MASWALI YA MADA, MADA YA 2.
MADA: MAENDELEO YA KISWAHILI:
KIDATO CHA NNE.
A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.
Wageni wa mwisho kuitawal Nchi ya Tanganyika na kuacha athari mbalimbali kutoka lugha ya Kiswahili ni:-
Waarabu
Waingereza
Wareno.
Wajerumani.
Ni kwa vipi Waingereza walichangia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili katika shughuli za kiutawala?
Kuanzisha kamati ya lugha na kuanzisha kampuni ya uchapishaji wa vitabu.
Kuwafukuza Waarabu wa Omani.
Kuanzisha mafundisho ya elimu ya kutafsiri Biblia.
Kuwafundisha wazungu wa kilowezi.
Waingereza walisanifisha lugha ya Kiswahili ili:-
Waweze kupata urahisi wa kufanya mawasiliano na watu wa Afrika Mashariki na kuimarish utawala wao.
Kuwafukuza wakoloni wa Kijerumani.
Kurahisisha utumiaji wa Kiswahili Ulaya.
Kuwapa moyo Watanzania wa kujitawala.
Kihistoria, lugha ya Kiswahili imeanzia katika;
Visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Upwa wa Afrika ya Mashariki
Nchini Mogadishu na Samalia.
Pwani ya nchi ya Kenya.
Moja ya taasisi zinazochangia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania ni?
UKUTA
TFF
UDASA.
UKATA
SEHEMU B: JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI:
Mambo yaliyosaidia kukua na kueneza kwa lugha ya Kiswahili enzi za utawala wa Waingereza ni
______________________
_____________________
____________________
___________________ na
_____________________
Ili kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania baada ya uhuru, Serikali iliunda Taasisi mbalimbali, moja ya Taasisi hizo ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Taja idara za TUKI.
_____________________
_______________________
______________________
_____________________ na
_______________________
Bainisha sababu tatu zilizosaidia kukua na kuenea haraka kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kuliko nchini Kenya na Uganda.
______________________
______________________ na
_______________________
SEHEMU C: MAJIBU YA MAELEZO MAREFU
Fafanua namna Taasisi ya elimu ya watu wazima inavyokuza na kueneza Kiswahili nchini Tanzania.
Eleza jukumu la Wizara ya elimu na mafunzo ya Ufundi katika kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania.
Eleza tathmini ya maendeleo ya Kiswahili nchini Tanzania wakati wa ukoloni.
Eleza tathmini ya maendeleo ya Kiswahili nchini Tanzani baada ya Uhuru.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page
KISWAHILI KIDATO CHA NNE.
MASWALI YAMADA
MADA: UHAKIKI WA KAZI YA FASIHI ANDISHI.
SEHEMU A:
KUCHAGUA.
1. Chagua jibu lililo sahihi kutoka katika maneno uliyopewa.
Moja ya vigezo vya uhakiki ni?
Dhima ya uhakiki
Ukweli wa mambo yanayoelezwa
Fani na maudhui
Maudhui na falsafa
(ii) Ufundi na uzuri wa kisanaa katika fasihi hujulikana kama?
Fasihi
Uhakiki
Maudhui
Fani
(iii) Vifuatavyo ni vipengele vya maudhui katika fasihi isipokuwa;
Ujumbe
Dhamira
Wahusika
Falsafa.
(iv) Zifuatazo ni tanzu za fasihi andishi isipokuwa?
Hadithi
Riwaya
Tamthiliya
Ushairi.
(v) Moja ya kigezo cha kufaulu kwa mtuzi wa kazi ya fasihi ni?
Kubainisha matatizo yaliyomo kwenye jamii yake na kupendekeza njia sahihi ya kuyatatua.
Kuandika kazi ya kufasihi ya kuvutia
Kufuata ipasavyo vipengele vya uhakiki.
Kubainisha wahusika wa kazi ya fasihi.
SEHEMU B:
2. Oanisha maneno yaliyo katika kifungu A ili yaendane nay ale ya kifungu B.
FUNGU: A | FUNGU: B |
|
|
SEHEMU C:
Jibu maswali yafuatayo kwa maelezo mafupi.
4. Fafanua vipengele vya fani na maudhui katika uhakiki wa kazi za fasihi .
5. Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie, eleza umuhimu wa kuhakiki vipengele hivi.
Msimamo wa mwandishi
Wahusika
Falsafa ya mwandishi.
USHAIRI:
Malenga Wapya TAKILUKI
Mashairi ya ChekaCheka T.A. Mvungi
Wasakatonge M.S. Khatib.
6. Ushairi ni utanzu wa kifasihi ambao hauna mchango wowote kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Jadili kauli hii kwa kutumia vitabu viwili ulivyosoma kati ya hivyo vilivyotajwa.
7. Jadili dhana ya matabaka inavyozorotesha ustawi wa jamii husika kwa kutumia diwani mbili ulizosoma kati ya hizo zilizotajwa.
8. Uhakiki wa kazi za ushairi na riwaya hutofautianaje katika vipengele hive?
Muundo
Mtindo
Wahusika
Picha na taswira.
9. Eleza kwa ufasaha dhana zifuatazo zitumikazo katika dhana ya uhakiki wa kazi ya kifasihi.
Mhakiki
Tahakiki
Msanii
Uhakiki.
SEHEMU D:
10. Andika NDIYO kwa kauli iliyo sahihi na HAPANA kwa kauli isiyo sahihi.
Riwaya ya watoto wa Mama N’tilie imeaksi jamii ya Tanzania katika suala la umaskin na athari za ulevi____________
Muundo katika ushairi hujumuisha idadi ya mistari katika ubeti____________
Mkusanyiko wa mashairi na tenzi mbalimbali ndani ya kitabu kimoja huitwa diwani_________
Falsafa ni wahusika ambao hujenga kazi ya fasihi_________
Fani na maudhui katika kazi ya fasihi zinaweza kutenganishwa________
Mhakiki ni msanii anayeiandika kazi ya fasihi kwa jamii yake iliyomlea na kumkuza_____
Mashairi, nyimbo, ngonjera na maghani ni baadhi ya kazi za kifasihi zilizomo kwenye utanzu wa ushairi___________
Uhakiki husaidia katika uboreshaji na uedelezaji wa kazi ya kifasihi___________
Dhana ya mtindo husaidia katika ubainishaji wa kazi ya msanii mmoja na msanii mwingine___
Migogoro na misuguano miongoni mwa wahusika wa kazi za fasihi husaidia katika uibuaji wa dhamira za msanii______
11. Soma beti mbili zifuatazo kutoka diwani ya WASAKATONGE kisha uhakiki vipengele vya fani na maudhui.
NAHODHA.
Nahodha,
Wang’ang’nia sukani,
Mechafuka, bahari siyo shwari,
Si shwari, pepo zinatuathiri,
Zaathiri, na mawimbi ni hatari,
Ni hatari, tufani meshamiri,
Meshamiri na mvual zitiriri,
Zitiriri, radi nazo si kadri,
Nahodha tosa nanga!
Nahodha,
Wang’ang’ania sukani,
Na jahazi, lenda mramamrama,
Mrama, na kupasuka matahima,
Mataruma, mkuku umeachama,
Meachama, tanga limo kudatama,
Kudatama, foromali yainama,
Yainama, chombo sasa kitazama.
12. Eleza kwa ufupi dhana ya mhakiki wa kazi ya fasihi.
13. Eleza umuhimu wa fasihi andishi katika jamii.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page
MASWALI YA MADA. MADA YA KWANZA.
MADA: UONGEZAJI WA MSAMIATI:
KIDATO CHA NNE.
A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.
Neno “Kizibo” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iittwayo:-
Kuambatanisha maneno
Kubadili mpangilio wa maneno
Kuangalia kazi ya kitu.
Kubadili mpangilio wa neno.
Ipi orodha ya maneno ambayo yameundwa kwa njia ya utohoaji wa maneno?
Bendera, meza, beseni na pesa.
Shuka, saa, doti na kigoda.
Bajia, leso, waya na ikulu.
Namba, elimu, papaya na ng’atuka.
Ipi kati ya njia zifuatazo za uundaji wa maneno si njia sahihi ya uundaji wa maneno.:-
Uambishaji.
