SAYANSI DARASA LA SITA : SURA YA KWANZA.

HEWA:

Msamiati

 • Hewa – Mchanganyiko wa gesi mbalimbali zisizoonekana na zinazozunguka katika angahewa.
 • Gesi – Aina ya maada ambayo haionekani wala kushikika.

Maana ya Hewa:

Hewa ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali zisizoonekana na zinazunguka katika angahewa. Gisi hizo ni:-

 1. Oksijen
 2. Kaboni dayoksaidi
 3. Naitrojen.

Sifa za hewa

 1. Hewa inachukua nafasi
 2. Hewa ni maada isiyoonekana
 3. Hewa ipo katika hali ya gesi.

Umuhimu wa hewa.

Hewa ni muhimu sana katika uhai wa binadamu na viumbe hai vingine. Yafuatayo ni umuhimu wa hewa.

1. Uhai wa viumbe.

 • Oksijeni inatumika na viumbe wote kuleta uhai. Binadamu tunahitaji Oksijen kupumua, mbegu inayoota inahitaji Oksijeni ili kumea.
 • Mimea inahitaji gesi ya kabonidayoksaidi inayopatikana kweney hewa kusamisi chakula chake.
 • Wanyama hubeba Oksijeni kwenye damu na kupeleka kweney seli ambako inasaidia kubadilisha chakula kwa nishati ya mwili.

2. Uunguzaji wa vitu.

 • Gesi ya Oksijeni inahitajika ili moto uwake
 • Gesi hii huruhusu kuungua kwa vitu mbalimbali mfano, karatasi, mkaa au hata kuni.
 • Ingine zinazitumia mafuta utumia Oksijeni ili kuunguza mafuta, ili kuzalisha nishati inayowezesha injini kufaya kazi.
 • Uchavushaji: Hewa husaidia kubeba chavua za ua kutoa sehemu ya kiume ya ua kwenda sehemu ya kike ya ua.
 • Maua hutoa harufu ambayo hubebwa na hewa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ambayo uwavutia viumbe kama ndege na wadudu, ambao wanapokula utomvu wa maua hubeba chavua na kusababisha uchavushaji na maua.

3. Uzalishaji umeme

 • Upepo ni hewa ambayo inatumiwa kusalisha nishati ya umeme. Upepo ni hewa inayosafiri kwa kasi kubwa. Sehemu zenye upepo mkali ufungwa mitambo ambayo utumia kuzalisha umeme.

4. Ukaushaji wa vitu:

 • Hewa inayotuzunguka hufanya maji kufyonzwa katika hali ya mvuke kutoka kwenye vitu mbalimbali kama mazao na udongo.
 • Nguo zilizofuliwa uanikwa kwenye eneo la wazi ambapo hewa hufyonza maji na kuziacha zikiwa kavu.
 • Mazao ya nafaka uwekwa sehemu ya wazi ili hewa inayozunguka ibebe unyevuvyevu na kfanya mazao yakauke. Nafak kama mahindi, uwele, mtama, ulezi na maharage ukaushwa kwa njia ya hewa.

5. Kupaa na kuelea kwa vitu:-

 • Ndege na viumbe wengine wanaweza kujongea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuruka angani.
 • Vitu vinavyoruka angani vina muundo maalumu unaosaidia kufanya vielee angani.

6. Usafirishaji wa mawimbi ya suti.

 • Tunaweza kusikia sauti za watu, ndege, wanyama na vitu mbalimbali kama kengele kwa sababu ya hewa.
 • Mawimbi ya sauti kutoka sehemu inapozalishwa kwenda sehemu nyingine husafirishwa na hewa.
 • Redio hupokea mawimbi ya sauti mbalimbali.

7. Kutengeneza mvua.

 • Maji katika sehemu mbalimbali yanapopata joto hugeuka. Kuna mvuke na huenda angani. Mvuke wa maji unapoenda angani hupoa, huganda na kutengeneza mawingu. Mawingu yanapokuwa mazito hutengeneza matone ambayo hudondoka kutoka angani kama mvua.

8. Kujaza matairi hewa –

 • Vyombo vya usafiri kama vile baiskeli, pikipiki na magari hutumia matairi ili kujongea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Matairi huvikwa kwenye magurudumu ya vyombo hivi na kujazwa hewa ili kuweza kutumika. Vyombo vya usafiri huweza kubeba mizigo mizito. Matairi yenye hewa hupunguza msuguano na barabara.

9. Kusawazisha jotoridi la dunia

 • Hewa huzunguka katka nchi kavu na juu ya maji kama ziwa, mito na bahari
 • Miale ya jua inapogonga sehemu ya chi kavu hasa kipindi cha kiangazi hufanya hali ya joto kuongezeka.

