STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2012
SAYANSI - 2012
Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwa kila swali.
1. Ili kudumisha afya ya mwili, tunapaswa:
kufanya mazoezi, kula chakula bora na kupumzika.
kulala sana, kula chakula bora na kucheza.
kutofanya kazi ngumu, kufanya mazoezi na kulala.
kufanya mazoezi na kushiriki michezo
kula vizuri na kufanya mazoezi muda wote.
Chagua Jibu
2.Ni kipi kati ya virutubisho vifuatavyo ni muhimu kwa mama mjamzito kupata kwa wingi?
Protini.
Kabohaidreti.
Mafuta.
Chumvichumvi.
Vitamini.
Chagua Jibu
3.Kukojoa mara kwa mara, kutoa mkojo mwingi na kupata kiu mara kwa mara ni dalili za ugonjwa upi?
Kansa.
Kisukari.
Kwashakoo.
Kifaduro.
Upungufu wa damu.
Chagua Jibu
4.Ni njia gani kati ya zifuatazo inafaa kumsaidia mtu aliyepata mshtuko uliotokana na kunaswa na waya wenye umeme?
Kumsukuma kwa mikono haraka.
Kuuvuta waya wa umeme uliomshtua.
Kutumia maji kuuzima umeme.
Kumvuta kwa kutumia kifaa kisichopitisha umeme.
Kumwacha mpaka umeme ukatike wenyewe.
Chagua Jibu
4.Ni njia gani kati ya zifuatazo inafaa kumsaidia mtu aliyepata mshtuko uliotokana na kunaswa na waya wenye umeme?
Kumsukuma kwa mikono haraka.
Kuuvuta waya wa umeme uliomshtua.
Kutumia maji kuuzima umeme.
Kumvuta kwa kutumia kifaa kisichopitisha umeme.
Kumwacha mpaka umeme ukatike wenyewe.
Chagua Jibu
6. Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI?
Kuvimba kwa matezi
Kupoteza uzito
Kuharisha kusikokoma
Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida.
Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.
Chagua Jibu
7. Zifuatazo ni njia za kujikinga na majanga mbalimbali katika mazingira isipokuwa:
kuchimba mahandaki
kujenga nyumba mbali na milima ya volcano
kuweka akiba ya chakula
kuishi maisha ya kuhamahama
kudumisha usafi katika mazingira
Chagua Jibu
8. Ni ipi kati ya zifuatazo ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali?
Mwanga
Hewa
Mafuta ya taa
Kabondayoksaidi
Mvuke
Chagua Jibu
9. Ni lipi kati ya matendo yafuatayo siyo sababu ya uharibifu wa mazingira?
Uchomaji wa karatasi
Maendeleo ya viwanda
Kuoga ziwani
Kutumia mbolea ya samadi
Kuoshea magari mtoni.
Chagua Jibu
10. Mfalme wa porini aliamuru wanyama wote walao nyama wauawe. Unafikiri ni nini kitatokea porini baada ya miaka mingi?
Mimea itaota kwa wingi
Idadi ya wadudu haitabadilika
Mimea itapungua
Wanyama walao majani watapungua
Mazingira yatabaki katika hali nzuri ya kuvutia.
Chagua Jibu
11. Kani za asili husababisha moja kati ya mambo yafuatayo katika mazingira:
Kutoonekana kwa samaki
Tetemeko la ardhi
Ongezeko la mimea
Upungufu wa umeme
Kukauka kwa mito.
Chagua Jibu
12. Ipi kati ya zifuatazo siyo njia sahihi ya kuhifadhi rutuba ya udongo katika shamba?
Kubadilisha mazao
Kupanda mimea jamii ya kunde.
Kupumzisha shamba.
Kutumia mbolea
Kupanda zao la aina moja mfululizo.
Chagua Jibu
13. Chura hupitia hatua kuu ngapi katika kukua kwake?
Moja
Saba
Sita
Tano
Nane.
Chagua Jibu
14. Mdudu yupi kati ya hawa wafuatao hupitia metamofosisi isiyokamilika?
Mbu
Kipepeo
Inzi
Nyuki
Mende
Chagua Jibu
15. Panya aliyekuwa amefungiwa kwenye kisanduku kilichokuwa na kipande cha nyama alikufa baada ya siku mbili. Ni kitu gani kilisababisha panya huyo kufa?
Alikula nyama iliyooza
Alikosa hewa ya kabondayoksaidi
Alikosa hewa ya oksijeni.
Alikosa maji ya kutosha baada ya kula nyama.
Alikosa mwanga ambao ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama.
Chagua Jibu
16. Ni kiumbe yupi kati ya hawa wafuatao ni amfibia?
Chura
Panya
Mjusi
Kobe
Kinyonga.
Chagua Jibu
17. Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?
Angani na ardhini
Ardhini na majini.
Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
Ardhini na mapangoni
Kwenye misitu.
Chagua Jibu
17. Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?
Angani na ardhini
Ardhini na majini.
Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
Ardhini na mapangoni
Kwenye misitu.
Chagua Jibu
19. Kuna aina kuu mbili za mbegu za mimea ambazo ni:
ghalambegu kuu na ghalambegu ndogo
monokotiledoni na daikotiledoni
daikotiledoni na kikonyo kikuu
mbegu zenye mizizi na zisizo na mizizi.
mbegu za asili na za porini.
Chagua Jibu
20. Miale ya mwanga wa radi inaonekana kabla ya kusikia mngurumo wa radi kwa kuwa: