STD VII URAIA_MAADILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2022
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
06 URAIA NA MAADILI
Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2022
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyoweka kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Mama 40)
Katika swali la 1- 40, chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu maalum (OMR) ya kujibia uliyopewa.
1. Misaada inayotolewa kwa wahitaji ni ya aina mbalimbali kulingana na uhitaji wa watu. Ni kundi lipi sio la wahitaji katika jamii?
Watoto yatima
Wanafunzi wa elimu ya juu
Watu wenye ulemavu
Wanaoishi katika mazingira hatarishi
Waathirika wa majanga
Chagua Jibu
2. Ofisa mtendaji wa kata hupatikanaje?
Huchaguliwa na madiwani
B Huchaguliwa na wananchi
C Huteuliwa na Halmashauri
D Huajiriwa na serikali
Huchaguliwa na wenyeviti wa mitaa
Chagua Jibu
3. Ni kipi kati ya vifuatavyo hakiwezi kuitambulisha shule?
Madarasa ya shule
Mipaka ya shule
Kaulimbiu ya shule
Nembo ya shule
Wimbo wa shule
Chagua Jibu
4. Mwanafunzi mwenye tabia nzuri ni lazima awe mwenye kujipenda. Nini maana ya kujipenda?
Kujisifia mara tote
Kuwakubali wengine
Kustahimili na kujikubali
Kujitegemea katika masomo
Kujithamini na kujikubali
Chagua Jibu
5. Ni kitendo gani kati ya hivi vifuatavyo kinaweza kutumika katika kutokomeza ukandamizaji wa kijinsia katika jamii?
Kutoa elimu kwa wote
Kutoa elimu kwa wanaume
Kutoa elimu kwa watu wazima
Kutoa elimu kwa watoto
Kutoa elimu kwa vijana
Chagua Jibu
6. Jambo lipi sio huduma inayoweza kutolewa kwa watu wenye ulemavu?
Ushauri
Uadilifu
Makazi
Msaada wa kiafya
Msaada wa kisheria
Chagua Jibu
7. Ni madhara gani hutokea kutokana na ukandamizwaji wa wanawake katika jamii?
Kuongezeka kwa vifo katika jamii
Kujengeka kwa matabaka katika jamii
Kuongezeka kwa ufahamu wa haki za binadamu
Kuongezeka kwa ndoa halali katika jamii
Kuongezeka kwa asasi za kiraia
Chagua Jibu
8. Kila raia wa Tanzania ana wajibu wa kulinda amani ya nchi. Ni kwa vipi utatimiza wajibu huu?
Kwa kutii sheria za nchi
Kwa kutii maelekezo ya wataalamu
Kwa kutoa taarifa kwa wafadhili
Kwa kutoa elimu kwa wazee
Kwa kutenda haki kwa watu wachache
Chagua Jibu
9. Katika jamii iliyostaarabika watu hujiheshimu na hujikinga na mambo yanayowaletea madhara. Je, kitendo hicho huitwaje?
Kujijali
Kuwajali wengine
Kujipenda
Kuwapenda wengine
Kujiamini
Chagua Jibu
10. Mahusiano mabaya baina ya wanajamii huleta athari gani?
Vurugu na upendo
Chuki na upendo
Umaskini na ujinga
Migogoro na mapigano
Umbea na umaskini
Chagua Jibu
11. Ni njia ipi bora zaidi ya kufikisha taarifa au maoni kwa uongozi wa shule kuhusu vitendo visivyofaa shuleni?
Kutumia sanduku la maoni
Kutumia mkutano wa wazazi
Kutumia wazazi ili kutoa malalamiko
Kutumia ubao wa matangazo
Kutumia Sanduku la Posta
Chagua Jibu
12. Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mapinduzi ameanzisha kitengo cha ushauri nasaha katika shule yake. Kitengo hicho kina umuhimu gani?
Kutoa mwongozo wa kutatua changamoto
Kueleza mipango ya shule kwa undani
Kudhibiti nidhamu za wanafunzi
Kuandaa mipango ya usafi shuleni
Kuandaa orodha ya wanafunzi wahitaji
Chagua Jibu
13. Ni kitendo gani hakihusiki katika kuchafua vyanzo vya maji?
Kuoga mtoni
Kufua nguo mtoni
Kukojoa pembezoni mwa mto
Kulima kandokando ya mto
Kutumia njia salama za uvuvi
Chagua Jibu
14. Kuna umuhimu gani wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana?
Huwasaidia kuhimili mihemko ya milli yao
Huwasaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko
Huwasaidia kuhimili ndoa za ukubwani
Huwasaidia kujenga ari ya kuwapenda wengine
Huwasaidia kufanya maamuzi kwa wachumba watarajiwa
Chagua Jibu
15. Riziki alielezwa umuhimu wa kushirikiana na wengine katika kutekeleza majukumu yake ya nyumbani na shuleni. Ni mambo yapi kati ya yafuatayo ni majukumu ya nyumbani?
Kufagia, kucheza na kumwagilia bustani
Kumwagilia bustani, kudeki na kuwa kiongozi
Kufagia, kudeki na kumwagilia bustani
Kupiga kura, kufagia na kudeki
Kudeki, kusafisha zahanati ya na kufagia
Chagua Jibu
16. Barabara, majengo ya shule na zahanati ni miundombinu ya jamii katika kijiji. Nani ana jukumu la kuilinda?
Kamati ya maendeleo ya kijiji
Afisa maendeleo wa kijiji
Wanakijiji wote
Jeshi la polisi
Walimu na wazazi
Chagua Jibu
17. Rasimali za taifa ni tunu zinazotakiwa kulindwa na kuhifadhiwa. Ni kundi lipi Tina wajibu wa kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa?
Maafisa wa polisi
Maafisa wa jeshi
Wananchi wote
Serikali ya kijijt
Viongozi wa serikali
Chagua Jibu
18. Ni mbinu ipi utaitumia kuwafanya wanafunzi wenzako wajitolee kufanya kazi za shuleni na nyumbani?
Kuwafundisha namna ya kufanya kazi
Kuwaadabisha iii wafanye kazi
Kuwahamasisha kufanya kazi
Kuwaonya ili wafanye kazi
Kuwaombea kwa Mungu
Chagua Jibu
19. Mwongozo unaohusu mbinu za kupanga mipango ya maendeleo ya shule hutumiwa na nani?
Mwalimu mkuu
Mwalimu mkuu msaidizi
Uongozi wa shule
Kamati ya shule
Serikali ya kijui
Chagua Jibu
20. Ni njia ipi haiwezi kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali?