STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2023
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Muda: Saa 1:30Mwaka: 2023
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote.
3, Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safe kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
9. Vifaa vya mawasiliano na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 40)
Katika swali 1 - 40, chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu hit() katika fomu ya kujibia (OMR) uliyopewa.
1. Ni ogani ipi katika mwili inaathirika zaidi kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi?
Ini
Figo
Mapafu
Moyo
Ubongo
Chagua Jibu
2. Takamwili zipi hutolewa na mapafu wakati wa kupumua?
Maji na oksijeni
Kabonidaioksaidi na maji
Maji na chumvi
Urea na maji
Kabonidayoksaidi na oksijeni
Chagua Jibu
3. Ikiwa umealikwa kuwaelimisha wanakuui kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, je, utawashauri kuepuka aina zipi za vyakula pindi wanapopatwa na ugonjwa huo?
Vyakula vyenye sukari
Vyakula vyenye joto
Vyakula vya baridi
Vyakula vilivyo na chumvi
Vyakula vyenye asidi
Chagua Jibu
4. Nini umuhimu wa seli hai nyeupe ndani ya mwili wa binadamu?
Kulinda mwili kutokana na vimelea vya magonjwa
Kugandisha damu katika jeraha jipya
Kusafirisha gesi ya oksijeni kutoka kwenye moyo
Kurekebisha joto la mwilini
Kuzuia vijidudu kuingia mwilini
Chagua Jibu
5. Sikio la kati lina vifupa vitatu vilivyoungana kwa mfuatano ambavyo hupokea mitetemo ya mawimbi ya sauti na kupitisha kwenda sikio la ndani. Je, upi ni mpangilio sahihi wa vifupa hivyo vitatu?
Fuame, nyundo, kikuku
Kikuku, fuame, nyundo
Kikuku, nyundo, fuame
Nyundo, fuame, kikuku
Nyundo, kikuku, fuame
Chagua Jibu
6. Katika ukuaji wa mimea, mizizi hukua kuelekea ardhini. Ni kwa nini mizizi ya mimea hukua kwa mtindo huo?
Kufuata hewa na maji
Kufuata maji na mwanga
Kufuata mwanga na madini
Kufuata maji na madini
Kufuata joto la wastani na hewa
Chagua Jibu
7. Umeombwa umsaidie mdogo wako wa kike kazi ya kubainisha viumbe hai na visivyo hai. Utachagua kundi lipi kuwakilisha viumbe hai?
Mti, gogo la mti, kipepeo na chura
Maji, mmea wa mhindi, samaki na chura
Kipepeo, chura, maji na mti
Samaki, mjusi, mti na kipepeo
Maji, nyuki, nyasi na nzi
Chagua Jibu
8. Mwalimu aliwafundisha wanafunzi wake kuwa udongo tifutifu ni bora zaidi kwa kilimo kuliko aina nyingine ya udongo. Ni sifa ipi inayoufanya udongo huo kuwa bora zaidi kuliko aina nyingine?
Una mabonge makubwa yanayozuia maji kupita
Una kichanga, mfinyanzi na maozo ya viumbe hai
Huruhusu maji kupita kwa urahisi zaidi
Hupitisha maji kwa taratibu sana
Hukauka haraka kuliko mchanga
Chagua Jibu
9. Baba yetu alitufundisha kulima kwa kubadilisha mazao kati ya jamii ya nafaka na mikunde. Unafikiri kufanya hivyo kuna faida gani?
Huongeza kaboni
Hurahisisha ukuaji wa mimea
Hurutubisha ardhi
Huzuia mmomonyoko wa udongo
Huzuia magonjwa
Chagua Jibu
10. Ukiandika neno SHULE kwenye karatasi nyeupe na kuliweka mbele ya kioo bapa, ni taswira ipi itaonekana katika kioo hicho?
Chagua Jibu
11. Moto umekuwa ukitumika kupasha joto miili yetu wakati wa baridi. Ni kwa njia gani joto hilo huufikia mwili?
Mzunguko
Mnururisho
Msafara
Mpitisho
Mvukizo
Chagua Jibu
12. Endapo umepewa nafasi ya kuishauri serikali kuhusu aina ya nishati itakayosaidia kuhifadhi mazingira, utashauri kutumika kwa aina gani ya nishati?
Fueli
Makaa ya mawe
Mafuta ya dizeli
Kuni
Jua
Chagua Jibu
13. Fundi simu aliangusha skrubu za simu kwenye mchanga alipokuwa akipuliza uchafu uliokuwa umejaa kwenye simu. Utamshauri atumie kifaa gani kuzipata skrubu kwa muda mfupi zaidi?
Hadubini
Sindano
Sumaku
Mfagio
Kurunzi
Chagua Jibu
14. Ni badiliko gani hutokea wakati wa kupika ugali kwa kutumia unga wa mahindi?
Kiumbo
Kimazingira
Kikemikali
Kimaada
Kiyabisi
Chagua Jibu
15. Ni kwa njia gani harufu huweza kusambaa kutoka ndani ya nyumba kwenda nje?
Osimosisi
Fotosinthesisi
Respiresheni
Foto-osmosisi
Difyusheni
Chagua Jibu
16 Sifa za badiliko la kikemikali ni tofauti na sifa za badiliko la kiumbo. Ni sifa ipi inaonesha badiliko la kikemikali?
Hakuna kitu kipya kinachotokea baada ya badiliko
Hakuna tofauti kati ya uzani wa awali na ule wa baada ya badiliko
Joto jingi hutumika au kutolewa wakati wa badiliko
Tabia ya kitu kinachotokea baada ya badiliko inafanana na kitu cha awali
Kitu cha awali kinaweza kurudia kwa urahisi half yake
Chagua Jibu
17. Kapira aliweka maji na mafuta ya taa kwenye chombo kimoja. Mafuta ya taa yalielea juu ya maji. Je, ni sababu ipi ilifanya mafuta ya taa kuelea juu ya maji?
Densiti ya mafuta ya taa ni ndogo kuliko densiti ya maji
Kanielezi ya mafuta ya taa ni kubwa kuliko kanielezi ya maji
Kani uvutano kwa maji ni kubwa kuliko kani uvutano kwa mafuta ya taa
Tungamo la maji ni dogo zaidi kuliko tungamo la mafuta ya taa
Tungamo la maji ni kubwa zaidi kuliko tungamo la mafuta ya taa
Chagua Jibu
18. Ni maada ipi ina kani ya mvutano kubwa zaidi kati ya molekyuli?
Chuma
Mbao
Hewa
Mvuke
Maziwa
Chagua Jibu
19. Mawasiliano ni muhimu katika jamii ili kupashana habari. Kifaa kipi kinatumika kama njia ya mawasiliano ya asili?
Chagua Jibu
20. Mwalimu wa TEHAMA aliwapa wanafunzi wa Darasa la Saba zoezi la kuchapa barua kwenye tarakilishi. Programu gani itatumiwa na wanafunzi hao kuchapa barua?