STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2020

JAMUHUR1 YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA 

MTIHANI WA KUMALIZA ELMU YA MSINGI

05 SAYANSI

Muda: Saa 1: 30 Mwaka: 2020

Maelekezo

l . Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR na katika kurasa zenye swali Ia 41 hadi 45 kwenye karatasi ya maswali.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi yajibu sahihi kwa swali Ia I hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya kwa swali Ia I hadi Ia 40 na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi Ia 45.

9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali la 1- 40. chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu hilo katika fomu maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Sifa zipi zinahusu mimea pamoja na wanyama

  1. Respiresheni, mjongeo na fotosinthesisi.
  2. Respiresheni, uzaaji na ukuaji.
  3. Ukuaji, uzaaji na fotosinthesisi.
  4. Mjongeo, uzaaji na transipiresheni.
  5. Ukuaji, respiresheni na fotosinthesisi.
Chagua Jibu


2. Kwa nini shamba la maharage halihitaji mbolea ya naitreti? 

  1. Maharage yanaweza kubadili naitrojeni kuwa naitreti.
  2. Maharage yanaweza kubadili ammonia kuwa nitreti.
  3. Maharage yanaweza kubadili naitrojeni kuwa ammonia. 
  4. Maharage yanaweza kubadili nitreti kuwa naitrojeni.
  5. Maharage yanaweza kubadili ammonia kuwa naitrojeni.
Chagua Jibu


3. Nini faida ya wadudu?

  1. Kusafirisha maua.
  2. Kula maua.
  3. Kukuza maua.
  4. Kuchavusha maua.
  5. Kupukutisha maua.
Chagua Jibu


4. Nini lengo la uzazi wa mpango katika familia?

  1. Kupunguza kuenea kwa magonjwa.
  2. Kuacha nafasi kati ya uzazi mmoja na mwingine.
  3. Kupunguza idadi ya watoto.
  4. Kupunguza idadi ya watoto wa kupeleka kliniki. 
  5. Kuwezesha watoto kupata huduma muhimu.
Chagua Jibu


5. Kwa nini inashauriwa kutovuta sigara? 

  1. Kuepuka saratani ya kifua na damu.
  2. Kuepuka saratani ya damu na ini.
  3. Kuepuka saratani ya mapafu na kifua.
  4. Kuepuka saratani ya ngozi na kifua. 
  5. Kuepuka saratani ya ini na mapafu.
Chagua Jibu


6. Jamii inawezaje kujikinga dhidi ya malaria? 

  1. Kwa kutumia vyandarua vyenye dawa.
  2. Kwa kumeza vidonge vya malaria.
  3. Kwa kufua chandarua.
  4. Kwa kuua plasmodiamu.
  5. Kwa kuzuia na kuua bakteria.
Chagua Jibu


7. Kwa nini inashauriwa kuchemsha maji ya kunywa?

  1. Ili kuyafanya yawe safi. 
  2. Ili kuyafanya yawe meupe. 
  3. Ili kuyafanya yawe salama. 
  4. Ili kuyafanya yawe ya moto. 
  5. Ili kuyafanya yawe matamu.
Chagua Jibu


8. Nini umuhimu wa gesi ya kabonidioksaidi kwa mimea?

  1. Hutumika katika kufanyika kwa maua.
  2. Hutumika katika uchavushaji.
  3. Hutumika katika respiresheni.
  4. Hutumika katika kufanyika kwa matunda. 
  5. Hutumika katika usanisi wa chakula.
Chagua Jibu


9. Ni sifa ipi ya wanyama katika kundi la amfibia inawatofautisha na ndege? 

  1. Kuwa na damu moto. 
  2. Mifupa mifupi. 
  3. Kutaga mayai. 
  4. Kuishi majini. 
  5. Kuishi nchi kavu.
Chagua Jibu


10. Ipi ni jozi ya magonjwa ya kurithi?

  1. Malaria na trakoma.
  2. Saratani na tetekuwanga.
  3. Selimundu na hemofilia.
  4. Trakoma na surua.
  5. Pepopunda na UKIMWI.
Chagua Jibu


I l . Nini mahitaji muhimu kwa uhai?

  1. Maji, chakula na hewa.
  2. Vitamini, maji na hewa. image
  3. Protini, wanga na madini.
  4. Maji, hewa na matunda.
  5. Hewa, mavazi na mwanga.
Chagua Jibu


12. Sehemu ipi ya uzazi kwa mwanamke inafanya kazi sawa na mrija wa manii kwa mwanaume?

  1. Ovari 
  2. Uterusi 
  3. Seviksi 
  4. Mrija wa Falopia 
  5. Uke
Chagua Jibu


13. Kwa nini maziwa ya mama ni umuhimu kwa mtoto?

  1. Yana jotoridi sawa na jotoridi la mama.
  2. Yana virutubisho na viini vya kinga ya asili.
  3. Yana jotoridi sawa na maziwa yaliyochemshwa.
  4. Hayana viini vya kuambukiza magonjwa. 
  5. Yanapatikana muda wowote yakihitajika.
Chagua Jibu


14. Ipi ni kazi ya mifupa?

  1. Kulinda misuli.
  2. Kutengeneza chembehai za damu.
  3. Kutengeneza chumvi.
  4. Kulinda mfumo wa damu. 
  5. Kulinda ngozi.
Chagua Jibu


15. Vyanzo vikuu vya protini ni vipi'?

  1. Maziwa, nyama na mayai.
  2. Maziwa, samaki na mboga mboga.
  3. Maziwa, samaki na matunda.
  4. Maziwa, nyama na karoti.
  5. Maziwa, samaki na mahindi.
Chagua Jibu


16. Ipi kati ya zifuatazo Sio kazi ya mate mdomoni?

  1. Kumeng'enya protini.
  2. Kumeng'enya wanga.
  3. Kulowesha chakula.
  4. Kulainisha chakula. 
  5. Kuwezesha umezaji wa chakula
Chagua Jibu


17. Nini chanzo cha ugonjwa wa kisukari?

  1. Ukosefu wa homoni ya thairoidi.
  2. Ukosefu wa homoni ya adrenali.
  3. Hitilafu katika tezi ya thairoidi.
  4. Hitilafu katika tezi ya pituitari.
  5. Hitilafu katika tezi ya kongosho.
Chagua Jibu


18. Ipi ni kazi ya ukutaseli katika mmea?

  1. Kutofautisha sehemu za chembehai ya mmea.
  2. Kufanya chembehai ya mmea kuwa Iaini.
  3. Kuunda umbo la chembehai ya mmea.
  4. Kuzuia maji yasitoke kwenye mmea. 
  5. Kuwezesha mmea kusanisi chakula.
Chagua Jibu


19. Popo yuko katika kundi gani la wanyama?

  1. Mamalia 
  2. Reptilia 
  3. Ndege
  4. Bundi 
  5. Amfibia
Chagua Jibu


20. Ni ushauri upi haumfai mwathirika wa UKIMWI

  1. Kutumia dawa kama ilivyoelekezwa na daktari.
  2. Kuwa na wapenzi wasio na UKIMWI.
  3. Kujikubali na kuelimisha wengine.
  4. Kuishi kwa matumaini na kujijali.
  5. Kula mlo kamili na kupima afya mara kwa mara.
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256