2014 - SAYANSI
Chagua herufi ya jibu lililo sahihi, kisha andika katika karatasi ya majibu/kujibia
1. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo husambazwa na inzi na mende?
- Tetekuwanga
- Kuhara
- Kifaduro
- Utapia mlo
- Homa ya matumbo
Chagua Jibu
2. ?pi kati ya yafuatayo sio sehemu ya mfumo wa damu?
- Bronchiole
- Valvu
- Auriko
- Capillari
- Ateri
Chagua Jibu
3. Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?
- Vaa nguo safi
- Nawa kwa sabuni
- Vaa glovu
- Sali
- Mruhusu apumzike
Chagua Jibu
4. ?pi kati ya yafuatayo ni ?ifa ya maji safi na salama?
- Yametekwa kwenye kisima.
- Yamehifadhiwa na kupoozwa kwenye mtungi wa maji
- Yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
- Yamechemshwa, yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
- Yasiwe na magadi mengi
Chagua Jibu
5. Upi kati ya magonjwa yafuatayo hauna chanjo?
- Kifua kikuu
- Pepopunda
- Surua
- Kifaduro
- Trakoma
Chagua Jibu
6. Gesi inayotumiwa na mimea kutengeneza protini ni:
- carbondayoksaidi
- haidrojen
- oksijen
- naitrojen
- gesi asilia
Chagua Jibu
7. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...
- joto na unyevu
- unyevu na mwanga
- upepo na mwanga wa jua
- mawingu na upepo
- unyevu na upepo
Chagua Jibu
8. Tunaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi kwa kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo:
- Kukata miti
- Kuongeza mbolea kwenye udongo
- Kuotesha nyasi
- Kuweka matuta lavenye maeneo ya mteremko
- Kupanda miti
Chagua Jibu
9. Shughuli za mwanadamu kama kilimo, ufugaji wa wanyama na uchimbaji madini vyote hutegemea:
- mito
- chemchemi
- ardhi
- umwagiliaji
- upepo
Chagua Jibu
10. Kinyonga hujibadili rangi yake ili:
- kutafuta chakula
- kupumua
- kuzaliana
- kutafuta maadui
- kujilinda dhidi ya maadui
Chagua Jibu
11. Mende hupitia hatua kuu ......... katika ukuaji wake?
- mbili
- tatu
- nne
- tano
- sita
Chagua Jibu
12. Yupi kati ya wanyama wafuatao hana uti wa mgongo?
- Buibui
- Popo
- Paka
- Mwanadamu
- Kuku
Chagua Jibu
13. Mojawapo ya kazi ya misuli katika mwili ni:
- kuzuia kutokwa damu
- kuwezesha mwendo
- kutengeneza selihai nyeupe
- kushikilia meno mahali pake
- kuiwezesha kunyooka
Chagua Jibu
14. Viungo katika mifupa huwezesha .........
- kuzuia mifupa kuvunjika
- mifupa iwe ya sawa
- kurahisisha kujongea
- kuupa mwili umbo
- mifupa kunyooka
Chagua Jibu
15. ..... hupinda unapopita kutoka maada ya aina moja kwenda nyingine.
- Upinde wa mvua
- Mistari sambamba
- Miale ya mwanga
- Lenzi
- Mwale na lenzi
Chagua Jibu
16. Mionzi ambayo hupinda zaidi mwanga unapopinda ni ile ya . ....
- rangi nyekundu
- njano
- bluu iliyoiva
- bluu
- zambarau
Chagua Jibu
17. Tazama mchoro ufuatao unaoonesha sehemu za ndani za mbegu ya haragwe....
Ni sehemu ipi inayohusika na kuilinda mbegu isiharibiwe na wadudu waharibifu mabadiliko ya jotoridi?
- 2
- 3
- 5
- 4
- 1
Chagua Jibu
18. Anga huonekana la rangi ya bluu kwasababu .
- hewa na maji ny vya rangi ya bluu
- rangi nyekundu inatawanywa zaidi kuliko rangi ya bluu
- uwezo wa kuona hupungua
- rangi ya bluu hutawanywa zaidi ya rangi nyingine
- wakati wa mawio jua huonekna kama la manjano
Chagua Jibu
19. Kipi kati ya vifuatavyo hakitumii sumaku?
- Kipaza sauti
- Simu ya mezani
- Redio
- Simu ya mkono
- Pasi
Chagua Jibu
20. Kipimio cha kazi ni:
- kilogramu
- Newton
- Tani
- Joule
- Gramu
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |