SURA YA PILI
HALI YA HEWA
Msamiati
Katika sura hii utajifunza kuhusu hali ya hewa ya mazingira yako. Hali ya hewa inahusisha jotoridi, mvua, mawingu na upepo wa sehemu husika. Katika sura hii utajifunza kipengele kimoja to cha hali ya hewa. Kipengete hiki kitahusu jotoridi to sehemu unayoishi. Utajifunza pia kipimo cha halijoto, mbinu za kujikinga na baridi na joto.
Kubaini jotoridi katika mazingira yetu
Maana ya jotoridi
Hali ya hewa inaweza kuwa ya joto au ya baridi. Hali hii huitwa jotoridi. Joto likiongezeka tunasema jotoridi liko juu na kunapokuwa na baridi jotoridi huwa chini.
Kidelezo: Kipimajoto
Athari za joto na baridi kwa wanyama na mimea
Soma majigambo yofuatayo kati ya joto na baridi, kisha jibu. maswall.
Joto: Mimi ni joto, chanzo changu ni jua. Jua Likiwa kaLi mimi huwa mkaLi pia. Nikifika tu baridi hutimua
Baridi: Mimi ni baridi, kiboko ya joto nikifika tu joto huhama.
Joto: Wee! Mimi nakausha maji ya mito, mabwawa na
visima. Hata mazao nayakausha na kusababisha njaa. Mimi ni mwamba kuliko wewe.Tena ni kiboko yako, hata viumbe hujificha nikichachamaa.
Baridi Thubutu! Hunishindi mimi. Nikichachamaa viumbe
hujikunyata. Hakuna kinachoweza kuishi. vyote wanaganda na kufa.
Joto: Sio kweli, hata ukizidi watu wanajifunika, na kuvaa nguo nzito ili kukudhibiti. Lakini mimi joto, watu wasipovaa nguo wanatoka jasho na kukosa raha. Namaliza maji mwilini mwao na wanaweza hata kufa. Hata vyakula vyao vinaoza kwa sababu yangu mimi.
Baridi: watu wanakaa kwenye vivuti chini ya miti na kustarehe. Wakiwa ndani wanajipulizia upepo kwa pangaboi. Wanaweka vitu vyao kwenye jokofu na maisha yanaenda vizuri. Wewe joto si lolote.
Joto: Sawa bwana, tusigombane. Sisi sote tuna faidatukiwepo
kwa kiasi na hasara kama tukizidi sana.
Maswali
Tazama picha ifuatayo, kisha jibu maswall.
Kielelezo: Wanafunzi wakisoma jotoridi kutoka kwenye kipimajoto
Maswali
www.learninghubtz.co.tz