SURA YA PILI

KUPENDA NA KUJIVUNIA SHULE YAKO

Msamiati

  • Hisani- tabia ya kupenda kumtendea mema mtu
  • Mnada- tukio la kuuza vitu kwa kushindanisha bei
  • Rasimu- andiko la mwanzo kabisa la jambo
  • Siha- hali ya kuwa na afya bora

Kushiriki katika kuleta maendeleo ya shule yako

  • Kila mtu anatakiwa kushiriki katika kuleta maendeleo kwenye jamii yake.
  • Shule ni sehemu ya jamii, hivyo ni muhimu mwanafunzi kushiriki katika kuleta maendeleo ya shule yake.
  • Mwanafunzi anaweza kushiriki kuleta maendeleo katika shule yake kwa kufanya yafuatayo:
  • Kulinda mali za shule kama vile vitabu, madarasa, vyoo na ofisi za walimu; samani na vifaa vya kufanyia usafi kama vile, majembe, mafyekeo, mapipa ya kuhifadhi takataka na fagio;
  • Kushiriki kufanya usafi wa mazingira ya shule;
  • Kushiriki shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule, kwa mfano, kusomba matofali na mchanga na kusafisha eneo au sehemu jengo linapojengwa;
  • Kushiriki kutoa maoni na mapendekezo kwa uongozi wa shule juu ya mambo yanayoweza kuisaidia shule kitaaluma na kijamii, na
  • Kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri mitihani ya ndani na nje ya shule kwa lengo la kuitangaza shule.

Vitu vinavyohitajika kwa ajili ya maendeleo ya shule

  • Yapo mahitaji muhimu ambayo yanatakiwa yawepo iii kuiwezesha shule kufanya vizuri na kupata sifa katika jamii na Taifa kwa ujumla.
  • Mahitaji haya huiwezesha shule kufanikisha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wake. Baadhi ya mahitaji ya shule ni pamoja na chakula, vifaa, maji, umeme, ardhi na fedha.

Chakula:

  • Shule inahitaji chakula iii kuwafanya wanafunzi na walimu kuwa na siha njema.
  • Aina za vyakula vinavyohitajika ni kama vile mchele, unga, mafuta, sukari, maharage, nyama, matunda na mboga za majani.
  • Vyakula hivi vikipatikana utendaji kazi wa walimu na wanafunzi huimarika.

Vifaa:

  • Shule inahitaji vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, chaki, manila na karatasi kwa ajili ya kuchapishia mitihani na nyaraka nyingine.
  • Pia, huhitaji vifaa vya kufanyia usafi kama vile fagio, fyekeo, majembe, mapanga na mapipa ya kuhifadhi takataka.
  • Vilevile, vifaa vya michezo vinavyohitajika ni mipira ya kuchezea, nyavu za magoli na nguo za michezo.
  • Aidha, shule inahitaji baadhi ya vifaatiba na inaweza kuhitaji vifaa vya malazi.

Maji:

  • Shule inahitaji maji safi na salama kwa afya ya walimu na wanafunzi na shughuli nyingine za maendeleo.
  • Maji yanahitajika kwa ajili ya kunywa, kupikia, kumwagilia maua, bustani na miti.
  • Pia, maji yanahitajika kwa ajili ya shughuli za ujenzi, na kufanya usafi kama vile kusafishia vyoo, madarasa, kufua nguo na kuoga.

Umeme:

  • Shule inahitaji umeme kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Umeme
    unahitajika kusaidia wanafunzi wakati wa kujifunza hasa nyakati za usiku.
    Aidha, umeme unahitajika kuendesha mashine za kuchapisha na kurudufu nyaraka mbalimbali kama mitihani na kuimarisha shughuli za ulinzi wa shule
  • Umeme husaidia shule kutimiza lengo lake la kutoa elimu bora kwa wanafunzi mathalan, somo la Sayansi na Teknolojia Iitafundishwa na kueleweka vizuri kukiwa na huduma ya umeme.

Ardhi:

  • Shule inahitaji ardhi ya kutosha kuwezesha shughuli mbalimbali kufanyika.
  • Ardhi husaidia kupatikana sehemu za kujenga miundombinu kama madarasa, ofisi za walimu, vyoo, maktaba na viwanja vya michezo mbalimbali.
  • Pia, ardhi husaidia wanafunzi kupata eneo la kulima mazao mbalimbali kwa ajili ya kujipatia chakula chao wenyewe.
  • Hivyo, kuwapo kwa ardhi ya kutosha huchochea maendeleo ya shule.

Fedha:

  • Shule inahitaji fedha iii iweze kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
  • Kwa mfano, shule inahitaji fedha iii iweze kuchapisha mitihani, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kujenga, na kukarabati miundombinu kama vile madarasa na vyoo.
  • Pia fedha huhitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla.
  • Mahitaji yaliyotajwa hapo juu yanaweza kupatikana kwa njia mbalimbali.
  • Baadhi ya njia hizo ni ruzuku kutoka Serikalini, michango ya wazazi au walezi, wanajumuiya pamoja na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Njia za kupata misaada ya kusaidia maendeleo ya shule

  • Uongozi wa shule unaweza kubuni njia mbalimbali za kutafuta misaada kutoka kwa wadau wa elimu.
  • Jambo muhimu la kuzingatia katika kutafuta misaada au michango kutoka kwa wadau ni kufuata sheria, kanuni na taratibu.
  • Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kutumiwa na shule kupata misaada:
  1. Kadi za michango kwa wadau wa elimu:
  • Uongozi wa shule unaweza kuandaa kadi za michango na kuzitumia kuomba misaada kwa wadau mbalimbali wa elimu.
  • Wadau wa shule ni pamoja na wazazi, viongozi wa Serikali katika ngazi za mitaa na Serikali kuu, taasisi binafsi, mashirika, wakulima na wafanyabiashara walioko jirani na shule.
  • Wadau wengine muhimu kwa shule ni wale watu waliosoma zamani katika shule hiyo.
  • Jambo la kuzingatia ni kwamba lazima Mwalimu Mkuu apate idhini ya kutafuta michango na misaada kutoka kwa viongozi wake.
  1. Harambee:
  • Uongozi wa shule unaweza kuandaa harambee kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, ofisi au vyoo.
  • Uongozi wa shule unaweza kualika viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na viongozi wa dini ill washiriki kwenye harambee.
  • Kupitia harambee hiyo, wageni waalikwa wanaweza kutoa misaada yao kwa njia ya fedha taslimu au vifaa kama mabati, nondo na saruji.
  1. Mnada:
  • Shule inaweza kuandaa mnada wa vitu mbalimbali ambavyo vitauzwa kwa watu.
  • Kwa mfano, shule inaweza kufanya mnada wa mazao kutokana na shughuli za kilimo shuleni.
  • Mazao kama mahindi, maharage na mifugo kama kuku, bata, ng'ombe, mbuzi na kondoo vinaweza kuuzwa kwa mnada na kuipatia shule fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kila siku.
  1. Chakula cha hisani:
  • Uongozi wa shule unaweza kukaribisha watu wenye nyadhifa mbalimbali kwenye jamii kama viongozi wa Serikali, asasi zisizo za kiserikali, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji kwa chakula cha hisani.
  • Baada ya kula chakula hicho, wageni hao hualikwa kuchangia fedha na mali kwa ajili ya kukamilisha jambo fulani.
  • Kwa mfano, kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu au ununuzi wa samani za shule.
  1. Wadau wa maendeleo ya elimu:
  • Uongozi wa shule unaweza kuwashawishi wadau wa maendeleo ya elimu au asasi zisizo za kiserikali ndani na nje ya nchi kutoa misaada mbalimbali kwa shule.
  • Wadau wanaweza kutoa fedha, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, vitendea kazi kama vile tarakilishi, fotokopia na vifaa vya ujenzi.
  • Baadhi ya shule nchini zimekuwa zikifadhiliwa na balozi za nchi mbalimbali kama Kanada, Swideni, Marekani, Uingereza pamoja na mashirika ya kitaifa na kimataifa.
  1. Kuhamasisha watu kujitolea nguvukazi:
  • Uongozi wa shule au mwanafunzi kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa wanaweza kuandaa mkakati wa kuhamasisha wananchi kujitolea nguvukazi katika kufanya shughuli mbalimbali za shule.
  • Wananchi wanaweza kuhamasika kujenga madarasa, maktaba, maabara, ofisi na vyoo kwa kujitolea nguvukazi.

(g) Michango ya hiari:

  • Uongozi wa shule unaweza kukaribisha watu binafsi kutoa michango ya hiari ili kuisadia shule kumudu uendeshaji wa shughuli za maendeleo.
  • Michango hii ya hiari inaweza kuwa fedha taslimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, chakula, malazi, vifaa vya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule.

Mpangokazi wa kujitolea ili kuiletea shule maendeleo

  • Mpangokazi wa kujitolea ni andiko lenye utaratibu maalumu wa jinsi ya kuratibu shughuli mbalimbali zinazofanyika bila malipo au kulazimishwa.
  • Ili kuwapo ufanisi katika kazi za kujitolea, inashauriwa mwanafunzi awe na mpangokazi wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya shule yake.
  • Mpangokazi huu waweza kuwa wa muda mfupi, yaani mwezi mmoja hadi mwaka mmoja au muda mrefu wa miaka miwili na kuendelea.
  • kupanda miti au kuwasaidia wanafunzi wenzake kufaulu vizuri mitihani.

Mpangokazi wa kujitolea unahusisha vipengele mbalimbali kama ifuatavyo:

(a) Malengo: Hili ni tamko la dhamira au dhumuni la kutekeleza jambo fulani shuleni. Katika kipengele hiki, mwanafunzi atabainisha lengo analotaka kufikia . kwa mfano lengo linaweza kuwa kuboresha Mazingira ya shule kwa kupanda miti au kuwasaidia wanafunzi wenzake kufaulu vizuri mitihani.

