LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 122
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI
MTIHANI WA MUHULA WA II DARASA LA VI
MUDA: SAA 1:30
MAELEKEZO KWA MTAHINIWA:
Mtihani huu una sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali SITA (6).
Soma maelekezo na ujibu maswali YOTE katika kila sehemu.
Tumia kalamu ya wino wa BLUU au MWEUSI kujibu maswali.
Simu za mkononi pamoja na vitu visivyoruhusiwa HAVITAKIWI
SEHEMU A: UFAHAMU
1. Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa kisha jibu swali la 1 mpaka la 5
i. Wanakijiji walipata mafunzo kuhusu nini?
Upishi wa vyakula
usafi wa mazingira
kutengeneza mafya
kupika mikate
kulima mazao [ ]
ii. Walijifunza njia bora za kupika na kuhifadhi chakula ili ____
Kuepuka magonjwa
chakula kisiharibike
kupata chakula kitamu
kitumike mwaka mzima
kuwa wasafi [ ]
iii. Kwa nini mwendesha mafunzo alisisitiza usafi wa vyakula na jiko?
Ili kupata chakula kitamu
ili kuwa naanuani za vyakula
ili chakula kisiharibike
ili kuepuka magonjwa
kulamboga za majani [ ]
iv. Chakula kilipikwa na kina nani?
Sankwaleto
wanakijiji
wakina mama
mafya
waendesha mafunzo [ ]
v. Andika umoja wa neno mafya kama lilivyotumika katika kifungu cha habari.
Majifya
mawematatu
mafiga
jifya
jivu [ ]
2. Chagua herufi ya jibu sahihi
i. Katika sentensi “Juma alikuwa anaandika darasani” neno alikuwa limesimama kama aina gani ya neno?
Kitenzi kikuu
kitenzi kisaidizi
kitenzi kishirikishi
kielezi cha nomino
kivumishi [ ]
ii. “Tunafundisha wanafunzi masomo yote ya biashara.sentensi hiyo ipo katika wakati gani?
Ujao
uliopita
timilifu
uliopo
mazoea [ ]
iii. Mjomba anauza kiwanja kilichoko mjini.neno lipi limetumika kama kielezi katika sentensi hiyo?
Mjomba
kiwanja
anauza
kilichoko
mjini [ ]
iv. Ukulima wa kisasa ________ kutiliwa mkazo ili kuinua uchumi wa nchi yetu.
Una budi
hauna budi
ni budi
si budi
hatuna budi [ ]
v. Kisawe cha neno adimu ni kipi?
Patikana
changa
chache
chenga
julikana [ ]
vi. Tulikuwa tukimshauri rafiki yetu asome kwa bidii ili aweze kufanikiwa maishani. Yeye hakutusikia kwani alitamani kupata utajiri kwa njia isiyo halali. Hivi sasa amekamatwa kwa kosa la wizi na anajuta kwa kusema?
Elimu haina mwisho
akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
tamaa mbele mauti nyuma
sikio la kufa- halisikii dawa nyingi
usiache mbachao kwa msala upitao [ ]
vii. Chakula chote kimemwagika sakafuni. Wingi wa neno chote ni upi?
Yote
zote
wote
pote
vyote [ ]
viii. Chombo maalumu cha majini kinachotumika kuvusha watu na mizigo kwenda ng’ambo ya pili huitwa _______
Daladala
pikipiki
basi
kivuko
baiskeli [ ]
ix. Mtu mwenye taaluma ya ujuzi wa kubuni,kutengeneza au kurekebisha majengo, barabara au mitambo anaitwaje?
Rubani
dereva
mkutubi
mhandisi
mhunzi [ ]
x. Malizia methali ifuatayo; mwanzo wa ngoma ni _______
Mdundo
lele
nyumbani
kucheza
kuimba [ ]
3. Oanisha maneno yaliyopo katika orodha A na yale ya orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi
ORODHA A
JIBU
ORODHA B
(i) Ukumbi maalumu wa kulia chakula
[ ]
Maarifa
Zuru
Bwalo
Makumbusho
Maabara
Kituo
(ii) Jengo au chumba maalumu kinachotumika kwa ajili ya majaribio na utafiti wa kisayansi.
[ ]
(iii) Jengo lenye maonyesho ya vitu vya kale kazi za sanaa au sampuli za malighali.
[ ]
(iv) Enda mahali Fulani kwa madhumuni ya kutembelea nakujifunza jambo.
[ ]
(v) Elimu au ujuzi aupatao mtu kutokana nakusoma, kusikia au kutenda.
[ ]
SEHEMU B
4. Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko mzuri wa mawazo unaoleta mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E
Pigia mstari neno lililotofauti. kodi, rushwa, ushuru, ada .
6. Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo
Ndugu watanzania, shime tujitokezeni. Kuhesabiwa muhimu, mipango kukadiria Wala tusibabaike, kusikiliza majungu Sensa kwa maendeleo,kuhesabiwa muhimu
Mipango kukadiria, kwa kila mtanzania, Elimu nayo afya,kila raia apate, Barabara nayo maji, kila sehemu sawa Sensa kwa maendeleo, kuhesabiwa muhimu,
Muhamasishe na ndugu, hata na Yule jirani. Wote wakajitokeze, mapema kuhesabiwa, Wasihusishe sihiri, imani zisizofaa. Sensa kwa maendeleo, kuhesabiwa muhimu.
Maswali
Shairi hii limeundwa na mishororo mingapi katika kila ubeti?_______________________
Mshororo wa pili katika ubeti wa kwanza una jumla ya mizani mingapi?_______________
Andika kibwagizo cha shairi hili ________________
Andika vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu mstari wa tatu ___________na_____
Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa katika shairi hili.__________________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 116
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA KWA SHULE ZA MSINGI
MACHI 2025
DARASA LA SITA KISWAHILI
1. Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa kisha ujibu maswali kipengele cha i-v
i. Mganga alikuwa kijana mwenye sifa ziizovutia wanakimi. Ni ipi kati ya zifuatazo sio za Mganga?
(A) alipenda maendeleo
(B) hakuwa na lugha ya kubembeleza
(C) hakupiga vita ufisadi
(D) alipenda uwazi
(E) alikuwa jasiri na mwenye msimamo
ii. Nini maana ya msemo " ibuka kidedea?" kama ilivyotumika kwenye habari?
(A) kushindwa
(B)kushinda
(C)kupigwa kidedea
(D) kuongoza kijiji
(E) kupigania haki
iii. Viongozi wa kipp wanapatikana kwa njia gani?
(A)kuteuliwa
(B)kupendekezwa
(C)kuteuliwana Rais
(D)kutangazwa na bwana Jumbe
(E)kwa kupigiwa kura na wanakijiji
iv. Nani ni kati ya wafuatao siyo mgombea?....
(A)Mzee Lukuminga
(B)Bwana Jumbe
(C)Mganga
(D) Mzee Mdula
(E) Mzee Mtashi
v. Kijijigani kilifanya uchaguzi wa viongozi?
(A)cha Muungano
(B) Kijiji cha Kalemela
(C) Kijili cha Maendeleo
(D) Kijiji cha Songambele cha Uchaguzi
2. Sarufi na m.atumizi ya lugha.
i. Kama ungalisoma
(A)ungeshinda
(B) ungalishinda
(C)ungelishinda
(D) ungashinda
(E) utashinda
ii. Kwenye jando watu hutahiriwa na
(A)ngariba
(b)manju
(c)kungwi
(D) bawabu
(e)kasisi
iii. Wezi waligeukana na kupigana sana. Sentensi hii ipo katika kauli ipi?
(a)kutenda
(b)kutendwa
(c)kutendana
(d)kutendeana
(e)kutendeka
iv. Maana ya nahau "kumezea mate" ni
(A) kuelewa maneno
(B)kutoboa siri
(c) kukaa bila kuongea
(D)kuongea sana
(E)kutamani
v. Mama amesema rntoto aliyepotea amepatikana akiwahai. Hii ni aina gani ya sentensi?
(A) shurutia
(B) changamano
(C) ambatano
(D) sahili
(E) tata
vi. Walikotoka kuna mvua. Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?
(A)mazoea
(B)shurutia
(C)uliopo
(D)uliopita
(E)ujao
vii. Neno lenye maana sawa na abadani ni ?
(A)katu
(B)daima
(C)ibada
(D)kuta
(E)akili
viii. Kilomo si tajiri hapa kijipni. Neno " si " ni aina gani ya neno?
(A) nomino
(B)kielezi
(C)kitenzi
(D) kivumishi
(E) kihisishi
ix. Kiambishi cha wakati cha neno "utalia" ni
(A)-a-
(B) -ta-
(C)-u-
(D) –i-
(E) tali
x. Alisema kuwa hawezi kuongozana na ninyi. Neno" ninyi" lipi katika nafsigani?
(A)ya kwanza umoja
(B)ya pili wingi
(C) ya tatu wingi
(D) ya kwanza wingi
(E) ya pili umoja
3. 0anisha kifungu 'a' na kifung-u 'b' ili kuleta maana.
KIFUNGU A
MAJIBU
KIFUNGU B
i. Mchelea mwana kulia
A. Kuongeza habari abari zauongo
ii. Ona cha mtemakuni
B. Kuliko kurni nenda rudi
iii. Nitupacho kwake dhahabu
C mbegu
iv. Dau la mnyonge
D. vumilia
v. Kutia chumvi
E. pata shida au taabu
vi. Ona haya
F. moyo
vii. Heri kenda shika
G. Haliendi joshi
viii. Mazishi yake ni furaha kwa watu
H. HUlia mwenyewe
ix. Piga moyo konde
I. Ona aibu
x.Chungu cha mwitu hakiwapiki wapishi wake wakaiva
J. Mzinga wa nyuki
K. inzi
L. miguu
SEHEMU B
4.Sentensizifuatazo zimechanganywa, zipange ili ziletemtiririko unaotakiwa kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E.
i. Bustani zina faid a nyingi sana
ii. Si hivyo to bali zipo bustani za maua pia.
iii. Kwanza huvutia macho ya watu na wadudu.
iv. Bustani ni kilimo cha matunda na mbogamboga
v. Muhimu zaidi hutupatia kivuli na matunda.
5. Tumia maneno katika kisanduku kujaza swali la i hadi v kwa kuandika jibu sahihi. katika nafasi iliyoachwa wazi.
i..............................................
ii.............................................
iii......................................
MWALIMU MKUU,
SHULE YA MSINGI AZIMIO,
S.L.P 57,
MTAKUJA.
Ndugu,
iv.........................................
Tafadhali husika n.a kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Mimi mwanafunzi wa darasa la saba katika shule yako. Ni heshima kwangu kukuandikia barua hii kukujulisha kuwa nimepatwa na msiba, hivyo itanilazimu kuchelewa kurudi shuleni ili niweze kuhudhuria maziko ya marehemu mzee Kilusu kwani ni babu yangu. Kwa taarifa hii naomba nitoe taarifa kuwa nitarejea shuleni siku yaJumatatu. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kunielewa.
Wako mtiifu,
v...............................
Kazaweni Juma Kausa
SEHEMU C
6: Jaza nafasi wazi
i. Andika jina jingine la mnyama mbogo
ii. Andika neno moja badala ya kifungu cha maneno Meza, kiti, kabati, dawati
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 110
OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA NUSU MUHULA WA KWANZA 2024
SOMO: KISWAHILI DARASA: VI
Sikiliza kwa makini habari itakayosomwa na Mwalimu kisha jibu swali la 1-5 kwa kuandika herufi ya jibu hilo atika mabano.
Katika sherehe ziliundwa kamati mbalimbali ili kufanikisha sherehe hiyo. Kamati ya mazingira alihudumu nani? A. Panya B. Bundi C. Kipepeo D. Mjusi E. Nyuki [ ]
Wanakamati wote walikuwa wanapatikana katika eneo wanaloishi lijulikanalo kama A. Ukumbini B. Kwenye sherehe C. Harusini D.Darini E. Kamati [ ]
Paka ,Panya, Bundi na Mjusi wote walikuwa katika kamati lakini chini ya uongozi wa nani kati yao? A. Paka B. Bundi C. Panya D. Mjusi E. Kipepeo [ ]
Ukumbi ulipambwa kwa maua, nakshi na vito mbalimbali. Vito hutengenezwa kwa kutumia A. Maua B. Mapambo C. Madini D. Taa za rangi E. Urembo Urembo [ ]
Wanakijiji walikuwa na shauku ya sherehe ya mwaka. Hii ilipelekea kuwa na maandalizi kabambe. Neno shauku limetumika likiwa na maana ya A Pilikapilika B. Mshawasha C. Tahayari D. Kabambe E. Furaha [ ]
Chagua herufi sahihi kisha andika kwenye mabano
Timu ya waalimu wa shule za Mwamba na Kifaru walicheza mpira wa kirafiki. Kiambishi cha neno walicheza ni
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikombo tunapenda kutoa shukrani setu za dhati kwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kubali ombi letu la kutembelea ombi letu la kutembelea bunge ili v).......................
Tulijifunza mambo mengi na tulipata uelewa wa kutosha kuhusu shughuli za bunge. Mwisho tunawashukuru waheshimiwa wabunge wote kwa ushirikiano waiotuonesha wakati wote tuliokua huko.
Wako watiifu:
Wanafunzi wa darasa la sita.
HABARI
Siku moja katika kijiji cha Darini kulikuwa na pilikapilika za hapa na pale. Wanakijiji walikuwa na shauku ya sherehe ya mwaka. Shauku ilichochewa na maandalizi kabambe yaliyofanywa kwa kuunda kamati mbalimbali. Kiongozi mkuu aliitwa bundi, alimteua Paka mkuu wa kamati ya vinywaji, Panya alipewa kazi ya kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi. Mjusi alikuwa muandaaji wa vyakula vya sherehe. Kamati ya mapambo iliyokuwa chini ya uongozi wa kipepeo iliupamba ukumbi kwa maua, nakshi na vito mbalimbali. Kila aliyefika ukumbini aligawiwa vinywaji avipendavyo na chakula akitakacho Ama kweli sherehe ilifana.
Ndoo ______imejaa maji (A) hili (B) kile (C) hii (D) hiki[]
_______mwalimu alifundisha somo la Kiswahili (A) kesho (B) kesho kutwa (C) jana (D) leo [ ]
Kwa kutumia herufi”dha” unaweza kuunda neno ____ (A) sikio (B) themanini (C) methali (D) dhamana [ ]
Neno wewe lipo katika nafsi gani? (A) ya I umoja (B) ya II umoja (C) ya III wingi (D) ya II wingi [ ]
Wao walikuwa hawana furaha. Taja aina ya nafsi katikati sentensi hii. (A) nafsi ya pili wingi (B) nafsi ya kwanza wingi (C) nafsi ya tatu wingi (D) nafsi ya tatu umoja [ ]
______ mlikuwa washindi (A) sisi (B) yeye(C) wao (D) ninyi [ ]
Wingi wa neno “mimi” ni _________(A) wao (B) sisi (C) ninyi (D) wengi [ ]
SEHEMU B:
Andika sentensi zinazokosekana katika hali ya umoja na wingi
UMOJA WINGI
_____________sisi tunakula nyama
Wewe unakula nyama _________________________
___________________wao wakula nyama
Mimi nitasoma habari ________________________
___________________ sisi ni wanafunzi
Andika sentensi zifuatazo katika kauli taarifa
Nitarudi kuwaandalia chai.
____________________________________
Sipendi majungu.
______________________________________
Sijamwona kaka yangu.
_______________________________________
Tutafunga shule mwisho wa mwezi.
_______________________________________
Nitawatembelea Juma lijalo.
________________________________________
Piga mstari neno ambalo ni tofauti na mengine
Mfano: mbu, mbuzi, mbung’o,nzi,kunguni.
Ng’ombe,nyani, chui, njiwa, kondoo
Ukucha, kidole, mkono, kiwiko, uso
Wali, ugali, chai,pilau,kande
Shati,blanketi, kofia, suruali, kaptura
Bata, mbuni,nyoka,chiriku, kunguru
Jaza nafasi zilizowazi kwa kutumia maneno yaliyomo kwenye kisanduku
Kilele
Mshahara
Kidari
Yatima
Semadari
Panda
Karne
Mbuni
Chui
Tetekuwanga
Almasi
Paa
_____________________ ni aina ya ugonjwa unaoambukiza
Sehemu ya nyumba ya juu __________________
Sehemu ya juu yam lima __________________
Mtoto aliyefiwa na wazazi______________
Aina ya madini magumu yanapatikana ardhini ______________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 97
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI- MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA-2023
DARASA LA SITA
MUDA: 1.30
MAELEKEZO
Karatasi hii ina kurasa nne zenye maandishi yenye sehemu A,B, C,D na E zenye maswali arobaini na tano (45).
Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
Kumbuka kuandika majina yako, na shule yako kwenye karatasi ya kujibia.
Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
Tumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi kwa maswali yote uliyopewa.
SEHEMU A
Sikiliza kwa makini kifungu cha habari. Kisha jibu swali la 1 – 5
Umaskini hauwezi kuondolewa kwa maneno matupu kama vile kuukemea au kuutangaza katika vyombo vya habari. Tunaweza kuondoa umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Ni kazi bure kwa Mkulima, kwa mfano kuendelea kufyeka mashamba mapya kila mara kwa matarajio ya mavuno mengi. Kilimo kinahitaji mkulima awe na juhudi ya kufanya kazi yake. Kilimo cha jembe la mkono hakitamwondolea mkulima umaskini, kutaendelea kumchosha, kumzeesha na kumfanya maskini maisha yake yote. Mkulima lazima abadili fikra zake kuhusu kilimo ili aitumie ardhi kwa usahihi. Hivyo hana budi alime kwa kutumia jembe la kukokotwa na wanyama kazi ambao tunao wengi, kwa kufanya hivyo ataweza kulima shamba kubwa kwa muda mfupi.
Mkulima wa sasa ashauriwe kupanda mbegu zilizochaguliwa vizuri, yaan mbegu bora. Akipanda mbegu zisizokuwa bora, asitarajie kuvuna mazao bor na mengi hata kama mvua zitakuwa nyingi. Mbegu bora hutoa mazao bora. Ni muhimu sana mkulima azingatie kanuni za kilimo bora apande kwa nafasi, apalilie kwa wakati, atumie dawa kuua wadudu waharibifu wa mazao shambani vilevile mkulima atumie mbolea hasa aina ya samadi.
MASWALI
Neno “Umaskini” tunaweza kulifananisha na neno lipi kati ya maneno yafuatayo? (A)ukwasi (B)Utajiri (C)ufukara (D)upungufu (E)Uzee
Mwandishi anasema umaskini hautaondolewa kwa maneno bali utaondolewa kwa kufanya nini? (A)kwa kufuata kanuni za kilimo, kutumia jembe la kukokotwa na wanyama na kutumia mbegu bora (B)kutumia mbegu za asili zilizokakamaa (C)kwa kukopa fedha nyingi benki kwa ajili ya kilimo (D)kwa kutegemea kilimo cha mvua (E)kwa kulima kilimo mseto bil utaratibu.
Wanyama gani wanaotumika katika kurahisisha kazi ya kilimo hapa Tanzania. (A)nguruwe (B)swala (C)ng’ombena punda (D)Twiga na nyati (E)simba na ngiri
Nini maana ya neno “fikra” kama lilivyotumika kwenye habari uliyosoma (A)fariji (B)wazo (C)uelewa (D)ubongo (E)akili
Kutokana na habari uliyoisikia samadi ni mbolea inayotokana na nini? (A)mimea (B)gesi vunde(C)viwanda (D)kinyesi cha wanyama (E)Mabaki ya vyakula.
Chagua jibu sahihi
Neno lipi kati ya maneno yafuatayo ni jumuishi kwa maneno haya “nyanya, vitunguu, pilipili na tangawizi. (A)nafaka (B)matunda (C)vinywaji (D)vitoweo (E)viungo
Sote tunacheza mpira uwanjani neno uwanjani limetumika kama aina gani ya maneno. (A)kivumishi (B)kielezi (C)kitenzi (D)Kiwakilishi (E)nomino
Nomino inayotokana na kitenzi “Cheza” ni ______ (A)chezeka (B)mpira (C)anacheza (D)mchezo (E)chezea
Maneno yenye maana sawa katika lugha ya kiswahili hujulikana kama _____ (A)visawe (B)vitawe (C)vitenzi (D)vidahizo (E)vitate
Kitenzi kinachotokana na nomino uvuvi ni _(A)vuna (B)vua (C)samaki (D)nyavu (E)vuta
Katika neno “sikujua” kiambishi kipi kinaonesha ukanushi (A)siku (B)jua (C)a (D)-ku- (E)si-
Nini kinyume cha neno duni (A)thamani (B)kidogo (C)dhaifu (D)kikubwa (E)Imara
Wote tulimpokea mgeni rasmi. Sentensi hi ipo katika kauli ya (A)kutenda (B)kutendwa (C)kutendea (D)kutendeana (E)kutendwa
Mtaalamu wa Elimu ya Nyota huitwa _________ (A)mtabiri (B)dazeni (C)mnajimu (D)mkalimani (E)mwanang’aa
Mwana wetu ameenda shuleni _________ afya yake si nzuri (A)Ikiwa (B)pamoja na hayo (C)ili (D)kama (E)ingawa
“Wimbo huu hauimbiki” sentensi hii iko katika kauli __________ (A)kutendana (B)kutendeka (C)kutendwa (D)kutendeana (E)kutenda
Alikaa kimya __________ alisikia tukimwita (A)kwa kuwa (B)japokuwa (C)kwa vile (D)pia (E)vile vile
Alimsihi asimwadhibu. Sentensi hii ipo katika kauli ipi? (A)halisi (B)kutendewa (C)taarifa (D)pevu (E)kutendeana
“Huyu unaemuona hapa ni mama yangu na yule pale ni baba yangu” “huyu” na “yule” ni aina gani ya maneno? (A)vivumishi (B)vielezi (C)vitenzi (D)viwakilishi (E)nomino
Nini kinyume cha neno “huzuni”? (A)masifu (B)farakana (C)sifia (D)chukia (E)Furaha
Kivumishi ni neno linalotoa taarifa zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi, katika sentensi hii “wanafunzi wale wanapenda kucheza mpira” neno lipi limetumika kama kivumishi (A)wanafunzi (B)mpira (C)wanapenda (D)wale (E)kucheza
“Nyumba imeezuliwa kwa upepo mkali” sentensi hii ipo katika kauli gani_____ (A)kutendwa (B)taarifa (C)halisi (D)kutendewa (E)kutenda
Ili tuvune mazao bora na mengi ______ tulime kwa juhudi na maarifa (A)ni budi (B)hatuna budi (C)budi (D)hawana budi (E)hamna budi
Baba atamkanya mjomba ili aache ulevi. Sentensi hii ipo katika wakati gani? (A)timilifu (B)ujao (C)uliopo (D)mazoea (E)uliopita
Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana sawa na neno shehena? (A)Robota (B)bidhaa (C)mzigo (D)roda (E)furushi
Baada ya Ali kuasi Ukapera wazazi wake walimpongeza. Kuasi ukapera maana yake ni _ (A)kuacha kazi ya kutumikisha (B)kuacha kucheza mpira (C)kuacha wizi (D)kupata kazi (E)Kuoa
Walimu walipigwa na butwaa baada ya kuona matokeo ya darasa la saba. Nahau “kupigwa butwaa” maana yake ni (A)kushangaa (B)kustuka (C)kukimbia (D)kulia (E)kufurahi
Methali isemayo “mdharau mwiba mguu huota tende” ina maana sawa na methali ipi ___ (A)maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge (B)usipoziba ufa utajenga ukuta (C)mwenda pole hajikwai (D)fuata nyuki ule asali (E)penye miti hapana wajenzi
Nini maana ya nahau “ana mkono wa birika” (A)mwizi (B)mfupi (C)mkarimu (D)umepinda (E)mchoyo
Maana ya nahau “piga jeki” ni ipi? (A)kumweka mtu (B)kumuumiza mtu (C)kumwonea mtu (D)kumwadhibu mtu (E)kumsaidia mtu
Neno “Mwangwi” ni jibu la kitendawili kipi kati ya vifuatavyo (A)huku ng’o na huko ng’o (B)jinamizi laniita lakini silioni (C)huku pili na huko pili (D)kila niendapo ananifuata (E)sirudi tena kwa mjomba
Ipi maana sahihi ya neno “aghalabu” (A)Mara nyingi (B)mara moja (C)mara chache (D)mara dufu (E)mara nyingine
SEHEMU B: Utungaji
Panga sentensi zifuatazo ili ziletee habari yenye mtiririko mzuri kwa kuzipa herufi A B C D E
Vile vile matunda huongeza damu mwilini
Kula matunda kuna saidia kuponyesha magonjwa na vidonda haraka
Hivyo matunda yana umuhimu mkubwa katika miili yetu
Pia husaidia macho kuona vizuri katika mwanga hafifu
Lakini watu wasiokula matunda hupata maradhi kama vile ugonjwa wa fizi macho na ngozi.
SEHEMU C: Ufahamu
Baraka alizaliwa huko mkoani Mbeya mwaka 1978. Alizaliwa katika mwaka ambao nchi ya Tanzania iliingia vitnai na nchi ya Uganda. Baba yake Baraka alitamani kumwita mwanaye jina “Vita” kwa sababu alizaliwa mwaka wa vita. Mama yake Baraka hakuafiki kumwita mtoto wa jina la “Vita” kwani aliamini jina la mtu ndiyo mtu mwenyewe. Hivyo kumwita mtoto vita ingeweza kumfanya mtoto huyo kuwa ni mwenye kupenda vita au vurugu za aina nyingine. Kwa hiyo baada ya malumbano na mjadala wa muda mrefu, wakafikia muafaka wa kumwita mtoto wao Baraka. Jina lenye maana na tafsiri vizuri na isiyokuwa na mashaka
MASWALI
Baraka alizaliwa lini
Nani alitamani jina “Vita”
Kwa nini mama yake Baraka alikataa kumwita mtoto wake vita
Neno “malumbano”katika habari hii lina maana gani
Baba alitaka mtoto wake aitwe “Vita” kwa sababu gani?
TUMIA MANENO HAYA KUJAZA NAFASI ZILIZO ACHWA WAZI (andika herufi ya jibu sahihi)
A. NAKUSANYAB. JINAC. MTIHANI D. MAELEKEZO E. MAREKEBISHO
Kila ifikapo wakati wa mtihani ninajiandaa kikamilifu. Mtihani uletwapo kwenye chumba cha mtihani mimi husali. Nikiruhusiwa kuanza kufanya mtihani hatua zangu ni kama ifuatavyo: Hatua ya kwanza 36. __________. Hatua ya pili husoma 37. _____________________ya mtihani. Baada ya hapo huaanza kufanya 38. _________________________. Nifikapo swali la mwisho hukagua karatasi ya maswali na kufanya 39. ____________________. Baada ya hatua zote huwa nimeridhika , hivyo 40. _____________________mtihani nikiwa na
uhakika wa kufaulu.
Soma kwa makini shairi lifuatalo na kisha jibu maswali 41-45 majibu mafupi
Kasimama kizimbani, popo anatetemeka, Kaitwa mahakamani, popo kujibu shitaka, Atakiwa abaini, kwa ulimi kutamka, Ajitetee bayana, ni mnyama au ndege.
Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea,
Sinajadinakunguru, ikiwapundamilia,
Mimi ni mnyama huru, amini ninakuambia, Tukidaiwa ushuru, kwa wanyama nalipia.
Ni kweli popo napaa, na mabawa ninayo, Lakini mimi nazaa, hili halina utata, Kuwa ndege nakataa, sina undugu na bata, Nakataa katakata, mimi si ndege nasema.
Maswali
41. Popo anakataa kuwa Si ndege kwa sababu gani?__________________________________________________
42. Katika ubeti wa pili popo anasema “sina jadi na kunguru”. Usemi. “sina jadi” una maana gani?____________
Simu ni chombo kinachotumika kupelekea nakupokeleamawimbi ya sautibaina ya mtu na mtu papo kwa hapo. Zipo aina mbalimbaliza simu kama vilesimutambanatelegramn.kambazomtuhuwezakupatamawasilianoanayotaka.Simutambanisimuambayowatuwengihuwanazokwamawasilianonanitofautinatelegramambayohuandikwakwakutumiagharamakubwa.
Hivyo basi simu ni chombo muhimu sana cha mawasiliano ambacho hutupautandawaziwamambomengiyanayoendeleadunianzimahasakatikamasualayabiashara,uchuminasiasa.Vilevilesimuikitumiwavizuriinaweza kuleta faida kubwa kwa mtumiaji yaani kupata elimu na maarifamapya,
pia simu ikitumiwa vibaya inawezakumletea mtumiaji madhara makubwakatika jamii kwa kuiga tabia fulani ya mtu au kujifunza mambo yasiyoendananajamiiyake.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 76
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA KWA SHULE ZA MSINGI
MTIHANI MWA MWISHO WA MUHULA-MEI-2023
DARASA LA SITA
KISWAHILI
MUDA: SAA 1:30
MAELEKEZO
Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu
Jibu maswali yote
Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
Tumia penseli ya HB tu
Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani
SEHEMU A: UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa na msimamizi kisha jibu swali 1 – 5 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu sahihi katika fomu yako ya kujibia.
Kutokana na habari uliyosikiliza, ni nani aliyezungumziwa?
(a) Amani(b) Bibi(c)Wananchi(d) Bibi na Amani(e) Kilole
Amani alimuuliza swali gani bibi yake? (a)Kama unajua kusoma na kuandika (b)Kama unajua kuandika (c)Kama unajua kusoma (d)Kama unajua kuimba na kuandika (e) kama unajua kuimba
Amani anaishi katika kijiji cha Kilole. Je, Amani anaishi na nani?
(a)Bibi (b)Babu(c)Shangazi(d)Mjomba(e)Babu na Bibi
Kwa mujibu wa habari uliyosikiliza. Amani ana tabia gani?
(a)Mvivu(b)Mdadasi(c)Mkarimu(d)Mchapakazi na mdadisi(e)Mpole
Kichwa cha habari hii kinafaa kiwe kipi miongoni mwa hivi?
(a)Kijiji cha Kilole (b) Amani(c)Amani na bibi yake(d)Kilole (e)Bibi
Katika swali la 6 – 35 weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi
Neno machweo lina maana ipi kati ya hizi zifuatazo?
“Kazi mbaya si mchezo mwema” methali inayofanana na methali hii ni ipi kati ya hizi zifuatazo? (a)hewala haigombi (b)mchezea tope humrukia (c) mcheka kivu asiyefikwa na jeraha (d)lila na fila havitengamani (e)mcheza kwao hutunzwa
Wanafunzi wale wanapenda kucheza mpira. Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi? (a)wanafunzi (b)wale (c)wanapenda (d)mpira (e) kucheza
Katika lugha ya kiswahili neno “staftahi” lina silabi ngapi?
(a)sita (b)tano (c)nne(d)tatu(e)saba
“Ukitaka kuruka agana na nyonga”. Sentensi hii iko katika aina gani ya sentensi kati ya hizi? (a)sahihi (b)ambatano (c)changamano (d)tegemezi (e)shurutia
Ipi ni maana ya kitendawili “nyumba yangu imeungua mwamba wake umebaki”
(a)mfupa (b)njia(c)kaburi(d)kisima(e)mlima
Kuwa na Nyota ya jaha maana yake ni ______ (a)jua la mchana (b)Nyota ya asubuhi
(c) Bahati nzuri (d)Bahati mbaya (e)Bahati nasibu
Wewe ni mtoto mdogo sana. Sentensi hii iko katika nafsi gani?(a)ya kwanza umoja
(b)ya pili umoja(c)ya tatu wingi(d)ya pili wingi (e)ya kwanza umoja na wingi.
Watu hufanya kazi mbalimbali ili kuweza kujipatia kipato. Mtu anayefanya kazi ya kutunza na kuazima vitabu anaitwa Mkutubi. Je! Mtu anayefanya kazi ya kuzibua vyoo anaitwa nani? (a) kuli (b)topasi (c) toinyo (d)chepe (e)zubaifu
Bwana Afya aliuliza, kuna umuhimu gani wa kuchemsha maji ya kunywa? Je sentensi hii iko katika kauli ipi kati ya zifuatazo? (a)taarifa (b)halisi (c)tata (d)tungo huru (e)kutenda
Ali anakula wali ____ maharage. (a)na (b)kwa (c)ni (d)ya (e)pamoja
Simba mkali amepita shuleni kwetu. Mchanganuo wa sentensi hii ni upi kati ya michanganuo ifuatayo? (a)T+N+V+W+E (b)N+E+V+T+W (c)V+E+T+W+N (d)N+V+T+E+V (e)N+V+E+T+V
Kinyume cha methali isemayo; “Ngoja ngoja yaumiza matumbo” ni ______ (a)bendera hufuata upepo. (b)mtu hujikuna hajipatiapo (c) mwisho hadhuru maiti (d)haraka haraka haina Baraka (e) asiyesikia la mkuu huvunjika guu
Wakoloni walitunyanyasa lakini hatimaye unyanyasaji huo ulifika ukingoni kwani ___Ni methali ipi kati ya zifuatazo inamalizia sentensi hii? (a)hakuna marefu yasiokuwa na ncha (b)mchumia juani hulia kivulini (c)ukiona vyaelea ujue vimeundwa (d)umoja ni nguvu utengano ni udhaifu (e)bandubandu humaliza gogo.
Kazi ya Daudi ni kazi ya kijungujiko. Je! Kazi ya kijungujiko ni kazi ya aina gani? (a)Kazi ya kuchimba vyoo (b)kazi ya kujitolea (c)Kazi ya kufundisha wanafunzi (d)kazi isiyo rasmi au inayotosha mahitaji yam lo tu. (e) kazi ya kikoa
Ikiwa mzizi wa neno “PIK” tukiunda neno litakalokuwa katika wakati uliopita nafsi ya kwanza umoja hali ya kutenda tunapata neno. (a)alipika (b)nilipika (c)walipika (d)tulipika (e)nimepika
Akikosekana maana inakosekana. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?(a)kitabu
(b)Kamusi(c)magazeti(d)shairi(e)Vipeperushi
Mashairi ya kimapokeo yamegawanyika katika aina mbalimbali. Je ubeti wa shairi wenye mistari minne huitwaje?(a)mshororo (b)tarbia (c)Kituo (d)Kibwagizo (e)mizani
Mnyama ambaye amekuwa laini bado hajazaa anaitwa _____
(a)mtamba(b)Mbuguma(c)Maksai(d)fahali(e)beberu
Nenda ukawasikilize watakachokueleza uniletee mrejesho. Katika sentensi hii mtenda ni nafsi ya ngapi? (a)ya kwanza umoja (b) ya pili umoja (c)ya tatu wingi
(d) ya kwanza wingi (e)askari mwenye cheo cha juu
Ali ni askari kazu. Ali ni _____ (a) trafiki (b)kanga (c)bunduki (d)mpelelezi
(e) askari mwenye cheo cha juu
Jambazi alihukumiwa kwa kuua mfanyabiashara. Sentensi hii iko katika hali gani?
(a)hali timilifu(b)hali ya kuendelea(c) hali isiyodhihirika (d)hali ya mazoea (e)hali tata
Tungo changamano ni tungo yenye vishazi vingapi?(a)viatu(b)viwili
(c)vinne(d)vitano(e) kimoja
Kisawe cha jogoo ni jimbi, kisawe cha beseni ni karai. Je kisawe cha kinyonga ni ____
(a)bomba(b)hua(c)lumbwi(d)kelbu(e)baghala
Katika neno anacheza. Kipi ni kiambishi njeo?(a)-a-(b)-na- (c)-chez-
(d)-a-(e)-cheza-
Lipi kati ya maneno yafuatayo si kivumishi likiambatanishwa na nomino? (a)Yule
(b)nzuri(c)polepole(d)huyo(e)hawa
SEHEMU B:
Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A – E ili zilete maana kamili kwa mujibu swali la 36 – 40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi
Niliogopa lakini nilipiga moyo konde
Nilirudi nyuma kidogo nikaokota fimbo na kumpiga
Jumamosi iliyopita mama alinituma sokoni
Nilipokuwa njiani nilimwona nyoka
Aliniambia ninunue nyanya, vitunguu, sukari na mafuta
SEHEMU C:
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo
Masebo ni mwalimu anayefundisha katika shule ya Msingi Maendeleo iliyoko wilaya ya Masasi. Anakaa katika kitongoji cha usafi kilichopo umbali wa kilometa tano kutoka shuleni. Siku moja mwalimu Masebo alikuwa anakwenda shuleni. Pembezoni mwa msitu wa kijiji aliwaona vijana watatu, vijana hao walikuwa wakikata miti kwa kutumia mapanga na mashoka na kuivundika pembeni. Aliwatambua vijana hao kuwa ni Juma, sadiki na Joseph. Mwalimu Masebo alisikitika sana. Alisimamisha pikipiki yake haraka na kwenda katika eneo lile. Alianza kuwafokea vijana wale kwa kukata miti mingi kiasi kile. Vijana wale walishangaa sana.
Maswali:
Juma, Sadiki na Joseph walikuwa wanafanya nini msituni?
Mwalimu Masebo aliona nini pembezoni mwa msitu wa kijiji?
Je! Ukikuta watu wanaoharibu mazingira utafanya nini?
Kwa nini mwalimu Masebo alisikitika sana?
Kwa nini tunashauriwa kutokata miti ovyo?
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Amani anaishi na bibi yake katika kijiji cha Kilole. Anamsaidia bibi yake shughuli za nyumbani. Anamsaidia kusafisha nyumba, kupika, kuosha vyombo na kufua. Juzi Amani alimuuliza bibi yake; bibi unajua kusoma? Bibi akajibu ninajua kusoma na kuandika. Amani akasema sawa bibi, kesho nitaleta kitabu changu ili tusome pamoja.
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu swali la 31 – 40 kwa kuandika herufi ya jibusahihi
Umma ulipozinduka na wakawauliza wafalme walivyotajirika kinyume na matarajio yaumma, kulikuwa na vita……”watu wetu wanatuonea”. Watu hawakuwaelewa….hawakurudinyuma,walichukuakilichochao.Hiindiohadithiyakisiwachawafalme!Kijijihichokilikuwanaviwanda mbalimbalivilivyosaidia kujenga nakuinua uchumiwake.
Waliteuliwa wakurugenzi wa aina aina waliosaidiwa na watumishi wengi kukamilisha serayao ya kazi lakini shetani mbaya – pesa! Alikuwa sehemu hii. Wakurugenzi walikula,wahasibu walikula, watumishi pia walikla. Kwa ufupi kila mtu alikula. Walipoona wanatakakushikwa kwa makosa ya kula kilicho cha umma, wakachoma moto kiwanda chao ilikupoteza ushahidi. Hasara ilibaki kwa umma. Wao wakaanzisha miradi iliyowalisha kwakutumiapesaza umma.
Wengine nao walipoona hayo nao wakaiga. Matokeo yake vikajengwa vijiji kama vile vyawafalme. Umma pia ukashtuka, ukawauliza na kisha kuchukua haki zao kwa nguvu. Hivyohadithi iliyotamba mwanzo ikawarudia tena watu hawa na ukweli ukabaki kuwa jamiiisiyojuakiinicha matatizoyake haiwezikuyatatua.
Katika habari hii hapa juu, Methali ipi inaweza kuwa na mafunzo sawa na habari hii hapojuu?
Kisawechaneno‘utajiri’ni
SEHEMUE:USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 41 hadi 46 kwa kuandika herufi ya jibusahihi
Nami nashika kalamu, maana menilazimu.Nawataka mfahamu, kuhusu mambo muhimu,Maana mekuwa ngumu, kuachwa na wahujumu,Rushwaniaduiwa haki,wananchitupingeni.
Mepewa majina mengi, lukuki yaso idadi,Maana walafi ni wengi, kila siku wanazidi,Waheshimiwa na wengi, wamekuwa wakaidi,Rushwaniaduiwa haki,wananchi tupingeni.
Inaitwa takrima, au chai ya mgeni,Mnapotaka huduma, basi mikono nyosheni,Na mkijiweka nyuma, huduma isahauni,Rushwa niaduiwa haki,wananchitupingeni.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 65
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI WA MWISHO WA MWAKA
KISWAHILI
DARASA LA SITA
2022
JIBU MASWALI YOTE
SEHEMU A
Sikiliza kwa makini habari inayosomwa na msimamizi kisha jibu maswali 1 – 5 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuandika katika karatasi ya kujibia.
Fisi na sungura walialikwa kwenye karamu moja. Basi wakajiandaa kwa safari. Kabla ya kuondoka Sungura akamwambia fisi, “Bwana huko tunakokwenda nimesikia ni kwa watu waungwana. Hivyo inabidi tubadilishane majina yetu”. Fisi akadakia, “Wasema kweli?” Sungura akamwambia Fisi, “Ndivyo. Hivyo mimi nitakuwa ‘cha wageni’ na wewe utakuwa ‘cha wote’. Fisi akakubali. Walipofika huko wakakaribishwa. Muda wa chakula ulipofika, mtoto mmoja akawa analilia chakula cha wageni. Mama yake akamwambia, “Hicho ni chakula cha wageni” Sungura aliposikia hivyo akamwambia Fisi, “Umesikia? Chakula hicho ni changu mimi cha wageni. Wewe subiri cha wote”. Basi ikabidi sungura ale chakula chote na kumwacha Fisi na njaa.
Fisi na sungura walialikwa wapi?
Shambani
Kwenye karamu
Mwituni
Ugenini
Cha wote
Nani alililia chakula?
Fisi
Sungura
Mtoto
Wageni
Mama
kwa nini fisi hakula chakula?
Chakula kilikuwa kibaya
Alikuwa ameshiba
Wenyeji walimkataza
Hakupendezwa nacho
Sungura alimdanganya kuwa chakula kilikuwa ni chake.
Sungura ana tabia gani?
Watoto
Wanyama
Sungura na fisi
Huruma
Uchoyo
Nani walialikwa kwenye sherehe?
Watoto
Wanyama
Sunguru na fisi
Mama na mtoto
Dhihaka
Chagua herufi ya jibu na kisha andika katika karatasi ya kujibia.
“Wapiganaji wetu walipowasili visiwa vya Comoro walishangiliwa kwa …… “Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
Hofu
Mzaha
Shangwe
Mayowe
Dhihaka
Mawaziri wote wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa. Neno “Wote” limetumika kama aina gani ya neno?
Nomino
Kiwakilishi
Kitenzi
Kivumishi
Kiunganishi
Babu amemhamishia yule mbuguma kwenye zizi kubwa . Neno “Mbuguma” lina maana ipi?
Mbuzi dume anayelima
Ng’ombe dume anayelima
Kondoo jike aliyezaa
Ng’ombe jike anayelima
Ng’ombe jike anayeendelea kuzaa
“Chama kimeteka nyara sera ya serikali.” Wingi wa sentensi hiyo ni upi?
Vyama vimeteka nyara masera ya serikali
Vyama vimeteka nyara sera ya serikali
Vyama vimeteka nyara serikali
Vyama vimeteka nyara sera za serikali
Vyama vimeteka nyara visera vya serikali
Nyumba ya ndege huitwaje?
Mzinga
Kiota
Korongo
Banda
Shimo
“Wanafunzi hodari watapewa zawadi”. Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?
Ujao
Timilifu
Uliopita
Mazoea
Uliopo
Maji yamejaa “Pomoni”. Neno “pomoni” ni aina ipi ya neno?
Nomino
Kiwakilishi
Kielezi
Kihisishi
Kivumishi
Kati ya maneno “Sherehi, Sherehe, Shamrashamra, Halfa, Tafrija” neno lipi halihusiani na mengine?
Sherehi
Sherehe
Shamrashamra
Hafla
Tafrija
Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na “thubutu”?
Ufidhuli
Ujasiri
Umahiri
Ukakamavu
Utashi
“Kuzua kizaazaa” ni msemo wenye maana gani?
Ushabiki
Upendeleo
Malumbano
Masikikitiko
Majungu
Mtu anayetafuta kujua jambo Fulani kwa kuuliza maswali huitwaje
Mawazo
Mbeya
Mfitini
Mdadisi
Mjuaji
Neno “Mchakato” lina maana ya mfululizo wa ……..
Mawazo
Maoni
Shughuli
Safari
Fikra
Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno “shehena”?
Roda
Furushi
Mizigo
Bidhaa
Robota
Mtu aliezaliwa na wazazi wa rangi mbalimbali huitwaje?
Albino
Mkimbizi
Mhamiaji
Chotara
Mzawa
Baada ya miaka minne kalunde ……. Mafunzo yake ya udaktari. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
Aliitimu
Alihimidi
Aliitimisha
Alihitimu
Halihitimu
Methali isemayo “katika msafara wa mamba na kenge wamo” Iko sawa na methali ipi kati ya zifuatazo.
Akutukanaye hakuchagulii tusi
Kila kiboko na kivuko chake
Amulikaye nyoka huanzia miguuni mwake
Tajiri na mali yake maskini na mwanawe
Hakuna masika yasiyo na mbu.
Diengi anapenda kuwarairai watu. “Kurairai watu” ni msemo wenye maana ipi?
Kuwasihi watu ilia pate cheo anachokipenda
Kusema na watu kwa maneno mazuri
Kusema na watu ili uwape chochote
Kusema watu kwa ajili ya kuwatapeli
Kuwabembeleza watu ili wasimpangie kazi.
Msemo “kubarizi” maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya ………..
Sherehe
Mkutano
Mazungumzo ya kawaida
Burudani
Chakula cha pamoja
Methali isemayo “Kila mtoto na Koja lake” ina maana gani?
Kila binadamu ana mapungufu yake
Kila mtoto ana mapungufu yake
Kila mtoto ana wazazi wake
Kupewa sifa mbaya
Kupewa sifa chache
Nahau isemayo “Kuvishwa kilemba cha ukoka” ina maana gani?
Kupewa sifa unazostahili
Kupewa sifa mbaya
Kupewa sifa nyingi
Kupewa sifa chache
Kupewa sifa usizostahili
Tegua kitendwali kifuatacho; “Nyumbani kwangu kuna jinni mnywa maji”
Kikombe
Kata
Kinywa
Kibatari
Mtungi
“Wakulima wa kahawa wa wilaya ya mbinga wamepewa heko kwa kuzalishana kahawa bora”
Kupewa tunzo
Kupewa pongezi
Kupewa heri
Kupewa zawadi
Kupewa hawala
Methali isemayo, “Mwenda pole hajikwai” inafanana na methali ipi kati ya zifuatazo?
Haba na haba hujaza kibaba
Fuata nyuki ule asali
Awali ni awali hakuna awali mbovu
Mchumia juani hulia kivulini
Baada ya dhiki faraja
Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haifanani na zingine?
Mtegemea nundu haachi kunona
Nazi haishindani na jiwe
Mlinzi wa kisima hafi kiu
Mchumia juani hulia kivulini
Baada ya dhiki faraja
Mwamba ngoma …….. kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hiyo?
Hualika watu wengi
Hufanya maandalizi mengi
Huimba nyimbo nyingi
Ngozi huvutia kwake
Hucheza na jamaa zake
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 31 – 35 kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya majibu.
Nimekwisha peleleza , karibu kila mahali,
Mule wanamotangaza, matangazo lugha mbili,
Juu kuwa kingereza, chini kuwa Kiswahili,
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe kingereza.
Kitangazwe kingereza, baada ya Kiswahili
Hivi tutapotimiza, lugha itakuwa ghali,
Hivi mnayofanyiza, sana mnaidhalili,
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe kingereza
Serikali bembelezwa, tafakari tafadhali,
Jambo hili kueleza, kwa zingine serikalini
Kiswahili kutangaza, kuwa chini twakidhili
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe kingereza
Tuache kukipumbaza, kwa andiko au kauli,
Kwa nyuma kukisogeza, kukipa kisulisuli,
Lazima kuyafukuza, yawezayo kikatili,
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe kingereza
Na wenyewe kujikaza, kwa bidi za kimwili
Kiswahili kutukuza, tukivalie bangi,
Ngomani kutumbuiza, waume kwa wanawali
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe Kingereza
MASWALI
Katika shairi hilo mstari wa pili katika ubeti wa pili una mizani mingapi?
Tano
Mbili
Kumi na sita
Nane
Thelathini na tatu
Katika ubeti wa nne vina ni vipi?
Za na li
La na li
La na ya
Ju na za
Tu na li
Kituo ni kipi katika shaiti hili?
Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali.
Kitangazwe kingereza, badala ya Kiswahili
Serikali bembeleza, tafakari tafadhali.
Tuache kukipumbaza, kwa andiko na kauli
Juu kiwe Kiswahili, chini kiwe kingereza.
Shairi hili linahimiza kuhusu nini?
Kudumisha na kuendeleza mila
Kudumisha na kuendeleza jadi zetu
Kudumisha lugha ya kingereza
Kudumisha na kuendeleza Kiswahili
Kudumisha na kuendeleza lugha
Ujumbe unaopatikana katika shairi hili unafanana na methali ipi?
Asiesikia la mkuu huvunjika guu.
Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu
Mkono usioweza kuukata ubusu
Ukitaka cha uvunguni sharti uiname
Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani
SEHEMU B
UTUNGAJI
Umepewa habari yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bili mtiririko sahihi wa mawazo katika maswali 36 – 40. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E. weka kivuli katika hefuri ya jibu sahihi.
Hivyo mazoezi huleta afya, kwa hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi.
Lakini mtu asiyefanya mazoezi anapata maradhi ya moyo; atanenepa kupita kiasi, kwa hiyo atapata ugonjwa wa kuumwa mgongo na magoti.
Mazoezi ya viungo yanachangamsha misuli ya mwili, mifupa na ubongo.
Mtu anaefanya mazoezi anaepuka magonjwa ya moyo na msukumo wa damu.
Watu wengi hupenda kufanya mazoezi.
SEHEMU C
UFAHAMU
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 41 – 45 kwa kuandika lililo sahihi.
Mpendwa kaka Yohana,
Natumaini hujambo na unaendelea vizuri na masomo yako. Nimefurahi kusikia kwamba umechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. Ndugu wote wanakupongeza na kukutakia kila la kheri katika masomo yako. Soma kwa bidii Zaidi kwani elimu ni bahari na haina mwisho.
Baba na mama walifurahi sana baada ya taarifa za kuchaguliw kwkao kwa njia ya simu kutoka kwa shangazi. Wanamshukuru sana shangazi kwa kukuwezesha na misaada yake mingi kwako ya hali na mali. Baba ameahidi kumtembelea shangazi tarehe ishirini mwezi wa kumi na moja mwaka huu ili kumkabidhi zawadi aliyomuandalia kutokana na ukarimu wake kwak.
Rafiki yake Juma alifika hapa nyumbni akisema kwamba picha nikutumie. Hamisi amekuandalia zawadi ambayo atakukabidhi utakapokuja nyumbani wakati wa likizo yako ya mwisho wa muhula tunu amesema atakutembelea, lakini uwe mwangalifu unapoongea naye asije akakuchezea katika masomo yako.
Akupendae daima,
Mdogo wako Tumaini
MASWALI
Neno “ukarimu” lina maana ipi:
Mwandishi wa barua hii ametumia msemo “Kuchezea shere” Misemo huo una maana ipi?
Katika barua hii mwandishi anafananisha elimu na nini?
Lengo la Tumaini kumwandikia kaka yake barua lilikuwa lipi?
UmepewaInshayenyesentensitano (5) zilizoandikwabilamtiririkosahihiwamawazo. Zipangesentensihizoiliziwenamtiririkowenyemantikikwakuzipa A, B, C, D na E ilikujibumaswali 31 – 35
31.Tutaendelea kusaidiananakushirikianakatika mambo mbalimbalihasa katikashughuli za kiuchumi, kielimunakijamii
32.Kumekuwa namwingilianowatamaduni za kigenikatikanchizetumfanomavazi, lugha, ngoma, nyimbo, milanadesturi
33.lakini katika Kijiji chetu cha Tupendanetumeamuakudumishaupendonaushirikianomiongonimwetu.
(B)ndiyomudawakupumzika (C)ndiyomudawakulea Watoto (D)ndiyomudawakusinzia (E) ndiyomudawakushindanjaa
SEHEMU E UFAHAMU
Soma kwamakinikifungu cha habarikifuatachokishajibumaswaliyanayofuata
MiongonimwamashujaaambaohawawezikusahaulikakatikahistoriayanchiyetuniMtwaMkwawa. Huyualikuwakiongoziwakabila la waheheMkoani Iringa. Baba yakeMkwawaalitwaMunyigumba. Mkwawaaliongozamapambanomakalidhidhiyawajerumanikuanziamwaka 1891 hadimwaka 1898. Alifanikiwakuwauawajerumaniwengiakiwemoaliyekuwakamandawakikosi cha kijerumanialiyejulikanakwajina la Emili Zelwski. Mara baadayakuuawakwakamandaZelwiskiMnamomwaka 1891, Gavanawaujerumanialiwamuruwanajeshi wake wamtafuteMkwawakwanguvuzotehadiwamkamate. BaadayaMkwawakugunduakuwaamezidiwasananawajerumaniakaamuakujiuakwakujipigarisasiyeyenamlinzi wake kwakuhofiaasikamatwenawajerumani.
41.kwa mujibuwakifunghiki cha habari, nishujaaganihawezikusahaulikakirahisikatikahistoriayanchiyetu?
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 52
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI DARASA LA SITA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA
SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI KUTOKANA NA HABRI ULIOSOMEWA
Mwandishi anasema mwezi huangaza kwa sababu
Unaakisi mwanga wa jua
Unatoka usiku
Uko angani,
Unatoa nuru yake
Huangaza
Kwenye mwezi hakuna kimbuga kwa sababu, (a) kuna mawe tu (b) hakuna upepo (c) pako kimya (d) hakuna maji (e) hakuna miti
Mtu akiwa kwenye mwezi kisha akaongea hawezi kusikika kwa vile, (a) hakuna upepo (b) kuna joto kali (c) hakuna maji (d) hakuna hewa (d) kuna kila kitu
Ardhi ya kwenye mwezi ina……………(a) vumbi na majani (b) mawe na miti (c) mawe na vumbi (d) majani na miti (e) maji tu
Binadamu hawezi kuishi kwenye mwezi kwa sababu (a) hakuna miti wala hewa (b) hakuna nuru wala maji (c) kuna baridi na vumbi (d) hakuna maji na hewa (e) kuna unyevu
SARUFI: Chagua herufi ya jibu sahii
Sote tunacheza mpira uwanjani. Neno uwanjani limetumika kama aina ya neno gani?
Nini kinyume cha neno Dunia? (a) thamani (b) kidogo (c) dhaifa (d)kikubwa (e) imara
Wote tulimpokea mgeni rasmi. Sentensi hii ipo katika kauli ya (a) kutenda (b) kutendewa (c) kutendea (b) kutendeana (e) kutendwa
Mtaalamu wa elimu ya nyota huitwa……(a) mtabiri (b) dazeni (c) mnajimu (d) mkalimani (e) mwanaanga
Kuwa na shingo ngumu ni…………………………(a) kuwa na shingo isiyogeuka (b) kuwa mkaidi (c) kuwa mvumilivu (d) kubeba mzigo (e) kubeba mzigo mzito
Neno lipi linakamilisha methali ifuatayo? ……..mpishe (a) mwenye nguvu (b) mkimbizi (c) mwanafunzi (d) mwenye busara (e) usimpige
Mtu anayetenda kinyume na asemavyo kwa wenzake huitwa……….(a) mnafiki (b) mwongo (c) mhuni (d) mkweli (e) longolongo
Maana ya Nahau “Tia nanga” ni (a) kuondoka kwa meli (b) kusimama kwa meli (c) kuogelea majini (d) kuzama (e) kuibuka
Kamilisha methali ifuatayo. “Jino la pembe……………….” (a) si jino (b) husaidia jina (c) dawa ya pengo (d) husaidia kutafuna (e) sio dawa ya pengo
Nyumbani kwangu kuna jinni mnywa maji…..(a) kikombe (b) kibatari (c) maji (d) mtungi (e) pipa
Neno “kubarizi” maana yake ni…………………(a) kupunga hewa (b) sherehe (c) mkutano (d) chakula ( e) kubanika
Baada ya Edson kuasi ukapera, wazazi wake walimpongeza. Kuasi ukapera maana yake ni……
(a) kuacha kazi ya kutumikisha (b) kuacha kucheza mpira (c) kuacha wizi (d) kupata kazi (e) kuoa
Mama anauza vitumbua, baba anafanya kazi ya ulinzi. Sentensi hii ni………..(a) ghangamano (b) tegemezi (c) sahihi (d) shurutia (e) ambatana
Maimu ni mtoto wa kitukuu change, hivyo maimu ni (a) mpwa wangu (b) kiningina (c) kilembekezi (d) kilembwe (e) kijukuu
Mpenda chongo huona…………..(a) marumaru (b) kengeza (c) karibu (d) vizuri (e) mbali
Walimu walipigwa na butwaa baada ya kuona matokeo ya darasa la saba. Nahau “kupigwa na butwaa maana yake ni? (a) kushangaa (b) kushtuka (c) kukimbia (d) kulia (e) kufurahi
Methali isemayo; “Mdharau mwiba mguu huota tende” ina maana saw ana methali ipi? (a) maji ukiyavulia nguo shart uyaoge (b) usipoziba ufa utajenga ukuta (c) Mwenda pole hajikwai (d) fuata nyuki ule asali (e) penye miti hapana wajenzi
Nini maana ya nahau’” Ana mkono wa birika” (a) mwizi, (b) mfupi (c) mkarimu (d) umepinda (e) mchoyo
Maana ya kitendawili “ Nyumba yangu imeungua umebaki mwamba wake “ ni (a) njia (b) kaburi (c) mfupa (d) mti (e) kisima
Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana saw ana neno shehena? (a) robota (b) bidhaa (c) mzigo (d) roda (e) furushi
Maana nyingine ya neno mafichoni ni; (a) waziwazi (b) kivulini (c) faraghani (d) pembezoni (e) hadharani
Mwanamke huyu alikaa………………….baada ya kufiwa na mme wake. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii? (a) eda (b) head (c) arobaini (d) fungate (e) edaha
Neno “mwangwi” ni jibu la kitendawili kipi kati ya vifuatavyo? (a) huku ng’o na huko ng’o (b) jinamizi laniita lakini silioni (c) huku pili na huko pili (d) kila niendapo ananifuata (e) sirudi tena kwa mjomba.
Ipi maana sahihi ya neno “aghalabu” (a) mara nyingi (b) mara moja (c) mara chache (d) mara dufu (e) mara nyingine
SEHEMU B: UTUNGAJI: Panga sentensi zifuatazo ili zilete habari yenye mtiririko mzuri kwa kuzipa herufi A, B, C, D, na E
Vile vile matunda huongeza damu mwilini
Kula matunda kuna saidia kuponyesha magonjwa na vidonda haraka
Hivyo matunda yana umuhimu mkubwa katika miili yetu
Pia husaidia macho kuona vizuri katika mwanga hafifu
Lakini watu wasiokula matunda huapata maradhi kama vile uonjwa wa fizi, macho na ngozi
SEHEMU C. UFAHAMU: Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 41-45
1. Twakushukuru karima, kwa zawadi ulotupa
Ingawa umeichuma, sifa kwako tunakupa
Jemedari kama chuma, mpenda yalotukuka
Buriani Magufuli, kwa mola twakuombea
2. yote ulitotufanyia, Daima twakukumbuka
Kaziyo ilitukuka, samia kuendeleza
Tanzania ya viwanda, hakika yawezekana
Buriani Magufuli, kwa Mola twakuombea
Jibu Maswali yafuatayo
Kichwa kinachofaa shairi hili ni……………………………….
Vina vya kati katika ubeti wa kwanza mshororo wa pili ni ………………………….na………………………
Shairi hili lina beti ngapi?...............................
Neno Buriani lilivyotumika linamaana gani?
Shairi hili lina mizani ngapi kwa kila mshororo?
KISWAHILI DARASA LA SITA
MAELEKEZO KWA MSIMAMIZI
Zingatia yafuatayo kabla ya kusoma maelekezo kwa watahiniwa.
Hakikisha unasoma hadithi kwa sauti na taratibu kwa mara ya kwanza huku ukizingatia alama zote za uandishi zilizopo katika hadithi hiyo. Unaposoma kwa mara ya pili ongeza kidogo kasi ya usomaji
Muda utakaotumia kuwasomea watahiniwa hadithi ni dakika tano (05) na muda utakaotumika kwa watahiniwa kujibu maswali ni dakika tano (05). Sehemu hii itafanyika kwa dakika kumi (10)
Wasomee watahiniwa kwa sauti maelekezo (1 hadi 3)
MAELEKEZO KWA WATAHINIWA
Nitasoma kwa sauti hadithi mara mbili, hivyo kila mmoja asikilizie kwa makini.
Nikisoma hadithi kwa mara ya kwanza, sikiliza bila kujibu maswali na nikimaliza kusoma kwa mara ya pili, jibu swali la 1 hadi 5 kisha endelea kujibu maswali mengine (6 hadi 45)
Ninaanza kusoma kifungu cha habari/hadithi sasa hivyo sikiliza kwa umakini.
KIFUNGU CHA HABARI
Mara kadhaa nyakati za usiku tunaona mwezi ukiangaza angani. Mwezi hauna nuru yake yenyewe, bali huangaza kwa sababu unaakisi mwanga kutoka kwenye jua.
Mwezi hauna mimea kwa vile hauna maji. Ardhi yake imejaa mawe na vumbi tu. Ijapokuwa kuna vumbi hakuna kimbunga. Hii ni kwa sababu kwenye mwezi hakuna upepo; vile vile hakuna hewa. Hewa ndiyo hufanya sauti isikike.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 33
MINISTRY OF EDUCATION, REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
STANDARD SIX EXAMINATION SERIES
KISWAHILI, MID TERM SEPTEMBER 2021
ANSWER ALL QUESTIONS
SEHEMU A: SARUFI
Ili nifaulu mtihani wangu.........nijifunze kwa bidii.
Budi
Ni budi
Sina budi
Sio budi
Si budi
Viongozi wanatuhimiza tufanye “utundu” wa kisayansi. Neno “utundu” limetumika kama aina ipi ya maneno?
Nomino
Sifa
Kivumishi
Kiwakilishi
Kiunganishi
Neno lipi linakamilisha sentensi hii? “waziri aliwataka wananchi waudhibiti uchumi wao ili..........na mabadiliko yaliyopo.
Usiasiliwe
Usiadhiriwe
Usiashiriwe
Usiathiliwe
Usiathiriwe
Sentensi ifuatayo iko katika kauli ipi? “ shule yetu imeharbiwa na upepo”
Kutenda
Kutendana
Kutendeana
Kutendewa
Kutendea
Sikumkuta mtu........nyumbani.
Yoyote
Yeyote
Wowote
Awaye
Yote
“Alisema yeye hatakwenda”. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo imebadilisha kauli hii taarifa kuwa kauli halisi?
Alisema haendi
Alisema yeye ataenda
Mimi sitaenda
Kuwa sitaenda
Alisema mimi nitaenda
Katika sentensi ifuatayo ni neno lipi limetumika kama kivumishi? “Jana mwalimu alivaa shati nadhifu”
Nadhifu
Jana
Alivaa
Mwalimu
Shati
Ipi maana sahihi ya neno “aghalabu”
Mara nyingine
Mara chache
Mara nyingi
Mara dufu
Mara kwa mara
Nani amesema kwamba mwalimu mkuu amehamishwa? Neno lipi katika sentensi hiyo ni kiwakilishi?
Nani
Amesema
Mwalimu
Mkuu
Amehamishwa
Jana waziri alitoa hotuba nzuri. Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi?
Jana
Alitoa
Waziri
Hotuba
Nzuri
Katika sentesi ifuatayo, neno linalokosekana ni lipi? Ni lazima tuwe waangalifu kwani..........wengi.
Hasidi
Husuda
Mahasidi
Aside
Maasidi
Katika neno “wananifuata” kiambishi kinachoonesha wakati ni kipi?
Fua
Ata
Na
Ni
Fuata
Neno lipi kati ya haya lina maana sawa na neno “suriama”
Zeruzeru
Chotara
Mzuri
Mlimbwende
Msichana
Kama ungaliniomba mapema.........
Nitakusaidia
Ningelikusaidia
Ningekusaidia
Ningalikusaidia
Nikusaidie
Ng’ombe walifugwa zizini. Sentensi hii ipo katika hali ya
Kutenda
Kutendwa
Kutendea
Kutendewa
Kutendana
Anapenda kukaa bure............ana nguvu za kufanya kazi.
Angalau
Iwapo
Sipokuwa
Pamoja
Japokuwa
“Wizi wa mali za shule umetokea jana usiku”. Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kitenzi?
Mali
Shule
Wa
Ya
Umetokea
SECTION B: MSAMIATI
Jeni alikuwa na..........aliposikia habari za ajali ile.
Dukuduku
Tama
Shauku
Njozi
Fikira
Neno lenye maana sawa na “ufukara” ni lipi?
Ukwasi
Usawa
Mkukuta
Ukata
Utemi
Mahindi, ngano, nazi, machungwa, mihogo, viazi na mtama. Andika kwa neno moja
Nafaka
Matunda
Mizizi
Mazao
Mimea
Fundi atengenezaye herein, pete na mikufu huitwaje?
Sofara
Mfuaji
Sonara
Mnajimu
Fundi
Neno la kiswahili lenye maana sawa na mwisho ni
Mwanzo
Kifo
Tamati
Utangulizi
Pembezoni
Kumwonea mtu kijicho ni
Kumwona mtu kwa jicho dogo
Kumnyanyasa
Kumwonea wivu
Kumsakama
Kumtuliza
Tembo aliweza kuvunja tawi la mti kwa kutumia..........wake.
Mkungu
Mkonga
Mkia
Ulimi
Pembe
Mtu anayenadi na kuuza vitu mnadini anaitwa
Dalali
Mzabuni
Muuzaji
Mbinguzi
Mchuuzi
Jumanne alikimbia..........ya farasi
Kawaida
Mithili
Kama
Mfano
Mbio
Kinyume cha “aghalabu” ni
Abadani
Kamwe
Mara nyingi
Nadra
Mara chache
Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na neno “shaghalabagala”
Mpangilio
Ovyo ovyo
Vizuri
Faragha
Mafichoni
Mtu anayeacha kazi ya ajira baada ya kutimiza umri wake kutokana na kanuni anaitwa?
Mzee
Mchapakazi
Mstaafu
Mstaarabu
Muhitimu
“Urafiki wetu ni kama pete na kidole” Maneno ambayo ni viunganishi ni
Kama” na “ni”
“urafiki” na “wetu”
“wetu” na “pete”
“kama” na “na”
“pete” na “kidole”
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
Maana ya nahau “kupiga chuku” ni
Kusema kweli daima
Kutoa maelezo ya uongo
Kutia maneno chumvi
Kukataa katakata
Kuona mengi
Kindendawili kisemacho “wana wa mfalme ni epesi sana kujificha” maana yake ni
Ulimi
Masikio
Pua
Macho
Kope
Methali yenye maana sawa na methali “upele humwota asiye na kucha”
Usimwage mchele penye kuku wengi
Penye nia pana njia
Akili nyingi huondoa maarifa
Penye miti mingi hakuna wajenzi
Mwenda pole hajikwai
Mbwa mwitu wamemzunguka kumlinda. Maana ya kitendawili hiki ni
Ulimi na meno
Nywele kichwani
Mate na meno
Mti na miiba
Pua na mdomo
Nini maana ya nahau “ashakumu si matusi”
Samahani kwa haya nitakayosema
Tafadhali usitamke matusi
Tafadhali sikiliza
Sikiliza kwa makini
Kata kauli
SECTION D: UTUNGAJI
Umepewa insha yenye sentensi 5 zilizoandikwa bila mpangilio sahihi zipange sentensi hizo ili zililete mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E.
Aliposhuka nikamlaki kwa furaha na kuelekea nyumbani pamoja
Kumbe basi hilo ndilo alilosafiria rafiki yangu
Ingawaje sikuchelewa lakini nilijawa na wasiwasi pale kituoni
Baada ya kuangaza macho upende wa magharibi nikaona basi la kwanza likijitoma pale kituoni
Kulipopambazuka nilioga haraka nikavaa upesi kuelekea kituo cha mabasi
SEHEMU E: USHAIRI
Soma shairi kwa makini, kisha jibu maswali 41-45 kwa kuchagua jibu sahihi
Kusahau ni kubaya, kwani kwaleta majuto,
Kwamtia mtu haya, achekwe kama mtoto,
Kunapoteza hedaya, yeye kuleta kipato
Mtu atafuta jembe, kumbe lipo mabegani.
Ataivunja safari, awaulize jirani,
Moyoni atafakari, ameliacha kwa nani,
Yafaa uwe jasiri, tenda mambo kimakini,
Mtu atafuta jembe, kumbe lipo mabegani.
Maswali
Katika ubeti wa kwanza mtunzi ametumia neno “hedaya” kama
"Meno ya mbwa hayaumani "ni methali ipi inaweza kufanana na hii?
Mwana kidonda mjukuuu kovu
Akipenda chongo huita kengeza
Maneno matupu hayavunji mfupa
Damu nzito kuliko maji
Heri mrama kuliko kuzama
Jinamizi laniita lakini silioni. Maana ya kitendawili hiki ni
Jua
Mwangwi
Radi
Popo
Mwezi
Uzururaji umepigwa marufuku .nahau" umepigwa marufuku ina mana gani?
Umezoeleka
Umepigwa winda
Umekithiri
Umekatazwa
Umepigwa konde
" Mwenye nguvu ---" neno lipi linakamilisa methali hii?
Mfunge
Usimkamate
Mkimbie
Usimpige
Mpishe
SEHEMU C (Alama 6)
USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 3136 kwa kuweka katika herufi ya jibu sahihi katika fomu ya kujibia.
Wanafunzi siklliza, nawapa huu wosia Nataka kuwaeleza, mambo muhimu Kwanza ninawapongeza, hapa mlipofikia Hongereni, hongereni, hongereni kuhitimu
Hapa mlipolikia, kamwe msije bweteka, Malengo kuyafikia, huu ni mwanzo hakika, Usije kuvisikia, vitabuvyo kamwe taka, Hongereni hongereni, hongereni kuhitimu
Shuleni mmejifunza, masomo kwa hakika, ICiswahili ni cha kwanza, lugha hamkuichoka, Kwa ari mkijifunza, mbele kita wapeleka, Hongereni hongereni, hongereni kwa kuhitimu
Safari miaka saba, yenye raha na karaha, Mlichopataisi haba, mwende nacho kwa furaha, hicho kidogo kihaba, kisilete majeraha,
Hongereni hongereni, hongereni kwa kuhitimu
Mshairi anaposema " mlichokipata si haba"ana alaana gani?
Mlichokipata si kelele
Mlichokipata si kidogo
Mlichokipata si duni
Mlichokipata si dhaifu
Mlichokipata si kibaya
Vina katika ubeti wa pili ni vipi?
Ha na ka
A na ka
Ho na ho
Hi na mu
U na vi
Wazo kuu katika shairi hill ni lipi?
Kuhitimu ni jambo muhimu
Elimu ya msingi ni bora zaidi
Kujiendeleza kielimu ni muhimu
Kiswahili ni somo la muhimu
Kuhitimu ni lazima
Kichwa kinachofaa kwa shairi hill ni kipi?
Ushauri kwa wahitimu
Kuhitimu si fahari
Elimu ya Msingi
Wanafunzi wahitimu
Fahari ya kuhitimu
Kinyume cha neno " karaha" ni kipi?
Amani
Kero
Furaha
Adhabu
Adabu
Neno "bweteka" kama lilivyotumika kwenye shairi hilo lina maana ipi?
Kudhihaki
Kudhalilika
Kudhoofika
Kuridhika
Kudhihirika
SEHEMU D (ALAMA 4)
UTUNGAJI
Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la 37-40. Zipange sentensi hizo ill ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A,B,-C. na D
Ili mpate kuyajua ni lazima mjifunze kwa bidii na maarifa ill muweze kufaulu mitihani yenu.
Ninyi ni vijana wadogo wenye matumaini ya kupata maendeleo katika maisha yenu ya baadaye.
Endeleeni kusoma na kujifunza kwa bidii kwani elimu ni bahari haina mwisho.
Elimu ndiyo itakayoweza kuwafungulia njia za kupata maendeleo hayo katika safari hii ya kuelimika zaidi.
SEHEMU E (Alama 10)
UFAHAMU
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu swali 41-45 .c va kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.
Zamani babu zetu walitabiri mvua wao wenyewe bila kuwa na vyombo vya kisasa. Suala linalozungumziwa sasa ni mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa jamii nzima, mabadiliko haya yamekuwa makubwa kiasi cha'kutisha.
Kila mtu ana wasiwasi kuhusu mvua ambazo huchukua muda mrefu bila kunyesha. Ukosefu wa mvua huleta ukame na njaa ambayo umechangiwa na bianadamu kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu ambazo huongezeka kwa haraka siku hadi siku, kwa upande mwingine huonekana kama ni maendeleo.
Mifano inayoonyesha matumizi hayo ni ujenzi wa nyumba, nishati kwa ajili ya kupikia, mbao na magogo kwa wingi kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo ili maendeleo yawe chanya jamii inalazimika kupanda miti kwa wingi ilii kukidhi mahitaji yao. Aidha, ni vema kuzingatia kuwa ukataji wa miti kwa wingi ni chanzo kikubwa cha mito na vijito kuvva na maji haba au kukauka kabisa.
MASWALI
Kichwa cha habari kinachofaa kwa habari hii ni ----
Neno "haba" kama linavyotumika katika habari hii lina maana sawa na neno
Ili maendeleo yawe chanya jamii inalazimika kufanya nini?
Ukame na njaa husababishwa na ukosefu wa......
Watu wa zamani waliweza kutabiri mvua kwa kutumia.....
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 21
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI- MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
DARASA LA SITA
MUDA: 1.30
MAELEKEZO
Karatasi hii ina kurasa nne zenye maandishi yenye sehemu A,B, C,D na E zenye maswali arobaini na tano (45).
Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
Kumbuka kuandika majina yako, na shule yako kwenye karatasi ya kujibia.
Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
Tumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi kwa maswali yote uliyopewa.
SEHEMU : A SARUFI
Chagua herufi ya jibu sahihi kisha uiandike kwenye karatasi ya kujibia uliyopewa
1. Gari langu ni bovu, lake ni zima. Neno lake limetumika kama aina ipi ya neno?
Kielezi
Kitenzi
Kiwakilishi
Nomino
Kivumishi
2. Anakuja kufanya nini? Sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi?
Kwanza umoja
Tatu wingi
Tatu umoja
Pili wingi
Pili umoja
3. Neno mlimbwende lina silabi ngapi?
Nne
Tatu
Sita
Saba
Kumi
4. Nitakula chakula changu chote. Ipi ni kauli taarifa ya sentensi hii?
Alisema kuwa atakula chakula chake chote
Alisema kuwa nitakula chakula changu chote
Alisema kuwa nitakula chakula
Alisema nitakula chote
Alisema kuwa chakula chake chote atakula
5. Kipi ni kiambishi cha wakati katika neno watamaliza?
Ha
Wa
Ma
Li
ta
6. Kinyonga anatembea polepole. Neno polepole ni aina gani ya neno?
Kielezi
Kiwakilishi
Kivumishi
Kitenzi
Nomino
7. Ipi ni ngeli ya neno embe?
A-WA
LI-YA
U-YA
I-ZI
U-ZI
8. Kipi ni kinyume cha neno ezua?
Ezeka
Paa
Paua
Panua
Panda
9. Hakuna mwalimu__________ darasani
Yoyote
Yeyote
Lolote
Wowote
Kokote
10. Shangazi amejengewa nyumba na baba. Sentensi hii ipo katika kauli gani ?
Kutenda
Kutendewa
Kutendeka
Kutendwa
kutendesha
11. Neno lipi halilandani na mengine?
Bahasha
Stempu
Anwani
Sahihi
ukuta
12. Huko____ alikoelekea simba
Ndimo
Ndiko
Ndipo
Ndilo
ndicho
13. Wamekuja wote isipokuwa Munira. Neno isipokuwa llimetumika kama aina ipi ya neno?
Kitenzi
Kiunganishi
Kivumishi
Kiwakilishi
kihisishi
14. Kipindi cha mvua za rasha rasha hujulikana kama
Kifuku
Kipupwe
Vuli
Kiangazi
Masika
15. Upi ni mzizi wa neno fundisha
fundi___
fund___
fundish____
fundis___
fundisha
16. Ipi ni nomino ya dhahania kati ya hizi?
Iringa
Usingizi
Miti
Ndege
jozi
17. Pete ya dada imetengenezwa na mzoefu sana.
Mwashi
Mhunzi
Sonara
Rubani
Nahodha
18. Nilimsisitiza Aisha kuwa kusoma kwa bidii ili afaulu vizuri.
Hatuna budi
Hawana budi
Hana budi
Sina budi
Hamna budi
19. Nomino ya kitenzi lia ni…………
Kilio
Somo
Nakala
Mafundisho
Malio
20. Wingi wa sentensi paka anakunywa maziwa ni__
Mapaka yanakunywa maziwa
Paka yanakunywa maziwa
Mapaka yamekunywa maziwa
Paka wanakunywa maziwa
Paka anakunywa ziwa
SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI
Chagua herufi ya jibu sahihi.
21. Methali ipi haisisitizi juu ya ushirikiano?
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
kidole kimoja hakivunji chawa
figa moja haliinjiki chungu
kidole kimoja hakipigi kofi
chelewa chelewa utakuta mwana si wako
22. Methali ipi inasisitiza juu ya umuhimu wa undugu?
damu nzito kuliko maji
haba na haba hujaza kibaba
upele humwota asiyekuwa na kucha
penye miti hapana wajenzi
siku za mwizi ni arobaini
23. Juma ana kichwa cha panzi. Hii ina maana kuwa Juma ni__________
mwongo
mzoefu
msahaulifu
mkweli
kichwa kikubwa
24. Malizia methali hii, ukila nyama ukumbuke………
kuguguna mfupa wake
kula mfupa wake
kubeba
kubakiza
kushukuru
25. Fimbo ya mtemi haina fundo. Lipi ni jibu la kitendawili hiki?
Moshi
Njia
Nyoka
Mti
kichwa
26. Kinachokufaa ni kile ulichonacho, methali yenye kubeba maelezo haya ni.
hamadi kibindoni
wema hauozi
ajali haina kinga
kiburi si maungwana
mwenda pole hajikwai
27. Tegua kitendawili hiki, kulia kwake ni kicheko kwetu____
radi
mvua
upepo
njia
popo
28. Metahli ipi inalandana na ile isemayo meno ya mbwa hayaumani
siku za mwizi ni arobaini
zimwi likujualo halikuli likakwisha
asiyeuliza hana hajifunzalo
chembe na chembe mkate huwa
sanda ya mbali haiziki maiti
29. Nahau ya kuwa popo ina maana gani?
Kigeugeu
kuwa mnyama
kuwa msahaulifu
kuwa mwoga
kuwa tajiri
30. Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji. Jibu la kitendawili hiki ni
kikombe
kibatari
kitabu
kisima
shimo
SEHEMU C: USHAIRI
Soma shairi hili kisha jibu maswali yafuatayo
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali, kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili, watoto wake wakaja , ili kumtaka hali, wakataka na kauli, iwafae maishani.
Akatamka mgonjwa , ninaumwa kwelikweli, hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali roho naona yachinjwa , kifo kinanikabili, kama wakata kauli , sema niseme nini?
MASWALI
Chagua herufi ya jibu sahihi kisha iandike kwenye karatasi ya kujibia.
31. Neno kauli kama lilivyotumika katika ubeti wa kwanza wa shairi lina maana gani?
Tamko
Muhtasari
Maradhi
Ugonjwa
Vina
32. Kuna mizani mingapi katika kila mstari
Kumi
Nane
Kumi na sita
Tisa
Nne
33. Vina vya katikati ubeti wa pili ni?
li
wa
njwa
ja
nj
33. shairi hili lina beti ngapi?
Tatu
Tano
Nne
Moja
Mbili
34. wakakata na kauli, iwafae maishani lipi ni jina la mstari huu?
