SAYANSI LA TANO : SURA YA KWANZA

VIUMBE HAI

SIFA YA VIUMBE HAI

Umahiri.

Kufikia mwisho wa mada hii, mwanafunzi aweze;

 • Kutofautisha viumbe hai na visinyo hai kwenye mazingira yake
 • Aenyesho kwa vitendo jinsi mimea inafuata mwanga
 • Kwa michoro hatofautishe kati ya mimea aina ya monokotiledoni na daikotiledoni.
 • Aonyeshe mabadiliko yanayotokea katika ukuaji wa mimea.
 • Atambua wanyama hatari na wanyama rafiki katika mazingira yake.
 • Aweke viumbe hai katika makundi mbalimbali.

Msamiati

 1. Mapezi –Viungo vilivyopo mgongoni, mashavuni na ubavuni mwa samaki ambavyo humwezesha kuogelea.
 2. Matamvua- Viungo vyenye nyuzinyuzi vilivyo ndani ya shavu la samaki vyenye kazi ya kuvuta na kuchuja hewa inayoingia na kutoka ndani ya mwili wake.
 3. Ugwemgongo – Ute wenye neva za fahamu ulio ndani ya pingili za uti wa mgongo.
 4. Poikilothemia- wanyama ambao joto la mwili hubadilika kulingana na mazingira.

Viumbe hai wana sifa kuu saba ambazo ni kula, kupumua, kuitikia vichocheo, kujongea, kuzaliana, kutoa takamwili na kukua. Maelezo ya sifa hizo ni kama ifuatavyo:

(a) Kula

 • Viumbe hai hula chakula kinachopatikana katika mazingira yao. Vyakula huvipatia viumbe hai virutubisho mbalimbali kama vile protini, wanga, mafuta, madini na vitamini.
 • Vyakula hivi huvifanya viumbe hai kukua na kupata nguvu. Vilevile, chakula husaidia mwili kujikinga na magonjwa mbalimbali.

(b)Kupumua

 • Kupumua ni kitendo cha kuvuta hewa ndani na kuitoa nje ya mwili wa kiumbe hal.
 • Wanyama huvuta hewa ya oksijeni ndani ya mwili na kutoa hewa ya kabonidayoksaidi nje ya mwili. Pia, mimea huvuta hewa ya kabonidayoksaidi na kutoa hewa ya oksijeni wakati wa usanishaji chakula.

(c) Kuitikia vichocheo

 • Viumbe hai huitikia vichocheo kutoka ndani na nje ya mwili. Mfano wa vichocheo ni mwanga na joto.
 • Wanyama huitikia vichocheo kwa kutumia milango ya fahamu ambayo ni pua, ngozi, macho, ulimi na masikio. Mimea huitikia vichocheo kupitia mizizi, shina, matawi, majani na maua.

(d) Kujongea

 • Viumbe hai hujongea kwa kutumia njia mbalimbali. Kujongea ni kitendo cha kusogea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine au kubadili ueiekeo.
 • Pia mimea hujongea lakini hufanya hivyo kwa taratibu sana kiasi kwamba ni vigumu kuona mjongeo huo kwa urahisi.

(e) Kuzaliana

 1. Viumbe hai wote huongezeka idadi kwa njia ya kuzailana. Wanyama huzaliana kwa njia ya kutaga mayai au kuzaa watoto hai. Mimea huzaliana kwa kutumia mbegu au kuotesha mashing na vipandikizi.

(f) Kutoa takamwili

 1. Viumbe hai wote hutoa takamwili kwa njia mbalimbali. Takamwiii hizo hutolewa katika hall ya hewa na majimaji.
 2. Wanyama hutoa maji na chumvichumvi nje ya mwili kwa njia ya mkojo na jasho. Pia hutoa gesi kwa njia ya kupumua. Mimea hutoa taka katika hall ya maji, gesi na utomvu.

