Sura Ya 2 : Matamshi Ya Herufi

Katika sura hii utajifunza kutamka, kusoma na kuandika maneno yenye sauti za herufi s na th, z na dh, t na r, g na gh kwa usahihi.

Kutamka maneno yenye sauti za herufi s na th kwa usahihi.

Tazama picha na namba zifuatazo, kisha fanya zoezi tinatofuata.

Zoezi la 1

1. Tamka majina ya vita unavyoviona katika picha namba 1 hadi 5.

2. Tamka kwa sauti namba 80 na 30

3. Taja sauti ya mwanzo inayosikika unapotamka maneno samaki, sabuni, sarafu na saa.

4. Taja sauti ya mwanzo inayosikika unapotamka namba 80 na 30.

Zoezi la 2

Soma maneno yafuatayo kwa sauti.

(a) saa (b) sahani (c) subiri (d) soko (e) safari (f) sabuni (g) saruji (h) msumari (i) usafi (j) pasi (k) fenesi (t) msusi (n) thetathini (n) themanini (o) thamani (p) thubutu (r) theluji (s) urithi

Zoezi la 3

Nakili sentensi zifuatazo katika daftari tako. Kisha chagua neno sahihi kwa kupigia mstari.

  • Mfano (Samaki, thamaki) ni chakula bora.

(a) Mimi ninaoga kwa kutumia maji safi na (sabuni, thabuni)

(b) Tuna anaishi karibu na (thoko, soko).

(c) Mwanafunzi mtiifu amepata alama (semanini, themanini).

(d) Mimi ninapenda kuta (fenesi, fenethi).

(e) Bibi huosha (sahani, thahani) kabla ya kuweka chakula.

Kutamka maneno yenye sauti za herufi z na dh kwa usahihi

Tazama picha zifuatazo kisha fanya zoezi

Zoezi la 4

1. Tamka majina ya vitu unavyoviona katika picha namba 1 na 2.

2. Taja sauti ya mwanzo inayosikika unapotamka maneno haya.

(a) zawadi zutia zahanati zeze zao zabibu

(b) dharau dhaifu dhoofu dhoruba

Zoezi la 5

Soma kwa sauti maneno haya.

(a) ziwa (b) mnazi (c) zeze (d) zizi (e) zuia (f) nazi (g) zito (h) zamani (i) mzazi (j) maziwa (k) dhoofu (l) dharura (m) madhara (n) dhahabu (o) adhabu (p) dhambi (r) dhuru (s) dhuluma (t) dhoruba (u) dharau

Zoezi la 6

Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kuchagua neno sahihi.

Mfano Dhahabu hupatikana Tanzania. (zahabu, dhahabu)

1. Mimi ninapenda kupiga . . . . . . . . (dheze, zeze)

2. Gunia litilojaa viazi ni . . . . . . . . . . (dhito, zito)

3. Pamba ni . . . . . . . . . la biashara. (zao, dhao)

4. Mama alisema kuwa kuiba ni . . . . . . . . (dhambi, zambi)

5. Tuma alikwenda kuwatembelea . . . . . . . . wake. (wadhazi, wazazi)

Kutamka maneno yenye sauti za herufi l na r kwa usahihi.

Soma kwa sauti maneno haya.

(a) ladha (b) lazima (c) Linda (d) lain (e) lami (f) elea (g) lima (h) mali (i) Liza (j) alika (k) kalia (L) koroboi (m) barabara (n) ridhia (o) redio (p) rika (r) jeraha (s) raba (t) robo (u) rudi (v) bure (w) roho (y) ruhusa (z) riadha

Zoezi la 8

Tazama picha zifuatazo, kisha tunga sentensi mbili kwa kilo picha.

Mfano

1. Huu ni mlango.

2. Nyumba yetu ina mlango mzuri.

Zoezi la 9

I. Andika maneno yafuatayo kwa usahihi.

Mfano zuli — zuri

(a) bule . . . . . . . (b) ria . . . . . . .

(c) rami . . . . . . . . (d) ledio . . . . . . . . . .

(e) luhusa . . . . . . . . .

(f) balabala . . . . . . . . . .

(g) loho . . . . . . . . . (h) jelaha . . . . . . . . .

2. Soma kwa sauti maneno uliyoandika katika swali la kwanza.

Kutamka maneno yenye sauti za herufi g na gh kwa usahihi.

Soma kwa sauti maneno haya

(a) gari (b) gauni (c) ugali (d) fagio (e) gego (f) gitaa (g) goti (h) gunia (i) guta (j) ugua (k) ghali (I) ghala (m) lugha (n) ghorofa (o) gharama

Zoezi la 11

Taza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia herufi g au gh. Kisha soma kwa sauti maneno haya.

(a) —ari (b) — ali

(c) lu — a (d) —unia

(e) —ogo (f) —arama

(g) u — ua (h) —ala

(i) —asia (j) — oti

(k) — itaa (t) — orofa

1. Nakili jedwali la maneno yafuatayo katika daftari lako. Kisha weka alma ya vema ( ✔ ) kwa kila neno sahihi na kosa ( ✖ ) kwa neno lisilo sahihi.

samaki gorofa dhambi ruka
zawadi subiri thoko ziwa
saruji sabuni gali sukari
dhiwa ledio lugha dhulumu
thamaki ulithi rara luhusa

2. Orodhesha maneno yote yasiyo sahihi kutoka katika jedwali la swali la kwanza. Yaandike maneno hayo kwa usahihi.

Mfano ledio — redio

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256