SURA YA PILI

MAENDELEO YABINADAMU NA ZANA ZA UZALISHAJI MALI

Dhana ya zana

 • Zana ni kifaa chochote ambacho hutumiwa na binadamu iii kumwezesha kufanya kazi zake za kila siku. Binadamu, kwa nyakati mbalimbali, ameweza kubuni na kutengeneza zana kama vile visu, mikuki, majembe, mashoka na vifaa vingine vingi.
 • Zana za kufanyia kazi zinaweza kutumika kulima, kukata, kufyeka, kuchonga, kujilinda, kusuka na kuwinda. Binadamu ameweza pia kubuni vyombo kama vikapu, vyungu na majokofu. Ubunifu na utengenezaji wa zana na vyombo mbalimbali umemwezesha binadamu kufanya kazi kwa ufanisi.
 • Binadamu huishi kwa kuchangamana na kukabiliana na mazingira yake iii kuyaboresha na kuishi maisha bora zaidi. Kwa hiyo, ubunifu, uundaji na utumiaji wa zana ndicho kigezo kinachomtofautisha binadamu na wanyama wengine.
 • Maendeleo ya binadamu yamebadilika kwa nyakati tofauti kutokana na zana alizotumia.
 • Malighafi inayotumika kwa wingi kutengeneza zana ndiyo inayokitambulisha kipindi husika. Kutokana na muktadha huo tunapata vipindi mbalimbali vya maendeleo ya binadamu ambavyo ni; Zama za Mawe, Zama za Chuma na Zama za Teknolojia ya kisasa ya kidijitali

Zama za Mawe

 • Binadamu alianza kutengeneza na kutumia zana kwa mara ya kwanza katika Zama za Mawe.
 • Alitumia zana hizo katika uwindaji wa wanyama na ndege, uchimbaji wa mizizi kuangua matunda kwa ajili ya chakula pamoja na kutengeneza mavazi yake. Kwa hiyo, Zama za Mawe zilianza mara binadamu alipoanza kutengeneza na kutumia zana za mawe.

Maendeleo katika Zama za Mawe

 • Binadamu wa kale aliishi duniani yapata miaka 3 000 000 Kabla ya kuzaliwa Kristo (K.K). Katika kipindi hicho, binadamu aliweza kujenga historia ya maisha yake hapa duniani.
 • Kwa uwezo wake wa kutumia akili, alivumbua mambo mengi iii kukabiliana na vikwazo ambavyovingekwamisha maendeleo yake. Mathalani, alibuni na kutengeneza zana za kuzalisha mahitaji yake ya msingi.
 • Mahitaji hayo ni chakula, makazi na mavazi. Uwezo wa kutengeneza zana sahihi na kuzitumia ndiyo unaomtofautisha binadamu na wanyama wengine waliomtangulia kama sokwe ambao wamekaa duniani kwa miaka 30 000 000 K.K. Historia inaonesha kuwa fuvu Ia kichwa cha binadamu wa kwanza liligunduliwa Kaskazini mwa Tanzania, wakati huo Tanganyika, katika Bonde Ia Olduvai mwaka 1959.
 • Mgunduzi wa fuvu hilo alikuwa ni mtaalamu wa akiolojia aliyeitwa Dkt. Louis Leakey na mkewe Dkt. Mary Leakey.
 • Katika kipindi hiki binadamu wa kale alitumia mawe kutengeneza zana za kufanyia kazi. Utumiaji wa mawe kutengeneza zana ulijulikana kama Zama za Mawe. Zama ni kipindi fulani cha wakati katika maisha.
 • Zama za Mawe zimegawanyika katika vipindi vitatu. Vipindi hivyo ni Zama za Mawe za Kale, Zama za Mawe za Kati na Zama za Mawe za Mwisho.

Zama za Mawe za Kale

 • Zama hizi zilidumu kuanzia miaka 3 000 000 K.K hadi miaka 300 000 K.K. Katika kipindi hiki, binadamu aliishi kwa upweke.
 • Watu walikuwa wachache sana na walikutana au kushirikiana kwa nadra. Kwa mfano, watu wachache walishirikiana kumfukuza mnyama hadi kumuua na kisha kula nyama yake.
 • Baada ya hapo kila mmoja alirejea kwenye makazi yake. Daima walikuwa wakihamahama kutafuta chakula, maji na sehemu za kujihifadhi.
 • Zana zao zilikuwa duni na za matumizi ya muda mfupi. Kwa mfano, binadamu aliokota jiwe au kipande cha mti na kuangua tunda. Vilevile, alitumia mfupa wa mnyama kuchimba mizizi na wadudu kwa ajili ya chakula.
 • Baada ya hapo alizitupa zana zake na kubeba mawindo ya mnyama, ndege, mizizi au matunda aliyoyapata.
 • Zana hizi zilitumiwa pia kufukuza au kupigana na wanyama wakali waliowashambulia binadamu kama simba na tembo.
 • Wakati ule binadamu alifanana zaidi na sokwe ama nyani. Mwili wake ulikuwa na nyweie nyingi na kichwa chake kilikuwa kidogo sana ukilinganisha na ukubwa wa mwili wake. Alitembea kwa mikono na miguu.
 • Hivyo, hakuweza kubeba zana kwa muda mrefu. Kadiri muda ulivyopita alianza kutengeneza zana kwa kuchonga mawe iii kupata ncha na umbo alilolitaka. Kielelezo namba 1 kinamwonesha binadamu wa Zama za Mawe za Kale akitengeneza Zana za Mawe.
 • Hii ilimwezesha kupata vipande vidogovidogo ama vyenye ncha kali vilivyowiana na malengo yake. Kielelezo namba 2 kinaonesha maumbo ya baadhi ya zana za kipindi cha Zama za Mawe za Kale.

Kielelezo namba 2: Zana za Zama za Mawe za Kale

Chunguza picha katika kielelezo namba 2. Kisha, wasilisha majibu yako darasani.

 1. Eleza kwa kifupi faida au manufaa unayodhani binadamu aliyapata kwa kutumia zana za mawe wakati wa Zama za Mawe za Kale.
 2. Bainisha changamoto unazodhani binadamu alizipata kwa kutumia zana kama hizo.

Masalia ya zana za Mawe za Kale

 • Masalia ya zana za Zama za Mawe za Kale yamegundulika katika sehemu nyingi za Tanzania. Baadhi ya maeneo hayo ni Bonde la Olduvai mkoani Arusha, Isimila mkoani Iringa, Bonde la Mto Kagera mkoani Kagera na katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma. Kielelezo namba 3 kinaonesha baadhi ya maeneo yenye masalia ya zana za Zama za Mawe na michoro ya kale iliyogunduliwa.
 • Vilevile, katika maeneo kadhaa nchini Tanzania, ipo michoro ya kale ya mapangoni iliyochorwa na binadamu wa enzi hizo. Michoro kama hiyo inaonekana hadi sass katika mapango ya Kondoa kama ilivyooneshwa kwenye ramani ya masalia ya zana za Zama za Mawe na michoro ya kale Napo juu.
 • Inadhaniwa kwamba michoro hiyo ilikuwa na malengo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwafunza watoto na vijana mambo muhimu katika jamii. Mfano, michoro hiyo ilionesha zana za kuwindia, mbinu za uwindaji, utamaduni wa jamii za kale na aina za wanyama katika mazingira yao. Kielelezo namba 4 kinaonesha baadhi ya michoro ya kale ya mapangoni iliyopo nchini Tanzania.


Zama za Mawe za Kati

 • Kipindi hiki kilidumu kuanzia miaka 300 000 K.K hadi 50 000 K.K. Ni kipindi kilichoambatana na mabadiliko makubwa katika maisha ya binadamu. Kwanza, binadamu alianza kutembea kwa miguu.
 • Mikono yake aliitumia kutengeneza vitu, kuokota, kushika na kutumia zana. Mabadiliko haya,aliambatana na mabadiliko muhimu mengine katika maumbile, mfano uwezo wa kufikiri na kufanya mambo mbalimbali.
 • Mathalani, tofauti na sokwe ambaye alitembelea miguu minne, mabadiliko ya kimaumbile yalimuwezesha binadamu wa Zama za Mawe za Kati kuanza kutembelea miguu miwili akiwa wima. Hivyo, aliweza kuona mawindo na maadui kwa mbali kuliko wakati alipokuwa akitembea kwa miguu na mikono.
 • Vilevile, uwezo wake wa kufikiri uliongezeka kadiri alivyokabiliana na mazingira yake. Kielelezo namba 5 kinaonesha jinsi maumbile ya binadamu yalivyoendelea kubadilika tangu alipoanza kutembea kwa miguu hadi sasa.

Kielelezo namba 5: Hatua mbalimbali katika mabadiliko ya binadamu


 • Pili, ustadi na kasi ya kutengeneza zana viliongezeka. Katika hatua hii, binadamu wa kale alibuni na kutengeneza kwa ustadi zaidi aina nyingiza zana.
 • Zana hizo zilikuwa bora, imara zaidi na za kufanyia kazi mahususi. Mifano ya zana hizo za Zama za Mawe za Kati ni mishale, uta, visu na shoka.
 • Katika kipindi hiki binadamu alianza pia kuvaa ngozi za wanyama zilizolainishwa na zile zilizotokana na magome ya miti baada ya kuyapondaponda na kuyalainisha.
 • Hata hivyo, aliendelea kuishi kwa kuhamahama na hakuwa na makazi ya kudumu. Kielelezo namba 6 kinaonesha baadhi ya mifano ya zana za Zama za Mawe za Kati.

Kielelezo namba 6: Baadhi ya zana za Zama za Mawe za Kati

Ugunduzi wa moto

 • Wakati binadamu akiboresha zana za mawe, binadamu aligundua moto, mwishoni mwa Zama za Mawe za Kati.
 • Moto ulitokea wakati akigongagonga na kusugua mawe iii kuyawekea umbo na makali aliyotaka. Mchakato huo ulizalisha cheche na moto ukawaka.
 • Kadiri muda ulivyopita binadamu alipata ujuzi na mbinu anuwai za kutengeneza moto. Njia mojawapo ilikuwa ya kupekecha vijiti viwili vikavu, ambapo kipekecheo huitwa ulindi na kipande kinachopekechwa huitwa uwimbombo. Kielelezo namba 7 kinahusu utengenezaji wa moto katika Zama za Mawe za Kati.

Kielelezo namba 7: Binadamu wa kale akitengeneza moto kwa kupekecha vijiti viwilivikavu

Umuhimu wa ugunduzi na matumizi ya moto

 • Ugunduzi na matumizi ya moto ulileta maendeleo makubwa katika maisha ya binadamu. Kwa mfano, binadamu alianza kuchoma nyama na vyakula vingine iii kuvilainisha na kula kwa urahisi, badala ya kula vyakula vibichi.
 • Vilevile, alichoma majani kufukuza wanyama wakali na kusafisha maeneo. Kuanzia kipindi cha Zama za Mawe za Kale binadamu alikuwa akiishi mapangoni. Hivyo basi, moto ulimwezesha kupata mwanga na kuongeza joto ndani ya mapango.
 • Zaidi ya hayo, ugunduzi wa moto ulimwezesha binadamu kusafiri na kuishi katika sehemu zenye baridi kali duniani.
 • Baadaye, moto ulisaidia kutengeneza gundi iliyotumika katika uvishaji wa vichwa vya mishale au mikuki kwenye mipini.Zama za Mawe za Mwisho

Kipindi hiki kilidumu kuanzia miaka 50 000 K.K hadi miaka 3 500 K.K. Kipindi hiki kiliambatana na ubunifu wa zana bora zaidi kuliko kipindi cha Zama za Mawe za Kati. Zana za zama hizi zilikuwa na kazi mahususi kama kuchuna ngozi za wanyama na kulima.

