KISWAHILI DARASA LA III SUBJECT NOTES
SURA YA : 1  Sauti zinazounda maneno

Sura ya 01 : Sauti zinazounda maneno

Ukijifunza sura hii utaweza kusoma silabi na maneno yenye sauti za herufi gh, py, nz, sw, lw, ky, tw, ng’w, nyw nashw.

Huu ni mwendelezo wa sauti za herufi ulizojifunza darasa la pili.

Kusoma na kuandika maneno yenye sauti za herufi

gh, lw, py, nz, sw na tw.

Soma kwa sauti maneno haya.

(a) ghali (b) Kulwa (c) nzi (d) swali (e) twanga

(f) mpya (g) gharama (h) Kilwa (i) nzige (j) swala

(k) tweta (l) jipya (m) ghairi (n) Nzega (o) swaga (p) kutwa

(a) ghali (b) Kulwa (c) nzi (d) swali (e) twanga

(f) mpya (g) gharama (h) Kilwa (i) nzige (j) swala

(k) tweta (l) jipya (m) ghairi (n) Nzega (o) swaga (p) kutwa

Soma habari hii, kisha jibu maswali yanayofuata.

Darasa jipya

Neema na Kulwa ni marafiki. Wote wanasoma katika Shule ya Msingi Mkwajuni. Mwaka jana walikuwa darasa la pili. Mwaka huu wameingia darasa la tatu. Shule ya Msingi Mkwajuni ilifunguliwa wiki ya kwanza ya mwezi Januari. Siku ya kufungua shule wanafunzi wote walifika shuleni mapema. Walifanya usafi wa mazingira ya shule, kisha wakasimama mstarini.

Swaiba alikuwa mwalimu wa zamu. Aliwasalimia wanafunzi na kuwatakia heri ya mwaka mpya. Aliwaeleza kuwa kila mwanafunzi anapaswa kusoma kwa bidii. Aidha, anapaswa kuzingatia sheria za shule. Aliwaeleza wanafunzi kuwa vyumba vya madarasa vimebadilika. Wanafunzi waliokuwa darasa la kwanza mwaka uliopita, wataingia chumba cha darasa la pili.

Wanafunzi waliokuwa darasa la pili wataingia chumba cha darasa la tatu. Baada ya matangazo, wanafunzi waliingia madarasani.

Wanafunzi wa darasa la tatu walianza mwaka wakiwa na furaha. Kila mwanafunzi alikuwa na hamu ya kuanza kusoma katika darasa jipya. Walipoingia darasani, mwalimu wa darasa aliwaongoza kuchagua viongozi. Neema alichaguliwa kuwa dada wa darasa na Ghalibu kuwa kaka wa darasa.


Maswali

1. Rafiki yake Neema anaitwa nani?

2. Neema na rafiki yake wanasoma shule gani?

3. Nani alikuwa mwatimu wa zamu?

4. Kwa nini wanafunzi wa darasa la tatu watikuwa na furaha?

Zoezi la 1

1. Soma kwa sauti maneno yaliyokolezwa wino katika habari uliyosoma.

2. Unganisha sauti za herufi gh tw py nz sw tw na a e i o u kuunda silabi.

Mfano Ukiunganisha sauti ya herufi gh na sauti ya herufi a unaunda silabi gha

(a) gh a gha

(b) lw - -

(c) nz --

(d) sw --

(e) tw - -

3. Tenganisha silabi zilizounda maneno.

Mfano

 • wanafunzi wa na fu nzi
 • waliaswa wa li a swa
 1. walianza
 2. jipya
 3. anapaswa

4. Tenganisha sauti za herufi katika sitabi.

Mfano : pya - py a

 1. swa
 2. nzu
 3. ghi
 4. lwa
 5. twe

1. Soma maneno yafuatayo kwa sauti.

(a) ghala (b) ghorofa (c) funza (d) kwanza (e) panzi (f) rut (g) kanzu (h) kitanzi
(i) nzige (j) swati (k) sweta (l) swata (m) mswaki (n) jipya (o) mpya (p) upya (r) Kilwa (s) Kulwa (t) twanga (u) tweta (v) twiga (w) twisha (y) patwa (z) kutwa

Zoezi la 3

Soma sentensi zifuatazo kwa sauti.

(a) Mwalimu amewauliza wanafunzi maswali.

(b) Baba amenunua nguo kwa bei ghali.

(c) Mwanafunzi ameanza kwenda shuteni.

(d) Huu ni mwaka mpya.

(e) Mjomba amejenga nyumba ya ghorofa.

(f) Kilwa ni mji mzuri.

(g) Kaka yake Kulwa anaitwa Mpetwa.

Zoezi la 4

Tunga sentenst mbiti kwa kila neno.

(a) mpya (b) ghati (c) swati (d) nzuri (e) Kutwa

Soma mazungumzo kati ya Sungura na Chui, kisha fanya mazoezi.


Sungura Habari za leo kaka Chui.

Chui Nzuri!

Sungura Leo umekunywa maji?

Chui Sijanywa maji.

Sungura Ooh! itabidi nimuagize Pweza atuletee maji kutoka baharini, "Leo bahari ni shwari".

Chui Hapana! Kuna binadamu anayeitwa Ng'wale anauza maji.

Sungura Inaonekana humpendi Pweza.

Chui Si kweli! Sina uadui na Pweza.

Sungura Nafikiri tuwaache wote. Tuagize maji kutoka kwa Kyando.

Chui Nakubaliana na wewe. Maji anayouza Kyando ni safi sana.

Sungura Kweli! Itabidi tununue hayo.

Chui Sawa mdogo wangu.

Zoezi la 5

Andika maneno yenye sauti za herufi zifuatazo kutokana na mazungumzo utiyoyasoma.

(a) ky (b) pw (c) ng'w (d) nyw (e) shw (f) nz

Zoezi la 6

1. Tafuta maneno yenye sauti za herufi nyw shw pw nz tofauti na mazungumzo utiyosoma.

Mfano

 • nyw - nywele
 1. shw -
 2. pw -
 3. nz -

2. Soma kwa sauti silabi hizi.

(a) pwa (b) kya (c) ng'wa (d) pwi (e) nywa (f) shwi (g) kye (h) shwa (i) ng'wi (j) Kyo (k) ng'we (() nywe

3. Soma kwa sauti sentensi hizi.

(a) Bibi yangu anaishi Kyela.

(b) Baba anapenda kula pweza.

(c) Mzee Ng'wandu amejenga nyumba nzuri.

(d) Hali ya bahari ni shwari.

Zoezi la 7

Andika maana za maneno yafuatayo kwa kuchagua jibu sahihi.

Mfano shwari — hali ya ututivu.

Maneno Maana
 1. shwari
 2. ghali
 3. pweza
 4. kitanzi
 5. uadui

(i) kamba au uzi utiofungwa kwa duara

(ii) yenye bet kubwa

(iii) halt ya kutendeana ubaya baina ya watu

(iv) kiumbe wa baharini

(v) hali ya ututivu

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256