SAYANSI 2017
Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatasi ya kujibia.
1. Ipi kati ya tabia zifuatazo humwezesha ndege kuruka hewani?
- Mifupa milaini iliyo na manyoya.
- Miili iliyochongoka na mifupa iliyo wazi ndani.
- Mfupa iliyoungana.
- Uwepo wa mifupa mingi.
- Mifupa imara ya mabawa iliyo imara.
Chagua Jibu
2. Makundi makuu ya viumbe hai ni:
- Mimea na ndege
- Mimea na mijusi
- Wanyama na majani
- Mimea na wanyama
- Wanyama na bakteria
Chagua Jibu
3. Ipi kati ya aina zifuatazo za mbegu hujisambaza zenyewe?.................
- Nazi na pamba
- Kunde na mbaazi
- Kunde na papal
- Embe na pera
- Chungwa na mbaazi
Chagua Jibu
4. Chunguza Kielelezo Namba 1, kisha chagua jibu lenye mpangilio sahihi wa zilizoonyeshwa kwa alama A - D.
Kielelezo Na. 1
- Nyuzi, uboho njano, uboho nyekundu, gegedu.
- Uboho nyekundu, gegedu, uboho njano, kano.
- Gegedu, kano, uboho njano, uboho nyekundu.
- Kano, njano, gegedu, uboho njano, uboho nyekur.: _
- Uboho njano, gegedu, kano, uboho nyekundu.
Chagua Jibu
5. Chunguza Kielelezo Namba 2 kisha jibu swali linalofuata
Kielelezo Na. 2
Kifaa katika Kielelezo Namba 2 hutumia tabia ipi ya mwanga?..............
- Kuakisiwa
- Mpitisho
- Mwachano
- Mgeuzo
- Mtawanyiko
Chagua Jibu
6. Magonjwa yapi kati ya yafuatayo huzuiliwa kwa chanjo?................
- Surua na kifaduro
- Kichocho na malaria
- Kuhara na mkamba
- Ukimwi na kisukari
- Kifua kikuu na tetekuwanga
Chagua Jibu
7. Kitu gani muhimu mwanamke mjamzito anapaswa kuzingatia?...............
- Kula chakula kingi cha wanga anapokaribia muda wa kujifungua
- Kufanya kazi ngumu ili awe mkakamavu.
- Kuhudhuria kliniki na kula mlo kamili.
- Kulala mara kwa mara.
- Kutumia sabuni zenye manukato wakati wote.
Chagua Jibu
8. Ugonjwa unaotokana na tatizo la upumuaji ni
- pumu
- malaria kali
- kuzimia
- kifafa
- kisukari
Chagua Jibu
9. Kitu gani kitatokea endapo mfumo wa fahamu utasimama kufanya kazi?.............
- Mtu ataanza kutetemeka.
- Mtu ataanza kuhisi udhaifu.
- Mtu ataanza kuhisi maumivu makali mwilini.
- Kukosekana kwa mawasiliano ndani ya mwili.
- Mtu ataanza kupungua uzito.
Chagua Jibu
10. Mojawapo ya dalili za unyafuzi ni.....................
- uso kufanana na wa mzee
- macho meupe na mafua
- tezi ya shingo kuvimba
- kuhisi baridi na kutapika
- tumbo kubwa na kuvimba miguu
Chagua Jibu
11. Njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama ni.............
- kitanzi na sindano
- njia ya asili
- sindano na vidonge
- vidonge na kondomu
- kondomu na sindano
Chagua Jibu
12. Njia bora ya kuepuka utapiamlo ni ..............
- kutumia dawa za kinga mara kwa mara.
- kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mlo kamili.
- kula mboga za majani kwa wingi.
- kutumia madawa ya kuongeza virutubisho mwilini.
- kuongeza idadi ya milo kwa siku.
Chagua Jibu
13. Mtu aliyepigwa na shoti ya umeme anaweza kusaidiwa kwa kutumia ..................
- miguu
- kipande cha chuma
- ubao mkavu
- mikono
- ubao mbichi
Chagua Jibu
14. Vipande viwili vya ubao safi vilivyofungwa kwenye sehemu mfupa ulipovunjika husaidia
- kuzuia kutokwa damu
- kukipa joto kidonda.
- kuimarisha sehemu iliyovunjika.
- kutibu sehemu iliyovunjika.
- kuunganisha sehemu iliyovunjika
Chagua Jibu
15. Gesi inayotumika kuzima moto ni ................
- haidrogeni
- kabondayoksaidi
- naitrojen
- kaboni
- oksijeni
Chagua Jibu
16. HIV haienezwi kwa ......
- kujamiiana
- kuchangia sindano
- kuumwa na mbu
- kuchangia nyembe
- kuwekewa damu
Chagua Jibu
17. Uhusiano kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI ni kwamhz
- Ni rahisi kupata maambukizi ya UKIMWI kama umeambukizwa magonjwa yato-,na kujamiiana.
- Magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana ni sawa na UKIMWI.
- Dawa za kutibu magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana zinaweza kutumik,aUKIMWI.
- Magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanaenezwa -- kujamiiana pekee.
- Majongwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanatibika.
Chagua Jibu
18. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ina maana sahihi ya UKIMWI?...............
- Kupoteza kinga ya mwili,
- Kinga kubwa ya mwili.
- Kukosekana kwa kinga mwilini
- Upungufu wa kinga mwilini.
- Uwezo wa kinga ya mwili.
Chagua Jibu
19. Mbinu mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni...............
- kutenga eneo la watu wenye virus! vya UKIMWI.
- kuepuka kushirikiana vifaa vya chakula na watu wenye virusi vya UKIMWI.
- kula chakula bora na kunywa mail safi.
- kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
- kufanya mazoezi ya mwili.
Chagua Jibu
20. Vitu vilivyorushwa angani hurudi chini.............
- kwa sababu ya uzito
- kwa sababu ya nguvu ya msuguano
- kwa sababu ya nguvu ya hewa
- kwa sababu ya nguvu ya sayari
- kwa sababu ya nguvu ya uvutano
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |