STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2006
SAYANSI 2006
SEHEMU A
Chaguajibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi yakoya kujibia.
1. Katika mambo yafuatayo, lipi linawakilisha badiliko la kiumbo?
Maji kuwa mvuke
Kuchoma karatasi
Asali kubadilika kuwa pombe
Chuma kupata kutu
Kuni kuwa mkaa
Chagua Jibu
2. Mojawapo ya yaliyoorodheshwa hapa chini husaidia kuhifadhi mazingira nayo ni:
kukata miti kwa ajili ya kuni na kujenga;
kubadilibadili mazao ya kupanda shambani;
kutumia mbolea ya chumvi chumvi;
kusafisha mashamba kwa kukatua;
kufuga ng'ombe kwa wingi.
Chagua Jibu
3. Madini iliyo ngumu kuliko nyingine zote ni ipi?
Almasi
Makaa ya mawe
Shaba
Ulanga
Dhahabu
Chagua Jibu
4. Nyama, samaki, maziwa na mayai ni vyakula vya:
kutia nguvu
kulinda mwili
kujenga mwili
kutia joto mwili
kuhitaji mbinu bora za kuhifadhi.
Chagua Jibu
5. Mimea hujipatia maji na madini ya chumvi chumvi kwa njia inayowakilishwa na herufi L katika mchoro ufuatao. Njia hiyo ni ipi?
mjongeo wa maji na madini
translokesheni
fototropizimu
Osmosis
fotosinthesis
Chagua Jibu
6. Gurudumu kapi ni mashine ... ... ...
tata itumikayo kupandisha vitu juu
imara iliyoshikishwa na gurudumu dogo
yenye meno yanayoingiliana na ya gurudumu jingine
rahisi itumikayo kupandisha vitu juu
nayotumika kufungia maunzi pamoja.
Chagua Jibu
7. Namba gani katika mchoro ufuatao inawakilisha tezi itoayo homoni ambayo humfanya mtu asipate ugonjwa wa kisukari?
1
2
3
4
5
Chagua Jibu
8. Meli inaelea katika maji (baharini au ziwani) kwa sababu ina:
nafasi kubwa tupu iliyojaa hewa ndani
nafasi yenye hewa kidogo
uzito mdogo kuliko maji
mstari wa plimsoli unaozuia maji
ujazo nene mdogo kuliko maji
Chagua Jibu
9. Jaribio hili (chunguza kwa makini mchoro ufuatao) hudhihirisha kvvamba mwanga
husafiri na kugawa vitu sehemu mbili
husafiri katika mstari mnyoofu
husafiri na kupinda upitapo katika media tofauti
husafiri ndani ya maji kwa kujikunja
husafiri na kusababisha vitu kupinda
Chagua Jibu
10. Mnyororo wa baiskeli hupitia gia mbili (tazama mchoro ufuatao). Gia iliyozungushwa na tairi la nyumba ina meno 20 na ile iliyounganishwa na pedali ina meno 50. Iwapo pedali zitafanya mizunguko miwili, tairi la nyuma litazunguka mara .........
Tano
Nne
Tatu
Moja
Nyingi
Chagua Jibu
11. Sehemu zinazofanya mfumo wa mzunguko wa damu ni damu yenyewe,
ubongo na mishipa ya damu
mapafu na mishipa ya damu
moyo na mishipa ya damu
moyo na mishipa ya fahamu
moyo na ubongo
Chagua Jibu
12. Uzito wa mzigo x katika mchoro ufuatao ni:
kilo 200
kilo 2.5
kilo 25
kilo 250
kilo 36.2
Chagua Jibu
13. Tendo Ia kuvunjavunja na kubadili chakula ili kiweze kunyonywa au kufyonzwa na mwili hujulikana kama
kumeng'enya
kurutubisha
kusharabu
eksrisheni
respiresheni
Chagua Jibu
14. Chunguza mchoro ufuatao kwa makini. Je, ni kitu kipi chembe zake zimeachana sana?
Chagua Jibu
15. Ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo husababishwa na ukosefu wa vitamini?
Kifua kikuu
Kiseyeye
Tetekuwanga
Malaria
Kuhara
Chagua Jibu
16. Usumaku unaweza kuondolewa kwa kufanya yafuatayo:
kugongagonga na kupasha joto ikiwa imening'inizwa Mashariki-Magharibi
Kuining'iniza Mashariki-Magharibi na kuiosha
Kuizungusha koili na kupitisha umeme
Kuizungushia koili na kuichoma
Kuigongagonga na kuzungushia koili
Chagua Jibu
17. Uvuvi wa samaki kwa kutumia baruti ni njia mojawapo ya:
kukuza sayansi
kuua magugu maji yanayochafua mazingira
kuharibu mazalio ya samaki na kuchafua mazingira
kuondoa aina ya samaki wakubwa
kuwafukuza papa wakali wasiwale samaki wadogo wadogo
Chagua Jibu
18. Sehemu inayooneshwa kwa herufi Z katika mchoro ufuatao huitwa
nyukliasi
vakyuli
saitoplazimu
ukuta wa seli
epithiliamu
Chagua Jibu
19. Ni ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo huweza kuzuiwa kwa chanjo?
Kifaduro
Kisonono
Malaria
Homa ya matumbo
Kipindupindu
Chagua Jibu
20. Kati ya matendo yafuatayo, ni yapi huongeza kasi ya mmomonyoko wa ardhi?