SAYANSI - 2018
SEHEMU A
Chagua herufi ya jibe sahihi, kisha andika katika karatari ya rnajibu/kujibia.
1. Ipi jozi sahihi kati ya zifuatazo inahusu sehemu za uzazi katika mimea na wanyama?............
- Chavua katika mimea na manii katika wanyama
- Filamenti katika mimea na fallopian katika wanyama
- Tunda katika mimea na korodani katika wanyama
- Maua katika mimea na uterasi katika wanyama
- Mbegu katika mimea na ovari katika wanyama
Chagua Jibu
2. Ili mimea iweze kuendelea kuishi katika mazingira yake inahitaji:
- hewa na udongo
- hewa na maji
- udongo na mbolea
- udongo na maji
- jotoridi na hewa
Chagua Jibu
3. Mpunga kuzaliana kwa kutumia:
- majani
- mbegu
- mizizi
- mashina
- matawi
Chagua Jibu
4. Kundi lipi linawakilisha wanyama wenye uti wa mgongo?
- Nyoka, nge, buibui na mamba
- Konokono, nyoka, kenge na samaki
- Kenge, nyoka, bulbul na samaki
- Konokono, samaki, chura na mamba
- Mjusi, nyoka, kenge na mamba
Chagua Jibu
5. Kiwavi ni hatua mojawapo ya ukuaji wa:
- nyuki
- rnbungo
- funza
- mende
- kipepeo
Chagua Jibu
6. Zipi kati ya zifuatazo ni sifa za viumbe hal?
- Kukua, kupumua, kusanisi chakula, kujongea
- Kukua, kupumua, kulala, kujongea
- Kukua, kupumua, kujongea na kuzaliana
- Kukua, kuona, kujongea na kuzaliana
- Kukua, kusanisi chakula, kujongea na kuzaliana
Chagua Jibu
7. Umeme unasababishwa na mtiririko wa:
- elektroni
- protoni
- nyutroni
- chaji
- atomi
Chagua Jibu
8. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya kinyonga?............
- Hubadili mlio wa sauti yake
- Huchagua aina ya chakula
- Hubadili rangi ya mwili
- Hatoi taka mwili
- Hubadili mwendo
Chagua Jibu
9. Yupi kati ya wafuatao ni mamalia?............
- Konokono
- Bata
- Popo
- Mjusi
- Chura
Chagua Jibu
10. Ipi kati ya zifuatazo siyo kazi ya mizizi katika mimea?..............
- Kusharabu madini ya chumvi.
- Kusharabu maji
- kushikilia mmea
- Kutengeneza chakula cha mmea
- Kutunza chakula cha mmea
Chagua Jibu
11. Gesi ipi hupunguzwa angani na mimea?..................
- Kabondioksaidi
- Oksijeni
- Haidrojeni
- Kabonimonoksaidi
- Naitrojeni
Chagua Jibu
12. Ili maji yawe salama kwa kunywa yanapaswa kifanywa nini?
- Kuchemshwa na kufunikwa
- Kuchujwa na kuhifadhiwa
- kuchemshwa, kuchujwa na kuhifadhiwa
- kuwekwa juani kutwa nzima na kupozwa
- Kuwekwa kwenye mtungi na kufunikwa
Chagua Jibu
13. Yafuatayo ni mahitaji muhimu kwa uhai na ukuaji wa mimea isipokuwa:
- Mbolea za viwandani
- Maji
- Hewa ya kabondayoksaidi
- Mwanga wa jua
- Udongo wenye rutuba
Chagua Jibu
14. Hewa inayohitajika kwa wanyama iii waishi ni:
- Oksijeni
- Kabondayoksaidi
- Nitrojeni
- Haidrojeni
- Kabonimonoksaidi
Chagua Jibu
15. Mtu anayekula vyakula vyenye mafuta kwa wingi anaweza kupata:
- beriberi
- Kifafa
- Shinikizo la juu la damu
- Kisukari
- Shinikizo la chini la damu
Chagua Jibu
16. Ugonjwa unaosababishwa na hitilafu katika chembe hai nyekundu za damu huitwa:
- beriberi
- selimundu
- saratani ya damu
- kisukari
- kifua kikuu
Chagua Jibu
17. Ni gesi ipi hupungua katika chumba kilichofungwa madirisha wakati kina moto wa mkai.
- Haidrojeni
- Kabonimonoksaidi
- kabondayoksaidi
- Oksijeni
- Natrojeni
Chagua Jibu
18. Ni kitu gani tunaweza kutumia iii tunaweza kuona taswira zetu vizuri?
- Kioo mbinuko
- Kioo mbonyeo
- Kioo bapa
- Lenzi mbinuko
- Lenzi mbonyeo
Chagua Jibu
19. Kwa nini ni muhimu kuosha matunda kabla ya kula?
- Kuondoa sumu
- Kuondoa vimelea
- Kuondoa utomvu
- Kuondoa harufu mbaya
- Kuondoa chumvichumvi
Chagua Jibu
20. Sehemu ipi ya mfumo wa umengenyaji chakula inahusika na umengenyaji protini?
- Mdomo
- Utumbo mwembamba
- Utumbo mpana
- Umio
- Tumbo
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |