STD VII URAIA_MAADILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

URAIA NA MAADILI

Muda : Saa 1:30 Mwaka: 2021

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR,

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jihu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

7. Ukigundua kuwa herufi uliyoweka kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali is 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45

9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali la 1-40, chagua jibu kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi katika Fomu maalum ya kujihia (OMR) uliyopewa.

1 . Utekeleiasji wa demokrasia katika nchi yoyote unakuwa na viashiria vyake. Yafuatayo yanaonesha kukua kwa demokrasia nchini Tanzania isipokuwa

  1. uwepo wa uadilifu wa viongozi.
  2. kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki.
  3. kuwepo kwa uhuru wa kutoa mawazo.
  4. kuwepo kwa utawala wa sheria.
  5. utekelezaji wa haki za binadamu.
Chagua Jibu


2. Ni tendo lipi kati ya yafuatayo linaonesha kuwajali watu wengine?

  1. Kuwaepusha katika mambo yenye madhara
  2. Kusalimia walimu kwa heshima
  3. Kufagia darasa kila siku
  4. Kunyosha nguo za shule
  5. Kuwabebea rafiki zako madaftari
Chagua Jibu


3. Yupi katika muundo wa serikali ya wilaya ana wajibu wa kujadili na kufanya uamuzi wa masuala ya maendeleo?

  1. Katibu tawala
  2. Mkurugenzi mtendaji
  3. Ofisa tarafa
  4. Mkuu wa wilaya
  5. Kamati ya ushauri
Chagua Jibu


4. Watu wenye mahitaji maalumu hujisikia vizuri na kujiamini wanapopendwa na kuthaminiwa katika jamii. Ni tendo gani linapaswa kuepukwa tunapotoa huduma kwa watu wa kundi hili?

  1. Kuwapa huduma sahihi za afya
  2. Kuwachagua katika uongozi wa kisiasa
  3. Kuwatenga kwenye nafasi za uongozi
  4. Kuwasaidia kwenye masuala ya kisheria
  5. Kuchagua maneno sahihi tunapoongea nao
Chagua Jibu


5. Jukurnu lipi kali ya haya yafuatayo sio la mtoto katika familia?

  1. Kulea watoto wadogo
  2. Kushiriki kwenye usafi
  3. Kutunza mifugo
  4. Kuandaa chakula
  5. Kuchimha shimo la taka
Chagua Jibu


6. Zifuatazo ni sheria muhimu za shule zinazotakiwa kufuatwa na wanafunzi shuleni isipokuwa

  1. kutopigana shuleni.
  2. kuchelewa kufika shuleni.
  3. kuhudhuria masomo darasani.
  4. kuvaa sare zinazotakiwa shuleni.
  5. kuheshimu viongozi wa shule.
Chagua Jibu


7. Jukumu la uongozi wa shule ni kusimamia nidhamu na matokco mazuri kitaaluma. ni jukumu la mwalimu wa taaluma shuleni?

  1. Kufuatilia afya za wanafunzi
  2. Kusimamia shughull za darasani
  3. Kusimamia usafi wa shule
  4. Kuendeleza michezo shuleni
  5. Kuwaunganisha walimu na wazazi
Chagua Jibu


8. Ni kwanini wakati mwingine bendera ya taifa hupepea nusu mlingoti?

  1. Kuomboleza kifo cha kiongozi wa kitaifa
  2. Kuadhimisha siku ya kifo cha kiongozi wa kitaifa
  3. Kusherehekea kuzaliwa kwa kiongozi wa kitaifa
  4. Huonesha nchi kuadhimisha sikukuu za kitaifa
  5. Kusheherekea siku ya uhuru
Chagua Jibu


9. Uharibifu wa mazingira husababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama vile kuchoma misitu. Kipi kifanyike ili kutatua tatizo hili?

  1. Kukusanya takataka na kuzichoma moto
  2. Kupika kwa kutumia mkaa
  3. Kutumia mbolea za viwandani katika kilimo
  4. Kutupa takataka shimoni
  5. Kutoa elimu ya utunzaji mazingira
Chagua Jibu


10. 1pi sio changamoto zinazoikabili jamii katika utunzaji wa mazingira?

  1. Ujenzi holela
  2. Gharama za juu za nishati mbadala
  3. Matumizi ya nishati ya jua
  4. Umaskini
  5. Ubovu wa miundombinu
Chagua Jibu


11. Ni mbinu ipi inaweza kutumika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa ufanisI zaidi?

  1. Sanaa za maonesho
  2. Ngoma za jadi
  3. Nyimbo za kigeni
  4. Kupata unasihi
  5. Kupata ushauri kutoka kwa wazee
Chagua Jibu


12. Yafuatayo ni matendo yanayohusu kulinda uhuru na umoja wa kitaifa isipokuwa

  1. kutii sheria za nchi.
  2. kulinda mipaka ya nchi.
  3. kuheshimu haki za binadamu.
  4. kukemea vitendo viovu.
  5. Kuheshimu wazee.
Chagua Jibu


13. Kuna madhara gani kwa watoto kujihusisha na vitendo hatarishi katika jamii?

  1. Kukosekana kwa usalama wa watu na mali
  2. Kukosekana kwa malezi mema
  3. Kuongezeka kwa vitendo vya uadilifu
  4. Kupungua kwa uzalendo
  5. Kuongezeka kwa utii wa sheria za nchi
Chagua Jibu


14. Kuna madhara gani kwa mwanafunzi wa kike kupokea zawadi kutoka kwa watu asiowafahamu?

  1. Kupoteza bahati yake
  2. Kuathirika kisaikolojia
  3. Kupungua kwa uadilifu
  4. Kutengwa na jamii
  5. Kushambuliwa kingono
Chagua Jibu


15. Kwanini watu wengi hupenda kutupa uchafu jalalani?

  1. Wanaogopa kuonekana
  2. Wanaogopa kuadhibiwa
  3. Wanaepuka kuchafua mazingira
  4. Wanaogopa kukiuka desturi zao
  5. Wanaonesha uzalendo
Chagua Jibu


16. Liliani alipewa kazi ya kusafisha ubao, aliifanya kazi hiyo vizuri sana na kwa wakati. Kitendo hicho hujulikanaje?

  1. Nidhamu binafsi
  2. Ustahimilivu mkuu
  3. Uadilifu binafsi
  4. Jukumu binafsi
  5. Umakini mkubwa
Chagua Jibu


17. Kila siku za mwisho wa juma, Hamisi huwasaidia wazazi wake kuhudumia kuku wao. Kitendo hicho hujulikanaje?

  1. Kuwapa haki wanafamilia
  2. Kujali familia
  3. Kujitolea katika familia
  4. Kutimiza wajibu
  5. Kuonesha upendo kwa familia
Chagua Jibu


18. Je, mwanafunzi anapaswa kufanya nini kuvuka barabara pasipo kusababisha ajali?

  1. Kutafuta eneo lenye taa za kijani
  2. Kusimamisha magari kwa kupunga mikono
  3. Kutumia eneo lenye alama ya pundamilia
  4. Kutafuta eneo lenye taa za barabarani
  5. Kutafuta eneo lenye matuta barabarani
Chagua Jibu


19. Neema ni mwanafunzi anayefika shuleni kwa wakati kila siku. Kitendo hiki kinamaanisha nini?

  1. Woga wa adhabu
  2. Kupenda kusoma
  3. Kupenda kusifiwa
  4. Kutii sheria za shulee
  5. Kuogopa walimu
Chagua Jibu


20. Ni tendo lipi halijengi uhusiano mzuri katika jamii?

  1. Kuwa mkweli na muwazi
  2. Kujali na kuhifadhi rasilimali
  3. Kushirikiana katika shughuli za maendeleo
  4. Kujijali na kukosa uadilifu
  5. Kujitolea katika shughuli za maendeleo
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256