SAYANSI 2007
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasi ya kujibia.
1. Umuhimu wa vyakula vya kabohaidreti mwili ni
- Kujenga mwili
- Kulinda mwili
- Kutia nguvu
- Kuweza kufikiri
- Kuongeza joto
Chagua Jibu
2. Ukiwa katika chumba chenye giza na ghafla taa ikawashwa kitatokea nini kuhusu jicho?
- Mboni ya jicho itaongezeka ukubwa
- Mbona ya jicho itabaki vilevile
- Lenzi ya jicho itabinuka
- Mboni ya jicho itapungua ukubwa
- Kelele za nguvu zitasikika
Chagua Jibu
3. Kikohozi kikavu, homa, kutoka jasho usiku na kukohoa damu ni dalili za . . . . . .
- Kifua kikuu
- Tetekuwanga
- Pepopunda
- Homa ya matumbo
- Kifaduro
Chagua Jibu
4. Michoro katika kielelezo namba 1 inawakilisha seli katika mwili wa binadamu ambazo kazi zake ni:
|
Kielelezo Na. 1 |
- Kuzuia na kukinda mwili
- Kusafirisha oksijeni
- Kugandisha damu
- Kurekebisha joto
- Kusafirirsha taka mwilini
Chagua Jibu
5. Mtu mwenye kiribatumboni ni rahisi zaidi kupata ugonjwa gani?
- Moyo na msukumo mkubwa wa damu
- Kansa
- Unyafuzi
- Kuvia kwa ukuaji wa akili
- Kwashakoo
Chagua Jibu
6. Vinyesi na vitu vya wanyama na mimea vilivyooza
- Huufanya udongo usifae kwa kilimo
- Vinakaribisha wadudu wengine wanaoharibu mazao
- Vinaongeza mbolea ya mboji kwenye udongo
- Havina umuhimu katika udongo
- Vinatumika kama chombo kwa wavuvi.
Chagua Jibu
7. Mwanga na sauti vina tabia moja tu. Je tabia hiyo ni ipi?
- Kupinda
- Kuakisi
- Kusharabiwa
- Kupita kwenye vakyumu
- Kusambaa
Chagua Jibu
8. Kuhifadhi vyakula katika jokofu ni njia ambayo ..
- Hufanya vyakula vikae muda mrefu bila kuharibika
- Inapunguza kazi ya kupika mara kwa mara
- Inapoteza ladha na kuvifanya vioze iwapo vitakaa siku nyingi
- kugeuza chakula kuwa barafu
- inapunguza gharama ya kwenda sokoni.
Chagua Jibu
9. Ukiweka sarafu ya shilingi 20 katika beseni lenye maji, sarafu hiyo inaonekana mepansa juu. Hali hiyo hutokea kwa sababu .........
- Sarafu hiyo ni nyepesi
- Macho yanamatatizo
- Mwanga umenyooka
- Maji ni kidogo
- Mwali wa mwanga hupinda unapoingia katika maji
Chagua Jibu
10. Kwa nini chupa za soda na bia hazijazwi hadi pomoni?
- Kwa ajili ya nafasi ya gesi
- Husaidia kufungwa chupa kwa urahisi
- Kuruhusu kutanuka wakati ya joto
- Kupunguza gharama
- Ikijazwa huweza kumwagikia mnywaji
Chagua Jibu
11. Volkano hai hutoa kimiminika kizito katika uso wa dunia kiitwacho:
- Lava
- Kreta
- Gesi
- Volcano
- Maji
Chagua Jibu
12. Kwa nini kwa kawaida mwanga unaonekana kwanza kabla ya muungurumo wa radi ingawa vyote vinatokea pamoja?
- Mwanga unamawimbi makubwa kuliko sauti
- Mishipa ya fahamu ya macho inafanya kazi haraka kuliko mishipa ya fahamu ya kusikia
- Mwendokasi wa mwanga ni wa haraka kuliko sauti
- Mwanga na sauti kwa kawaida husafiri wima
- Mawimbi ya sauti hayasafiri katika hewa
Chagua Jibu
13. Vipi kati ya Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha uchafuzi wa hewa?
- Maji machafu ya viwandani, spiriti na ujenzi wa biashara
- Moshi, Majivu na mbolea
- Moshi wa viwandani na matokeo ya kuungua kwa petrol
- Misitu asili, viwanda na mbolea
- Mbolea, mboji na maji machafu ya viwandani
Chagua Jibu
14. Ni kiumbe kipi kati ya vifuatavyo huishi kwenye maji?
- Inzi
- Buibui
- kaa
- Panzi
- Mende
Chagua Jibu
15. Ukuaji wa mbu hupitia katika hatua/kuu nne. Mtiririko sahihi wa ukuaji huo ni . . . . . . . . .
- Yai, pupa, lava, mbu
- Pupa, yai, lava, mbu
- Yai, lava, pupa, mbu
- Lava, yai, pupa, mbu
- Pupa, lava, yai mbu
Chagua Jibu
16. Kitendo cha mmea kufuata mwanga katika kielelezo na 2 huitwa .........
|
Kielelezo Na. 2 |
- Kutembelea
- Kukua
- Kujongea
- Kuitikia kichocheo
- Kuhisi
Chagua Jibu
17, Chanzo cha chakula kwa wanyama ni .........
- Mmea
- Mimea na nyama
- Mimea kwa hebivora na nyama kwa canivora
- Maziwa
- Maharage
Chagua Jibu
18. Vyombo vya kupikia Vina mikono iliyotengenezwa kwa mbao na plastiki kwa sababu ...m
- Haipitishi joto haraka
- Haipitishi joto
- Husharabu joto
- Huakisi joto
- Hutunza joto kwa muda mrefu
Chagua Jibu
19. Kuta, sarafu na dari ya nymba ya utangazaji vimewekewa Vitu Iaini ili.
- Kupunguza sauti
- kuakisi
- Kuongeza sauti na nguvu
- kufanya sauti kuwa Iaini na safi
- Kupunguza mwamgwi
Chagua Jibu
20. Kuna uhusiano gani kati ya sumaku na umeme.
- Zote ni nishati za kemikali
- Zote ni sakiti za umeme
- Kuliko na sumaku lazima kuwe na umeme
- Kuliko na umeme lazima kuwe na sumaku
- Zote zinatoa nishati ya mwanga
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |