SAYANSI DARASA LA TANO : SURA YA PILI

USANISHAJI CHAKULA

MSAMIATI

  1. Epidemisi- seli za gamba la nje katika mimea au wanyama
  2. Floemu- mirija myembamba ambayo husafirisha chakula kutoka kwenye jani kwenda sehemu mbalimbali za mmea kwa
  3. Ni muhimu kutambua kuwa wanyama hawana uwezo wa kutengeneza chakula chao. Tofauti na wanyama, mimea ina uwezo wa kujitengenezea chakula.
  4. Kitendo cha mmea kujitengenezea chakula huitwa usanishaji wa chakula au fotosinthesisi. Usanishaji wa chakula hufanyika katika sehemu maalumu ya mmea.
  5. Katika sura hii, utajifunza sehemu ya mmea inayofanya kitendo cha usanishaji.
  6. Pia, utajifunza namna mmea unavyoweza kujitengenezea chakula kwa kutumia hewa ya kabonidayoksaidi, maji na nishati ya mwanga wa jua.


SEHEMU KUU ZA MIMEA.

Mimea ina sehemu kuu tatu. Sehemu hizo ni mizizi, shina na majani. Usanishaji wa chakula hufanyika katika majani.

Sehemu za nje za jani

Sehemu kuu za nje za jani ni ncha, kikonyo, vishipa jani, kingo ya jani, lamina na vena kuu.

Angalia na chunguza sehemu za nje za jani, kisha soma kwa makini maelezo yanayofuata.

leaf-1

Kazi ya sehemu mbalimbali

  1. Kikonyo- huunganisha jani na shina au tawi la mmea. Pia, huunganisha vena kuu na vishipajani. Kazi za kikonyo, vena kuu na vishipajani ni kusafirisha maji, madini na virutubisho kutoka kwenye shina kwenda kwenye jani na kusafirisha chakula kilichotengenezwa na jani kwenda kwenye shins na sehemu nyingine za mmea.
  2. Lamina- ni sehemu laini ya jani. Sehemu hii ina seli zenye kloroplasti. Kloroplasti zina dutu zinazoitwa chanikiwiti au umbijani. Chanikiwiti au umbijani ni dutu zinazohusika na usanishaji wa chakula. Vilevile, lamina in vishimo vidogovidogo vinavyoitwa stomata. Kazi ya stomata ni kupitisHa hewa ya oksijeni, hewa ya kabonidayoksaidi na maji katika hali ya mvuke

Sehemu za ndani za jani

  • Jani likikatwa mshazari na kuangaliwa kwa kutumia hadubini huonesha sehemu kama epidemisi ya juu, selisafu za kati na epidemisi ya chini.

Chunguza kielelezo namba 2, kisha soma kwa makini maelezo yanayofuata.

leaf-structure-9-638

Epidemisi ya upande wa juu na wa chini wa jani

  1. Sehemu za ndani za jani hulindwa na utando pamoja na epidemisi za upande wa juu na chini ya jani. Utando wa chini na juu wa jani, pamoja na epidemisi, ni angavu.
  2. Hivyo, husaidia mwanga wa jua kupenya na kuingia kwenye sehemu za kati ya jani. Utando na epidemisi ya chini ya jani una vishimo vidogovidogo vinavyoitwa stomata.

Seli safu ya kati

  1. Sell hizi zipo katikati ya epidemisi ya upande wa juu na wa chini wa jani. Seli safu ya kati ina sehemu kuu tatu. Sehemu hizi ni sell, nafasi ya hewa na vifereji vipitishi, yaani zailemu na floemu.
  2. Baadhi ya sell hizi zina kloroplasti ambazo hubeba chanikiwiti au umbijani. Nafasi za hewa zinasaidia kutembea kwa kabonidayoksaidi kwa ajili ya usanishaji chakula na oksijeni baada ya usanishaji chakula.
  3. Vifereji vipitishi husafirisha maji na virutubisho kwenda kwenye sehemu zote za jani na kutoa chakula kilichotengenezwa kwenye jani kwenda sehemu nyingine za mmea kwa matumizi na uhifadhi.

Usanishaji chakula

  1. Mimea ina uwezo wa kutengeneza chakula chake Hi iweze kuishi. Kitendo hicho huitwa usanishaji chakula au fotosinthesisi.
  2. Kitendo hicho hufanyika katika sehemu ya jani yenye sell zenye kioroplasti. Umbijani au klorofili zilizomo ndani ya kioroplasti husharabu nishati ya mwanga wa jua.
  3. Hivyo, mmea hutumia maji, hewa ya kabonidayoksaidi pamoja na nishati ya mwanga wa jua katika umbijani iii kutengeneza chakula aina ya kabohaidreti au wanga.

Kitendo chote cha usanishaji chakula kinaweza kufupishwa kwa kutumia kanuni hii:

Maji + kabonidayoksaidi +mwanga wa jua +umbijani kabohaidreti +oksijeni

  1. Mahitaji muhimu ya mmea katika kujitengenezea chakula, hupitia njia mbalimbali zikiwemo mizizi na majani.
  2. Kwa mfano, mizizi ya mmea ina vinyweleo ambavyo hutumika kusharabu maji yaliyoko kwenye udongo. Kisha, maji kayo husafirishwa hadi kwenye majani kwa ajili ya usanishaji.
  3. Vilevile, maji hupelekwa katika sehemu mbalimbali za mmea.


Kielelezo namba mizizi

Kuchunguza jinsi mimea inavyosharabu maji.

Fuata yafuatayo;

Mahitaji;

  • Bika 3
  • Maji yenye rangi 3
  • Mashina matatu ya seleri
  • Spinachi au mmea wa aina hiyo.

Hatua

1. Chukua bika 3 na kila bika weka maji yenye rangi tofauti ndani yake.

2. Chukua mashina 3 ya seleri, kisha tumbukiza ndani ya bika zenye maji ya rangi. Angalia kielelezo namba 5

3. Subiri mabadiliko kwa muda wa saa sita au zaidi kisha chunguza matokeo.

4. Kama hakuna matokeo ya wazi kata wima au ulalo shina la mmea na chunguza ndani.

Baada ya muda utagundua kua shina la mmea wa seleri limebadilika rangi. Hii inadhihirisha kuwa mmea husharabu maji.

Mmea unavyopata hewa na mwanga.

Majani hupitisha hewa ya kabonidayoksaidi kupitia kwenye stomata. Wakati wa mchana, stomata hufunguka iii ziingize hewa ya kabonidayoksaidi na wakati wa usiku, stomata hujifunga.

image

Kielelezo namba mizizi

Majani ya mimea yana umbijani ambayo husharabu nishati ya mwanga wa jua

Kuhifadhiwa kwa chakula kwenye mmea

  • Baada ya usanishaji chakula kukamilika, chakula husafirishwa kupitia vifereji vipitishi viitwavyo floemu hadi kwenye sehemu mbalimbali za mmea.
  • Chakula hicho huhifadhiwa kwenye mizizi, shina, majani na mbegu. Mazao kama mihogo na viazi vitamu huhifadhi chakula katika mizizi.
  • Mazao kama mahindi, ngano na maharage huhifadhi chakula kwenye mbegu. Vilevile, mazao kama miwa, magimbi, karoti na tangawizi huhifadhi chakula katika shina.

image

Kielelezo namba mizizi

Umuhimu wa usanishaji chakula

  1. Usanishaji wa chakula husaidia kupatikana kwa chakula kwa ajili ya viumbe hai.
  2. Mmea hutengeneza chakula kupitia usanishaji na hivyo kuendelea kukua. Chakula hicho ndicho kinacholiwa na wanyama na binadamu. Kwa mfano; mihogo, viazi, ndizi na maharage ni matokeo ya usanishaji. Bila kitendo cha usanishaji chakula, wanyama na mimea wangetoweka.
  3. Usanishaji chakula ni njia ya asili ya kurudisha hewa ya oksijeni inayotumika wakati wa kupumua. Hewa hii ni muhimu kwa uhai viumbe.

4. Usanishaji chakula unasaidia katika kupunguza kiwango cha kabonidayoksaidi katika hewa na hivyo husaidia kuweka msawazo sahihi wa hewa.

Ufupisho wa mada.

  • Mimea ina sehemu tatu kuu, mizizi, shina na majani
  • Usanishaji chakula hufanyika kwenye mizizi
  • Sehemu za nje za jani ni kama vile, ncha, kikono,kingo,kishipajani,vena kuu, lamina, na kikonyo
  • Usanishaji wa chakula ufanyika katika sehemu ya ndani ya jani
  • Stomata inaruhusu hewa na maji kupita katika jani
  • Kitendo cha usanishaji chakula uitwa pia fotosinthesisi
  • Usanishaji chakula unahitaji, maji, kabonidayokisaidi, nishati ya mwanga na umbijani.
  • Umbijani husaidia kunasa nishati ya jua
  • Matokeo ya usanishaji chakula ni kabohidirati na oksijeni
  • Floemu ni mshipa inayosaidia kusafirisha chakula kutoka kwenye majani hadi kwenye sehemu ya kuhifadhi kama mizizi.

www.learninghubtz.co.tz

MTIHANI WA MWISHO WA MADA : USANISHAJI CHAKULA

SEHEMU A.

CHAGUA JIBU SAHII

1. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

  1. joto na unyevu
  2. unyevu na mwanga
  3. upepo na mwanga wa jua
  4. mawingu na upepo
  5. unyevu na upepo

2. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:

  1. mmea kukosa madini joto
  2. mmea kushindwa kusanisi chakula
  3. majani ya mmea kukauka
  4. majani ya mmea kuwa njano
  5. maj ani ya mmea kupukutika.

3. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:

  1. osmosis
  2. difyusheni
  3. msukumo
  4. mgandamizo
  5. mjongeo

4. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?

  1. Wadudu
  2. Mimea
  3. Wanyama
  4. Virusi
  5. Ndege

5. Ipi kati ya zifuatazo siyo kazi ya mizizi katika mimea?..............

  1. Kusharabu madini ya chumvi.
  2. Kusharabu maji
  3. kushikilia mmea
  4. Kutengeneza chakula cha mmea
  5. Kutunza chakula cha mmea

6. Gesi ipi hupunguzwa angani na mimea?..................

  1. Kabondioksaidi
  2. Oksijeni
  3. Haidrojeni
  4. Kabonimonoksaidi
  5. Naitrojeni

7. Ni mmea gani ya hizi hauifadhi chakula katika shina?

  1. Miwa
  2. Magimbi
  3. Viazi
  4. Karoti
  5. Tangawizi..

8. Katika jani, umbijani hupatikana kwa wingi wapi?

  1. Epidamisi ya juu
  2. Epidamisi ya chini
  3. Seli linzi
  4. Stomata
  5. Selisafu za kati

9. Ni sehemu gani ya jani yenye seli zenye kloroplasti?

  1. Kikonyo
  2. Lamina
  3. Kingo
  4. Kishipajani
  5. Vena kuu

10. Usanishaji chakula hufanyika katika sehemu gani kuu ya mimea?

  1. Mizizi
  2. Majani
  3. Shina
  4. Ua
  5. Jani

SEHEMU B.

Jaza nafasi zilizowazi.

  1. Taja mahitaji makuu yanayowezesha mmea kutengeneza chakula
  2. Kitendo cha mimea kuitengenezea chakula huitwa………………..
  3. Kabohaidrati hutengenezwa katika sehemu ipi ya jani la mmea?
  4. Vitundu vidogo vidogo vilivyo kwenye sehemu ya chini ya jani huitwa?
  5. Sehemu inayosharabu nishati ya mwanga katika jani ni….
  6. Matokea ya usanishaji chakula katika mmea ni ……………na …………………
  7. Hewa ipi hutumika katika usanishaji chakula…………………
  8. Taja mimea mitatu inayohifadhi chakula katika shina
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256