2015 -SAYANSI
Chaguajibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatariya kujibia.
1. Lipi kati ya makundi yafuatayo linawakilisha sifa za viumbe hai?
- Kufa, kula na kuona
- Kufa, kuzaa na kubadilika rangi
- Kupumua, kuishi na kusikia
- Kupumua, kuzaa na kutembea.
- Kujongea, kupumua na kuzaa.
Chagua Jibu
2. Mbegu chotara kwa wanyama na mimea ni bora kwa sababu gani?
- Hurefuka sana na hazihitaji mbolea.
- Hutoa mazao mengi na hustahimili magonjwa.
- Hukomaa haraka na hutoa mazao yenye uzito mkubwa.
- Hazihitaji virutubisho na hustahimili magonjwa.
- Hukomaa haraka na hazihitaji dawa.
Chagua Jibu
3. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?
- Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini.
- Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
- Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
- Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
- Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.
Chagua Jibu
4. Damu huchukua oksijeni na kutoa kabondayoksaidi kupitia:
- Viribaehewa
- Kuta za mapafu
- Koromeo
- Kapilari
- Pua
Chagua Jibu
5. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:
- mmea kukosa madini joto
- mmea kushindwa kusanisi chakula
- majani ya mmea kukauka
- majani ya mmea kuwa njano
- maj ani ya mmea kupukutika.
Chagua Jibu
6. Fototropizimu ni kitendo cha mmea kuota kuelekea kwenye:
- mwanga
- kani ya mvutano
- maji
- giza
- kemikali.
Chagua Jibu
7. Sehemu ya chembe hai inayohusika na kutawala shughuli zote za chembe hai huitwa:
- saitoplazimu
- vakuoli
- kloroplasti
- kiwambo cha seli
- nyukliasi
Chagua Jibu
8. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha viumbe hai wenye sumu isipokuwa
-
-
-
-
-
Chagua Jibu
9. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:
- osmosis
- difyusheni
- msukumo
- mgandamizo
- mjongeo
Chagua Jibu
10. Ni tezi ipi kati ya zifuatazo huratibu utendaji wa tezi zingine zote katika mwili wa binadamu?
- Kongosho.
- Pituitari
- Thairoidi
- Adrenali
- Parathairoidi
Chagua Jibu
11. Sehemu ya kike ya ua inayohusika na uzazi ni:
- stameni
- staili
- ovari
- Petali
- Sepali
Chagua Jibu
12. Tofauti kati ya tunda na mbegu ni:
- Mbegu ina tunda.
- Tunda huota.
- Tunda lina kotiledoni mbili.
- Mbegu huota.
- Mbegu haziliwi.
Chagua Jibu
13. Mambo muhimu kwa ajili ya afya na uhai ni:
- kucheza mpira wa miguu, kuoga, kufua nguo na kula sana.
- kula, kuwa msafi, kupumzika na kucheza.
- kufanya mazoezi, kula chakula bora, kupumzika na kuwa msafi.
- kula mayai, kuburudika, kulala na kusafisha mazingira.
- kuoga, kula na kulala.
Chagua Jibu
14. Vyakula vyenye kabohaidreti huwezesha mwili:
- kuhimili magonjwa
- kuwa na joto
- kukua kwa haraka
- kuwa na nguvu
- kuwa mwororo
Chagua Jibu
15. Kati ya yafuatayo ni yapi magonjwa yasiyoambukiza?
- Malaria, mafua na kisukari.
- Pumu, kisukari na kipindupindu.
- Kichocho, safura na matende
- Kuhara, homa ya matumbo na pumu
- Pumu, kifafa na tetekuwanga.
Chagua Jibu
16. Mapumziko baada ya kazi ni muhimu kwa sababu gani?
- Mwili hupoa.
- Mwili hutulia.
- Mwili hurejesha nishati.
- Mwili hufanya shughuli nyingine.
- Mtu hupata fursa ya kulala.
Chagua Jibu
17. Magonjwa yanayozuilika kwa kutumia chanjo ni :
- Pumu, kifaduro, malaria na kipindupindu
- Kifua kikuu, malaria, pumu na surua
- Surua, dondakoo, kifua kikuu na kifaduro
- Malaria, surua, kifua kikuu na kipindupindu
- Dondakoo, kifua kikuu, UKIMWI na surua
Chagua Jibu
18. Wakazi wa Mlalo hula maharage, nyama na wali kwa afya zaidi wanahitaji kuongeza:
- samaki
- mboga za majani
- kuku
- mkate
- kunde
Chagua Jibu
19. Kipi kati ya vifuatavyo kinaweza kupungua mwilini kwa kushiriki katika michezo na mazoezi?
- Sukari
- Protini
- Sumu
- Uchafu
- Fati
Chagua Jibu
20. Kipi kati ya vifuatavyo siyo njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa malaria?
- Kufyeka nyasi
- Kufukia madimbwi
- Kutumia chandarua
- Kupuliza dawa
- Kuchoma moto taka
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |