SAYANSI 2010
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi na kuandika herufi inayohusika mbele ya namba ya kilo swali katika karatasi ya kujibia.
1. Ipi kati ya zifuatazo si faida ya michezo kwa afya zetu?
- Husaidia kujenga misuli
- Huzuia mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara
- Husababisha shinikizo la damu
- Huleta burudani
- Hudumisha afya ya mwili
Chagua Jibu
2. Maji yaliyochanganywa na sukari na chumvi ni huduma ya kwanza kwa mtu. anayesumbuliwa na
- Malaria na kuumwa kichwa
- Kuhara na kutapika
- Uti wa mgongo na homa ya matumbo
- Kifua kikuu na mafua
- Kuvunjika mguu au mkono
Chagua Jibu
3. Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa
- UKIMWI
- Trikomona
- Kaswende
- Klamedia
- Trakoma
Chagua Jibu
4. Ni vitamin ipi kati ya zifuatazo hutengenezwa mwilini kwa kuwepo mwanga wa jua?
- Vitamini A
- Vitamini B
- Vitamini C
- Vitamini D
- Vitamini E
Chagua Jibu
5. Chanjo ina manufaa gani kwa binadamu?
- Hupunguza maumivu
- Huponyesha maradhi
- Huzuia magonjwa
- Hurudisha vitamin na madini mwilini
- Hurudisha seli chakavu mwilini
Chagua Jibu
6. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?
- Wote walioko hewani
- Basili
- Plasimodiamu
- Fungi
- Amiha
Chagua Jibu
7. Viwanda havipaswi kujengwa karibu na makazi ya watu kwasababu
- ujenzi wake huchukua eneo kubwa
- sehemu kubwa ya taka za viwandani huwa na kemikali ambazo ni sumu
- mitambo ya viwandani hutoa sauti kubwa hivyo kuathiri ngoma za masikio
- viwanda husababisha watu kuhamahama makazi
- wenye viwanda hawaweki mazingira yao katika hall ya usafi
Chagua Jibu
8. Vitendo vifuatavyo huharibu vyanzo vya maji isipokuwa
- kukata miti
- kuchoma misitu
- kulisha wanyama wengi kupita kiasi kwenye vyanzo vya maji
- kutupa taka za kemikali katika vyanzo vya maji
- kuchota maji ya kupikia toka kwenye vyanzo vya maji
Chagua Jibu
9. Asilimia kubwa ya uso wa dunia imefunikwa kwa maji. Sehemu kubwa ya maji haya hupatikana kwenye
- bahari
- Mito
- maziwa
- mabwawa
- madimbwi
Chagua Jibu
10. Mahali palipoinuka panafaa zaidi kujenga choo cha shimo kwasababu
- ni rahisi kujenga ukuta
- harufu itakuwa mbali na usawa wa ardhi
- si rahisi kuharibika upesi
- maji yatakuwa mbali na usawa wa choo chenyewe
- choo hakitafurika kwa muda mfupi
Chagua Jibu
11. Maji yanayobubujika kutoka ardhini hujulikana kwa jina gani?
- Bahari
- Ziwa
- Chemichemi
- Bwawa
- Mto
Chagua Jibu
12. Vitu muhimu katika uotaji wa mbegu ni
- udongo, mwanga wa jua na maji
- udongo, hewa na maji
- joto la kiasi, maji na hewa ya oksijeni
- joto la kiasi, udongo na mwanga wa jua
- maji, udongo na hewa ya kabonidayoksaidi
Chagua Jibu
13. Kundi la viumbe hai waishio majini na nchi kavu hujulikana kama
- Amfibia
- Athropoda
- Samaki
- Ndege
- Mamalia
Chagua Jibu
14. Kati ya viumbe wafuatao ni yupi si mamalia?
- Popo
- Nyangumi
- Simba
- Sungura
- Mamba
Chagua Jibu
15. Chunguza Kielelezo Namba 1 kwa makini kisha jibu swali lifuatalo
Kielelezo Na.1
Kiumbe aliyeoneshwa katika kielelezo Namba 1 huishi kwa kutegemea
- asali
- Nyama
- nafaka
- vyakula vya majini
- maada zilizooza
Chagua Jibu
16. Mmea uliochorwa katika kielelezo Namba 2 una sifa ya kuishi wapi?
Kielelezo Na. 2
- Kwenye misitu minene
- Majini
- Kwenye majani marefu
- Jangwani
- Milimani
Chagua Jibu
17. Kwanini baadhi ya mimea haipukutishi majani yake wakati wa masika?
- kuhifadhi maji yake
- kuruhusu transipiresheni
- kuhifadhi chakula chake
- kuhifadhi udongo
- kuufanya udongo uwe na rutuba
Chagua Jibu
18, Mchoro katika kielelezo Namba 3 unaonesha picha ya ua
Ni sehemu gani ya ua huvutia wadudu kuja kulichavua
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
Chagua Jibu
19. Umeme unaotolewa katika seli kavu, chanzo chake ni nishati gani?
- Jua
- Kimakanika
- Sauti
- Sumaku
- Kikemikali
Chagua Jibu
20. Kibata alitumia nyutoni 50 kusukuma ukuta kutwa nzima bila mafanikio. Je, lipi sahih: kutokana na tukio hilo?
- alitengeneza kazi
- alitumia kani kubwa sana
- hakufanya kazi yoyote
- alifanya kazi nzuri
- alitumia kani ndogo
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |