SURA YA PILI
UTENZI
Ufahamu
Soma utenzi ufuatao, kisha jibu maswali yanayofuata
Teknolojia ya kisasa


Zoezi la kwanza: Ufahamu
1Katika ubeti wa kwanza, mwandishi analenga kuwapa soma gani
wasomaji?
- Wakati gani teknolojia ya kisasa hutumika?
- Teknolojia ya kisasa ina faida gani?
- Maendeleo gani yameletwa na teknolojia ya kisasa?
- Teknolojia ya kisasa imeleta mabadiliko yapi?
- Mtunzi ana maana gani anaposema, "Giza tumeshalipiku"?
- Katika ubeti wa 11, kifungu cha maneno "dunia kama kijiji" kina rnaana
gani? - Teknolojia ya kisasa inasaidiaje katika kukusanya kodi?
- Kwa nini "makini yahitajika" katika kutumia teknolojia ya kisasa katikajamii yako?
- Umejifunza nini kutokana na utenzi huu?
Zoezi la pili: Msamiati
Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi moja kwa kila neno
Mfano:Ufaulu wa somo la kiswahili katika mitihani wa darasa la saba umeongezeka
- Somo
- Geua
- Aali
- Epesi
- Sawia
- Boresha
- Masafa
- Utandawazi
- Ubunifu
- Tija
Zoezi la tatu: Vitendawili
Tegua vitendawili vifuatavyo kwa kuandika jibu lake kwenye mabano
Mfano: Nina mdomo lakini sina mikono wala miguu.(nyoka)
Nyumba yangu ni kubwa lakini mlango mdogo.(chupa)
- Chumba changu kikubwa lakini nalala peke yangu.
- Akamatwapo mkiani, hutii amri.
- Nina mwanangu, ukimkata hakatiki.
- Tunda langu la ajabu, juu nyama, katikati ngozi na ndani mchanga.
- Ukimkata shingo leo, kesho anayo nyingine.
- Mama hana miguu lakini mtoto anayo.
- Bunduki yangu ikilia, sauti husikika dunia nzima.
- Hubeba mishale kila aendako.
- Baba akipiga mbizi, huibuka na ndevu nyeupe.
- Ukimgusa mwanangu, mimi hucheka.
Zoezi la nne : mazoezi ya lugha
A. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo:

B. Andika sentensi zifuatazo katika wakati uliopita.
Mfano:Baba amejenga kituo cha kulelea watoto yatima.
Baba alijenga kituo cha kulelea watoto yatima.
- Serikali itatoa mikopo ya fedha kwa wajasiriamali wadogo.
- Mjomba anatunga utenzi kuhusu maadili ya jamii.
- Mwandishi ataikosoa jamii kwa kuendekeza imani potofu.
- Mwalimu hatungi mtihani wa muhula wa pill.
- Dereva ataendesha gari kwa umakini mkubwa.
- Kiranja hasimamii usafi wa mazingira ya shule.
- Wanakijui watachagua viongozi wa kijiji chao.
- Wanafunzi wanachimba shimo la takataka shuleni.
- WanachUo watasafiri kuelekea mbuga ya wanyama.
- Kwaya ya shule yetu itatumbuiza kwenye Sherehe za Muungano.
C. Andika kinyume cha maneno yafuatayo:
- Dhurika
- Nuna
- Karibisha
- Mkarimu
- Taifisha
- Werevu
- Imara
- Afiki
- Ghali
- Patikana
D. Jaza neno moja sahihi katika sehemuiliyoachwa wazi kutoka kwenye mabano
- Mti huumatunda mazuri sana. (amezaa,umezaa, yamezaa, imezaa)
- Wajasiriamalini wabunifu wamepewa mtaji wa biashara. (ambaye, ambayo, ambao, ndiye)
- Huyu............mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa
Darasa la Saba. (ndio, ndiyo, ndiye, ndiwe) - Ukulima wa kisasabudi kutiliwa mkazo iii kuinua
uchumi wa nchi yetu. (una, ni, si, hauna) - Angalikuwa mwizina wenzake. (angakamatwa,angelikamatwa, angalikamatwa, angekamatwa)
- Wachezaji walichelewa kuingia uwanjani walielekezwa wafike mapema. (ama, ingawa, kwa sababu, kwakuwa)
- Tabia mbayakatika jamii. (haufai, zinapendwa,zinapaswa,hazifai)

Wanafunzishamba Ia shule sasa hivi. (anapalilia,
walipalilia, atapalilia, wanapalilia. - Micheya mikahawa imepandwa shambani.
(wazuri, mzuri, mizuri, kizuri) - Mwaka jana, BahatiDarasa la Sita. (alikuwa,atakuwa, amekuwa, anakuwa)
E. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika kauli halisi.Mfano:Dada aliuliza kuwa unapenda mchezo gani."Unapenda mchezo gani?" Dada aliuliza.
Polisi alisema kwamba tunatakiwa kutii sheria bila shuruti."Mnatakiwa kutii sheria bila shuruti," polisi alisema.
- Mwalimu amesema kwamba twende upesi.
- Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilisema kwamba tunasajililaini za simu zetu iii kuzuia uhalifu.
- Bwana Afya aliuliza kuwa kuna umuhimu gani wa kuchemsha maji ya kunywa.
- Mwanafunzi mwenzangu alisema kwamba kalamu yangu inaandikavizuri sana.
- Mgeni aliuliza kuwa mimi ni nani.
- Waziri alisema kwamba ajira huchochea ukuaji wa uchumi.
- Mwalimu alisema kwamba nidhamu ni msingi wa maendeleo yataaluma shuleni.
- Mtabiri wa hali ya hewa alisema kwamba mwaka ujao kutakuwana mvua nyingi.
- Kiranja alisema kwamba kila mwanafunzi atatakiwa kuja na ufagiokwa ajili ya usafi.
- Daktari alimwambia mgonjwa kuwa anaumwa ugonjwamalaria.