STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2021

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.

9. Vifaa vya mawasiliano na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali 1 - 40, chaguajibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi yajibu hilo katika fomu maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Mfumo wa utoaji takamwili katika mwili wa binadamu umeundwa na ogani kuu nne. Ogani ipi inahusika na utoaji wa kabonidayoksaidi na maji katika hali ya mvuke? 

  1. Mapafu 
  2. Figo 
  3. Ini 
  4. Pua 
  5. Ngozi
Chagua Jibu


2. Mzee alionekana akiyumbayumba barabarani baada ya kunywa pombe nyingi. Je, ni sehemu gani ya sikio iliathiriwa na pombe?

  1. Kikuku. 
  2. Ngoma ya sikio. 
  3. Vifereji nusuduara. 
  4. Koklea. 
  5. Neva za akustika.
Chagua Jibu


3. Baadhi ya watu wana matatizo ya kutoona vizuri wakati wa usiku. Matatizo haya yanasabishwa na ukosefu wa vitamini ipi?

  1. A
  2. B1
  3. B2
  4. D
  5. C
Chagua Jibu


4. Mama alikuwa akihisi kizunguzungu na mwili kuishiwa nguvu. Baada ya daktari kumfanyia uchunguzi alibaini kuwa ana upungufu wa damu. Je, utamshauri ale vyakula vya aina gani?

  1. Vyakula vyenye sukari ya kutosha. 
  2. Vyakula vyenye madini ya ayani.
  3. Vyakula vyenye mafuta ya kutosha. 
  4. Vyakula vya wanga pekee. 
  5. Vyakula visivyo na chumvi.
Chagua Jibu


5. Rafiki yako anashindwa kuona vizuri mpira uliowekwa karibu naye. Je, utamshauri atumie aina gani ya miwani?

  1. Lenzi mbinuko 
  2. Lenzi mbonyeo 
  3. Lenzi mbili 
  4. Lenzi kubwa 
  5. Lenzi ndogo
Chagua Jibu


6. Kaka yangu alijikata kwenye kidole wakati alipokuwa anamenya viazi vitamu. Alifunga jeraha kwa kutumia bandeji, lakini damu iliendelea kutoka kwa muda mrefu. Je, damu ya kaka yangu ilikuwa na upungufu gani?

  1. Seli hai nyeupe 
  2. Chembe sahani 
  3. Plazima 
  4. Madini 
  5. Seli hai nyekundu
Chagua Jibu


7. Wakulima walielimishwa na mtaalam wa kilimo kuacha kutumia njia za kilimo zinazosababisha mmonyoko wa udongo. Je, ni njia ipi hawapaswi kuitumia wakulima hao?

  1. Kupanda miti shambani. 
  2. Kulima kwa matuta. 
  3. Kulima kwa kufuata kontua. 
  4. Kulima kwa kufuata ngazi. 
  5. Kusafisha shamba kwa kutumia moto.
Chagua Jibu


8. Ni kundi lipi linawakilisha wanyama wenye uti wa mgongo?

  1. Nyoka, Punda, Konokono na Fisi.
  2. Mjusi, Kipepeo, Pundamilia na Simba.
  3. Mamba, Swala, Tembo nå Panzi.
  4. Swala, Mamba, Kiboko na Twiga.
  5. Konokono, Kaa, Tembo na Pundamilia.
Chagua Jibu


9. Mdogo wako alistaajabu kuiona alama ya fuvu la kichwa kwenye nguzo za umeme na kwenye makopo ya dawa za chooni. Alama hiyo kwenye sehemu hizo huashiria nini? 

  1. Sumu au hatari 
  2. Inashika moto 
  3. Inamomonyoa na kuunguza 
  4. Inalipuka 
  5. Inakereketa
Chagua Jibu


10. Wanafunzi wa Darasa la Tano walifanya jaribio la kutengeneza sakiti rahisi kwa kutumia selikavu, waya na balbu. Je, ni kundi lipi lilifanikiwa kuwasha balbu?



A
B
C
D
E
Chagua Jibu


ll. Mwanafunzi alishuhudia jengo la Shule likibomoka kwa kupigwa na radi. Unapendekeza nini kifanyike kwenye majengo ili tatizo kama hili lisitokee katika majengo mengine?

  1. Yajengwe kwa mawe. 
  2. Yajengwe kwa ukuta mnene. 
  3. Yawe na ukuta wa kuzuia radi. 
  4. Yafungwe waya wa ethi. 
  5. Yafungwe kikinga radi.
Chagua Jibu


12. Mfanyakazi wa kiwanda cha nondo ameingiwa na chembechembe za chuma machoni na anahitaji msaada. Je, utafanya nini ili kumsadia?

  1. Kumuosha uso wake kwa maji safi na sabuni.
  2. Kutumia sumaku itakayonasa chembechembe hizo.
  3. Kutumia pamba ya masikioni kuziondoa chembechembe hizo.
  4. Kutumia kitambaa safi kufuta ndani ya jicho.
  5. Kumwinamisha chini ili chembechembe hizo zidondoke.
Chagua Jibu


13. John alitazama maji yaliyotulia akaona sura yake. Kitendo hicho kinaonesha tabia gani ya mwanga?

  1. Kusafiri 
  2. Kupinda 
  3. Kupenya 
  4. Kuakisiwa
  5. Kusharabiwa 
Chagua Jibu


14. Sababu ipi inaifanya gesivunde kuwa nzuri kuliko kuni kama chanzo cha nishati? 

  1. Ilaitoi moshi wakati wa kutumia. 
  2. Inatoa gesi ya oksijeni.
  3. Inatoa gesi ya kabonidayoksaidi. 
  4. Haina gharama katika uzalishaji. 
  5. Inatumika kwa kiasi kidogo.
Chagua Jibu


15. Mmea hufyonza molekyuli za maji toka kwenye udongo kupitia kwenye mizizi kwenda sehemu mbalimbali. Ni njia ipi ambayo mmea hutumia kufyonza maji?

  1. Osimosisi 
  2. Difyusheni 
  3. Usambazaji 
  4. Uenezi 
  5. Kunyonya
Chagua Jibu


16. Ni tendo lipi litasababisha kutokea kwa maada mpya?

  1. Kuyeyuka kwa sukari kwenye maji. 
  2. Kuchacha kwa maziwa.
  3. Kubadilika kwa maji kuwa mvuke. 
  4. Kuongeza chumvi kwenye chakula. 
  5. Kuchemsha mchanganyiko wa nta na maji.
Chagua Jibu


17. Rafiki yako amekuomba umsaidie kufungua Program jedwali. Je ni hatua zipi utazifuata?

  1. Bofya menu ya start → Microsoft office →Programu jedwali. 
  2. Bofya menu ya start→Microsoft word → Programu jedwali. 
  3. Bofya menu ya start → program jedwali → Microsoft office.
  4. Bofya menu ya start →Y programu jedwali → Microsoft word. 
  5. Bofya menu ya start → Microsoft office → Microsoft word.
Chagua Jibu


18. Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Makuti anataka kubadilisha mfumo wa kutunza kumbukumbu kutoka kwenye mfumo wa daftari la mahudhurio kwenda kwenye mfumo wa kielektroniki. Utamshauri kutumia mashine gani?

  1. Runinga 
  2. Tarakilishi 
  3. Kisimbuzi 
  4. Kashamfumo 
  5. Ruta
Chagua Jibu


19. Mwalimu wa somo la Sayansi na Teknolojia alitaka uwe na barua pepe ya gmail. Je hatua ipi ni ya kwanza kufuata ili kupata barua pepe?

  1. Kutembelea anwani ya tovuti "www.gmail.com".
  2. Kujaza taarifa zote zinazotakiwa katika fomu ya gmail.
  3. Kujaza namba ya simu na terehe ya kuzaliwa katika fomu ya gmail.
  4. Kuchagua aina ya anwani unayotaka kutumia katika gmail.
  5. Kutembelea tovuti ya "www.yahoo.com" na kuandika nywila kwa usahihi.
Chagua Jibu


20. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa redio nyingi katika kijiji cha Magunga zinatumia antena aina ya kitanzi kidogo. Je, wanapata hasara gani kutokana na matumizi ya antena za aina hiyo? 

  1. Husababisha uharibifu wa redio.
  2. Husababisha upotevu wa nishati ya umeme. 
  3. Husababisha uharibifu wa spika.
  4. Zinahitaji gharama kubwa ya matengenezo. 
  5. Zina mwingiliano wa mawimbi.
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256