201 6 - SAYANSI
SEHEMU A
Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.
1. Ili mbegu ichipue inahitaji:
- Maji, udongo na hewa
- Mvua, hewa na udongo
- Unyevu, udongo na jotoridi
- Maji, hewa na jotoridi
- Maji, mwanga na upepo
Chagua Jibu
2. Wadudu wanapohama toka ua moja kwenda lingine wanfanya hivyo ili:
- kuzalisha mimea
- kuepuka maadui
- kutafuta nekta
- kutafuta harufu
- kusambaza mbegu
Chagua Jibu
3. Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......
- Tumbo
- Figo
- Mapafu
- Moyo
- Ubongo
Chagua Jibu
4. Aina kuu mbili za mashine ni:
- ngumu na laini
- rahisi na tata
- za kumenya na kutwanga
- puli na roda
- roda na katapila
Chagua Jibu
5. Mojawapo ya njia za kuondoa takamwili katika mwili ni:
- kutema mate
- kukojoa
- kuoga
- kunawa mikono
- kutoa machozi
Chagua Jibu
6. Mbegu ya kike ambayo haijarutubishwa huitwa:
- kondo
- yai
- uterasi
- ovari
- mrija wa falopio
Chagua Jibu
7. Angalia kielelezo namba 1 ambapo jotoridi lioneshwa kwa nyuzi za sentigredi kisha jibu maswali yanayofuata.
Mbegu itakayoota ni ya chombo kipi?
- Chombo A
- Chombo B
- Chombo C
- Chombo D
- Chombo A na D
Chagua Jibu
8. Sehemu zinazounda mfumo wa upumuaji katika mwanadamu ni:
- pua, mdomo na tumbo
- mapafu, pua na ini
- pua, mapafu na masikio
- koromeo, mapafu na kongosho
- mapafu, pua na mdomo
Chagua Jibu
9. Mdudu yupi kati ya wafuatao huleta hasara kwa mkulima akiwa katika hatua ya pili ya ukuaji?
- Inzi
- Kipepeo
- Panzi
- Mbungo
- Mbu
Chagua Jibu
10. Usafirishaji wa chakula mwilini hufanywa na:
- moyo
- damu
- misuli
- mapafu
- maji
Chagua Jibu
11. Tazama kwa makini kielelezo namba 2 kisha jibu maswali yanayofuata:
Alama Y inawakilisha sehemu iitwayo:
- petali
- filamenti
- chavulio
- pistili
- ovari
Chagua Jibu
12. Mbegu za mimea uhifadhi chakula katika:
- mizizi
- majani
- shina
- kotiledoni
- tunda
Chagua Jibu
13. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana?
- Polio
- Kipindupindu
- Pepopunda
- Kaswende
- Tetekuwanga
Chagua Jibu
14. Nini kitatokea iwapo idadi ya wanyama wanaokula nyama katika eneo ni kubwa kulikc idadi ya wanaokula majani?
- Majani yatapungua
- Majani yatabakia kama yalivyokuwa awali
- Majani yatanyauka
- Majani yataongezeka
- Majani yataliwa
Chagua Jibu
15. Lipi kati ya mafungu yafuatayo ya vyakula hulinda mwili?
- Samaki na maziwa
- Ugali na ndizi
- Maharagwe na karanga
- Mayai na kabichi
- Matunda na mboga za majani
Chagua Jibu
16. Umuhimu wa asidi ya haidrokloric katika tumbo ni:
- kubadili hali ya besi katika tumbo
- kulainisha mafuta tumboni
- kuongeza uchachu tumboni
- kumengenya vyakula vya sukari tumboni
- kuua wadudu wanaoingia tumboni na chakula.
Chagua Jibu
17. Nini tofauti kati ya malaria na homa ya matumbo?
- Malaria hushambulia mishipa ya damu, homa ya matumbo hushambulia neva za fahamu.
- Malaria husababishwa na mbu, homa ya matumbo husababishwa na inzi.
- Malaria hutibiwa kwa siku nne, homa ya matumbo hutibiwa kwa siku saba.
- Malaria husababishwa na plasmodiam, homa ya matumbo husababishwa na bakteria.
- Malaria huambatana na maumivu ya kichwa, homa ya matumbo huambatana na maumivu ya uti wa mgongo.
Chagua Jibu
18. Kipi kati ya vifuatavyo vinapaswa kudumishwa?
- Kutumia kikombe kimoja wakati wa kunywa maji.
- Kunawa mikono kabla ya mlo katika karai moja.
- Kupika mboga za majani na nyama kwa muda mrefu.
- Kuchemsha na kuchuja maji ya kunywa.
- Kuogelea katika mito na mabwawa.
Chagua Jibu
19. Viungo vinavyohusika katika kutoa takamwili mwilini ni:
- figo, ini na moyo
- ini, ngozi na figo
- mapafu, moyo na figo
- moyo, figo na ngozi
- Ngozi, Ini na Moyo
Chagua Jibu
20. Mbungo husababisha ugonjwa uitwao ....
- homa ya matumbo
- nagana
- malale
- matende
- homa ya ini
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |