SURA YA PILI

NISHATI

Nishati ya umeme

Umeme ni nini?

 • Umeme ni nishati inayotokana na vyanzo mbalimbali vikiwemo jua, upepo, maji na fueli,
 • Vyanzo hivyo huzalisha umeme kwa kutumia mitambo mbalimbali kama paneli za jua na kinuupepo. Pia, hutumia vifaa kama jenereta, dainamo, selikavu na betri.

Kuzalisha umeme kwa kutumia maji

 • Nguvu ya maji inayotokana na maporomoko hutumika kuzalisha umeme.
 • Tabaini zilizounganishwa kwenye jenereta huzungusha maji kwa kasi. Tabaini ni mashine inayozungushwa na msukumo wa maji.
 • Kitendo hiki kinapoendelea umeme huzalishwa. Hapa Tanzania, maporomoko ya maji yanayozalisha umeme yanapatikana Kidatu (Morogoro) na Mtera (Iringa).
 • Sehemu nyingine ni Bwawa la Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro), Kihansi (Mororogo), Pangani na Hale (Tanga).

Kuzalisha umeme kwa kutumia jua

 • Jua lina uwezo wa kuzalisha umeme. Miale ya jua hukusanywa na kifaa maalumu kinachoitwa paneli ya sola.
 • Paneli ya sola hubadilisha nishati ya mwanga wa jua kuwa nishati ya umeme. Paneli hizo huweza kuunganishwa na betri na kutunza umeme kwa matumizi mbalimbali.

Kielelezo Namba 1. Paneli ya solar.

Kuzalisha umeme kwa kutumia upepo

 • Umeme pia huweza kuzalishwa kwa kutumia upepo. Upepo unapovuma, mabapa ya kinuupepo huzungushwa.
 • Kinuupepo ni mashine ya kufua umeme inayotumia msukumo wa upepo. Kasi ya upepo husababisha jenereta Iililounganishwa na kinuupepo kuzalisha umeme.
 • Mpaka sasa, mitambo ya kuzalisha umeme huu kwa wingi katika nchi ya Tanzania inapatikana katika mkoa wa Singida.

Kielelezo Namba 2. Nishati ya Upepo.

Kuzalisha umeme kwa kutumia fueli

 • Fueli hutoa nishati ya joto ambayo hubadilishwa na kuwa nishati ya umeme.
 • Fueli hizo ni dizeli, petroli, makaa ya mawe na gesi asilia. Vifaa kama jenereta hutumia nishati hizo kuzalisha umeme.
 • Kuna mitambo inayozalisha umeme mkubwa kwa kutumia dizeli. Mitambo hiyo ipo Ubungo Dar es Salaam na Dodoma.
 • Pia, mitambo mingine ya dizeli huzalisha umeme mdogo unaotumika shuleni, zahanati, makanisani na misikitini.

Kielelezo Namba 3. Mitambo ya gesi Mtwara.

 • Mitambo ya gesi asilia hupatikana Mtwara na Kinyerezi I na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
 • Umeme unaotengenezwa na vyanzo mbalimbali hutiririka kupitia njia maalumu. Njia hiyo imeundwa na chanzo cha umeme, waya, swichi, na kifaa kinachotumia umeme.
 • Muunganiko wa vifaa hivi ambavyo umeme hupitia huitwa sakiti. Umeme hutiririka ikiwa sakiti imekamilika.
 • Kama umeme hautiririki inaashiria kutokamilika kwa sakiti. Umeme hautiririki kwenye sakiti endapo waya umekatika au swichi imezimwa.

Mabadiliko ya nishati ya umeme

 • Nishati ya umeme inaweza kubadilishwa kutoka nishati moja kwenda nyingine kutegemea kifaa kilichotumika.
 • Kwa mfano, kurunzi hutumia nishati ya umeme kutoka kwenye selikavu na kutoa nishati ya mwaga na joto.

Matumizi ya nishati ya umeme

Soma habari hii kwa makini

 • Siku moja, Rehema na wanafunzi wenzake walikuwa wakitoka shuleni. Walipokuwa njiani, waliona gall kubwa Iffilokuwa limesimama karibu na ofisi ya Mtendaji Kata. Nje ya ofisi hiyo walionekana vijana wengi wakishangilia.
 • Vijana wawili walielekea kwenye miango wa gari hilo na kuufungua. Walishusha makasha mengi na kuyapeleka katika ofisi ya Mtendaji Kata. Rehema na wenzake walisogea karibu ili waone makasha hayo yalikuwa na nini.
 • Waligundua kuwa ndani ya makasha kulikuwa na vifaa mbalimbali vya umeme. Vifaa hivyo vilikuwa betri, nyaya za umeme, soketi na paneli za sola.
 • Rehema na wenzake waliamua wasiondoke bila kujua kazi ya vitu hivyo. Mtendaji Kata aliwaambia kuwa, ni vifaa vitakavyotumika kuunganishia umeme unaotokana na nishati ya jua. Hivyo, muda si mrefu kutakuwa na umeme unaotumia mionzi ya jua kijijini kwao.
 • Baada ya wiki moja nyumba nyingi zilikuwa zimewekewa vifaa maalumu vinavyojulikana kama paneli za sola. Wananchi katika !qui hicho walianza kutumia umeme unaotokana na mionzi ya jua kwa shughuli mbalimbali. Rehema alifurahi kwanialiweza kutumia nishati ya umeme kwa kazi mbalirnbali za nyumbani. Vilevile, Rehema aliweza kujisomea wakati wa usiku, kusikiliza redio, na kuangalia runinga.
 • Halikadhalika, Rehema aliweza kunyoosha nguo zake kwa kutumia pasi ya umeme kwa haraka na kuwahi shuleni.
 • Siku moja Rehema alimuomba mwalimu awaeleze wenzake jinsi chao kilivyofaidika na umeme. Mwalimu alimpa nafasi naye akawaeleza kuwa, umeme hutumika kwenye jiko kwa ajili ya kupikia.
 • Vilevile, hutumika katika jokofu iii kuhifadhi vyakula na kwenye mashine za kutengenezea vinywaji. Halikadhalika, hutumika kwenye pampu za kusukumia maji na mashine za kunyolea nywele.
 • Mwalimu aliongezea kueleza kuwa, umeme hutumiwa kuchomelea vyuma na kuendeshea mitambo viwandani. Hivyo, nishati ya umeme husaidia kutoa ajira kwa watu.
 • Umeme ni rafiki unapotumiwa kwa kuzingatia kanuni na masharti. Hata hivyo, mwalimu aliwaeleza wanafunzi kuwa, hitilafu ya umeme husababisha moto, mlipuko na hata kifo. Wanafunzi walimshukuru mwalimu na Rehema kwa kutoa elimu kuhusu matumizi ya umeme.