Kielelezo namba 8 kinaonesha baadhi ya mifano ya zana hizo.

Kielelezo namba 8: Zana za Zama za Mawe za Mwisho


Makazi ya binadamu wa Zama za Mawe za Mwisho yamegundulika katika mapango mbalimbali kandokando ya mito na maziwa. Maisha yao yamehusishwa pia na mabaki ya zana kama mawe mapana ya kusagia nafaka, mitego ya wanyama na mabaki ya mifupa mikubwa ya wanyama kama tembo na twiga. Inasadikiwa kwamba wanyama hao waliwindwa kwa kutumia mishale ya miti.

Kuanza kwa ufugaji

 • Zana za aina nyingi na bora zaidi za kipindi cha Zama za Mawe za Mwisho zilimwezesha binadamu kufanya kazi mbalimbali katika kukabiliana na mazingira yake.
 • Miongoni mwa mafanikio ya zana za Zama za Mawe za Mwisho ni kuwa binadamu alianzisha ufugaji wa wanyama na ndege kwenye makazi yake iii kurahisisha na kuongeza upatikanaji wa mavazi na chakula kama nyama, ngozi na maziwa.
 • Aidha, mbwa alikuwa ni miongoni mwa wanyama wa mwanzo kufugwa na binadamu wa kale. Hivyo, ufugaji ulimuondolea binadamu wa kale utegemezi mkubwa wa wanyama na ndege pori katika kujipatia mahitaji muhimu ya maisha.

Kuanza kwa kilimo

 • Moja ya matokeo ya ufugaji mwishoni mwa Zama za Mawe za Mwisho ilikuwa ni kuanzisha makazi ya kudumu.
 • Binadamu alilazimika kwenda kutafuta chakula na kisha kurudi katika makazi yake. Makazi ya kudumu yaliambatana na kuotesha au kupanda mazao ya chakula.
 • Kwa hiyo, ufugaji wa wanyama na kilimo yalikuwa mapinduzi makubwa katika maisha ya binadamu. Baadhi ya viashirio na umuhimu wa mapinduzi ya kilimo na ufugaji katika maendeleo ya binadamu mwishoni mwa Zama za Mawe za Mwisho ni:
 • Binadamu aliweza kupata chakula cha kutosha na ziada. Hivyo aliacha

kutumia muda wake mwingi kutafuta wanyama, ndege, mizizi na matunda;

 • Upatikanaji wa chakula kwa wingi uliongeza kasi ya kuzaliana na hivyo kuchochea ongezeko la watu;
 • Kuishi pamoja kulihimiza kuibuka kwa lugha, ikiwa kiungo muhimu cha mawasiliano baina ya wanajamii;
 • Ongezeko la watu katika makazi ya kudumu kulikuza ushirikiano na kuchochea kuibuka kwa uongozi katika jamii husika;
 • Upatikanaji wa chakula cha kutosha uliwapatia binadamu hawa muda wa ziada ambao waliutumia kufanya kazi za sanaa na ufundi kama vile ufinyanzi, uhunzi, uchongaji wa vyombo anuwai na ususi;
 • Ulikuwa mwanzo wa mgawanyo wa kazi baina ya jinsi ya kike na kiume, baina ya rika za watoto, vijana na wazee; na
 • Jamii zilianza kuwa na makundi mbalimbali yaliyozalisha mali kama wawindaji, wavuvi, wakulima, wafinyanzi, wachongaji, wahunzi, wasusi na wafugaji.
 • Hali hii ilisababisha wanajamii kubadilishana bidhaa ili kupata mahitaji au bidhaa wasizozalisha.
 • Huu ulikuwa ni mwanzo wa biashara miongoni mwa wanajamii na jamii jirani.

Ulinganisho wa maendeleo katika vipindi vya Zama za Mawe

 • Katika kila awamu ya Zama za Mawe binadamu alipiga hatua muhimu za maendeleo. Hii ilitegemea sans uwezo wake wa kupambana na mazingira ili kuboresha maisha yake na kiwango cha upevu wa ubongo wake au uwezo wake wa kufikiri.
 • Uwezo huu ulikuwa ukiongezeka kadiri alivyokuwa akifanya kazi na kuchangamana na mazingira yake, wakiwamo pia binadamu wengine.
 • Jedwali lifuatalo linalinganisha tofauti za viwango vya maendeleo ya binadamu katika Zama za Mawe za Kale, Zama za Mawe za Kati na Zama za Mawe za Mwisho.


Zama za Chuma

 • Zama za Mawe za Mwisho zilifuatiwa na Zama za Chuma. Zama hizi zilianza miaka 3 500 K.K na zinaendelea hadi sasa.
 • Wakati huo ndipo binadamu aligundua chuma na kutengeneza zana za chuma. Udongo wenye chembechembe za chuma ulipashwa joto kali hadi kutoa majimaji ya chuma.
 • Maji hayo yalikusanywa katika vyombo maalumu yakapozwa, kuganda na kupondwa iii kutengeneza au kufua zana anuwai za chuma. Kielelezo namba 10 kinaonesha wahunzi wakiwa kwenye mchakato wa kufua zana za chuma.

Aina za zana za chuma na matumizi yake

 • Zana hizi zilikuwa imara zaidi, bora na za kudumu kuliko zana za mawe. Zana zilizotengenezwa ni kama vile shoka kwa ajili ya kukatia miti, kukatakata nyama na kufanya shughuli za ulinzi.
 • Zana nyingine zilikuwa ni mikuki kwa ajili ya kuwinda na kujikinga na maadui na mishale iliyotumika kuwinda wanyama wakubwa na wadogo na kuwindia ndege. Aidha, ilifuliwa miundu kwa ajili ya kufyeka mimea na kusafisha maeneo ya kulima na kupanda mbegu za mazao anuwai. Vilevile, vilitengenezwa visu kwa ajili ya kuchuna wanyama na kukatia nyama. Pia, yalitengenezwa majembe kwa ajili ya kulima na kuchimba mizizi na wanyama wafukuao. Baadhi ya zana hizo zimeoneshwa katika Kielelezo namba 11(a) na 11(b).

Kielelezo namba 11(a): Baadhi ya zana za chuma za kale zisizo na mipini

Kielelezo namba 11(b): Baadhi ya zana za chuma za kale zilizo na mipini


Manufaa ya matumizi ya zana za chuma

Zana za chuma zilikuwa na matumizi na manufaa mengi kwa binadamu wa kale kama vile:

 1. Kupanua kilimo
 • Umadhubuti wa zana za chuma uliwezesha binadamu kupanua kilimo kwa kufyeka, kulima na kupanda mazao katika maeneo makubwa zaidi.
 • Aidha, watu walianza kufuga mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo na ndege kama kuku na bata.
 1. Kuongezeka kwa idadi ya watu na uongozi wa jamii
 • Upanuzi wa kilimo ulichangia kupatikana kwa chakula kingi na cha aina mbalimbali. Hivyo watu wakawa na afya, wakazaliana kwa wingi na vifo vitokanavyo na lishe duni vikapungua.
 • Hali hii ilisababisha jamii kupanuka na hivyo kuwapo haja ya kuanzisha uongozi katika jamii husika.
 1. Kuibuka kwa mafundi na wasanifu
 • Baada ya kuwa na uhakika wa chakula watu walipata muda wa ziada kufanya kazi nyingine.
 • Hivyo, waliibuka mafundi na wasanifu ambao walikuwa tegemeo la wazalishaji mall wengine kwa kuwatengenezea vitendea kazi muhimu.
 • Mfano, wafinyanzi walifinyanga vyungu na mitungi. Kundi jingine ni la wasusi ambao walisuka majamvi, mikeka, vikapu na nyungo kwa matumizi ya wanakaya.
 • Vielelezo namba 12 na 13 vinaonesha wasusi na wafinyanzi wa kale wakiwa kazini. waliibuka mafundi ambao walitengeneza majembe ya wakulima,siaakina visu kwa wawindaji na vinu vya kutwangia nafaka kwa kayanbalimbali.
 • Kielelezo namba 14 kinaonesha wachongaji wa zamani wakiwakazini.

Kielelezo namba 14: Wasanii wa kale wakichonga kazi ya sanaa

 1. Kuibuka kwa mgawanyo wa kazi na majukumu katika kaya na katika jamii
 • Ongezeko la shughuli za uzalishaji mali katika kaya kulichochea haja ya kugawana kazi kwa kuzingatia jinsi, umri na rika.
 • Hivyo, wanaume walifan­ya kazi za nguvu kama kuwinda, kusafisha mashamba, kulima na kulinda familia au jamii. Wanawake walifanya kazi za nyumbani kama kupika, kulea watoto, kutunza wazee na wagonjwa.
 • Watoto wa kike waliwasaidia mama zao, ilihali watoto wa kiume walichunga mifugo na kusaidiana na baba zao.
 1. Mwanzo wa kubadilishana bidhaa
 • Uzalishaji wa ziada wa bidhaa za aina tofauti ndani na nje ya jamii mbalimbali vilichochea haja ya watu kubadilishana bidhaa iii kukidhi mahitaji yao.
 • Huu ulikuwa mwanzo wa kufanya biashara baina ya wanajamii.


(f) Mabadiliko ya utamaduni

Maendeleo yaliyotokana na matumizi ya zana za chuma, yalichangia kuleta mabadiliko katika utamaduni wa jamii husika, hususani katika mavazi na lugha.

(I) Mavazi

Watu waliboresha mavazi ya ngozi na magome ya miti na hivyo kujisitiri vizuri, kujipamba na kujikinga na baridi. Katika jamii nyingine wasanii walipondaponda magome magumu ya miti maalumu na kuyalainisha, kisha kutengeneza mavazi yaliyovaliwa na wanajamii. Kielelezo namba 16 kinaonesha mtawala wa kale na walinzi wake wakiwa wamevalia ngozi na magwanda yaliyotokana na magome ya miti. Hatua hii iliboresha mavazi ya binadamu tofauti na zama zilizotangulia.

.

(ii) Lugha

Kadiri jamii zilivyozidi kupanuka na uhusiano kuongezeka, lugha mbalimbali ziliibuka kuwezesha mawasiliano. Vivyo hivyo, uhusiano wa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa ulisababisha kuibuka na kukua kwa lugha mbalimbali.


Zama za Teknolojia ya Kisasa ya kidijitali

 • Hadi sasa tumeshaona mabadiliko ya binadamu katika kutengeneza zana za kumwezesha kufanya kazi na kuzalisha mali.
 • Tumeshaona Zama za Mawe ambazo binadamu alitengeneza zana zilizotokana na mawe na kuzitumia katika shughuli mbalimbali.
 • Zana hizo aliziboresha kwa vipindi vitatu yaani, Zama za Mawe za Kale, Zama za Mawe za Kati na Zama za Mawe za Mwisho. Zama za pill ni zama za chuma. Katika zama hizi binadamu alitengeneza zana bora zaidi na kupanua uwezo wa kuboresha maisha yake.
 • Sehemu hii itahusu zama ya tatu ambayo ni Zama za Teknolojia ya Kisasa ya kidijitali.
 • Zama za Teknolojia ya Kisasa ya kidijitali ni mwendelezo na uboreshaji wa zama za chuma kwa kutengeneza kompyuta na mashine za aina mbalimbali.
 • Mashine hizo ni pamoja na mashine za viwandani, injini za magari, treni, meli, ndege, matrekta na mashine za kurahisisha kazi za maofisini.
 • Zama za Teknolojia ya kisasa ya kidijitali zimempa binadamu uwezo wa kuzalisha mali kwa wingi na kwa muda mfupi na kurahisisha njia za usafiri.
 • Zama za Teknolojia ya kisasa ya kidijitali zimeweza kurahisisha kazi za binadamu. Zama hizi za mashine na kompyuta zimemwezesha binadamu kugundua aina mbalimbali za teknolojia za kisasa.
 • Angalia kielelezo namba 17 kinachoonesha matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kilimo kwa njia ya trekta.

Kielelezo namba 17: Kilimo cha kisasa kwa kuturnia trekta

 • Faida za kulima kwa trekta ni pamoja na kulima eneo kubwa, kupanda mbegu nyingi kwa mistari, kuvuna mazao mengi kwa haraka na hivyo kuokoa muda.
 • Hata hivyo, kuna hasara katika kulima kwa kutumia trekta. Hasara hizo ni pamoja na kukandamiza ardhi, gharama kubwa za uendeshaji na kujaza moshi mwingi hewani na hivyo, huchangia uharibifu na uchafuzi wa mazingira.

Zana za uzalishaji mali za sasa

 • Licha ya matumizi ya zana za Zama za Teknolojia ya kisasa, siku hizi zana za uzalishaji mali ni nyingi zaidi na zinatumiwa kwa njia na kazi tofauti.
 • Mifano ya zana hizo ni zana zitumikazo kwa mikono na zana za kukokotwa na wanyama. Zana zitumiwazo kwa mikono
 • Kundi hill linajumuisha zana za kawaida kama mapanga, mashoka, majembe, nyundo na misumeno. Zana hizi zinc manufaa na upungufu zinapotumika.
 • Zana hizi zinapatikana kwa gharama ndogo na hivyo ni rahisi kununuliwa na watu wengi. Vilevile, ni rahisi kuzitumia. Upungufu wake ni pamoja na utendaji kazi kwenda polepole sang.
 • Kwa mfano, kulima shamba kwa jembe la mkono kunamchosha mkulima na kutumia muda mrefu. Kwa upande mwingine, kukata miti kwa msumeno wa kawaida huchosha na huchukua muda mrefu. Hii ni tofauti na kukata miti kwa kutumia msumenonyororo unaotumia mafuta ya dizeli. Vielelezo namba 18 na 19 vinaonesha aina za misumeno.

Kielelezo namba 18: Msumeno wa kawaida wa mkono

Kielelezo namba 19: Msumenonyororo

 1. Zana za kukokotwa na wanyamakazi

Zana hizi ni plau, mkokoteni na toroli. Matumizi ya zana hizi ni mengi na yana faida nyingi. Kwa mfano, plau hutumika kwa kulima, mkokoteni hubeba mizigo na watu na toroli hutumika kwa kazi za kubeba mizigo. Kielelezo namba 20 kinaonesha mtu anayesafirisha mananasi kwa mkokoteni unaokokotwa na punda.

 • Hata hivyo, kuna upungufu katika kutumia zana hizi. Kwa mfano, zinabeba mizigo kidogo zikilinganishwa na malori.
 • Vilevile, wanyamakazi huchoka, hususani mizigo ikiwa mizito kuliko uwezo wao.
 • Kwa kawaida wenye wanyama hawa huwachapa iii watembee haraka au wavute mzigo kwa nguvu zaidi. Kitendo ambacho ni kinyume na haki za wanyama.

Faida na athari ya kutumia zana za kisasa

 • Kama tulivyoona hapo juu, matumizi ya zana za kisasa yana athari chanya na athari hasi. Jedwali lifuatalo Iinaonesha hali hiyo:


www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256