SURA YA PILI

NISHATI

Msamiati

 • Fikicha- weka katikati ya vidole au viganja viwili na kusugua
 • Kandili-Taa ya chemli inayowaka kwa utambi na mafuta
 • Karabai- taa ya utambi ambayo hutiwa upepo na kuwaka kwa mafuta ya taa
 • Kurunzi- taa ya mkononi ambayo hutumia betri au umeme
 • Mwanga- mwako wa jua , taa na kitu chochote kitoacho nuru
 • Nyororo- kitu laini
 • Pekecha- zungusha zungusha zungusha kitu kwa lengo la kutoboa kitu kingine
 • Taswira- picha ya kitu
 • Tobwe- tundu, shimo au uwazi
 • Upawa- ni kifaa chenye uwazi ndani mithili ya kijiko kikubwa kinachotengenezwa kutokana na mti au kifuu cha nazi ambacho hutumika katika mapishi.

Kwenye mazingira tunayoishi kuna vitu mbalimbali vinavyotoa nishati. Nishati ni nguvu inayowezesha kazi mbatimbali kufanyika. Tunapotumia vitu kama kurunzi, jiko na ngoma tunaweza kutambua aina mbalimbalti za nishati. Kuna aina tatu za nishati. Aina hizi ni nishati ya sauti, joto na mwanga.

Nishati ya sauti

Chunguza picha hizi, kisha soma maetezo yanayofuata.

Kidelezo : Vitendo vya kutoa sauti

Sauti ni aina ya nishati inayotokana na mitetemo ya vitu mbalimbali. Sauti husaidia mawasiliano kufanyika. Nishati hii husambaa kutoka kwenye chanzo kwenda sehemu nyingine. Unapopiga ngoma, filimbi au gitaa kinachotokea ni sauti.

Vilevile, vyanzo vingine vya sauti ni kinanda, tarumbeta, gitaa na kengete. Pia, watu wanapoongea au kuku anapoita vifaranga vyake, kinachotokea ni sauti

Kutambua sauti inavyosafiri katika hewa

Chunguza wakati kengete inapogongwa

 1. Je, wanafunzi wanapokusanyika wanatoka upande gani?
 2. Je, mawimbi ya sauti yanaeLekea upande gani.?
 3. Umegundua nini kuhusu sauti inayosafiri katika hewa?

Kuakisiwa kwa sauti

Sauti inapokutana na kizuizi au kitu kigumu kama ukuta au mwamba huakisiwa. Sauti iliyoakisiwa huitwa mwangwi.

Kufanya kitendo cha kutoa mwangwi

Ingia kwenye Chumba kisicho na kitu ita kwa sauti kubwa.

Je, unasikia nini?

Kuchunguza kama sauti husafiri katika maji

Mahitaji;

Beseni, maji na jiwe dogo

Hatua;

Jaza maji kwenye beseni. Hakikisha maji yametulia kwenye beseni. Dondosha kipande cha jiwe katikati ya beseni ya maji

Je, unasikia na unaona nini? Andika unachokisikia na kuona

Sauti husafiri katika maji kama ilivyo katika hewa.

Unapodondosha kitu kwenye maji, sauti hutokea pamoja na mawimbi.

Mawimbi yanaonesha jinsi sauti inavyosafiri katika maji. Pia, hata ukiwa ndani

ya maji unaweza kusikia sauti toka sehemu moja hadi nyingine.

Kuchunguza sauti inavyosafiri kupitia kamba

Mahitaji

 1. Karatasi ngumu
 2. Kamba ya manila
 3. Gundi

Hatua

 • Kunja karatasi upate mifano miwili ya spika
 • Unganisha karatasi uktumia gundi
 • Funga kamba ndefu kwenye pande zote mbili kwenye spika ulizozitengeneza
 • Mwambie rafiki yako akuite akitumia upande mmoja wa spika
 • Upande mwingine weka sikioni
 • Andika ulichokisikia

Mwanafunzi mmoja akiongea, mwingine atasikia kupitia spika iiiyounganishwa kwa kamba. Hivyo, inaonesha kuwa sauti husafiri katika kamba.

Chunguza picha, kisha fanya kazi namba 5.

Kieldezo : Kusafiri kwa sauti kwenye chuma

Kuchunguza sauti inayosafiri kupitia chuma

Mahitaji;

 • Kipande cha chuma
 • Rula

Hatua

 • Chukua kipande kirefu cha chuma na uweke mezani
 • Mwambie rafiki yako aweke sikio lake kwenye upande mmoja wa kipande hicho
 • Gonga kipande cha chuma kwa kutumia rula
 • Muulize anasikia nini uandike
 • Weka sikio lako upande mmoja wa chuma
 • Mwambie rafiki yako agonge chuma
 • Andika unachosikia

Tumeona kuwa hewa, maji, kamba ya manila na chuma hupitisha sauti. Hii inaonyesha kuwa vitu vigumu, vimiminika na hewa husafirisha sauti. Sauti inatumika katika mawasiliano

Nishati ya joto

Toto ni mojawapo ya aina za nishati. Nishati ya joto inaweza kusafiri kutoka kwenye chanzo cha joto kwenda kwenye hali ya ubaridi. Nishati ya joto

husafiri katika vitu vigumu, vimiminika na gesi. Kwa mfano, joto husafiri katika chuma (vitu vigumu), maji (vimiminika) na hewa (gesi).

Tazama picha hizi, kisha soma maelezo yanayofuata.

Kielelezo: Vyanzo vya nishati ya joto

Picha a inaonesha jua kama nishati ya joto.Vilevile jua ndio chanzo kikuu cha nishati ya joto: Picha b na c zinaonesha vitendo vya kupika chakula kwa

kutumia kuni na mkaa,. Kuni na mkaa ni chanzo cha nishati ya joto. Picha d nae zinaonesha vitendo vya kupika chakula kwa kutumia umeme na, gesi. Umeme

na gesi pia ni vyanzo vya joto.

Kudhibitisha namna ya kupata Joto

Hatua

 1. Fikisha viganja vya mikono yako. Andika unachohisi wakati wa kufikicha viganja vya mikono
 2. Chukua kijiti cha mti uliokauka
 3. Pekecha kijiti cha mti kwenye kipande cha mti uliokauka
 4. Gusa kijiti cha mti sehemu inayopekechwa
 5. Andika unachohisi ukigusa katika kijiti unachopekecha

Utagundua kuwa msuguano wa aina yeyote ukifanyika joto hutokea

Iota husafiri kwa urahisi katika vitu vigumu (yabisi)kutiko vimiminika au gesi. Baadhi ya vitu vigumu vinavyopitisha joto kwa urahisi ni chuma na bati.

Vipo vitu vigumu visivyopitisha joto kwa urahisi kama vile ptastiki au mbao kutokana na asili ya vitu

Joto husafiri kwa njia kuu tatu ambazo ni;

 • Mpitisho- ni njia ya usafirishaji wa nishati ya joto katika vitu vigumukwa mfano chuma
 • Mnururisho- ni njia ya usafirishaji wa nishati ya joto katika gesi mfano hewa
 • Msafara- ni njia ya usafirishaji wa nishati ya joto katika vimiinika kwa mfano katika maji

Matumizi ya nishati ya joto


Vilevile, tunatumia joto kupikia chakuta na kukaushia nguo na vyakula. Matumizi mengine ya joto ni kuchemsha maji ya kunywa, kuangulia vifaranga na

kuchoma nyama.

Nishati ya mwartga

Chunguza picha hizi, kisha soma maelezo yanayofuata.

Vyanzo vya nishati ya mwanga

Mwanga ni aina mojawapo ya nishati. Picha namba a, na c zinaonesha vyanzo mbalimbali vya nishati ya mwanga. Vyanzo hivyo ni vile vya asili na visivyo vya

asili. Jua ndiyo chanzo kikuu cha asili cha mwanga. Vyanzo vya mwanga visivyo vya asiti ni mshumaa, kibatari, karabai, kanditi na kurunzi..

Tabia ya nishati ya mwanga

Kuchunguza mwanga unavyosafiri katika hewa

Chunguza asubuhi na maperna jua linapochomoza.

Je, unaona nini? Weka kumbukumbu ya kile unachokiona.

Ukiamka asubuhi na mapema wakati jua tinaanza kuchomoza utaona miale ya mwanga. Miale hii huonekana inasafiri katika mistari iliyonyooka.

Mwanga ni n.ishati inayotuwezesha kuona. Pia,inawezesha ukuaji wa mimea.

Kuchunguza vitu vinavyopitisha na visivyopitisha mwanga

Mahitaji - glasi, karatasi ngumu isiyo na tobwe, karatasi ngumu yenye tobwe, kitabu, kurunzi na maji

Hatua

 1. Weka glasi iliyojaa maji juu ya dawati.
 2. Weka karatasi ngumu yenye tobwe mbele ya glasi.
 3. Weka karatasi ngumu isiyo na tobwe upande wa pili wa glasi.
 4. Elekeza mwanga wa kurunzi kwenye tobwe.

Je, unaweza kuona mwanga wa kurunzi katika karatasi ngumu isiyo na tobwe?


Miale ya mwanga imetoka kwenye kurunzi na kupita wenye tobwe. Kisha miale hiyo hupita kwenye maji na glasi na kutoka nje.

Mwanga huweza kupita kwenye baadhi ya vitu kama vile maji na glasi. Mwanga hauwezi kupenya katika baadhi ya vitu kama kitabu na karatasi ngumu.

Tabia za mwanga ni

 • Kusafiri katika mstari mnyoofu
 • Kuakisiwa
 • Kupinda


www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256