SAYANSI 2008
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbeleya kila swali katika karatasi yakoya kujibia.
1. Licha ya kusaidia kujenga misuli michezo huimarisha nini?
- Miguu
- Viungo vya mwili
- Viungo vya kichwa
- Mikono
- Viungo vya sehemu ya juu ya mwili
Chagua Jibu
2. Faida kubwa ya uzazi wa mpango kwa familia ni .........
- kuwapa watoto elimu
- kufanya idadi ya watoto kuwa kubwa
- kuweza kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia
- kuepuka matatizo
- kuwa na uwezo wa kutoa huduma zote muhimu kwa familia
Chagua Jibu
3. Ni kundi lipi kati ya makundi yafuatayo hutoa mafunzo ya Huduma ya kwanza pamoja na huduma yenyewe?
- Msalaba mwekundu
- Angaza
- Askari wa zimamoto
- Wasamaria wema
- Askari wa usalama barabarani
Chagua Jibu
4. Chakula kinachoupatia mwili virutubisho vyote katika uwiano sahihi ni:
- mlo wenye protini
- mlo wenye protini na kabohaidreti
- mlo kamili
- chakula kilichopikwa vizuri
- chakula kinachonukia vizuri
Chagua Jibu
5. Namanji anaonekana kupinda miguu. Unafikiri anakosa madini gani?
- Kalsiamu
- Sodiamu
- Magnesiamu
- Chuma
- Aluminiamu
Chagua Jibu
6. Yafuatayo ni magonjwa yanayoweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo kwa watoto:
- Kifaduro, polio, pepopunda na surua
- Kuhara, tetekuwanga, surua na homa ya matumbo
- Polio, unyafuzi, pepopunda na kifaduro
- Tetekuwanga, utapia mlo, surua na polio
- UKIMWI, kifua kikuu, pepopunda na kuhara damu
Chagua Jibu
7. Degedege husababishwa na:
- ugonjwa wa mafua ya ndege
- kikohozi kikali
- homa kali
- kipindupindu
- UKIMVVI
Chagua Jibu
8. Mama Katu ameingia chumbani na kumkuta mumewe ameanguka chini baada ya kushituliwa na umeme. Mama Katu atamsaidia mumewe kwa:
- kumpa maji safi ya kunywa
- kumpa maziwa
- kumtikisa kwa nguvu
- kumpulizia hewa
- kumwogesha
Chagua Jibu
9. Hewa ni mchanganyiko wa:
- Oksijeni
- kabondayoksaidi
- gesi
- mvuke
- maji na oksijeni
Chagua Jibu
10. Maji katika hali ya mvuke ni:
- Mawingu
- mvua
- barafu
- umande
- unyevu
Chagua Jibu
11. Moja kati ya hatua ziifuatazo huzuia mmomonyoko wa udongo:
- Kupunguza wingi wa miti
- Kuchoma misitu
- Kupanda miti
- Kukwatua nyasi
- Kuongeza idadi ya mifugo
Chagua Jibu
12 Kiwavi ni lava wa
- panzi
- mende
- chura
- kipepeo
- mbu
Chagua Jibu
13.Jambo lipi linaweza kusababisha kutokea kwa "badiliko chanya" katika maliasili ya mazingira?
- Kuvua samaki kwa kutumia sumu
- Kulima holela kwenye miinuko
- Kukata miti ovyo karibu na vyanzo vya maji
- Kuvua samaki kwa kutumia baruti E. Kupanda miti na nyasi
Chagua Jibu
14.Zifuatazo ni sifa muhimu zinazotambulisha viumbe hai. Unafikiri ni sifa ipi haihusiki?
- Kupumua
- Kukua
- Kujitengenezea chakula
- Kujongea
- Kuzaliana
Chagua Jibu
15.Sehemu ya mbegu inayotunza chakula cha mbegu inayoota ni:
- ghala
- ganda
- embryo
- kijusi
- kikonyo
Chagua Jibu
16. Chunguza jani la mmea lililooneshwa kwenye kielelezo kisha jibu swali linalofuata.
Jani hilo unaweza kulifananisha na jani la mmea upi kati ya ifuatayo?
- Mpunga
- Mtama
- Kunde
- Mahindi
- Mnazi
Chagua Jibu
17. Nta hutengenezwa kutoka katika ......... ya nyuki.
- Matezi
- Mabawa
- Macho
- Miguu
- Mafumbatio
Chagua Jibu
18.Sehemu ya ua inayovutia wadudu wanaokuja katika mmea na kusaidia uchavushaji na uchukuaji wa poleni inaitwaje?
- Petali
- Sepali
- Stigma
- Kikonyo
- Pistili
Chagua Jibu
19. Mgongo wa chura ni mfupi ili kumwezesha .........
- kukimbia
- kulala
- kupaa
- kuruka na kutua
- kugeuka
Chagua Jibu
20.Kipi kati a Vitu vifuata husafirisha •oto kwa haraka zaidi?
- A
- B
- C
- D
- E
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |