STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2013
SAYANSI 2013
Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwa kila swali.
1. Ni sehemu zipi za mwili zinahusika na utoaji wa takamwili?
Ngozi na figo
Tumbo na figo
Bandama na ini
Ini na tezi
Mapafu na moyo
Chagua Jibu
2. Kundi lipi limeainisha wanyama wenye uti wa mgongo?
Konokono, mjusi na kenge
Papasi, panzi na mbungo
Chura, mamba na mchwa
Kuku, popo na bata
Nyoka, panzi na mbuzi
Chagua Jibu
3. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?
Vyura
Samaki
Mamba
Mbu
Nyoka
Chagua Jibu
3. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?
Vyura
Samaki
Mamba
Mbu
Nyoka
Chagua Jibu
5. Ni sehemu ipi ya ua hupokea mbegu za kiume?
Stigma
Staili
Testa
Ovyuli
Petali
Chagua Jibu
6. Uhusiano uliopo kati ya viumbe hai na visivyo hai katika mazingira unaitwa
kutegemeana
wando chakula
ikolojia
mlishano
mizania asili.
Chagua Jibu
7. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?
Wadudu
Mimea
Wanyama
Virusi
Ndege
Chagua Jibu
8. Tezi inayodhibiti matendo ya ukuaji wa mwili na kulinda mwili dhidi ya magonjwa huitwa
kongosho
adrenalini
pituitari
thairoidi
gonadi
Chagua Jibu
9. Wanyama wenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu ni wale wa kundi la
Ndege
Amfibia
Reptilia
Samaki
Mamalia
Chagua Jibu
10. Maji safi na salama ni maji ambayo
hayana rangi yoyote
yamepoozwa kwenye mtungi
yamechotwa bombani
yamechotwa kisimani
yamechemshwa na kuchujwa
Chagua Jibu
11. Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana kwa binadamu kwa kuwa
huenezwa kwa njia ya hewa
hujitokeza wakati wa masika tu
husababisha mwili kupoteza maji
hauna tiba wala kinga
chanzo chake halisi bado hakijulikani
Chagua Jibu
12. Mwanafunzi wa Darasa la Sita alipumulia hewa ndani ya neli jaribio yenye myeyuko usiokuwa na rangi, kisha akatikisa neli jaribio hiyo. Baada ya kuitikisa myeyuko ulionekana kuwa na rangi nyeupe. Je, kemikali gani ilikuwa kwenye myeyuko usiokuwa na rangi?
Asidi ya haidrokloriki
Salfa
Asidi ya salfyuriki
Haidrojeni
Haidroksaidi ya kalsiamu
Chagua Jibu
13. Homoni inayodhibiti sukari katika mwili wa binadamu huitwa.
amilesi
glukozi
insulini
ayodini
pepsini
Chagua Jibu
14. Himoglobini katika chembe chembe nyekundu za damu inafanya kazi gani?
Kupambana na bakteria
Kusafirisha oksijeni mwilini
Kusafirisha takamwili
Kubeba vimengenyo vya chakula
Kusambaza taarifa mwilini.
Chagua Jibu
15. Ili kuimarisha mifupa na meno, mtoto anahitaji
kalsiamu, sodiamu na ayani
wanga, mafuta na protini
vitamin A, wanga na matunda
vitamin A, kalsiamu na fosforasi
mayai, matunda na wanga
Chagua Jibu
16. Ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina ya basili ambao hushambulia mapafu huitwa
kifaduro
surua
kichocho
polio
kifua kikuu
Chagua Jibu
17. Ni magojwa yapi kati ya yafuatayo huitwa magojwa ya kuambukiza?
Surua, polio na kifaduro
Kifua kikuu, kisukari na saratani
Surua, matende na UKIMWI
Kifaduro, pumu na kikohozi kikali
Surua, malaria na kisukari.
Chagua Jibu
18. Kemikali inayotumika kubaini uwepo wa chakula aina ya wanga inaitwa.
besi
asidi
spiriti
ayodini
chumvi
Chagua Jibu
19. Ingawa wanyama huvuta hewa ya oksijeni na kutoa hewa ya kabondayoksaidi, hewa hizi hazipungui wala kuongezeka kwenye mizazi kwa kuwa.