Kutohoa.
Kuambatanisha maneno.
Kutafsiri.
Lipi kati ya maneno yafuatayo limeundwa kwa njia ya kufananisha sauti?
Malapa.
Redio
Kikunio.
Shati.
B: JAZA NAFASI ZILIZO WAZI:
Neno “Kikunio” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iitwayo__________
Mfano wa neno lililoundwa kwa njia ya uambishaji ni ________________
Maneno motomot, mbalimbali, sawasawa, yameundwa kwa njia ya______________
Neno “Kipanya” limeundwa kutokana na njia ipi?_________________
Njia mbili za uundaji wa maneno ni __________________ na ________________
Mfano wa neno lililoundwa kwa kufupisha maneno ni ________________
C: MAJIBU YA MAELEZO MAREFU:
Eleza namna maneno yaliyoundwa katika miktadha ya:
Maendeleo ya kiuchumi
Maendeleo ya sayansi na teknolojia
Mabadiliko yo mfumo wa siasa
Maendeleo ya mfumo wa tiba
Maendeleo ya kiutamaduni.
Eleza umuhimu wa kuongeza msamiati katika lugha. Toa oja tano.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page
KISWAHILI KIDATO CHA NNE.
MASWALI YAMADA
MADA: UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI.
SEHEMU A:
KUCHAGUA.
1. Chagua jibu lililo sahihi kutoka katika maneno uliyopewa.
Ipi si kweli kuhusu kanuni za utunzi wa mashairi ya kimapokeo?
Vina
Muundo
Mizani
Wahusika
(ii) Utunzi wa mashairi ya kwa kufuata muundo wa mistari mitatu kwa kila ubeti huitwa.
Tathnia
Tarbia
Tathlitha
Takhmisa
(iii) Zipo aina mbili za mashairi, nazo ni;
Mashairi ya kimamboleo na kisasa
Mashairi ya kimapokeo na kimamboleo
Mashairi ya mtindo na muundo
Mashairi ya kikasuku na kihakiki.
(iv) Vipera vya ushairi katika fasihi ni?
Ngonjare, tenzi, nyimbo na mashairi
Hadithi, Visasili, ngonjera an mashairi
Muziki wa dansi, nyimbo, ngonjera na riwaya
Nyimbo, muziki, tenzi na majigambo.
(v) Ipi si kweili kuhusu dhana ya ushairi?
Ni utanzu wa mashairi
Ni lugha ya mkato
Ina matumizi ya picha na taswira
Ina muundo wa beti.
SEHEMU B:
2. Oanisha maneno yaliyo katika kifungu A ili yaendane nay ale ya kifungu B.
FUNGU: A | FUNGU: B |
|
|
SEHEMU: C
3. Andika NDIYO kwa kauli iliyo sahihi na SIYO kwa kauli isiyo sahihi.
Ushairi ni utanzu wa fasihi wenye kutumia lugha ya mjazo au masimulizi _______
Muundo wa kazi za kishairi unatofautiana na muundo katika tanzu nyingine za fasihi___________
Matumizi ya picha na taswira ni kigezo muhimu zaidi katika utunzi wa kazi za kishairi kuliko kazi nyingine za fasihi zisizo za kishairi__________
Mashairi ya kimapokeo yana ubora zaidi kimaudhui kuliko aina nyingine ya mashairi____
Idhini ya kishairi husaidia katika kufupisha na kuyakatiza maneno ili kuleta urari wa vina na mizani_________
Katika utunzi wa mashairi utoshelezi haubainiki katika kila ubeti husika_____
Mashairi na tenzi hutofautiana katika idadi ya mizani tu._______
Nyimbo hutofautiana na maghani ka sababu nyimbo huimbika.______
Ngonjera hutofautiana na mashairi kwa sababu ngonjera ina muundo wa kimajibizano baina ya wahusika________
Ushairi hudumisha na kuendeleza amali za jamii._________
SEHEMU D:
4. Tunga shairi lenye beti nne kuhusu “UMUHIMU WA ELIMU”.
5. Tunga ngonjera yenye beti sita kuhusu “USAWA WA KIJINSIA”.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page