(g) Kukua

 1. Viumbe hai hukua kwa kuongezeka kimo na uzani. Kukua ni kitendo cha kuongezeka kwa uzito, ukubwa na umbo la sell.
 2. Katika kazi miiyoifanya utagundua kwamba, mimea na wanyama wana sifa zinazofanana. Sifa hizo ni kula, kujongea, kupumua, kuitikia vichocheo, kuzaliana, kutoa takamwili na kukua.
 3. Hata hivyo, baadhi ya sifa huwatofautisha wanyama na mimea. Sifa mojawapo ni namna ya kujongea. Wanyama huweza kujongea kutoka sehemu moja hadi nyingine.
 4. Kujongea katika mimea hutokea katika sehemu za mmea. Kwa mfano, shina la mnlea hitijongea kufuata mwanga na mizizi hujongea kufuata maji. Kujongea huRu ni kwa taratibu sana ukilinganisha na kujongea kwa wanyama.
 5. Tofauti nyingine ni kuwa mimea hujitengenezea chakula kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya kabonidayoksaidi, lakini wanyama hawajitengenezei chakula.

Makundi ya viumbe hai

 • Katika mazingira tunamoishi kung viumbe hai wa aina kuu mbili; mimea na wanyama. Utagundua kwamba kundi la wanyama linajumuisha viumbe mbalimbali.
 • Kwa mfano, minyoo, sisimizi, mbu, mbwa, samaki na binadamu. Kundi la mimea pia linajumuisha viumbe ambao wanatofautiana kimaumbile, njia za uzazi na makazi. Kwa mfano, mchungwa, mharage na nyasi ni kundi moja.
 • Makundi haya ya wanyama na mimea yamegawanyika katika makundi madogomadogo yenye sifa zinazofanana. Kwa mfano, kuku na kunguru wanafanana zaidi kuliko kuku na ng'ombe, ingawa wote wako katika kundi moja la wanyama.

Makundi ya mimea

 • Mimea imegawanyika katika makundi makuu manne. Katika sehemu hii, utajifunza makundi mawili ambayo ni mimea inayotoa maua na mimea isiyotoa maua.

Mimea inayotoa maua

 1. Mimea inayotoa maua ni ile ambayo ua ndiyo sehemu maaiumu ya uzazi. Ua hubadilika kuwa tunda na ndani ya tunda mbegu hukua na kukomaa.
 2. Mifano ya mimea hii ni ngano, maharage, miembe, njegere na alizeti. Mimea hii ndiyo mingi zaidi kuliko mimea isiyotoa maua na inapatikana katika mazingira mbalimbali hata yenye baridi kali sana.
 3. Mimea inayotoa maua ina matumizi mbalimbali kwa binadamu na wanyama wengine. Matumizi hayo ni chakula, dawa, kutengeneza nguo na kuni. Pia, mimea hii ni makazi ya wanyama.

Makundi ya mimea inayotoa maua

 1. Mimea inayotoa maua imegawanyika katika makundi mawili. Makundi hayo ni monokotiledoni na daikotiledoni.
 2. Majina ya monokotiledoni na daikotiledoni yametokana na idadi ya ghala katika mbegu. Mbegu ya monokotiledoni ina ghala moja wakati daikotiledoni ina ghala mbiii.
 3. Tofauti nyingine za mimea hii ni katika umbo la majani, vena, shina, mizizi na maua.
 4. Mimea aina ya monokotiledoni
 5. Mimea aina ya monokotiledoni ina mbegu ambazo zina kotiledoni au ghala moja. Kuwepo kwa ghala moja ndiyo sifa iliyoipa mimea hii jina la monokotiledoni.
 6. Neno monokotiledoni Iinamaanisha ghala moja. Mifano ya mimea ya monokotiledoni ni mtama, mahindi, ulezi, nazi na ngano. Vilevile, majani ya monokotiledoni yang vena zilizosambamba kufuata urefu wa jani. Mizizi yake ni ya nyuzinyuzi inayoota kwa pamoja kwenye kitako cha shina. Mimea hii haina mzizi mkuu.