  1. Muda: Hiki ni kipengele kinachoonesha wakati utakaotumika kufikia lengo lililokusudiwa katika kazi ya kujitolea. Muda unaweza kuwa saa, siku, wiki, mwezi au mwaka. Kwa mfano, unaweza kukadiria muda utakaotumia kuwasaidia wanafunzi wenzako iii wote mfaulu Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba.
  2. Mahitaji: Kipengele hiki hubainisha watu, vitu au vifaa vitakavyotumika kutekeleza lengo ulilojiwekea. Kwa mfano, kama unataka kutembelea wagonjwa waliolazwa hospitali, itabidi kuainisha vitu au vifaa utakavyohitaji kuwapelekea wagonjwa. Kuainisha mahitaji kutasaidia kubuni mkakati wa kupata watu au vitu vitakavyotumika kufikia lengo lililokusudiwa.
  3. Utekelezaji: Kipengele hiki huonesha namna utakavyotekeleza kwa vitendo shughuli za kujitolea. Kipengele hiki ni muhimu kwa kuwa hubainisha mkakati wa utekelezaji wa shughuli za kujitolea shuleni. Kwa mfano, iii kuboresha mazingira ya shule yako kwa kujitolea, utahitajika kubainisha kazi au shughuli utakazozifanya ndani ya muda fulani iii kufikia kusudio la kuwa na mazingira bora shuleni.
  4. Tathmini: Katika kipengele hiki mwanafunzi hupima ni kwa kiwango gani malengo yamefikiwa kulingana na rasilimali na muda uliopangwa. Tathmini huonesha mafanikio na upungufu na sababu zilizosababisha kutotekelezwa kwa kipengele fulani. Kwa mfano, kama ulipanga kuwasaidia wanafunzi wenzako kufaulu vizuri mitihani shuleni, utapima iwapo lengo limefikiwa ndani ya muda uliopangwa. Kumbuka, kuna tathmini endelevu, ambayo hufanyika wakati utekelezaji unaendelea, na tathmini tamati, ambayo hufanyika mwishoni.

Hatua za kuandaa mpangokazi wa kujitolea

Ili kuleta maendeleo shuleni kwa shughuli za kujitolea ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

  1. Uchambuzi wa mahitaji: Katika hatua hii, mwanafunzi huchambua mahitaji muhimu iIl kufikia lengo alilokusudia. Kwa mfano, iii uweze kuwasaidia wanafunzi wenzako kufaulu vizuri mitihani, lazima uainishe mahitaji muhimu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza vizuri. Mahitaji muhimu yanaweza kuwa ni pamoja na vitabu, muda wa kutosha wa kujisomea, na mahali pa kusomea.
  2. Ukusanyaji wa taarifa: Mwanafunzi iii uweze kufikia lengo ulilokusudia utawajibika kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wenzako, walimu na wafanyakazi wengine kuhusu namna ya kukabiliana na tatizo fulani shuleni. Kwa mfano, kama lengo lako ni kuwasaidia wenzako kufaulu mitihani, unaweza kukusanya taarifa zinazohusu wanafunzi wenye kuhitaji kusaidiwa na wale wenye uwezo ili uwashirikishe katika kufikia lengo lako.

(c) Uandaaji wa rasimu ya mpangokazi: Katika hatua hii, mwanafunzi huandaa andiko au mapendekezo ambayo yanaweza kurekebishwa au kukubaliwa na wanafunzi wenzake na watu wengine. Hatua hii hurasimisha mpangokazi wa kujitolea na hivyo kuwezesha kuanza matayarisho ya utekelezaji. Aghalabu, matayarisho ya utekelezaji yatahusisha wanafunzi, walimu na viranja watakaokuwa wamechaguliwa kushiriki kusaidia utekelezaji wa kazi za kujitolea zilizopangwa.

Umuhimu wa mpangokazi

  • Mpangokazi husaidia kubainisha rasilimali zinazohitajika iii kutimiza lengo fulani.
  • Kupitia mpangokazi, mwanafunzi huweza kuwa na ufanisi katika kutekeleza mikakati aliyojiwekea ili kufikia lengo lake. Ufanisi huongezeka kwani kila jambo huwa limebainishwa vyema.
  • Pia, mpangokazi husaidia kuratibu kazi zilizopangwa kufanyika kwa wakati na kwa ustadi wa hali ya juu. Hubainisha ni nani na kwa muda gani atahusika katika kazi fulani.
  • Kwa mfano, kama lengo lilikuwa kulima mbogamboga shuleni, mpangokazi utaonesha watu watakaohusika kumsaidia mwanafunzi anayejitolea kulima bustani ya mbogamboga ikiwa ni pamoja na watakaohusika kumpatia vifaa kama majembe, mbolea na mbegu.
  • Vilevile, mpangokazi hurahisisha kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda uliopangwa na kwa gharama nafuu. Aidha, kupitia mpangokazi, mwanafunzi atabaini kazi au shughuli za kutekeleza kulingana na vipaumbele vilivyowekwa.
  • Mpangokazi husaidia kubaini ni jambo gani Iinapaswa kutekelezwa kabla ya jingine.
  • Hali kadhalika, kupitia mpangokazi ni rahisi kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli na malengo yaliyokusudiwa.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256