Nishati ya mwanga

 • Nishati ya mwanga inaweza kuonekana kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile jua. Pia, huweza kutokea kwa kubadilisha nishati moja kwenda nishati nyingine.
 • Mfano nishati ya umeme hubadilishwa iii kupata nishati ya mwanga. Nishati hii huweza kuonekana inapokutana na vitu mbalimbali vinavyoruhusu na visivyoruhusu mwanga kupenya.

Vitu vinavyoruhusu na visivyoruhusu mwanga kupenya

 • Baadhi ya vitu vinaruhusu miale ya mwanga kupenya. Pia, vipo vitu visivyoruhusu miale ya mwanga kupenya.

Kielelezo Namba 4 kupenyeza kwa mwanga

 • Vitu vinavyoruhusu miale ya mwanga kupenya huitwa angavu, mfano kioo na gilasi. Vile visivyoruhusu miale ya mwanga kupenya huitwa vikinza nuru, mfano ubao, kitabu na ukuta.

Kutokea kwa vivuli

 • Kivuli ni sehemu yenye giza inayoonekana upande wa pili wa kitu kisichopitisha mwanga. Pia, umbo Ia kivuli huonekana kushabihiana na kitu kilichozuia mwanga kupenya.

Kielelezo Namba 5 kivuli

Soma habari ifuatayo kwa makini

Mwajuma na wenzake wanasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Shaurimoyo. Siku moja mwalimu wa somo Ia Sayansi aliwafundisha wanafunzi tabia za mwanga. Aliwaeleza kuwa tabia mojawapo ya mwanga ni kusafiri katika mstari mnyoofu. Vilevile, mwanga ukitua kwenye baadhi ya vitu vigumu huzuiwa na kutengeneza kivuli.

Mwalimu akawaambia, "Ninataka mfanye zoezi muone mwanga unapozuiwa nini kitakachotokea?" Mwalimu aliwaeleza, "Wakati wa asubuhi, jua likiwa linachomoza, simama sehemu ya wazi. Hakikisha jua linakumulika mgongoni na angalia nini kinatokea mbele yako. Pia, shika mpira mkononi, kisha nyoosha mkono wako upande wa jua na angalia chini. Kwa kutumia vitu mbalimbali, fanya vitendo hivyo na kuangalia matokeo yake."

Siku iliyofuata baada ya jua kuchomoza, Mwajuma na wenzake walielekea uwanjani iii kufanya uchunguzi. Walisimama kama walivyoelekezwa na mwalimu. Wakaona maumbo yenye giza mbele yao kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 12. Waliandika walichokiona na kuelekea darasani kuendelea na masomo.

Mwalimualiwauliza walichogundua baadaya kufanya uchunguzi. Mwanafunzi mmoja anayeitwa Kalunde alijibu, "Nimeona umbo jeusi ardhini mbele yangu." Mwajuma aliongezea kwa kusema, "Mimi niliona umbo linaloshabihiana na umbo langu." Mwanafunzi mwingine aliongeza, "Mimi niliona umbo langu pamoja na umbo la mpira."

Baada ya hapo mwalimu alieleza, "Hicho mlichokiona kinaitwa kivuli." Kivuli hutokea mwanga unapotua na kuzuiwa na kitu kisicho angavu. Kwa hiyo, kivuli ni matokeo ya kuzuiwa kwa mwanga kusafiri katika mstari ulionyooka. Aidha, kivuli hubadili uelekeo na ukubwa kadiri chanzo cha mwanga kinavyobadili uelekeo. Mwajuma na wenzake walifurahia somo kwa kuwa waligundua namna kivuli kinavyotokea.

Kuakisiwa kwa miale ya mwanga

Kielelezo Namba 6 kuakisi kwa mwanga

Kuakisiwa kwa mwanga ni kitendo cha kurudishwa kwa miale ya mwanga inapotua kwenye sura nyororo na inayong'aa. Mfano wa kifaa chenye sura nyororo na inayong'aa ni kioo bapa.

Miale ya mwanga inapotua katika nyuso nyororo zinazong'aa huakisiwa. Kuakisiwa kwa miale ya mwanga husababisha kutengenezwa kwa taswira mbalimbali katika nyuso hizo.

Kupinda kwa miale ya mwanga

Miale ya mwanga hupinda inapotoka midia moja kwenda midia nyingine angavu. Mfano, kutoka kwenye midia ya hewa kwenda midia ya maji. Hatuoni miale ya mwanga ikipinda bali tunaona matokeo ya kupinda kwa miale ya mwanga.

Kielelezo Namba 7 kupinda kwa mwanga.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

GO TO NECTA EXAMS