SAYANSI 2009
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi na andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi ya kujibia.
1. Unaweza kumhudumia mtu aliyezirai kwa:
- kumpa hewa safi
- kumtingisha kwa nguvu
- kumlaza kifudifudi
- kumbonyeza tumboni polepole
- kumwekea kitambaa cha maji baridi usoni
Chagua Jibu
2. . . . . . . . .. husababishwa na upungufu wa virutubisho vya vitamin A.
- Utapiamlo
- Ukavu macho
- Matege
- Kiribatumbo
- Unyafuzi
Chagua Jibu
3. Umuhimu wa kadi ya kliniki kwa watoto ni kuwezesha wahusika
- kujua tarehe ambayo mtoto alizaliwa
- kuhakikisha kuwa mtoto alizaliwa
- kufahamu maendeleo ya ukuaji wa mtoto
- kupata huduma za kiafya kiurahisi
- kwenda na wakati
Chagua Jibu
4. Mgonjwa anayeharisha anatakiwa kupatiwa huduma gani ya kwanza?
- kumpeleka kwa daktari mapema
- kumpa vidonge kupunguza maumivu
- kumpa maji yaliyochanganywa limau, sukari na chumvi
- kumpeleka kwa mganga wa kienyeji
- kumpa chakula cha kutosha
Chagua Jibu
5. Njia kuu inayoongoza kueneza virusi vya UKIMWI kwa watu ni:
- kutoboa masikio na pua
- kuwekewa damu
- kujamiiana
- ajali
- kudunga sindano
Chagua Jibu
6. Panda alikatazwa na mama yake kuchezea konokono. Unafikiria mama yake alikuwa anamwepusha na ugonjwa upi?
- kichocho
- kuhara
- malaria
- malale
- UKIMWI
Chagua Jibu
7. Todi alifungulia gesi toka kwenye mtungi na kuielekeza kwenye moto. Moto uliwaka zaidi. Je, mtungi ulikuwa na gesi gani?
- oksijeni
- kabondayoksaidi
- monoksaidi
- Haidroksaidi
- gesi ya upepo
Chagua Jibu
8. Baadhi ya majanga ya asili ambayo huweza kuhatarisha mimea na misitu ni:
- mvua zinazoambatana na tufani, ukame na volcano
- moto, ukame na volcano
- mvua zilizoambatana na tufani, moto na volcano
- moto, ukame na mvua zilizoambatana na tufani
- moto, kemikali za mimea na mifugo mingi kupita kiasi
Chagua Jibu
9. Wakati wa mchana mimea ya kijani hupunguza gesi gani kwenye anga?
- kabonidayoksaidi
- naitrojeni
- haidrojeni
- oksijeni
- naitret
Chagua Jibu
10. Inashauriwa mahali pa kujenga Choo cha shimo pawe:
- bondeni karibu na mto
- ndani ya nyumba ya kuishi
- mbali kidogo na nyumba ya kuishi
- tambarare sana
- karibu sana na nyumba ya kuishi
Chagua Jibu
11. Iwapo swala katika mlishano ufuatao wataongezeka, lipi litajitokeza kwa haraka? MAJANI → SWALA → SIMBA
- majani yatapungua
- simba watakufa
- idadi ya simba haitabadilika
- kiasi cha majani hakitabadilika
- majani yataongezeka
Chagua Jibu
12. Baada ya utungisho, kitoto chura huitwa:
- lava
- buu
- tunutu
- tedipoli
- yai
Chagua Jibu
13. Sehemu mbili za ua zinazoungana na kuwa stameni ni:
- mbegu na pistili
- staili na kikonyo
- ovari na sepali
- petali na sepali
- filamenti na kichavua
Chagua Jibu
14. Hatua ya pili katika ukuaji wa mende ni:
- lava
- tunutu
- buu
- mende kamili
- yai
Chagua Jibu
15. Kwa kawaida mimea hukua kuelekea wapi?
- kwenye maji
- kwenye mwanga
- mwelekeo wa upepo
- kwenye rutuba
- gizani
Chagua Jibu
16. Sehemu ya ua ambayo hupokea chavua au poleni huitwa:
- staili
- stigma
- ovari
- stameni
- ovuli
Chagua Jibu
17. Mchoro ufuatao unaonesha kiumbe anayeishi majini.
|
Kielelezo 1 |
Ni sehemu ipi ya mwili wake humsaidia kuogelea?
- U
- R
- T
- V
- S
Chagua Jibu
18. Ni ogani ipi inayohusika kubadili seli hai nyekundu za damu kuwa chembechembe za nyongo katika mwili wa binadamu?
- ini
- figo
- moyo
- mapafu
- wengu
Chagua Jibu
19. Vifuatavyo ni vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme isipokuwa:
- maporomoko ya maji
- nishati ya jua
- ngurumo ya mvua
- fueli
- upepo
Chagua Jibu
20. Eleza mabadiliko ya nishati yanayotokea katika Kielelezo kifuatacho wakati mvuke unapotumika kuzungusha kata upepo:
|
Kielelezo 2 |
- umeme kuwa sauti
- sauti kuwa joto
- joto kuwa kimakanika
- sauti kuwa umeme
- umeme kuwa sumaku
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |