SURA YA PILI

UKUAJI WA MIMEA.

Ukuaji ni mojawapo ya sifa za viumbe hai. Kukua ni kitendo cha kuongezeka kwa kimo, uzani na umbo la seli. Ukuaji katika viumbe – hai hautokei kwa kiwango sawa katika kipindi chote cha uhai.

Viumbe hai hukua kwa kasi mwanzoni hadi wanapofika hatua ya kukomaa, kisha ukuaji kuanza kupungua na hukoma kwa kipindi fulani na mwisho kiumbe hai hufa.

Mimea hukua vizuri pale inapopata mahitaji yake muhimu.

Mahitaji muhimu ya mimea.

Mimea inamahitaji makuu matano ambayo ni muhimu kwa ukuaji. Mahitaji haya ni:

  • Hewa
  • Maji, virutubisho, na joto.

Upatikanaji wa kutosha wa baadhi ya mahitaji na kukosekana kwa mahitaji mengine huadhiri ukuaji wa mimea. Kwa mfano, mimea ikipata mwanga wa jua wa kutosha lakini ikikosa maji au virutubisho, ukuaji huathirika.

Mwanga wa jua.

  • Jua linatoa nishati ya joto na mwanga ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mimea. Mimea hutumia nishati ya mwanga wa jua kutengeneza chakula chake majani ya mimea yana umbijani ambao husharabu nishati ya mwanga wa jua na huwezesha mimea kujitengenezea chakula chake.
  • Kitendo cha mimea kusanisi chakula kwa kutumia nishati ya mwanga wa jua huitwa usanisini.
  • Kasi ya usanisini inategemea mwanga wa jua, kadri mwanga wa jua unavyoongezeka ndivyo kiwango cha usanisini kinaongezeka.
  • Jua likiwa kali sana huharibu umbijani na kusababisha kupungua kwa kiwango cha usanisi wa chakula.
  • Mimea ikikosa mwanga wa jua shina lake huwa lembamba, refu na majani huwa na rangi ya manjano.
  • Ukosefu wa mwanga wa jua wa kutosha huathiri uwezo wa mimea kutengeneza chakula chake na hivyo kuathiri ukuaji.
  • Jua kali husababisha majani kukauka na udongo kukosa unyenyekevu na hivyo mimea kukauka na hatimaye kufa.

Hewa.

  • Geso ya kabonidayoksaidi utimiwa na mimea katika usanishaji chakula au usanisini. Gesi hii huchukuliwa na mimea kupitia matundu ya stomata yaliyopo kwenye majani.
  • Stomata hufunguka na kufyonza gesi ya kabonidayoksaidi inayotakiwa kukamilisha kitendo cha usanisinuru.
  • Licha ya kutumika wakati wa usanisinuru, kiwango cha gesi ya kabonidayoksaidi ubakia sawa angani. Hii usababishwa na upumuaji wa wanyama ambao huongeza gesi hii.
  • Ongezeko kubwa la gesi ya kabonidayoksaidi angani huathiri ukuaji katika mimea, katika siku za hivi karibuni kiwango cha gesi ya kabonidayoksaidi. Kimeongezeka sana kutokana na shughuli mbalimbali za binadamu.
  • Ongezeko la gesi hii hupunguza kiwango cha kufunguka na kujifunga kwa stomata, ikiwa kiwango cha carbon dioxide ni kikibwa, kwenye hewa, stomata hufunguka kwa muda mfupi na kupata kiwango cha kutosha cha gesi hii. Kitendo hiki huathiri kiwango cha maji yatakayofyonzwa na mizizi kwa ajili ya kuiwezesha mimea kufanya kitendo cha usanisinuru.

MAJI

  • Ni mojawapo ya kati ya mahitaji muhimu kwa maisha ya viumbe hai. Mimea huitaji maji ili kuweza kukua vizuri. Moja ni mojawapo kati ya mahitaji muhimu katika kitendo cha usanisi wa chakula. Maji hufyonzwa kutoka kwenye udongo kupitia kwenye mizizi. Ncha za mizizi zina vinyweleo vidogo vidogo ambavyo ndivyo vinavyosharabu maji kwa njia ya osimosisi.
  • Maji yakishapita katika vinyweleo vya mizizi huingia kwenye mizizi mkuu, kisha huingia katika shina ambapo husafirishwa hadi kwenye majani.
  • Tishu inayosafirisha maji katika mimea iko katika shina la mimea. Tishu hiyo huitwa Zailemu

Kazi ya maji katika ukuaji wa mimea.