Mimea aina ya daikotiledoni

 1. Mimea aina hii ina mbegu zenye ghala mbili. Kuwepo kwa ghala mbili ndiyo sifa iiiyoipa mimea hii jina la daikotiledoni.
 2. Jina hill Iinamaanisha kotiledoni mbili au ghala mbili. Mifano ya mimea ya aina hii ni miembe, maharage na kunde. Majani ya mimea hii yana vena zilizotanda kama wavu.
 3. Pia, mimea hii ina mzizi mkuu na mizizi mingine midogomidogo ambayo inaota kutoka kwenye mzizi mkuu.

Mimea isiyotoa maua

 1. Mimea isiyotoa maua ni ile ambayo maua sio sehemu ya uzazi. Mimea hii haitoi matunda lakini inatoa mbegu. Mbegu za mimea hii hazifunikwi ndani ya tunda, kwa mfano mbani, mvinje, na mwerezi.
 2. Mara nyingi mimea hii huwa ya kijani karibu muda wote wa mwaka. Mimea isiyotoa maua ni chanzo kizuri cha kuni na mbao. Mimea hii pia, hutumika kwa ajili ya kutengenezea karatasi na gundi. Vilevile, aina hii ya mimea ni makazi ya wanyama.

Sehemu za mmea

 1. Mmea una sehemu kuu tatu ambazo ni mizizi, shina na majani. Sehemu nyingine za mimea ni maua, matunda na mbegu. Sehemu hizo zina kazi mbalimbali ambazo zinawezesha mmea kukua vizuri.

Mizizi

 1. Kazi kuu ya mizizi ni kufyonza maji, madini na virutubisho kutoka kwenye udongo. Kazi nyingine ni kushikilia mmea kwenye udongo ili usianguke, pia huhifadhi chakula cha mmea.
 2. Mifano ya mimea inayohifadhi chakula kwenye mizizi ni mhogo na viazi vitamu.

Shina

 1. Kazi ya shina ni kushikilia majani, maua na matunda. Kazi nyingine ya shina ni kusafirisha maji, virutubisho na madini kutoka kwenye mizizi kwenda kwenye matawi na majani.
 2. Vilevile, baadhi ya mashina ya mimea kama vile miwa huhifadhi chakula.

Majani

 1. Kazi ya majani ni kusanisi au kutengeneza chakula cha mmea na kusaidia kuendelea kukua. Mimea mingi ina majani yenye stomata ambazo hufunguka na kufungika hivyo kurekebisha kiwango cha maji, oksijeni na kabonidayoksaidi inayoingia na kutoka katika mmea.

Maua na tunda

 1. Kazi kuu ya maua ni uzazi. Maua mengi yana harufu na rangi nzuri. Rangi na harufu hizo huwavutia wadudu ambao hutua kwenye ua. Wadudu hubeba chavua kutoka ua moja kwenda ua lingine.
 2. Kitendo hiki huitwa uchavushaji. Baada ya uchavushaji ua hutengeneza tunda. Tunda hubeba mbegu. Mbegu ikipandwa huota na kuwa mmea.
 3. Mmea huanzia kwenye mbegu. Mbegu huota na kutoa mmea mchanga wenye majani. Mmea ukishakomaa hutoa maua ambayo hutengeneza tunda. Ndani ya tunda huwemo mbegu ambazo huota tena na duru ya ukuaji huanza tena.

