KISWAHILI FORM ONE TOPICAL EXAMINATIONS
TOPIC : 1  MAWASILIANO

MASWALI YA MADA

MADA: MAWASILIANO:

KIDATO CHA KWANZA.

A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.

  1. Mawasiliano ni:___________

  1. Kufanya mawasiliano miongoni mwa wanajamii

  2. Kupashana habari miongoni mwa wanajamii kwa njia mbalimbali

  3. Kufanya majadiliano marefu.

  1. Lugha inatofautiana na Nyanja nyingine za mawasilianao kutokana na

  1. Lugha inatoa sauti nzuri.

  2. Lugha ina za kusemwa na binadamu.

  3. Lugha ina sauti nyingi.

  1. Moja ya sifa za lugha ni ____________

  1. Kufurahisha jamii.

  2. Kuathiri na kuathiriwa

  3. Kuipenda jamii.

  1. Mtungaji wa lugha ya Kiswahili hasa kijana mdogo anapowasalimia watu wazima “Jamani mambo zenu?”, atakuwa amekiuka;-

  1. Utamaduni wa lugha ya Kiswahili

  2. Utaratibu wa mawasiliano

  3. Ujumbe wa lugha ya Kiswahili.

  1. Sauti za lugha zipo za aina kuu mbili, nazo ni?

  1. Irabu na lugha

  2. Lugha na mawasiliano

  3. Irabu na konsonanti.

B: OANISHA MANENO YALIYO KATIKA FUNGU A ILI YAFANANE NA YALE YA FUNGU B.

FUNGU A

FUNGU B.

  1. Nyanja za mawasiliano

  2. Lafudhi

  3. Lugha mama

  4. Sarufi

  5. Sauti za ndege, wadudu na wanyama

  6. Kithembe

  7. Kiimbo

  1. Mazungumzo na maandishi

  2. Mifano ya ishara katika mawasiliano

  3. Mazingira.

  4. Matamshi ya mzungumzaji yanayotokana na lugha yake ya mwanzo.

  5. Kasoro aliyonayo mtu wakati wa utamkaji wa neno fulani.

  1. Lugha, ishara na ala za sauti

  2. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa utamkaji.

  3. Moja ya tanzu za lugha

  4. Lugha anayojifunza mtu tangu utotoni

  5. Hazina sifa ya kuwa lugha.

  1. Aina za lugha

  2. Kukonyeza na kutabasamu

  3. Kubadilika kwa lugha.



C: JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI.

  1. Tanzu za lugha ni _______________________ na _____________________

  2. Sauti za lugha ni za aina mbili, nazo ni ____________ na ___________________

  3. Ngoma na baragumu ni mifano ya ishara katika Nyanja __________________

  4. Idadi ya sauti za lugha za konsonanti ni ngapi? ______________

  5. Idadi ya sauti za lugha za irabu ni ngapi? _______________

  6. Taja mambo muhimu manne yaliyomo ndani ya dhana ya lugha.

  1. ___________________

  2. ___________________

  3. ___________________

  4. ___________________

D: ANDIKA NDIYO KWA KAULI ILIYO SAHIHI NA SIYO KWA KAULI ISIYO SAHIHI.

  1. Lugha ni moja ya Nyanja za mawasiliano__________

  2. Sauti za lugha zitolewazo na mwanadamu zisipokuwa na mpangilio mzuri zina sifa ya kuitwa lugha_____________

  3. Mtumiaji wa lugha akitamka neno “Kurara” badala ya neno “Kulala” atakuwa amekiuka sheria na taratibu zinazosimamia lugha ya Kiswahili __________

  4. Lugha mama huweza kuziathiri lugha za mtumiaji zinazofuatia.___________

  5. Lugha hutumika katika kutolea elimu katika ngazi ya shule za msingi, sekondari na vyuo______________

  6. Kiimbo cha kupanda katika lugha ya Kiswahili hutumika katika kauli za maswali______________

E: MAJIBU YA MAELEZO MAFUPI

  1. Eleza kwa ufupi kwa kutoa hoja tano kuhusu umuhimu wa lugha.

  2. Eleza tofauti tano zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi.

  3. Fafanua kwa ufupi sifa tano za lugha.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 2


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256