusu jotoridi to sehemu unayoishi. Utajifunza pia kipimo cha halijoto, mbinu za kujikinga na baridi na joto.

Kubaini jotoridi katika mazingira yetu

Maana ya jotoridi

Hali ya hewa inaweza kuwa ya joto au ya baridi. Hali hii huitwa jotoridi. Joto likiongezeka tunasema jotoridi liko juu na kunapokuwa na baridi jotoridi huwa chini.

Kidelezo: Kipimajoto

  • Kuna umuhimu wa kufahamu jotoridi la sehemu unayoishi. Hili itakusaidia kupanga shughuti zako.
  • Vilevile, itakuwezesha kuchagua nguo za kuvaa katika siku au kipindi husika. Jotoridi hupimwa kwa kifaa kinachoitwa kipimajoto.

Athari za joto na baridi kwa wanyama na mimea

Soma majigambo yofuatayo kati ya joto na baridi, kisha jibu. maswall.

Joto: Mimi ni joto, chanzo changu ni jua. Jua Likiwa kaLi mimi huwa mkaLi pia. Nikifika tu baridi hutimua

Baridi: Mimi ni baridi, kiboko ya joto nikifika tu joto huhama.

Joto: Wee! Mimi nakausha maji ya mito, mabwawa na

visima. Hata mazao nayakausha na kusababisha njaa. Mimi ni mwamba kuliko wewe.Tena ni kiboko yako, hata viumbe hujificha nikichachamaa.

Baridi Thubutu! Hunishindi mimi. Nikichachamaa viumbe

hujikunyata. Hakuna kinachoweza kuishi. vyote wanaganda na kufa.

Joto: Sio kweli, hata ukizidi watu wanajifunika, na kuvaa nguo nzito ili kukudhibiti. Lakini mimi joto, watu wasipovaa nguo wanatoka jasho na kukosa raha. Namaliza maji mwilini mwao na wanaweza hata kufa. Hata vyakula vyao vinaoza kwa sababu yangu mimi.

Baridi: watu wanakaa kwenye vivuti chini ya miti na kustarehe. Wakiwa ndani wanajipulizia upepo kwa pangaboi. Wanaweka vitu vyao kwenye jokofu na maisha yanaenda vizuri. Wewe joto si lolote.

Joto: Sawa bwana, tusigombane. Sisi sote tuna faidatukiwepo

kwa kiasi na hasara kama tukizidi sana.

Maswali

  1. Chanzo cha joto ni nini?
  2. Kifaa kinachotumika kupima jotoridi kinaitwaje?
  3. Joto kali lina Maathari gani kwa mimea na wanyama?
  4. Taja njia mbili za kujikinga na hali ya hewa ya baridi kali.
  5. Taja mbinu za kujikinga na hali ya hewa ya joto

Tazama picha ifuatayo, kisha jibu maswall.

Kielelezo: Wanafunzi wakisoma jotoridi kutoka kwenye kipimajoto

Maswali

  1. Ni. kifaa gani kinachoonekana katika picha?
  2. Kifaa kinachoonekana katika picha kinatumika kufanyia rani?

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256