Mizani
Vina
Mkarara
Mshororo
Mstari
35. Shairi hili lina majibizano ya pande ngapi?
Nne
Tatu
Nane
Moja
Mbili.
SEHEMU D: UTUNGAJI
Panga sentensi zifuatazo kwa mtiririko unaofaa kwa kuzipa herufi A,B,C,na D
36. Ilikuwa ni usiku wa manane
[ ]
37. Asubuhi yake tulianza safari ya kuelekea kijijini Manga
[ ]
38. Baba alipigiwa simu na kupewa taarifa ya msiba wa bibi yetu
[ ]
39. Baba alituamsha na kutupa taarifa zile na kutusihi tulale lakini
hatukupata hata lepe ya usingizi
[ ]
SEHEMU E: UFAHAMU
Soma vizuri habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo kwa usahihi.
Mfalme Bwanyenye wa nchi ya Ahadi hakupenda kuongoza kwa haki. Kila alichokisema yeye wapambe wake walikifanya kuwa sheria. Alivimba kichwa na kujiona yeye ndiye mwamba shupavu. Ulikuwa ni ufalme wa kimabavu. Haswa! Wanazuoni wengi walidai kuwa huo ni udiktekta. Kila mtu hakuwa salama, jela zilijaa watu wasio na hatia. Useme kipi uwe salama? Hilo lilikuwa ni fumbo kubwa, wengi kwa kuogopa walinyamaza kimya na kujifariji kwa kusema hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Walijiuliza yupo wapi Adolf Hilter, yule mtawala
wa Ujerumani aliyekuwa katili, yu wapi Mobutu wa Kongo aliyekuwa na nguvu tele? Naam, wote wamepita mithili ya radi.
MASWALI
40. Neno wanazuoni kama lilivyotumika katika habari hiyo lina maana gani
41. Mfalme Bwanyenye alitawala nchi gani?____________
42. Eleza maana ya methali iliyotumika katika habari hii ? __
43. Neno mithili kama lilivyotumika katika aya ya mwisho lina maana gani ?
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SIX EXAM SERIES 12
OFISI YA RAISI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA SITA
APRIL-2020 MUDA:SAA 2:00
KISWAHILI
MAELEZO KWA MTAHINIWA
MTIHANI HUU UNAMASWALI JUMLA YA 50
JIBU MASWALI YOTE
ANDIKA MAJIBU KWA HERUFI KUBWA
KAZI YAKO IWE SAFI.
SEHEMU A. Chagua jibu sahii katika uliopewa.
1. "Mwajuma amemwibia Mwanahamisi kalamu yake". Katika sentensi hii. "Mwajuma ni nani?
Mtendewa
Mtendana
Mtendeka
Mtenda
Mtendwa
2 "Uvumilivu ulimfanya Pendo apate zawadi. "Uvumilivu ni aina gani ya neno?
Nomino
Kitenzi
Kivumishi
Kihisishi
Kiwakilishi
3. Kauli ipi inaonesha hali ya kutendewa?
Tumechimba visima vyetu.
Tunachimbisha kisima chetu.
Tulichimbiwa kisima chetu.
Tumechimba kisima chetu.
Tutachimba kisima chetu.
4. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo, kifungu kipi kipo katika kauli taarifa?
Unataka kuondoka lini?
Alitaka kukuuliza unaondoka lini.
Ni lini wewe utaondoka?
Aliuliza, utaondoka lini?
Aliuliza kuwa ataondoka lini?
5. Mwenyekiti hakufika mkutanoni leo. Kitenzi "hakufika" kipo katika hali gani?
Mazoea
Kuendelea
Timilifu
Matarajio
Kanushi
6. Wingi wa sentensi "Mbuzi wamepotea" ni upi?
Mbuzi zetu zimepotea
Mbuzi yetu zimepotea
Mbuzi wetu wamepotea
Mbuzi zetu wamepotea
Mbuzi yetu wamepotea.
7. "Wanafunzi kenda walikwenda ziara nchini Kenya".neno wa ni aina gani ya neno?
Kivumishi
Kiwakilishi
Kielezi
Kitenzi
Nomino.
8. Ashura anacheza mpira wa miguu vizuri.katika sentensi hii,neno lipi limetumika kama kielezi?
Anacheza
Mpira
Vizuri
Ashura
Wa mguu.
9. Mtu anayetafsiri ana kwa ana katika lugha moja kwenda lungha huitwaje?
Msuluhishi
Mpatanishi
Mkalimani
Mfafanuzi
Mhubiri
10. "Sote tunafanya mtihani darasani". "darasani" limetumika kama aina gani ya neno?
Kielezi
Kivumishi
Kitenzi
Kiwakilishi
Nomino
11. "Tulicheza ngoma na kuimba usiku kucha.” Katika sentensi hii watenda ni nafsi ipi?
Ya tatu wingi
Ya pili wingi
Yapili umoja
Ya tatu umoja
Ya kwanza wingi.
12. ”Utundu wake ulimfanya ajulikane shuleni.” Neno "Utundu” limetumika kama aina gani
neno?
Kivumishi
Nomino
Kiwakilishi
Kitenzi
Kielezi.
13. "Mwanamuziki hodari aliimba nyimbo vizuri.” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? ........
Hodari
Aliimba
Mwanamuziki
Nyimbo
Vizuri
14. "Mgeni aliondoka alikofikia.............kuaga.” Kifungu kipi cha maneno kinachokamilishE sentensi hiyo kwa usahihi?
licha ya
pasi ya
bila kwa
bila ya
bila na
15. "Shuleni kwetu kuna upungufuwa . ....Ni neno lipi hukamilisha tungo hiyo kwa usahihi?
thamani
thamini
dhamini
zamani
samani
16. "Mtoto ametengeneza toroli Ia mti." Wingi wa sentensi hii ni upi?
Watoto wametengeneza toroli za miti
Watoto wametengeneza matoroli ya mti
Watoto ametengeneza matoroli ya miti
Watoto wametengeneza toroli za mti
Watoto wametengeneza matoroli ya miti
17. "Muda mfupi atakuwa anaingia uwanjani." Sentensi hii ipo katika wakati gani?
Uliopo
Uliopita
Wa mazoea
Ujao
Timilifu
18. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?
Fikiria
Dodosa
Uliza
Hoji
Saili
19. Tegua kitendawili kisemacho, " Atembeapo kila mara huringa hata kama kuna adui.”
Bata
Konokono
Kobe
Kanga
Kinyonga
20. "Siku hizi siri za mafisadi zimeanikwa juani.” Usemi "kuanikwa juani” una maana ipi kati ya hizi zifuatazo?
Kuelezwa waziwazi
Kusemwa hadharani
Kusemwa nje ya kikao
Kuelezwa hadharani
Kusemwa jukwaani
MATUMIZI YA LUGHA
SEHEMU B.
21. Badilisha sentensi zifuatazo kuwa katika wakati timilifu.
Wanafunzi wanapiga picha za ukumbusho
Mboni anawasimulia wenzake ndoto alioiota
Baba aliniambia nizime taa
Ninasoma kitabu cha hadith
Mama anatayarisha kifunguakinywa
25. oanisha nahau na maana zake
Nahau
Maana
Kalia kitako
Shika tama
Shingo upande
Tia moyp
Sina hali
Sikitika
Sijiwezi
Sengenya
Kutokuridhika
Kalia kiti
Kumpa mtu matumaini
SEHEMU C.
30. Andika NDIYO au HAPANA
Hadithi ni masimulizi ya kubuni……… …
Hadithi huburudisha na huelimisha…… …….
Ukiandika hadithi sio lazima kuweka alama za uandishi………… ….
Hadithi inaweza kusomwa au kusimuliwa……… ….
Hadithi huwekwa kichwa cha habari………… …………..
35. Tengua vitendawili vifuatavyo
Kuku wangu katagia mibani………… ……………..
Watoto wa tajiri wangua hulala na kutembea uchi… ……….
Mama hachoki kunibeba… …………..
Shamba langu ni kubwa lakini mazao ni machache mno……… ………
Wana wa mfalme ni wepesi sana kujificha……… ……………..
SEHEMU D.
SOMA KIFUNGU KIFUATACHO KISHA JIBU MASWALI
Matunda kama yalivyo mazao mengine ya kilimo yanatokana na mimea mbalimbali. Kwa mfano fenesi ni tunda litokanalo na mfenesi na chungwa hutokana na mchungwa. Maembe, mapapai, mananasi na mapera ni matunda matamu. Ubuyu, ukwaju na limau ni matunda machachu. Hata hivyo, karibu matunda mengi huwa machachu yakiwa mabichi, yakiiva huwa matamu.
Miaka ya hivi karibuni watu wengi wamepanda mimea ya matunda kwenye maeneo ya nyumba zao, hivyo kujipatia matunda kwa njia rahisi. Baadhi ya watu wanaoishi katika mikoa kama vile Tanga na Morogoro wamelima mashamba ya matunda na wameshaona faida ya kilimo hicho na kupanua mashamba yao. Licha ya watu hao kujipatia chakula bora, wameuza na kuwa na pato kubwa.
Matunda yana umuhimu mkubwa sana katika miili yetu. Matunda tunayokula yanaikinga miili yetu isipatwe na maradhi. Pia matunda yanaongeza damu mwilini, husaidia kuponyesha vidonda haraka na macho kuona vizuri katika mwanga hafifu. Watu wasiokula matunda hupata udhaifu wa fizi ambao husababisha fizi kutoa damu.
Aidha matunda ni kiburudisho wakati wa joto. Watu wengi wamekuwa wakisindika matunda ili kupata juisi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara.
MASWALI
41. Kichwa cha habari hii kinachofaa zaidi ni kipi?
Matunda kwa afya
Umuhimu wa matunda
Matunda chanzo cha pato
Matunda na ulinzi wa mwili
Matunda hujenga mwili.
42. "Watu wanaokula matunda huepuka magonjwa mengi,” ni methali ipi inaendana na kauli hii?
Heri kufa macho kuliko kufa moyo
Usiache mbachao kwa msala upitao
Kinga ni bora kuliko tiba.
Lisemwalo lipo na kama halipo laja.
Mwenye kovu usidhani kapoa.
43. Maji ya matunda yaliyokamuliwa huitwaje? .
Mvinyo
Juisi
Jusi
Rozera
Zabibu
44."Matunda yaliyoiva” ina maana sawa na ipi kati ya zifuatazo? ........
yenye ukakasi
machachu
matamu
mabichi
mabivu
45."Kilimo cha matunda kimekuwa cha faida kubwa kwao.” Methali ipi ambayo inaendana na maelezo hayo?
Jembe halimtupi mtu
Mla ni mla leo, mla jana kala nini?
Jisaidie Mungu Akusaidie
Mchumia juani hulia kivulini
Kula nanasi kwahitaji nafasi
46. Ni kwanini wakulima wa matunda hupanua mashamba yao?
Kupata chakula
Kupata kiburudisho
Kuongeza pato D.
Kupata sifa
Kupata mikopo
47. Matunda ya ubuyu na ukwaju yakiwa yameiva huwa na ladha gani?
Chumvi
Uchungu
Ukakasi
Ukali
Uchachu
48. Kazi kubwa ya matunda mwilini ni ipi?
Kuponyesha macho
Kuburudisha
Kujenga mwili
Kuponyesha vidonda
Kulinda mwilli
49. "Kusindika matunda” ina maana sawa na kifungu kipi kati ya vifuatavyo?
Kusaga na kukamua matunda
Kukamua matunda na kuyahifadhi
Kukamua na kuchuja matunda
Kuyasaga matunda yaliyoiva
Kuyaivisha matunda na kuyasaga
50. Umepata funzo gani kutokana na kifungu hiki cha habari?