Makundi ya wanyama

 • Kama ilivyo kwa mimea, wanyama pia wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni wanyama wenye uti wa mgongo kwa mfano, binadamu, ndege, mjusi, samaki na chura. Kundi la pili ni wanyama wasio na uti wa mgongo kwa mfano, panzi, konokono na minyoo.
 • Uti wa mgongo ni muunganiko wa pingili za mifupa inayoanzia kisogoni hadi sehemu ya chini ya kiuno. Kwa wanyama wenye mkia, pingili hizi hushuka hadi mkiani.
 • Ndani ya pingili za mifupa ya uti wa mgongo, kuna kiini au ugwemgongo ambao ni mwendelezo wa ubongo. Ubongo na sehemu hii ya ugwemgongo ndio hufanya mfumo wa fahamu. Pia, hufikisha taarifa katika sehemu mbalimbali za mwili kupitia neva.

Wanyama wasio na uti wa mgongo

 • Hili ni kundi kubwa sana is wanyama ikilinganishwa na kundi is wanyama wenye uti wa mgongo. Takribani wanyama wote ni wanyama wasio na uti wa mgongo.
 • Mfano wa wanyama hao ni panzi, jongoo, kipepeo, minyoo, mende, konokono, tegu na pweza. Wanyama hawa wanapatikana katika mazingira ya nchi kavu na majini. Ukichunguza katika sehemu unayoishi utagundua kwamba kila mahali wanyama hawa wapo.

Wanyama hawa wasio na uti wa mgongo wamegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:

 1. athropoda,
 2. minyoo
 3. konokono na ngisi.
 • Mifano ya wanyama wa kundi la athropoda ni kaa, panzi, buibui, tandu na jongoo. Hawa wote wana miguu iliyogawanyika katika pingili zilizounganishwa.
 • Kundi la pili ni la minyoo ambao wengine huishi mwilini mwa wanyama kama vile binadamu, baadhi yao huishi majini na wengine kwa mfano nyungunyungu huishi kwenye udongo.
 • Kundi la tatu ni la konokono na ngisi. Baadhi ya wanyama katika kundi
  hili, kwa mfano konokono, huishi nchi kavu. Kuna baadhi ya konokono ambao huishi ndani ya maji. Jamii nyingine ya kundi hili kwa mfano ngisi huishi baharini.

Wanyama wenye uti wa mgongo

 1. Wanyama wenye uti wa mgongo wamegawanyika katika makundi matano ambayo ni: samaki, amfibia, reptilia, ndege na mamalia.
 2. Makundi haya yana sifa maalumu zinazotofautisha kundi moja na lingine kama ifuatavyo:

Samaki

 1. Kuna aina mbalimbali za samaki na wote wanaishi ndani ya maji. Kuna kundi la samaki wanaoishi katika majichumvi. Mfano wa samaki hawa ni papa. Samaki wengine kama vile sangara na kambale huishi katika maji yasiyo na chumvi.
 2. Kuna samaki wenye magamba, kwa mfano perege na wasio na magamba kama vile kibua. Pia, samaki wanaweza kugawanyika katika makundi makuu mawili, ambayo ni samaki wenye mifupa migumu kwa mfano perege na wale wenye mifupa laini kama vile papa.

Sifa za wanyama katika kundi la samaki

 • Samaki wana damu baridi. Hivyo joto la mwili hubadilika kulingana

na mazingira.

 • Baadhi ya samaki milli yao imefunikwa kwa magamba yaliyopandana kuelekea mkiani.
 • Upande wa ubavuni mwa samaki kung mstari wa neva unaowasaidia kuhisi miguso na mielekeo ya mawimbi ya maji.
 • Samaki wana mapezi wanayotumia kuogelea na kubadili mwelekeo na mwendo.
 • Samaki hutumia matamvua yaliyofunikwa kwa gamba gumu Iiitwalo
  opekyulamu kupata oksijeni iliyo kwenye maji.
 • Umbile la samaki limechongoka kwa upande wa mbele iii kumsaidia
  kujongea kwa urahisi ndani ya maji.
 • Samaki huzaliana kwa kutaga mayai.
 • Juu ya mwili wa samaki kuna ute unaoteleza iii kumsaidia kupunguza
  ukinzani anapojongea.