Gesi zinazounda hewa

 • Hewa ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali – Gesi kama neoni, haidrojeni, heli, kriptoni na zenoni zipo kwenye hewa kwa kiwango kidogo sana.
 • Mvuke wa maji pia unaunda hewa, lakini kiwango chake hutofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Gesi zinazounda hewa:

Aina ya gesi

Asilimia katika hewa

 1. Naitrojeni

78%

 1. Oksijeni

20.9%

 1. Agoni

0.90%

 1. Kabonidayoksaidi

0.03%

 1. Gesi nyingine

0.17%

Oksijeni:

 • Gesi ya oksijeni ni asilimia 20.9 katika hewa
 • Gesi ya oksijeni huzalishwa na mimea wakati wa usanishaji chakula.

Kabonidayoksaidi + maji image kabohaidreti + Oksijeni.

Gesi ya oksijeni pia uzalishwa katika maabara kwa kutumia kampaundi mbalimbali. Mfano, Kloreti ya potasi.

Kloreti ya potasi kloridi ya potasi + oksijeni.

Umuhimu wa gesi ya Oksijeni

1. Upumuaji:

 • Wanyama na binadamu hutumia gesi ya oksijeni kupumua.
 • Binadamu anapumua hewa kwenda kwa mapafu ambayo huchukuliwa na damu na kupelekwa kwenye seli za mwili.
 • Oksijeni husaidia huchomaji wa chakula ili kuzalisha nishati katika mwili.
 • Mimea pia hutumia hewa ya oksijeni kuzalisha nishati ambapo gesi ya kabonidayoksaidi huzalishwa.
 • Wataalam wanaosafiri angani na wazamiaji pamoja na wakwea milima hutumia gesi ya oksijeni kwenye mitungi.

2. Hospitalini:

 • Gesi ya oksijeni hutumiwa na wagonjwa ambao wako katika hali mahututi au wana matatizo ya kupumua.

3. Vyombo vya usafiri:

 • Vyombo vya usafiri nchi kavu na kwenye maji hutumia mafuta. Mafuta hayo huuunguzwa ili kutoa nishati inayofanya vyombo hivi kujongea nchi kavu, kupaa angani na kuelea kwenye maji.
 • Oksijeni ndio gesi inayotumika kuunguza mafuta yanayotumika kwenye vyombo kama hivi.

4. Uchomeleaji wa vyuma:

 • Gesi ya Oksijeni hutumika katika kazi ya uchomeleaji wa vyuma. Gesi hii huchochea kuungua na kulainika kwa vyuma, hivyo kuwa rahisi kukata na kunganisha kwa vyuma.

5. Kabonidayoksaidi:

 • Gesi ya kabonidayoksaidi iliyopo kwenye hewa ni asilimia 0.03. Kabonidayoksaidi imeundwa na elementi mbili ambazo ni kaboni na oksijeni gasi. Hii hamna harufu wala rangi.
 • Upumuaji wa viumbe hai hutoa gesi ya kabonidayoksaidi. Gesi hii huzalishwa katika shughuli za uchachushaji, uunguzaji na uozaji wa vitu.
 • Gesi ya kabonidayoksaidi huzalishwa kwenye maabara kwa kuchanganya kampaundi za kaboneti na aside, mfano kaboneti ya kalisi + Asidi ya haidrokloriki Kloradi ya kalisi + maji + kabonidayoksaidi.

Umuhimu wa gesi ya Kabonidayoksaidi

 • Gesi hii ni muhimu katika usanishaji wa chakula cha mimea.
 • Mimea hutumia gesi ya kabonidayoksaidi na mwanga wa jua katika kusanisi chakula.
 • Gesi hutoa povu ambalo husaidia katika kuzima moto.
 • Kutengeneza mbolea ya chumvichumvi.
 • Kabonidayoksaidi inayotokana na upumuaji wa hamic kutumika kwenye viwanda vya mikate na nyumbani ili kufanya unga uumuke.
 • Gesi hii pia hutumika kwenye kiwanda kwa ajili ya kusindika vivywaji vya aina mbalimbali kama vile soda na juisi.

Athari za gesi ya kabonidayoksaidi.

 • Kumekua na ongezeko la uzalishaji wa gesi ya kabonidayoksaidi kutoka viwandani na kutokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji.
 • Miti husaidia kupunguza gesi ya kabonidayoksaidi kwenye mazingira.
 • Tunapaswa kupanda miti mingi na kuepuka kukata miti ovyo ovyo.
 • Kabonidayoksaidi hutengeneza utando ambao huzuia joto kupotea kwenye uso wa nchi. Hali hii husababisha ongezeko la joto duniani, ambayo huleta kuyeyuka kwa barafu hivyo kuongezeka kina cha maji baharini.

Nitrojeni:

 • Gesi hii huchangia asilimia 78% ya gesi zote zilizo katika hewa.
 • Gesi hii huzalishwa kwenye shughuli za kijiologia, kilimo, ufugaji na uchafu mijini
 • Gesi ya naitrojeni ni mihimu katika kutengeneza protini katika mimea na wanyama.
 • Gesi hii hubadilishwa na viumbe kama elementi au kampaundi.
 • Elementi hizi hufyonza pamoja na maji kupitia mizizi na kutumika katika kurutubisha mimea.
 • Naitrojen ikikosemana katika udongo mimea hukua taratibu, hudumaa, huzaa kidogo na majani huwa ya njano.

Matumizi ya Naitrogeni:

 • Kutengeneza mbolea ya chumvichumvi kama Urea, DAP, NPK, SA na Can.
 • Kutengeneza aside inayoitwa nitria, rangi mbalimbali na nailoni.
 • Hutumika hospitali kuhifadhi vitu mbalimbali kama vile mbegu na mayai ya uzazi, seli neva na damu.
 • Gesi ya naitrojeni piaa hutumika kuhifadhi vitu katika halijoto maalumu.

Agoni:

 • Hii ni gesi bwete inayopatikana hewani. Agoni pamoja na gesi bwete nyingine huunda asilimia 0.90 ya hewa
 • Huitwa gesi bwete kwani haichanganyikani na elementi nyingine kutengeneza kampaundi.
 • Hutumika kwenye taa za umeme na neli ng’aavu za taa za umeme.

Mvuke wa maji:

 • Maji hupatikana katika hali tatu – yabisi, kimiminiko na gesi au mvuke.
 • Mvuke wa maji hupatikana katika hewa kwa kiasi tofauti kulingana na eneo. Mvuke hutoka kwenye maji kama bahari, ziwa, mto na sehemu yanapokusanyika mimea hupoteza maji katika hali ya mvuke na kwenda kwenye angahewa. Mvuke unapofikia angani hupoozwa na kutengeneza matone ambayo hudondoka kama mvua. Wanyama nao hupoteza maji katika hali ya mvuke kwa njia ya jasho na upumuaji.

www.learninghubtz.co.tz

MTIHANI WA MWISHO WA MADA: SURA YA KWANZA

1. Chagua jibu sahihi katka maswali yafuatayo:

(i) Gesi ambayo mimea hutumia kusanisi chakula ni:-

 1. Oksijeni
 2. Kabonidayoksaidi
 3. Nitrogen
 4. Agoni.

(ii) Moto unahitaji gesi gani ili kuwaka?

 1. Kabonidayoksaidi
 2. Agoni
 3. Oksijeni
 4. Nitrojeni

(iii) Gesi mojawapo kati ya hizi hutumia kusindika vinywaji

 1. Nitrojeni
 2. Agoni
 3. Kabonidayoksaidi

(iv) Gesi ambayo inachangia asilimia 0.003 ya hewa kwenye angahewa ni:-

 1. Nitrojeni
 2. Kabonidayoksaidi
 3. Agoni
 4. Oksijeni

(v) Ni lipi ambalo sio matumizi ya kabonidayoksaidi?

 1. Kuzima moto
 2. Kuhifadhi chakula
 3. Kuunguza
 4. Kusanisi chakula

(vi) Gesi hii hutumika kwenye taa za umeme

 1. Agoni
 2. Helium
 3. Krypton
 4. Oksijeni

(vii) Ni yapi sio matumizi ya Oksijeni?

 1. Kuwasha moto
 1. Kutengeneza kula
 2. Kuhifadhi chakula
 3. Hospitali kwa wagonjwa waliozidiwa

(viii) Gesi hii utumia kuunda mbolea.

 1. Agoni
 2. Nitrojeni
 3. Kabonidayoksaidi
 4. Amonia

(ix) Ipi sio sifa ya hewa

 1. Ina harufu
 2. Haina rangi
 3. Haionekani
 4. Inachukua nafasi

(x) Ipi kati ya hizi sio sehemu ya hewa

 1. Oksijeni
 2. Hydrogeni
 3. Agoni
 4. Nitrojeni.

2. Jaza jedwali lifuatalo kwa kuandika jibu sahihi.

Aina ya gesi

Asilimia katika hewa

 1. ___________

78

 1. Oksijeni

_____________

 1. Agoni

____________

 1. ______________

0.03

 1. Gesi nyingine

____________

3. Andika kweli kama sentensi ni sahihi na si kweli kama sentensi sio sahihi.

 1. Mimea inategemea oksijeni kutoka kwa wanyama
 2. Hewa haina harufu wala rangi
 3. Kuna gesi nne tu zinazounda hewa
 4. Gesi ya kabondayoksaidi hutumika kuzima moto
 5. Mvuke unatoka baharini na kwenye mimea tu
 6. Binadamu haitaji gesi ya kabonidayoksaidi
 7. Gesi ambayo inatumia kuzima moto ipo kwenye hewa
 8. Nitrojeni ni muhimu kwani utumia kutengeneza chakula cha wanga.
 9. Gesi ya kabonidayoksaidi inachangia katika ongezeko la joto duniani.
 10. Mimea ndio yenye uwezo wa kutengeneza chakula kwa kutumia nishati ya jua

4. Eleza umuhimu wa hewa katika;

 1. Uhai wa viumbe
 2. Uunguzaji vitu
 3. Uchavushaji
 4. Uzalishaji umeme

5. Taja gesi nne zinzounda hewa

6. Andika matumizi mawili ya gesi zifuatazo

 1. Oksijeni
 2. Nioni
 3. Kabonidayoksaidi
 4. Nitrojeni
 5. Agoni.

7. Unaweza kuonyesha kuwa mvuke upo?

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256