STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2022
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2022
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio sail kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
9. Vifaa vya mawasiliano na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 40)
Katika swali 1 - 40, chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu bilo katika fomu ya kujibia (OMR) uliyopewa.
1. Mfumo wa mzunguko wa damu wa binadamu umeundwa na sehemu tatu. Sehemu hizo ni zipi?
Damu, moyo na mishipa ya damu.
Plazima, damu na mishipa ya damu.
Chembe sahani, moyo na sell nyekundu.
Tishu, moyo na sell nyeupe.
Plazima, tishu na chembe sahani.
Chagua Jibu
2. Dereva wa lori alipata ajali iiiyosababisha mwili wake kushindwa kuwa katika msawazo. Je, ni sehemu gani ya sikio lake iliathirika?
Nyundo
Vifereji nusu duara
Fuawe
Kikuku
Miatus
Chagua Jibu
3. Bwana chapombe aiipewa jina hilo kutokana na unywaji wa pombe uliokithiri. Ni ogani gani ina weza kuathirika kutokana na tabia hiyo?
lni
Figo
Mapafu
Moyo
Ubongo
Chagua Jibu
4. Nini kitatokea endapo mwanaume atapata ajali na korodani zake kuathirika kabisa?
6. Kwa nini seli za mmea zina uwezo wa kujitengenezea chakula chake zenyewe wakati seli za mnyama haziwezi?
Seli ya mmea ina saitoplazirmi.
Seli ya mmea ina maitokondria.
Seli ya mmea ina stomata.
Seli ya mmea ina chloroplasti.
Seli ya mmea ina nyukliasi.
Chagua Jibu
7. Unapojaza hewa kwenye puto ukubwa wake huongezeka na hewa ikizidi hupasuka. Ongezeko la ukubwa wa puto lina maana gani kisayansi?
Hewa huchukua nafasi.
Hewa ni nzito kuliko puto.
Hewa ina chembechembe ndogo.
Puto ni laini sana.
Puto linavutika.
Chagua Jibu
8. Iii wanyama waweze kuishi wanahitaji chakula kutoka kwenye mimea na vitu vingine kutoka katika mazingira. Je, ni vitu gani vingine wanahitaji tofauti na chakula?
Mwanga na joto.
Maji na upepo.
Hewa na virutubisho.
Mwanga na upepo.
Maji na hewa.
Chagua Jibu
9. Moja kati ya atomu iliyoko kwenye mbolea zilizo nyingi hupatikana hewani kama gesi. Je atomu hiyo ni ipi?
Agoni
Oksijeni
Haidrojeni
Naitrojeni
Kabonidayoksaidi
Chagua Jibu
10. Uendeshaji wa mitambo ya viwanda kwa kutumia nishati itokanayo na makaa ya mawe una athari gani9
Husababisha uchafuzi wa angahewa.
Huharibu mitambo ya viwanda.
Hutoa nishati ndogo sana.
Huzalisha hewa ya nitrojeni.
Nishati yake ina ukinzani mkubwa.
Chagua Jibu
11. Endapo itatokea vifaa vyote vya umeme ikiwemo runinga, radio na taa za shuleni kwenu vimezitna ghafla, je, ni hatua gani ya kwanza utachukuwa ill kutatua tatizo?
Kubadilisha fyuzi za vifaa hivyo.
Kukagua mfumo wa umeme.
Kubadilisha fyuzi za plagi.
Kubadilisha fyuzi za kikata umeme.
Kurekebisha swichi kuu.
Chagua Jibu
12. Mwindaji alilazimika kuwasha moto kwa kutumia miwani yake yenye lenzi mbinuko ill aweze kuchoma nyama. Ni tabia gani ya mwanga ilioneshwa na miwani hiyo ya mwindaji?
Kusharabiwa kwa mwanga.
Kukusanya kwa mwanga.
Kutawanya kwa mwanga.
Kuakisiwa kwa mwanga.
Kupinda kwa mwanga.
Chagua Jibu
13. Nyumba ya Bwana Matata ina vyumba vitatu na vyote.vinatumia umeme unaotoka kwenye njia kuu moja. Utatambuaje kama nyumba hiyo inatumia sakiti sambamba?
Glopu ya chumba cha kwanza ikiondolewa, glopu 2a. chumba cha pill na cha tatu zitazima.
Glopu ya chumba cha kwanza ikiondolewa, glopu.zaichumba cha pill na cha tatu zitaendelea kuwaka.
Glopu ya chumba cha pill ikiondolewa, glopu ya cha tatu itazima.
Glopu ya chumba cha tatu ikiondolewa, glopu ya 'cliumba cha pill itazima na ya chumba cha kwanza itaendelea kuwaka.
Glopu ya chumba cha pill ikiondolewa, glopu ya chumba cha kwanza itazima.
Chagua Jibu
14. Mtoto alikuwa akicheza nje mbali na jikoni, alihisi harufu nzuri ya chakula alichokuwa anapika dada yake. Ni kwa njia gani harufu hii ilimfikia mtoto?
Difyusheni
Respiresheni
Osmosisi
Molekyuli
Uyeyushaji
Chagua Jibu
15. Mada huonesha badiliko la kiumbo au kikemikali. Ipi ni mifano ya badiliko la kikemikali?
Chuma kupata kutu, kuchacha kwa maziwa na kuungua kwa mkaa.
Kuchacha kwa maziwa, kuoka mkate na kuyeyusha sukari kwenye mail.
Kupika chakula, kuoka mkate na kuchanganya chumvi na maji.
Maji kuwa barafu, kuchacha kwa maziwa na kuungua kwa mkaa.
Kuyeyusha sukari kwenye maji, kuungua kwa mkaa na kuoka mkate.
Chagua Jibu
16. Mwalimu wa TEHAMA aliwapa wanafunzi zoezi la kuingiza data kwenye mkekakazi. Je ni sell gani itaruhusu kuchapa data inayotakiwa?
Sell ya kwanza.
Sell amilifu.
Sanduku sell.
Safumlalo sell.
Safuwima sell.
Chagua Jibu
17. Ndugu Hamza anataka kununua antena kwa ajili ya kupokea mawimbi mbalimbali ya runinga na redio. Je utamshauri anunue aina gani ya antena?
Kitanzi
Yagi-Uda
Honi
Kipenyo
Akisi
Chagua Jibu
18. Mwalimu aliwapa wanafunzi zoezi la kubainisha aina za vitumi kwenye tarakilishi. Je kifaa kipi ni mfano wa vitumi ingizi?
Monita
Printa
Kibodi
Kipaza sauti
Kichakato kikuu
Chagua Jibu
19. Madilu anahitaji mashine ya kieletroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadhi na kutoa taarifa za mauzo katika duka lake. Je utamshauri anunue mashine gani?
Runinga
Tarakilishi
Kisimbuzi
Kadi kumbukizi
Sumakuumeme
Chagua Jibu
20. Kifaa kipi cha mawasiliano hupokea mawimbi ya sumakuumeme na kuyabadili kuwa sauti na picha?