Amfibia

 • Kundi hill Ia wanyama huishi majini katika hatua za awali za ukuaji. Mfano wa wanyama katika kundi hill ni chura. Kuna aina mbili za chura; chura ambao huishi kwenye maji na chura wanaoishi nchi kavu. Chura hutaga mayai ndani ya maji yasiyo na chumvi. Mayai yakianguliwa hutoa lava ambao huishi ndani ya maji wakipumua kwa kutumia matamvua. Lava wakiwa wakubwa, miguu huota na mapafu kukua. Katika hatua hii, chura huhamia nchi kavu.

Sifa za wanyama katika kundi la amfibia

 1. Amfibia wana ngozi laini yenye unyevu inayotumika katika kupumua.
 2. Viwambo vya masikio vilivyo pande zote mbili za kichwa nyuma kidogo ya macho huwawezesha kusikia.
 3. Amfibia wana matamvua katika hatua za awali za ukuaji: yaani lava na huwasadia katika kupumua. Wakikua hutumia mapafu na ngozi.
 4. Amfibia wana dame baridi, hivyo, halijoto ya mwili wa amfibia hubadilika kulingana na halijoto ya mazingira. Tabia hii huitwa poikilothernia.
 5. Amfibia wana miguu minne, miguu ya mbele ni mifupi na miguu ya nyuma ni mirefu.
 6. Kila mguu wa amfibia una vidole vitano vilivyounganishwa na ngozi

nyembamba.

 1. Amfibia hutaga mayai ndani ya maji, isipokuwa baadhi ya amfibia, kwa mfano, vyura wa Kihansi, ambao huzaa.
 2. Amfibia wana midomo mipana inayowawezesha kuingiza chakula kinywani kwa haraka na kwa urahisi.

Reptilia

Kundi hill linajumuisha wanyama wanaoishi nchi kavu na wanaoishi kwenye maji. Mifano ya reptilia wanaoishi nchi kavu ni mjusi, nyoka, kobe na kinyonga. Mifano ya reptilia wanaoishi maji6i na nchi kavu ni mamba kasa, baadhi ya nyoka na kenge. Baadhi ya wanyama katika kundi hill, kama vile mjusi na kenge wana miguu. Hata hivyo. wengine kama vile nyoka, hawana miguu na hujongea kwa kutambaa.

Sifa za wanyama katika kundi la reptilia

 1. Ngozi ya reptilia ni kavu na imefunikwa na magamba.
 2. Reptilia wengi wana milli iliyochongoka kuanzia kichwani hadi mkiani. Pia, mikia yao ni mirefu na miembamba.
 3. Baadhi ya reptilia, kwa mfano, nyoka, hawana miguu. Hawa hujongea

kwa msaada wa misuli ya tumbo na mnyumbuko wa mbavu na mwili kwa ujumla.

 1. Reptilia wengine, wana miguu yenye vidole vitano vilivyo na kucha, ambavyo huwasaidia kujongea.
 2. Midomo ya reptilia wengi ni mipana na imechongoka.
 3. Reptilia hutaga mayai.
 4. Halijoto ya milli yao hubadilika kulingana na halijoto ya mazingira, hivyo huitwa poikilothemia.
 5. Reptilia hutumia mapafu kwa ajili ya kupumua.

Ndege

Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo na manyoya. Baadhi ya ndege hufugwa na wengine huishi porini. Mifano ya ndege wafugwao ni kuku, bats, njiwa, kanga na kasuku. Mifano ya ndege waishio porini ni mwewe, bunch,. kunguru na mbuni. Ndege wengi huishi nchi kavu, ila baadhi yao huishi kwenye mail.

Sifa Za Wanyama Katika Kundi La Ndege

 1. Mwili wa ndege umechongoka nyuma na mbele. Umbo bib humsaidia

kuruka hewani bila kupata ukinzani mkubwa wa hewa. Sehemu ya katikati ya kiwiiiwili ni pana zaidi kuliko sehemu ya kichwa na mkia.

 1. Mwili wa ndege umefunikwa kwa manyoya ambayo humsaidia kuhifadhi joto Ia mwili. Pia, manyoya yanateleza III kuzuia maji yasiifikie ngozi.
 2. Ndege wana mabawa yenye manyoya marefu yanayomwezesha kuruka hewani. Hata hivyo, wapo ndege wasioruka. Hawa ni pamoja na pengwini, mbuni na kiwi.
 3. Mdomo wa ndege ni mgumu na umechongoka. Ndege wengine wana midomo mirefu na wengine wana midomo mifupi yenye ncha kali.
 4. Ndege wote wana miguu miwili yenye magamba na kila mguu una vidole vinne vyenye kucha ngumu.
 5. Joto la mwili wa ndege halibadiliki kulingana na mabadiliko ya halijoto ya mazingira. Hall hii huitwa homeothemia. Halijoto ya mwili wa ndege ni wastani wa nyuzi joto 40 za sentigredi.
 6. Ndege huzaliana kwa kutaga mayai.
 7. Ndege wengi hujongea kwa kuruka. Wepesi wa mifupa yao huwasaidia kuruka.

Mamalia

Mamalia ni kundi la wanyama wenye uti wa mgongo ambao huzaliwa wakiwa viumbe kamili. Milli ya mamalia ina vinyweleo ambavyo wingi wake hutofautiana miongoni mwao. Mamalia wengi huishi nchi kavu. Hutumia miguu miwili au minne kujongea. Wapo wanaoruka, kwa mfano popo. Wengine wanaishi ndani ya maji, kwa mfano nyangumi. Mifano ya mamalia ni binadamu, popo, nyangumi, panya, tembo, mbwa, punda, simba, farasi, pundamilia, chui, kangaruu, ngiombe. mbuzi, nyani na kondoo.

Sifa za wanyama katika kundi la mamalia

 • Mamalia hunyonyesha watoto wao maziwa ambayo hukusanyika katika viwele vyao.
 • Mamalia wana masikio yaliyojitokeza na yenye eneo kubwa Ia kukusanya mawimbi ya sauti.
 • Milli ya mamalia ina vinyweleo vinavyowasaidia kutunza joto la mwili.
 • Ngozi ya mamalia ina tezi za jasho isipokuwa nyangumi anayeishi ndani ya maji.
 • Mamalia wengi huzaa watoto walio hai. Mamalia wachache sana hutaga mayai. Wengine huzaa watoto ambao hawajakomaa na kuwatunza katika mfuko maalumu, mfano ni kangaruu.
 • Mamalia wanatembea kwa miguu minne isipokuwa binadamu anatembea kwa miguu miwili na ana rnikono miwili.
 • Mamalia walio wengi huishi nchi kavu na baadhi yao huishi kwenye

maji. Mifano ya mamalia waishio kwenye maji ni nyangumi na pomboo.

 • Halijoto ya mwili wa mamalia haibadiliki kulingana na mabadiliko ya

halijoto ya mazingira. Mamalia wana uwezo wa kuweka halijoto ya milli yao katika kiwango kinachohitajika. Hivyo huitwa homeothemia. Hall hiyo humwezesha kuishi katika mazingira ya halijoto tofauti.

 • Mamalia hutumia mapafu kupumua.

UFUPISHO WA MADA.

 1. Viumbe hai wana sifa kuu saba, ambazo huwatofautisha na vitu vingine visivyo hai.
 2. Sifa hizi ni kula, kupumua, kuitikia vichocheo, kujongea, kuzaliana, ktoa takamwili, na kukua.
 3. Vimbe hai viko katika makundi mawili makuu-mimea na wanyama
 4. Mimea ipo katika makundi mawili-mimea inayotoa maua na mimea isiyotoa maua.
 5. Mimea inayotoa maua ipo katika makindi mawili- mimea aina ya monokotiledoni na mimea aina ya daikotiledoni.
 6. Sehemu kuu ya mimea ni pamoja na mizizi, shina,majani na maua na matunda.
 7. Wanyama wanaweza kuwekwa katika makundi kuu mawili, wanyama wenye uti wa mgongo, na wanyama wasio na uti wa mgongo.
 8. Wanyama wenye uti wa mgongo ni pamoja na samaki, reptilia, ndege, na mamalia.
 9. Wanyama wasio na uti wa mgongo ni konokono, nyungunyungu, na panzi.

www.learninghubtz.co.tz

VIUMBE HAI : MTIHANI WA MWISHO WA MADA

SEHEMU A

CHAGUA JIBU SAHII

1………….Huruka juu kwa mabawa yenye manyoya

 1. Ndege
 2. Popo
 3. Mbu
 4. Kipepeo
 5. Panzi

2. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?

 1. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini.
 2. Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
 3. Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
 4. image001Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
 5. Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.

3. Kundi lipi limeainisha wanyama wenye uti wa mgongo?

 1. Konokono, mjusi na kenge
 2. Papasi, panzi na mbungo
 3. Chura, mamba na mchwa
 4. Kuku, popo na bata
 5. Nyoka, panzi na mbuzi

4. …………..hutaga mayai majini hata kama yeye huishi nchi kavu

 1. Kobe
 2. Kasa
 3. Chura
 4. Mamba
 5. Nyangumi

5…………………huishi majini lakini hutaga mayai yake nchi kavu

 1. Papa
 2. Kobe
 3. Mjusi
 4. Kasa
 5. Mamba

6……………ni mammalian lakini hana tezi za jasho

 1. Popo
 2. Nyangumi
 3. Mbwa
 4. Panya
 5. Sungura

7. ………………hunatoa mbegu lakini hautoi maua

 1. Mchungwa
 2. Mvinje
 3. Mhindi
 4. Mwembe
 5. Mpera

SEHEMU B.

8. Oanisha maneno katika sehemu A na Maelezo sahii kutoka sehemu B.

Sehemu A

Sehemu B

 1. Mende
 2. Samaki
 3. Mbwa
 4. Ndege
 5. Mwerezi
 6. Poikilothemia
 7. Nyoka
 8. Amfibia
 9. Monokotiledoni
 10. Daikotiledoni.
 1. Hulea kwa kunyonyesha watoto wao.
 2. Halijoto la mwili kubadilika kulingana na hali joto za mazingira.
 3. Mahindi na maharage
 4. Tembe
 5. Mbegu zenye ghala moja
 6. Hutumia matamvua kwa ajili ya kupumua
 7. Mbegu yenye ghala mbili
 8. Mmoja kati ya wanyama wasio na uti wa mgongo
 9. Hupumua kwa ngozi yenye unyevu
 10. Kundi pekee la wanyama wenye manyoya
 11. Reptilia wasio na miguu
 12. Mmea usitoa maua
 13. Kotiledoni tatu

SEHEMU C

Andika kweli au si kweli kwa sentensi iliyo sahihi na isiyo sahihi mtawalia.

 1. Wanyama aina ya ndege ndio pekee wenye damu baridi………………..
 2. Chura akizibwa pua anakufa………………………………
 3. Binadamu na panya wote wapo kwenye kundi moja…………..
 4. Mamba yupo katika kundi la mamalia…………………
 5. Popo ni ndege kwa kuwa anaruka……………………
 6. Ndege wote wana manyoya……………………..
 7. Kuna haina ya chura wanaozaa watoto hai bila kutaga mayai…………..
 8. Mamalia wote wanaishi nchi kavu………………………………………….
 9. Reptlia na amfibia wana damu baridi…………………………..
 10. Minyoo na mbu hawana uti wa mgongo.

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256