  • Maji husaidia kuyeyusha madini kwenye udongo ambayo husafirishwa na kutumiwa na mimea.
  • Kubeba kabohaidrets pamoja na virutubisho vingine na kuisambasa kutoka kwenye majani kwenda sehemu nyingine za mimea
  • Kusawazisha kiwango cha joto katika mimea.
  • Hufanya mimea kuwa imara iwapo kuna maji ya kutosha ndani ya seli.
  • Husaidia mimea kujitengenezea chakula chake.

Mahitaji ya maji yanatofautiana mmea mmoja hadi mwingine.

  • Kiwango sahihi cha maji ni muhimu kwenye mimea ili kuiwezesha kukua na kutoa mazao bora. Ukuaji wa mimea ya mpunga kwa mfano huitaji maji mengi.
  • Ukuaji mimea pia huathiriwa na udongo, udongo ukiwa na maji mengi, mizizi inaweza kuoza kwa kukosa gesi ya oksijeni.
  • Mimea ikikosa maji virutubisho vinavyohitajika haviwezi kufyonzwa kutoka kwenye udongo na kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali.
  • Ukosefu wa maji ya kutosha huathiri tendo la usanisinuru, hii husababisha mimea kuwa dhaifu na hatimaye kunyauka na kufa.

Virutubisho:

  • Mimea inahitaji virutubisho mbalimbali ili iweze kukua vyema.
  • Virutubisho hivi huchukuliwa na mimea kupitia kwenye mizizi, kutoka kwenye ardhi au sehemu nyingine ambayo mimea imepandwa kwa njia ya kufyonzwa.
  • Vinyweleo vidogo vidogo vilivyo kwenye ncha za mizizi hufyonza virutubisho kwa njia ya osimosisi, virutubisho vikishaingia katika vyinyweleo vya mizizi huingia kwenye mzizi mkuu, kisha huingia katika shina.
  • Virutubisho hivyo husafirishwa hadi kwenye majani kupitia tishu inayoitwa zailemu.
  • Sehemu kubwa ya virutubisho vinavyotumiwa na mimea hupatikana katika udongo au sehemu nyingine ambazo mimea huota katika maji bila kuwepo kwa udongo.
  • Virutubisho kama oksijeni, kaboni na haidrojeni hupatikana kutoka kwenye hewa.
  • Virutubisho vimegawanywa katika makundi makuu mawili ambayo ni:-

Virutubisho vikuu

Virutubisho visivyo vikuu.

  • Virutubisho vikuu vinahitajika kwa kiasi kikubwa na ni muhimu sana ukuaji, virutubisho hivyo ni vitatu navyo ni:- Naitrojeni, Fosforasi na Potasiamu.
  • Kwa kawaida upatikanaji wa virutubisho vikuu vinahitaji kuongeza mbolea kwenye udongo.
  • Virutubisho visivyo vikuu ni kalisi, magnesiamu, salfa klorini chuma, manganizi, zinki, shaba, boron, molibedeni nikeli oksijeni kaboni na haidrojeni

Kazi na athari za upungufu wa virutubisho kwa ukuaji wa mimea.

Aina ya Kirutubisho

Kazi ya kirutubisho

Athari za kukosekana kwa kirutubisho

Upatikanaji wa kirutubisho

Naitrojeni

Ukuaji wa majani

Kutengeneza protein

Kuyapa majani rangi ya kijani hivyo hutumika katika usanisi wa chakula

Hukuza mashina

Mimea kudumaa

Majani kuwa njano hivyo kukauka na kudondoka

Kupungua kiwango cha protini.

Kupungua kiasi cha maua

Mimea kukomaa kabla ya muda wake.

Katika udongo mbolea yenye naitrojeni na bakteria wenye uwezo wa kutengeneza virutubisho vyenye naitrojeni kutoka kwenye hewa.

Fosforasi

Husaidia katika usanisi wa chakula.

Husaidia ukuaji wa mizizi

Husaidia mimea kutoa maua na matunda.

Hupunguza uwezekano wa mimea kupata magonjwa

Huongeza ubora wa mazao

Mimea kukua taratibu na kudumaa.

Mimea kuchelewa kukomaa.

Kutoa mbegu dhaifu na matunda machache.

Udongo na mbolea yenye fosforasi.

Potasi

Muhimu ukuaji wa mizizi

Hutumika kusawazisha kiwango cha maji katika mimea.

Husaidia kusambaza kabohaidreti inayotengenezwa ili itumike vizuri

Inaongeza uwezo wa mimea kujiking na maradhi.

Inaongeza ubora, ukubwa na wingi wa matunda, mboga, nafaka na mbegu

Majani ya mimea kupoteza umbijani.

Mimea kukua taratibu na kudumaa

Mimea kua na shina dhaifu na kupata maradhi kirahisi.

Kupungua kwa ubora, ukubwa na wingi wa matunda, mboga nafaka na mbegu.

Udongo

Mbolea yenye potasi na majivu.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256